Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,679
- 149,868
Nawashauri mtafute siku katika hili Bunge linalotarajiwa kuanza mwezi huu mkutane chini ya kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni kisha mje na huu uamuzi.
Wote mkubaliane kuwasilisha nakala za vyeti vyenu vya elimu kwa kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni na kisha yeye aviwasilishe kwa katibu wa Bunge ili aviwasilishe Baraza la Mitihani kwa uhakiki na akionekana kusita basi nakala hizo KUB aziwasilishe NECTA yeye mwenyewe.
Au hilo likiwa gumu basi kila mbunge kwa wakati awasilishe nakala ya cheti chake NECTA kwa uhakiki na kila mbunge anaehakikiwa amuombe spika kutangaza kuwa mbunge fulani vyeti vyake vimehakikiwa na Baraza la Mitihani.
Spika,Naibu Spika au Wenyeviti wa Bunge wanaweza kutumia kipindi cha muda wa matangazo ya Bunge kutangaza majina ya wabunge waliohakiki vyeti vyao.
Naomba ieleweke hapa lengo ni kuthibitisha uhalali wa vyeti walivyovitaja katika CV zao au walivyowasilisha ofisi ya Bunge kama kuna huo utaratibu wa wabunge kuwasilisha vyeti vyao baada ya kuingia Bungeni na kama haupo basi utaratibu huo uanze licha ya kuwa hata darasa la saba anaweza kuwa mbunge kwa mujibu wa katiba yetu.
Ieleweke kuna tofauti ya kuthibitisha uhalali wa cheti na kutangaza matokeo yaliyoko katika cheti.
Hili likifanyika litaondoa manung'uniko kuwa nyie wanasiasa zoezi hili haliwahusu na kwamba nyinyi ni raia wa daraja lingine tofauti na watanzania wenzenu na pia mtajiweka karibu na wananchi wenu.
Mkitfanya hivi hata mawaziri na vigogo wengine wa serikali wataona aibu na kufanya hili zoezi liwe la kila mtu.
Mnaweza pia kuweka utaratibu wa kuhakiki na vyeti vyenu vya taaluma.
Wapinzani ili kushika dola mnapaswa kuwa wabunifu ikiwa ni pamojan na kufanya mambo ambayo CCM yanawashinda na hasa yale mambo ambayo wananchi wanayataka na si kukosoa serikali tu bali mnapaswa kuangalia na mambo mengine yatakayowajengea imani kwa wananchi na ambayo mnaweza mkayafanya hata kama hamko madarakani.