Uhakiki wa tabia za Paul Kagame,JPM na Museven na mustakabali wa JUAMA

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,030
3,908
Swali langu la leo ni kutaka kujua iwapo kuna mfanano wa kitabia kati ya viongozi hawa watatu.

Na Je ufanano wao unaweza kuwa na madhara gani kwa mustakabali wa Jumuia ya Afrika Mashariki-JUAMA

Binafsi nawaona kama despots ambao wanaweza kuwa na mipango ya tofauti sana tofauti na matarajio ya raia wa JUAMA

Tuwajadili
 
Despots? Subutu uwaambie usoni ndo ujue KATIBA ZA NCHI HIZI zinatoa madaraka gani kwao. On the other hand, katiba hizo hizo zimefanikisha kupatikana kwa PRESIDENTS tofauti kabisa na hawa ambao matokeo ya UONGOZI wao ni faraja ya kipekee kwa watu wao. Nikumbushie tu utawala wa awamu ya nne, tatu na mbili kwa Tanzania. Yupo yule aliehamishia IKULU MAREKANI kwa mfano tu. Stinks!
PK, M7 na JPM wanayo nia ya kweli kubadilisha nchi hizi kutoka JALALANI. Wewe unaetumia vijimaneno kama 'despots' umezaliwa kijiji gani? Hauoni kwamba priorities sio vijiambo vya kipuuzi bali ni kuhakikisha UTAJIRI wa nchi hizi unaleta maendeleo kwa watu wake baala ya KUWACHOTEA wazungu na makuwadi wao? You should be ashamed!
 
Kama PK na m7 wangekuwa wana nia ya kuwaletea maendeleo ya kweli wananchi wao sidhani kama bado wangekuwa madarakani
 
Despots? Subutu uwaambie usoni ndo ujue KATIBA ZA NCHI HIZI zinatoa madaraka gani kwao. On the other hand, katiba hizo hizo zimefanikisha kupatikana kwa PRESIDENTS tofauti kabisa na hawa ambao matokeo ya UONGOZI wao ni faraja ya kipekee kwa watu wao. Nikumbushie tu utawala wa awamu ya nne, tatu na mbili kwa Tanzania. Yupo yule aliehamishia IKULU MAREKANI kwa mfano tu. Stinks!
PK, M7 na JPM wanayo nia ya kweli kubadilisha nchi hizi kutoka JALALANI. Wewe unaetumia vijimaneno kama 'despots' umezaliwa kijiji gani? Hauoni kwamba priorities sio vijiambo vya kipuuzi bali ni kuhakikisha UTAJIRI wa nchi hizi unaleta maendeleo kwa watu wake baala ya KUWACHOTEA wazungu na makuwadi wao? You should be ashamed!
Ni kweli awamu zote kuanzia ya kwanza zimekuwa na matatizo tofauti tofauti. Zingine mbaya kwa sababu za ubinafsi wa viongozi waliosimamia awamu hizo. Na hii ya sasa nayo ina matatizo makubwa, na hawapendi wananchi wayajadili.

Tungependa kupata kiongozi mzuri pengine kama huyu, lakini akawa democrat. Unapoibana mahakama na kisha bunge likawa rubber stamp la kupitisha mawazo yako tu. Haisaidii kukufanya ufanikiwe ktk uongozi wako . Na hata hiyo nia njema yako ya kuhakikisha rasilimali za nchi zinainufaisha nchi, huenda inakuwa kazi bure mfano ni Colonel Gadhafi wa Libya. Alikuwa mzalendo halisi kwa nchi yake lakini hakutaka kusikia wa Libya wanafikiri nini juu ya mustakbali wa uongozi wa nchi yao. Mwishowe amemaliza vibaya na nchi ikamvunjikia.

Tuwasikilize na wenzetu wanasemaJe
 
Mambo yao waachie wenyewe...

Angalia tabia yako kwanza kama ni mbaya jirekebishe... kama ni nzuri keep it up...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom