Uhakiki ama mikiki mikiki?

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Nov 7, 2012
1,976
3,122
Wadau,

Kuna mambo yanaudhi, yanakera, yanatia uchungu na yanahuzunisha sana hasa yanapoathiri ustawi wa maisha yako na familia yako au jamii yako na kuona kwamba binadamu wenzetu tuliowapa dhamana ya kutuongoza ndo wamekuwa kama Mungu juu ya leo ama kesho yetu hivi kosa letu nini?

Kuwapa dhamana (hapa tuamini wote tuliwapa) mambo kama uhamisho, madaraja, incriment na ajira tunahangaika navyo karibu mwaka bila kujali ya kuwa tunawaumiza wengine linaweza kuwa ni jambo zuri lakini ni kwa muda gani hakuna ajuaye huku likileta maumivu (ilikuwa liwe kwa wiki mbili, ikawa miezi miwili sasa hivi ni infinitive).

Kama zoezi hili hadi leo litaendelea bila kuwa na njia ya kuruhusu mambo tajwa pia kuendelea basi tuna tatizo mahala (probably we can't think beyond the limit ), kumbuka teuzi hazija simama hizo ni ajira.

Je tutaendelea kukosa wauguzi, madaktari, walimu nk. kwenye zahanati na hospitali zetu na kwenye shule zetu hadi uhakiki usiojulikana mwisho lini uishe?

Je hatuna time frame work ya jambo hilo hata miaka mitano twende tu inawezekana tukasema uhakiki umeokoa billions of shillings lakini je athari zake kwa wagonjwa hospitalini, wanafunzi shuleni kwa kukosa madaktari, wauguzi au walimu (hata wa sayansi tumeshindwa kuweka mfumo wa kuwaajiri huku tukiendelea na uhakiki wa waliopo na wale wa arts wakisubiri zoezi liishe?), na uhamisho je nini athari zake kwa wanandoa?

Let's think beyond the limit malipo ya kiongozi kwa mpiga kura wake ni furaha inayoletwa na ustawi wa maisha yake na jamii yake na TUCTA kimya. TUCTA imekuwa TUTA la kuzuia maendeleo ya mfanyakazi.

Ni hayo tu maumivu ni makali ngoja nipate pain killer mke wangu na binti yangu nawaona mara mbili kwa mwaka na binti punde ataniita mjomba maana hakai nami atanijuaje na uhamisho hakuna hadi watakapo amua wenye nchi.
 
Unamwambia nani sasa waho wana kula wana lala vizuri kama kusikia wangesikia muda tu
 
eti uhakiki mpya unaanza tena Oct 3.safari hii tumepata viongozi waongo,waongo,mpk hasira.
 
Back
Top Bottom