Uhalali wa mtoto anayezaliwa kwa IVF miaka kadhaa baada ya baba kufariki. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhalali wa mtoto anayezaliwa kwa IVF miaka kadhaa baada ya baba kufariki.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by maringomashaka, Sep 24, 2012.

 1. m

  maringomashaka Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  In vitro fertilisation (IVF)
  Hii ni njia ambayo inatumika kupata mimba kwa wanandoa ambao wanamatatizo ya uzazi. Mara nyingi tatizo linakuwa kwa mwanamke hasa anayekuwa na tatizo la kuziba kwa mirija hasa yote miwili na kushindwa kuruhusu mbegu za kiume kupita ili zikakutane na yai lililopevuka kwa ajili ya kuchavusha mayai. Kwa ufupi kinachofanyika ni kwamba mayai ya mwanamke yanachukuliwa kutoka kwenye mfuko wa uzazi yanapokuwa yamekwisha komaa kwenye hatua yakuweza kuchavushwa na kutunga mimba pindi yanapokutana na mbegu za kiume. Mbegu za mwanaume zinakusanywa pia na kuchanganywa pamoja na mayai haya katika maabara maalumu kwenye chombo maalam ili mayai yaweze kuchavushwa. Baada ya sku kuanzia tatu hadi tano mayai yanakuwa yamechavushwa na kutengeneza mimba changa (zygote) ambayo inapandikizwa katika mfuko wa uzazi wa mwanamke na kuruhusiwa kukua kama mimba ya kawaida.

  Utafiti wangu usio wa kisayansi kuhusu uhalali wa njia hii katika misingi ya dini kadhaa hapa nyumbani ikiwa dini mbili kubwa za Kikristu na Kiislam umebainisha kuruhusiwa kwa njia hii kutokana na dharura ya maradhi ya matatizo ya uzazi, kwahiyo haina shaka kuwa ni njia mbadala kama njia ya kawaida ya kupata watoto imeshindikana. Hii inakubalika tu kama wawili hao ni wanandoa, hii ni kwa mtazamo wa kidini zaidi ila ni halali hata kama wawaili hawa hawakufunga ndoa kwakuwa kwa wenzetu wa Magharibi mwanamke anaweza kwenda kununua mbegu kutoka kwenye benki ya mbegu na kupandikizwa.

  Kutokana na maendeleo ya kisayansi na teknologia hivi saa, mbegu za mwanaume zinaweza zikahifadhiwa kwenye maabara maalam (sperm bank) na kutumika miaka kadhaa ijayo na kutengeneza mimba.

  SWALI:
  Chukulia mume amefariki na ameacha mbegu zake za kiume kwenye benki maalamu ya kuhifadhi mbegu za kiume (sperm bank). Baada ya miaka kadhaa ya kifo chake iwe mwaka mmoja au na zaidi mwanamke ameamua azae kwakutumia mbegu za marehemu mume wake, na akafanya hivyo na akafanikiwa kushika mimba na hatimae kuzaa
  1.) Kwa mitazamo ya kidini hususani dini hizi zetu mbili (Ukristo na Uislam) je mtoto atakubalika uwa amezaliwa ndani ya ndoa, kutokana na jibu lako ni kwanini iwe hivyo? Kuna maandiko yeyote yaliyojaribu kugusia juu ya hili?
  2.). Kwa mtazamo wa kimaadili ya jamii ya Kitanzania, mila na desturi zetu, je kuna uhalali wowote wa mwanamke kutumia mbegu za marehemu mumewe miaka kadhaa baada ya kifo chake? Jamii itaipokeaje? Je kama ni mke wa mtoto wako utaruhusu hilo lifanyoke
  3) Kwakuwa Dunia ina badilika kwa kasi kutokana na maendeleo ya sayansi na teknologia na kwakuwa sisi tunaishi kwenye Dunia ya uhalisia, je wewe unashauri nini juu ya hili kwa jamii na viongozi wa dini kwakuwa ukweli ni kwamba haya yametokea, yanatokea na yataendelea kutokea na ni hali halisi tunayoishi nayo kama si wewe, basi ndugu yako wa karibu, rafiki au mwanajamii.

  Note: Naomba mchango wenu wa kisayansi, kidini na kijamii juu ya hili. Mawazo yote ni mawazo muhimu na yanaheshimika na kupewa umuhimu sawa kwani hakuna mawazo ya Kipumbavu. Karibuni jamvini.
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  hapo namba moja, kidini, sidhani kama kuna maandiko yanayokataza, sijui kuhusu dinimnyingine ila biblia sidhani kama imekataza, na kama mmeambiwa nendeni mkaongezeke na kuijaza dunia jazeni tu, Mungu amemuumba binadamu kwa mfano wake, akampa akili na utashi atumie akili hizo, hivyo sioni ubaya wa kuzumia IVF

  sira 38: 1-2 mpe daktari heshima anayostahili,
  kwa sababu ya huduma zake kwako,
  kwa vile nae aliumbwa na Bwana.
  Maana kipaji chake cha kuponya chatoka kwa Mungu Mkuu;
  nae hupata zawadi kutoka kwa mfalme.
  Sira38:6 Bwana aliwapa watu maarifa na ujuzi,
  ili atukuzwe katika kazi zake za ajabu

  kuhusu sperm za mume, naamini familia za kiafrica zinaheshimu sana matakwa ya marehemu, kama marehemu alitaka hivyo na kwa mapenzi yao walikubaliana hivyo kwa nini wakatae?( hißuu ni mtazamo wangu binafsi tu lakini)
   
 3. m

  maringomashaka Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana kwa mchango wako ndugu yangu husasani hizo aya ulizozitoa. Tuendelee kuchangia
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Duh, kama mme amefariki mwaka mzima, wewe unaamua kupata mtoto? How?

  Kwa nini wasipandikize pale pale anapozitoa? Na kama walipanga kutoa kuzaa baada ya mwaka, kwa nini hizo mbegu azitoe mapema hivyo?

  Unajua raha ya mtoto mkubaliane wawili, lakini hii kumuamlia mmoja sina hakika sana kama huwa ni sawa.

  Na pili, kuhusu mzazi wa mume kukubali, sina hakika sana, maana inategemea na hisia za mtu, kuna mwingine anaweza ona ni jambo zuri maana itafidia 'loss' ya mtoto wake, mwingine anaona hapana ni kama kuongeza machungu au kama mme alikuwa na mali halafu hawakuwa na mtoto kabisa wengine wataona mke anajitafutia uhalali wa kurithi mali. Sio jibu la straight hapa.

  Kuhusu mambo ya dini, nadhani hapa kila mmoja anaweza chukulia tofauti. Umuhimu wa mtoto ukiizidi imani yako badi utaendelea na kupandikiza, au imani ikizidi hitaji la mtoto basi hutafanya. Hapa itategemea kipo mihimu kwako kwa muda huo.
   
 5. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  1)ndoa inaisha mmoja akifa.
  2)kama walikubaliana then its okay, personally siko comfortable using a deceased person's sperm but thats just me.
  3)IVF is okay for infertile couples (wagumba, lesbians etc). if the parents are willing and can care for the child then I see no objection. not advising on using deceased person's sperm as it may bring heartache ukimfikiria marehemu, pia its tougher for the child etc
   
Loading...