Tetesi: Uhakiki uliofanywa na NECTA haukugusa taasisi zote za umma

mzamivu

Member
Nov 23, 2012
17
45
Watanzania wanajua nini kilitokea baada ya ripoti ya uhakiki wa vyeti vya taaluma yani kidato cha nne na sita kutolewa ikiwa ni baada ya kusitisha ajira mpya, nyongeza ya mishahara, kupandishwa vyeo na utekelezaji wa miundo mipya ya utumishi.

Kwa sasa taasisi nyingi za serikali kama TANESCO, VETA, TBS na nyinginezo pamoja na serikali kuu zimetangaza ajira mpya. Hii ina maana ni ruksa baada ya zoezi la uhakiki wa vyeti kukamilika. Wapo watanzania wengi waliopoteza ajira kihalali kabisa kutokana na sakata hili lakini kuna malalamiko ya chini chini kwamba hili zoezi halijawagusa watumishi wote.

Imethibitika kwamba wakaguzi kutoka NECTA hawakupita katika taasisi zote za serikali. Ushahidi ni ile ripoti ya mwisho inayoonesha status ya uhakiki wa vyeti katika taasisi za umma ambapo baadhi ya taasisi au vituo havionekani kabisa vikitajwa na watumishi wake hawasomeki kabisa.

Huko ambako NECTA hawakupita bado kuna watumishi wenye vyeti feki na wanaendelea kula mshahara na posho mbalimbali kama kawaida na kuzidi kubana nafasi za watanzania wengine wenye sifa halali za kushika nafasi hizo. Mapungufu kama haya NECTA iyatazame na kuyafanyia kazi ili haki itendeke kwa watanzania wote.

Ikiwezekana kila mkuu wa taasisi ya umma awajibike ipasavyo pale itakapogundulika ana watumishi ambao hawana vyeti halali na bado anaendelea kuwalipa mishahara na stahiki nyingine. Pia mtumishi anayejijua kafoji cheti au hana kabisa na bado yupo kazini akikamatwa apelekwe mahakamani n kusomewa mashtaka kwa mujibu wa sheria.

Nawasilisha
 
Jabman

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
1,012
2,000
Tulikagua majeshi yote hakuna aliyefoji.
Wakuu Wa mikoa na Wilaya halikuwahusu
Bungeni tuliogopa wangekomaa na serikali maana wengi ni vihiyo.

Labda unikumbushe nilikosahau has a TISS. Huku usihoji tutakukuta mabwepande.
Walimu na manesi pamoja na watendaji Wa Kata na vijiji hawana madhara ndoo tuliokomaa nao.
 
VETA bado wako wengi sana. Vyuo vilivyotembelewa na NECTA havizidi 7 kama sikosei, na vipo zaidi ya 25 Tanzania nzima. Kuna kanda 8 pia na ofisi za makao makuu ambazo zote watumishi wake hawajaonekana kwenye ripoti inayoonesha status ya ukaguzi wa vyeti vya taaluma kwa taasisi za umma. Wahanga waliomo humo tunawafahamu na bado wanapeta wakati ndugu zetu wamesharudi vijijini kulima
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
25,706

Mkuu ni jukumu la HR husika kupeleka majina kuhakikiwa kuna muda utafika kama haujahakikiwa mshahara unafungiwa au HR husika atachukuliwa hatua
 
ki2c

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
2,649
2,000
Uhakiki uliopita haukua makini,kuna baadhi ya watu wameachwa hadi wenzao ambao waliingia nao kwakutumia vyeti feki nakuondolewa,wameshangaa wenzao wamebaki kwa vigezo vipi.. sasa haieleweki kama maafisa utumishi nao wanakula pesa au laa.. mimi nakumbuka nilikua napigiwa simu na walimu pamoja na manesi wengi wakiuliza niangalie majina,naangalia nayakuta ya baadhi yao tu sio wote.
 
Hili zoezi limefanyika kwa mapungufu mengi sana. Hofu kwa wafanyakazi ambao hawajahakikiwa ni mishahara yao kuja kuzuiwa siku za usoni ambapo itawapa usumbufu wale wasio na hatia
 
mzamivu

Member
Nov 23, 2012
17
45
Mkuu ni jukumu la HR husika kupeleka majina kuhakikiwa kuna muda utafika kama haujahakikiwa mshahara unafungiwa au HR husika atachukuliwa hatua
Ni kweli ma HR wengi hawajui kazi zao na ndiyo hapo itakuja kuwacost
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom