Uhakiki wa vyeti wanikosesha kazi na wasababisha mke wangu kuniacha

MP CHACHANDU

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
875
616
Mimi ni miongoni mwa vijana 3000 tulioajiriwa mwezi June 2016, niliajiriwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania kwenye mahakama ya wilaya nilipewa mkataba wa kazi na kuanza kufanya kazi na wenzangu tulioajiriwa kwenye kanda ya mahakama tulikuwa watu 348, tulipewa mikataba na barua za kazi na tulianza kufanya kazi baada ya kufanya kazi mwezi mmoja tulipewa barua za kusitishiwa ajira zetu kwa muda ili kupisha zoezi la uhakiki wa watumishi hewa.

Tulipowauliza maafisa utumishi wa mahakama kuwa lini wataturudisha kazini? Walitujibu kuwa uhakiki wa watumishi hewa ukiisha tutarudishwa kazini toka mwaka Jana mwezi wa sita 2016 tupo nyumbani hatupewi taarifa yoyote na wala hatujui hatima yetu tupo na mikataba ya kazi na barua za kupangiwa vituo vya kazi maisha yamekuwa magumu.

Kwa masikitiko makubwa mke wangu ameniacha Katoro anasema kuwa nilimdanganya sikuajiriwa na serikali kwenye Idara ya Mahakama, ameniachia watoto watatu wadogo mmoja ananyonya kisa mimi nimesimamishwa kazi kwa mda usiojulikana.

Nimeaibika kwenye jamii maana niliaga na kuwatarifu ndugu zangu kuwa nimepata ajira kwenye Mahakama sasa hivi ukoo unajua kuwa niliwadanya kabisa ukoo unaniongea vibaya kuwa niliwadanganya kuwa nimeajiriwa kumbe hakuna nalia sana na aibu hii iliyosababishwa na serikali majirani kila siku wananiulizia kuhusu ajira yangu hii maana walijua kuwa nimeajiriwa nashindwa kuwajibu nini nalia tu rais Magufuli, Katibu Mkuu Utumishi wa Umma, Waziri Angellah Kairuki mmenifanyia unyama huu Mungu yupo.

Baada ya kupangiwa kazi Kigoma nilipanga chumba nikahamisha na mizigo Yangu kutoka Geita mpaka Kigoma kwa gharama zangu niliposimamishwa kazi sikupewa pesa za kurudisha mizigo hiyo hivyo niliiacha Kigoma na nikarudi Geita na mke wangu na watoto wangu tulianza kulala chini ya cement maana magodoro tuliyaacha Kigoma kwenye nyumba ya kupanga nimelala chini na mke wangu na watoto mpaka mke wangu ameshindwa kuvumilia maisha haya mwishoe kanitoroka.

Nalia na watoto nifanyeje kisa nimesimamishwa kazi bila kosa, bora wasingeniajiri nisingehamisha mizigo yangu na ningeendelea na maisha na familia yangu kodi ya nyumba imeisha huko Kigoma nilipoacha, mizigo yangu mwenye nyumba anataka kuuza vitu vyangu ili apate fedha yake ya kodi inauma sana tena.

Serikali imekoswa huruma kiasi hiki omba yasikukute haya yaliyonipata.
 
Mke wako anakukimbia wakati wa Matatizo Lawama unaitupia kwa Mtukufu Raisi wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.. Mh. Joseph Pombe Magufuli..

Mkuu..!
Ni kosa kubwa sana kusema ngoja nilale tena kidogo kama dakika tano, ukiwa unajua fika kuwa muda wa kuamka kwenda kazini umeshafika..!

Amka..
 
aisee, naona hakuna uhalisia kwenye story yako.
umeajiliwa june 2016 una watoto 3. uyo mkeo ulishakua nae kitambo. suala la kusema amekuacha eti ulimdanganya kuhusu ajira si sahihi.
maisha yakiwa magumu mwanaume hutakiwi kulia. we ukilia mkeo afanyaje sasa?
ulishakua na maisha hadi kupata watoto wote hao. miezi sita haikufanyi ukose pa kuanzia.
wanaume tuache kulia lia. suala la mwanaume kula kwa jasho si nadharia.
 
Pole sana. Cha msingi sasa hivi sahau hiyo ajira. Itakuumiza kichwa. Jipange na uanze upya. Pia huna sababu ya kutangaza maisha yako ndio maana unahaha na ndugu na Majirani.
Mkuu kumbuka ukimwambia ndugu mmoja tu naye anamwambia mwingine nashindwa kuelewa aise ila asante kwa ushauri
 
aisee, naona hakuna uhalisia kwenye story yako.
umeajiliwa june 2016 una watoto 3. uyo mkeo ulishakua nae kitambo. suala la kusema amekuacha eti ulimdanganya kuhusu ajira si sahihi.
maisha yakiwa magumu mwanaume hutakiwi kulia. we ukilia mkeo afanyaje sasa?
ulishakua na maisha hadi kupata watoto wote hao. miezi sita haikufanyi ukose pa kuanzia.
wanaume tuache kulia lia. suala la mwanaume kula kwa jasho si nadharia.
Kwa hiyo unafurahia ? OK asante mkuu
 
Mke wako anakumbia wakati wa Matatizo Lawama unaitupia kwa Mtukufu Raisi wa Jamhuri Ya Muungano waTanzania.. Mh. Joseph Pombe Magufuli..

Mkuu..!
Ni kosa kubwa sana kusema ngoja nilale tena kidogo kama dakika tano, ukiwa unajua fika kuwa muda wa kuamka kwenda kazini umeshafika..!

