Uhai wa Jerry Muro hatarini

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MAISHA ya mtangazaji wa Shirika la Habari la Taifa kupitia Kituo cha Runinga cha TBC1, Jerry Muro, yanadaiwa kuwa hatarini kufuatia vitisho vya mauaji anavyopokea kwa njia mbalimbali ikiwemo ujumbe wa simu kutoka kwa watu wasiojulikana, Uwazi linathubutu kuanika.

Uchunguzi wa Uwazi kupitia rafiki yake wa karibu ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini umebaini kwamba, Jerry amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa hata kabla na baada ya kukamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani. Kwa mujibu wa rafiki huyo wa karibu, tangu Jerry aanze kufanya habari za uchunguzi juu ya ulaji rushwa wa askari polisi wa usalama barabarani na mafisadi, amekuwa akipokea simu na ujumbe mfupi kupitia simu yake ya kiganjani vinavyomtaka kuachana na habari hizo.

Taarifa ambazo ziko katika hifadhi ya Uwazi zinadai kwamba, licha ya vitisho hivyo, mtangazaji huyo aliwahi kuibiwa komputa yake ya mkononi 'laptop' na vielelezo vingine vya kazi ndani ya gari lake lililovamiwa na kuvunjwa mlango na watu wasiojulikana.

Ilibainika kwamba, Jerry alikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam, lakini hakufanikiwa kuvipata vitu hivyo.

Uchunguzi huo uliendelea kumimina kuwa, mtangazaji huyo aliwahi kushambuliwa na watu wasiojulikana mwishoni mwa mwaka jana.

Katika kuunga matukio, ilibainika pia kwamba, kitendo cha kutemewa mate na mzungu aliyekuwa ‘sekretari' wa Balozi wa Canada nchini akiwa kazini ni moja ya matukio yaliyozidisha hofu kwa kuwa linahesabiwa kama sehemu ya vitisho hivyo.

Katika kutafuta ukweli wa mambo hayo yote, uwazi lilifanikiwa kuzama ndani ya Kituo cha Polisi Kati na kubaini kuwepo kwa taarifa mbili zilizoripotiwa kituoni hapo na Jerry zenye kusomeka CD/RB/15133/2009 SHAMBULIO na CD/IR/4817/2009 SHAMBULIO.

Hata hivyo, uchunguzi zaidi uliofanywa na Uwazi ndani ya Kituo cha Polisi cha Oysterbay umebaini kwamba, Jerry aliwahi kufungua jalada la kesi namba 0B/RB/18555/2009 WIZI WA LAP TOP.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Uwazi liliwasiliana na Jerry kwa njia ya simu ili kueleza kile anachokijua juu ya vitisho vya mauaji na madai ya kupotelewa na vitu hivyo ambapo alikiri kukumbwa na mikasa hiyo.

Alisema: "Ni kweli, nimekuwa nikikumbana na matukio hayo mara kwa mara, Nahisi vitisho hivyo vinatokana na habari za uchunguzi ninazofanya, lakini kila nilipokumbwa na matukio hayo nilikuwa natoa taarifa polisi."
 
paragraph ya kwanza tu nimeishatosheka, kumbe chanzo chenyewe ulichotumia ni uwazi?????????????///////..................aaah, hayo magazeti ya akina hadija kopa bwana...............
 
Katika kuunga matukio, ilibainika pia kwamba, kitendo cha kutemewa mate na mzungu aliyekuwa ‘sekretari' wa Balozi wa Canada nchini akiwa kazini ni moja ya matukio yaliyozidisha hofu kwa kuwa linahesabiwa kama sehemu ya vitisho hivyo.

Mm! HAPANA. SI KWELI, NAKATAA.
 
Watu ambao huwa wanatuma death threats hawakusudii kuua. Wangekua wanakusudia kuna haja gani ya kumtishia?

Mtu yeyote anaweza kuamua kumtumia ujumbe wa simu, hata wafanyakazi wenzake kwa mfano. Hata mimi nikitaka!
 
Habari alizokuwa anatoa ni nzuri kwa wananchi pia ni za hatari sana, hivyo vitisho vya mauaji mara nyingi watu wengi wanapata hizo message. mlimsikia Slaa anasema kuhusu hizo message, Samuel (spika) naye ameshawahi kusema mpaka akaomba ulinzi lakini hayo mambo hayatokei. Hawa huwa ni marafiki ndio wanaotuma hizo message, maana unaambiwa, rafiki yako ndiye adui yako.
 
paragraph ya kwanza tu nimeishatosheka, kumbe chanzo chenyewe ulichotumia ni uwazi?????????????///////..................aaah, hayo magazeti ya akina hadija kopa bwana...............
Mku unakosea, magazeti ya uwazi yanatafiti sana kabla hayajaitoa hadithi kuu ya gazeti, sio maudaku kila ukurasa. Utakosa mambo mengine ya msingi sana kupitia huko.
 
Mku unakosea, magazeti ya uwazi yanatafiti sana kabla hayajaitoa hadithi kuu ya gazeti, sio maudaku kila ukurasa. Utakosa mambo mengine ya msingi sana kupitia huko.

haya magazeti pia najaribu kufikilia yatakuwa yanaandika habari za kweli nyingi tu lakini kwa kuwa yamekaa kimbea mbeya ndo maana tunashindwa kuyaamini
 
wamenyang'anya bastola yake, nasikia ilikua na uwezo mzuri sana kupiga na kushambulia, eti wanasema hata ndani ya maji inapiga......muulize RPC kanda maalumu DSM.

Hakuna watoto wa primary humu wa kusimulia hizi hadithi!

After all Jerry sio Tanzania; tuna issue muhimu kuliko yeye!

Kila le heri na udaku wenu!
 
Mku unakosea, magazeti ya uwazi yanatafiti sana kabla hayajaitoa hadithi kuu ya gazeti, sio maudaku kila ukurasa. Utakosa mambo mengine ya msingi sana kupitia huko.

So still hii ni HEKAYA na gazeti husika lina udaku walau ukurasa mmoja! Ambao ndio huu umeletwa kwetu!
 
Back
Top Bottom