S.N.Jilala
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 540
- 507
Uhalali wa Kuongoza Kisiasa (Political Legitimacy).
Kwanza kabisa tafiti nyingi zimesema kwamba hakuna uhalali wa kutawala au kuongoza ambao uko Kidunia japo Mataifa na Mashirika makubwa huwa wanapenda wakati mwingine kutuaminisha hivyo.
Uhalali unatokana na maeneo, watu walivyokubaliana wao wenyewe kulingana na wao wanavyoona inafaa kujitawala. Tatizo kubwa kupima kwamba watu wamekubaliana wenyewe ni ngumu kwa sababu kuna viongozi kwa matakwa yao na kwa kutumia unyonge wa wanaowaongoza, hutengeneza sheria na kanuni na kusema watu wamekubalina wenyewe kuwa au kufanya hivi.
Ndiyo maana likaibuka swala la Utawala bora Duniani ili kukabiliana na viongozi wa namna hii lakini bado watu katika Taifa husika wawe na maswala yao.Huwa inadhihirika tu kwamba watu hawajakubaliana kwa sababu Kiongozi hufika wakati anakosa uhalali wa kuongoza au kutawala kwa kutumia sheria hizohizo kandamizi na huamua kutumia mkono wa chuma au mtutu wa bunduki.
Kiongozi yoyote anayetumia mabavu ya hali ya juu kuongoza, ubabe, uonevu, fitina, kutotii katiba na sheria; huyu amekosa kabisa political letimacy yaani uhalali wa kuongoza kisiasa. Au anaweza kutii katiba na akakosa uhalali wa kutawala itategemea na mahitaji ya wananchi wake.
Uhalali wa kuongoza hauishii tu kwenye kufuata sheria kama ambavyo wengi tunavyoweza kufikiri, bali huenda mbali kabisa. Kwa mfano, ukishinda uchaguzi kwa kuiba kura, kutumia dola na kufanikiwa kuingia katika uongozi. Je utakuwa na uhalali wa kuongoza?
Legitimacy yaani uhalali wa kuongoza naweza kusema ni kati ya chanzo kikubwa cha migogoro yetu Duniani katika karne ya 20 na 21. Hasa Afrika changamoto hii ni kubwa sana. Tena uhalali wa kuongoza na kutawala kisiasa (Political Letimacy) una ukakasi sana kwa watawala wengi.
Uhalali wa Kutawala, Kuongoza na Kutoa Amri unaweza kukosa uhalali au kuwa na uhalali wa kisiasa (political legimacy) kwa mambo mbalimbali.
Mosi, yanaweza kuwa ya kisheria. Pili, kiutamaduni katika jamii husika. Tatu, kukosa kabisa uungwaji mkono na watu katika uongozi wako kwa sababu huna kismati kwa watu.
Uhalali wa Kuongoza kisiasa hutoweka wakati mwingine si kwa sababu eti unafuata katiba na sheria ya nchi. Je, hizo sheria zinakubalika?. Kama sheria ni kandamizi watu watakupinga pamoja na kwamba unazifuata.
Jambo lingine ni kufanya kinyume kabisa na watu wanavyotaka ufanye huku ukidhani watu hawaelewi ukweli.
Kwa mfano, Baba akiwa mlevi wa kupindukia anakosa kabisa legitimacy ndani na nje ya familia kuwafokea, kuwaonya watoto wake wanaokunywa bia. Anaweza akasema Mimi ni Baba Nina haki ya kulewa kila siku lakini akumbuke anakosa uhalali wa kuwaonya watoto.
Hivyohivyo, kama Mwanasiasa anahubiri jambo fulani kwa wananchi kama yeye halifanyi au yuko kinyume na matamko yake au matendo na anachokitamka anakosa uhalali wa kisiasa kulihubiri. Sasa kwa mfano, kama mwanasiasa anatuhumiwa kuwa ana vyeti feki atapataje Political Letimacy ya kuwaambia wafanyakazi kwamba nyie mna vyeti feki katika mikutano yake?. Hata kama kigezo ni kusoma na kuandia lakini uhalali kisheria unakosekana kwake!!.
Nimalizie kwa kusema hivi;
Ukiwa kiongozi lazima ujue uhalali wa kuwaongoza unaowaongoza uko wapi kwako?. Lazima utafakari sana kwani uhalali wa kuwaongoza unaowaongoza haupo kwenye katiba, sheria na kananu tu kama viongozi wengi wanavyodhani. Kwa mfano, nikiwa nahubiri amani na kusamehe wakati Mimi mwenyewe katika matendo yangu naonyesha kuwa MTU wa chuki na visasi, hakika nitakosa uhalali wa kuihubiri amani hiyo. Nikiihubiri amani nitaihubiri kwa njia hizohizo ninazoziamini za kutumia chuki na visasi. Kwa kufanya hivyo, nakosa uhalali kabisa wa kuihubiri amani.
29/04/2017