Amka..
Mkuu na wewe siyo wewe
 
Uliokuwa unakimbilia kutotoa watpto wote hao, hukujua kuna changamotp za maisha kama hizo? By the way ole sana.. Huyo mkeo hajui maana ya ndoa.. Ndoa ni maisha ya shida na raha.
 
Uliokuwa unakimbilia kutotoa watpto wote hao, hukujua kuna changamotp za maisha kama hizo? By the way ole sana.. Huyo mkeo hajui maana ya ndoa.. Ndoa ni maisha ya shida na raha.
Mkuu usichokijua ni sawa usiku wa Giza mungu akuongeze
 
Mimi ni miongoni mwa vijana 3000 tulioajiriwa mwezi June 2016 ,niliajiriwa na tume ya utumishi wa mahakama Tanzania kwenye mahakama ya wilaya nilipewa mkataba wa kazi na kuanza kufanya kazi na wenzangu tulioajiriwa kwenye kanda ya mahakama tulikuwa watu 348, tulipewa mikataba na barua za kazi na tulianza kufanya kazi baada ya kufanya kazi mwezi mmoja tulipewa barua za kusitishiwa ajira zetu kwa mda ili kupisha zoezi LA uhakiki wa watumishi hewa tulipowauliza maafisa utumishi wa mahakama kuwa lini wataturudisha kazini ?walitujibu kuwa uhakiki wa watumishi hewa ukiisha tutarudishwa kazini toka mwaka Jana mwezi wa sita 2016 tupo nyumbani hatupewi taarifa yoyote na wala hatujui hatima yetu tupo na mikataba ya kazi na barua za kupangiwa vituo vya kazi maisha yamekuwa magumu.

Kwa masikitiko makubwa mke wangu ameniacha katoro anasema kuwa nilimdanganya sikuajiriwa na serikali kwenye idara ya mahakama ameniachia watoto watatu wadogo mmoja ananyonya kisa mimi nimesimamishwa kazi kwa mda usiojulikana nimeaibika kwenye jamii maana niliaga na kuwatarifu ndugu zangu kuwa nimepata ajira kwenye mahakama sasa hivi ukoo unajua kuwa niliwadanya kabisa ukoo unaniongea vibaya kuwa niliwadanganya kuwa nimeajiriwa kumbe hakuna nalia sana na aibu hii iliyosababishwa na serikali majirani kila siku wananiulizia kuhusu ajira Yangu hii maana walijua kuwa nimeajiriwa nashindwa kuwajibu nini nalia tu rais magufuli ,katibu mkuu utumishi wa umma, waziri angellah kairuki mmenifanyia unyama huu mungu yupo.

Baada ya kupangiwa kazi kigoma nilipanga chumba nikahamisha na mizigo Yangu kutoka geita mpaka kigoma kwa gharama zangu niliposimamishwa kazi sikupewa pesa za kurudisha mizigo hiyo hivyo niliiacha kigoma na nikarudi geita na mke wangu na watoto wangu tulianza kulala chini ya cement maana magodoro tuliyaacha kigoma kwenye nyumba ya kupanga nimelala chini na mke wangu na watoto mpaka mke wangu ameshindwa kuvumilia maisha haya mwishoe kanitoroka nalia na watoto nifanyeje kisa nimesimamishwa kazi bila kosa bora wasingeniajiri nisingehamisha mizigo Yangu na ningeendelea na maisha na familia Yangu Kodi ya nyumba imeisha huko kigoma nilipoacha mizigo Yangu mwenye nyumba anataka kuuza vitu vyangu ili apate fedha yake ya kodi inauma sana tena .

Serikali imekoswa huruma kiasi hiki omba yasikukute haya yaliyonipata .

Yaani hata kama huyo mke angekuwa ni ndugu yangu, ningemwambia akuache mara moja. Mwanaume gani umekalia kulia lia kila siku kwenye mitandao. Nikuulize swali, darasani kwenu mlikuwa wangapi, na ni wangapi ambao mlikuwa mmeajiriwa na serikali, na je, hao wengine wamekuwa wanafanya nini mpaka sasa?, Je, unafikiri wewe ndo mwenye haki zaidi kuliko hao wengine ya kupata ajira serikalini?.
Achana na huu ujinga wa kulia lia, ukiendelea kulia lia bila ya kuchukua jukumu la kiume na kusimama ili uweze kuitunza familia yako, watu watakugongea mke wako mpaka ataolewa na mtu mwingine, ajabu anaweza wala siwe mtumishi serikalini.
Umeshaambiwa, ajira zikitangazwa, omba tena, sasa wasi wasi wako ni nini?? Merits zilizokufanya uajiriwe hapo awali zitakufanya uajiriwe tena safari hii. Labda uniambie kuwa ulipata hiyo ajira kwa mchongo, hapo itakuwa imekula kwako. Ikumbukwe kuwa kilichochukuliwa kutoka kwako ni ajira, na si elimu yako.

Mwisho kabisa nikuambie kuwa, wewe ni mwanaume, na mpaka umezaa watoto watatu, tambua kuwa ni jukumu lako kulea hiyo familia yako na si jukumu la mtu mwingine yeyote yule wala serikali. Na familia yako inapo sambaratika, wa kulaumiwa ni wewe mwenyewe na si mtu mwingine, kwakuwa wakati unaoa na kupata hao watoto hakuna mtu mwingine yeyote aliekuja kukusaidia.
 
Wewe ni mtaalam wa sharia bila shaka nakushauri umshitaki kwenye mahakama ya mapenzi&ndoa iliyoko Harare Zimbabwe kwa kuvunjia ndoa yako.
 
Back
Top Bottom