Watanzania wanajua nini kilitokea baada ya ripoti ya uhakiki wa vyeti vya taaluma yani kidato cha nne na sita kutolewa ikiwa ni baada ya kusitisha ajira mpya, nyongeza ya mishahara, kupandishwa vyeo na utekelezaji wa miundo mipya ya utumishi.
Kwa sasa taasisi nyingi za serikali kama TANESCO, VETA, TBS na nyinginezo pamoja na serikali kuu zimetangaza ajira mpya. Hii ina maana ni ruksa baada ya zoezi la uhakiki wa vyeti kukamilika. Wapo watanzania wengi waliopoteza ajira kihalali kabisa kutokana na sakata hili lakini kuna malalamiko ya chini chini kwamba hili zoezi halijawagusa watumishi wote.
Imethibitika kwamba wakaguzi kutoka NECTA hawakupita katika taasisi zote za serikali. Ushahidi ni ile ripoti ya mwisho inayoonesha status ya uhakiki wa vyeti katika taasisi za umma ambapo baadhi ya taasisi au vituo havionekani kabisa vikitajwa na watumishi wake hawasomeki kabisa.
Huko ambako NECTA hawakupita bado kuna watumishi wenye vyeti feki na wanaendelea kula mshahara na posho mbalimbali kama kawaida na kuzidi kubana nafasi za watanzania wengine wenye sifa halali za kushika nafasi hizo. Mapungufu kama haya NECTA iyatazame na kuyafanyia kazi ili haki itendeke kwa watanzania wote.
Ikiwezekana kila mkuu wa taasisi ya umma awajibike ipasavyo pale itakapogundulika ana watumishi ambao hawana vyeti halali na bado anaendelea kuwalipa mishahara na stahiki nyingine. Pia mtumishi anayejijua kafoji cheti au hana kabisa na bado yupo kazini akikamatwa apelekwe mahakamani n kusomewa mashtaka kwa mujibu wa sheria.
Nawasilisha