Uhalali wa jina TANZANIA kikatiba unatoka wapi?

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,789
Wana Majlis/Bodi
Nimesoma na kutafuta ukweli na uhalali wa jina hili Tanzania unatokana makubaliano gani? Makubaliano ya awali ya Muungano kama yalivyoanishwa kwenye " Articles of the Union" imeeleza wazi jina la jamhuri wala haikueleza mbadala kuhusu upatikanaji wa jina litakalo maanisha Jamhuri yaMuungano wala taratibu la kulipata jina hilo.

Aidha Makubaliano hayo hayakuridhiwa na Zanzibar wala Bunge la Katiba halikuwahi kuundwa kwa zaidi ya miaka 50 kupita. Lakini katika makubaliano hayo kwenye kipengele cha "Declaration of the United Republic" kuna maelezo yanayojitosheleza yafuatayo

"The Republic of Tanganyika and the People's Republic of Zanzibar shall, upon Union Day and ever after, be united into one United Sovereign Republic by the name of the United Republic of Tanganyika and Zanzibar.

Sasa huyu " TANZANIA" Kazaliwa na nani? na kwa ndoa ipi, ndani ya ndoa au nje, na imebarikiwa kwa sheria ipi?
 
Katiba ya muungano inataja hilo jina la Tanzania na ikaridhiwa na pande zote ikimaanisha kuwa walioridhia yaani bunge na baraza la wawakilishi wanaridhia yote ikiwemo jina la Tanzania ndani ya katiba.Wasingeridhia kwenye katiba lisingekuwa na uhalali kutumika kisheria.
 
1.Lilpotungwa neno Tanzania ulikuwa umeshazaliwa? Kama wakati huo ulikuwa tayari umekuwa hai 1964 Kulikuwa hakuna Baraza la Wawakilishi Zanzibar na "dcree" tu ndio iliokuwa inatumika. Hayo makubaliano yenyewe ya muungano hayakuwahi kuridhiwa upande wa Zanzibar seuze jina.Bora ni kusema kuwa Mwl Nyerere alikuwa anakerwa na jina Tanganyika na akatumia mwanya huo kulibadilisha alau kupata ladha kutamkwa.
2. Hakuna katiba ya Muungano, kwa vile makubaliano ya Muungano ya kupata Katiba ya Muungano hayakufanyika. Katiba ilioko ni ya Tanganyika. ilioazimwa"the interim Constitution" na kwa muda na muda wake umeshapita miaka 51iliopita. Makubaliano ya Muungano yalitaka Bunge la Katiba lifanyike ndani ya mwaka mmoja tokea makubaliano ya Muungano yalipofanyika: "Summon a Constituent Assembly composed of Representatives from Tanganyika and from Zanzibar in such numbers as they may determine to meet within one year of the commencement of the union for the purpose of considering the proposals of the Commission aforesaid and to adopt a Constitution for the united Republic.
 
1977 BUNGE na baraza la wawakilishi waliridhia katiba yenye jina la Tanzania ndani.Hivyo kutoa uhalali rasmi wa kutumia jina TANZANIA
 
Bado ulikuwa mtoto mdogo. Baraza la wawakilishi lilianzishwa na Rais Jumbe mwaka 1980.Sasa hiyo 1977 inatoka wapi?Usichanganye mjadala wa kuunganisha vyama vya TANU na ASP ? Hata utetezi wako usio na mashiko uwe kweli, kw hivyo unataka kusema jina la Tanzania kuanzia 1964 - 1977 lilikuwa linatumika kiharamu?
 
bunge lililohalalisha lilikuwa na wabunge wote wa Tanzanyika na ZANZIBAR
 
02b3fb2cb9e15897b244fb6003efe328.jpg
nafatilia mjadala kwa karibu sana.
 
Wana Majlis/Bodi
Nimesoma na kutafuta ukweli na uhalali wa jina hili Tanzania unatokana makubaliano gani? Makubaliano ya awali ya Muungano kama yalivyoanishwa kwenye " Articles of the Union" imeeleza wazi jina la jamhuri wala haikueleza mbadala kuhusu upatikanaji wa jina litakalo maanisha Jamhuri yaMuungano wala taratibu la kulipata jina hilo.

Aidha Makubaliano hayo hayakuridhiwa na Zanzibar wala Bunge la Katiba halikuwahi kuundwa kwa zaidi ya miaka 50 kupita. Lakini katika makubaliano hayo kwenye kipengele cha "Declaration of the United Republic" kuna maelezo yanayojitosheleza yafuatayo

"The Republic of Tanganyika and the People's Republic of Zanzibar shall, upon Union Day and ever after, be united into one United Sovereign Republic by the name of the United Republic of Tanganyika and Zanzibar.

Sasa huyu " TANZANIA" Kazaliwa na nani? na kwa ndoa ipi, ndani ya ndoa au nje, na imebarikiwa kwa sheria ipi?
Jina Tanzania ni mkakati maalumu wa Tanganyika( Nyerere) kuhakikisha Tanganyika inavaa koti la Muungano (pitia hoja za Tume ya Warioba/ Tume ya kuandaa Rasimu ya Katiba mpya na pendekezo la serikali 3). Tanganyika kuvaa koti la Muungano lina lengo la kuimeza Zanzibar.

Rasimu mpya ya Maintarahamwe kama alivyoiita Profesa Lipumba itatimiza lengo hilo.

Jina Tanzania pia lilikusudiwa kuficha jina la mshirika mmoja wa Muungano ambalo limekuwa dhambi na ilionekana kama uhaini kulitaja hadharani, Tanganyika.

Baada ya kubuniwa jina Tanzania,Tanganyika inajulikana kama Tanzania au Tanzania bara. Hii imefanya urahisi kwa watawala kuwagawia "maisha bora" aka umasikini wadanganyika. Lakini pia jina limetumika kuficha udini kwa ujanja wa hali ya kiwango cha Phd.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Mungu hawapendi wanafiki.
 
Back
Top Bottom