Uhakiki wa TIN Number, nimepoteza baadhi ya nyaraka, nifanyeje?

Kremme

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
471
495
Habari wana forum,

Nataka nikaanze kuhakiki TIN number kwa ajili ya driving license yangu. Ila nimepoteza ile karatasi yenye TIN number wakati napewa license 2014 na nakaribia kui renew license hapo february 2017.

Naombeni utaratibu nawezaje kuijua /kuipata ile TIN number kabla sijaenda kuhakiki? Na napoenda kuhakiki natakiwa nibebe vielelezo gani?

Natanguliza shukrani na heri ya mwaka mpya.
 
Kama una gari, kwenye kadi utaiona. Sasa kama ni leseni tu, nenda pale halafu taja majina matatu kama yalivyo kwenye leseni yako ya udereva, wao watasachi kimtandao, yatakuja majina mengi yanayofanana na ya kwako, lakini la kwako halisi litaonekana
 
Ally Hussein Juma
 
Utaratibu wa kujua TIN namba yako tembelea ofisi za TRA then utawapa majina yako matatu uliyoyatumia kipindi unachukua TIN.. lakin kama ni mmiliki wa gari tin ipo kwenye kadi yako..
Taratibu ya kufanya kuhakiki tin 1.kwa mwenye TIN ya biashara atatakiwa kufika ofisi ya TRA ambayo analipia kodi eg. Temeke au ilala au tegeta lakin kuna vituo maalumu kwa ajili ya uhakiki
2. Kwa mwenye TIN ambayo sio ya biashara anaweza kutembelea ofisi yoyote ya TRA ndani ya DSM. Zoezi la uhakiki deadline yake ni tarehe 31 january 2017. Fanya hima ndugu kahakiki.
 
Back
Top Bottom