Uhakiki wa vyeti TPA ulikua na lengo gani?

Kabalimu

Member
Jun 20, 2017
18
45
TPA nikatí ya tahasisi za mwanzo kuendesha zoezi la uhakíki wa vyeti mpaka mwezi wa 9/2016 wafanyakazi zaidi ya 500 walikwisha bainika kua navyeti feki lakini mpaka sasa wapo kazini
 

pecial

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
632
500
nikupe namba ya mkuu umwambie pengne mashushushu hawajamtonya hilo
 

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,598
2,000
Lengo la uhakiki ulilijua ndugu?
Ngoja nikueleze lengo la uhakiki angalau;
Uhakiki ule ulikuwa na malengo makuu mawili.
1.Kukwepa matumizi.
Kama ilivyo ada Tanzania au duniani hujiwekea utaratibu wa kisheria kuhusu kuboresha maslahi ya watumishi wake na hili huambatana na kuoanisha hali ya maisha na thamani ya fedha/shilingi katika muda maalumu. Hivyo Tanzania kisheria ilipaswa kuwapandisha vyeo na madaraja watumishi wake na bila kusahau kuwaongezea mshahara n.k.
Vitu hivi vyote vinapozingatiwa lazima pesa ihusike. Kwa kukwepa matumizi hayo serikali yako sikivu ikaanzisha zoezi hili linaloendelea kila kukicha.
2. Kupunguza wafanyakazi.
Pointi hii ni sambamba na ile ya awali ila utofauti ni mdogo tu. Ili wasipunguze kwa njia ya kawaida kama vile kutoa redundancy ambapo serikali ingelazimika kuwalipa wahanga fedha nyingi wakaamua kutafuta njia. Katika sekta ambayo taifa tunajivujia na tunaitegemea ni bandarini. Hivyo kama wangeondolewa wafanyakazi zaidi ya 400 TPA kwa mkupuo basi serikali ingepoteza mapato sana na shughuli nyingi za bandarini zingelala. Hivyo suala la kuondoa hawa wamiliki wa vyeti feki serikali waligusa sehemu ambazo impacts zake si za wazi sana. Kama vyeti feki walitimuliwa kwa ujambazi wa elimu je,ukiwa sectors fulani hauhesabiwi kuwa u jambazi wa elimu?
 

Super Sub Steve

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
15,983
2,000
Uhakiki wa vyeti ulikuwa una Lego la kuwapa dili maafisa wa NECTA.
Vyombo vya Usalama vikijipenyeza pale NECTA hasa wale wanaohakiki wataona uozo mwingi.Zoezi la uhakiki limekuwa mtaji kwa watu aiseeee,Kuna harufu ya Rushwa Necta

Sent using Jamii Forums mobile app
 

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
3,465
2,000
Nami nilikuwa mhakiki pale nashukuru nmalizia kibanda changu sasa muda si mrefu ntaitwa baba mwenye nyumba na kila mwez navuta mpunga kutoka kwa mafeki wangu!jaman maisha oyeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom