Uhafifu wa vifaa ya ujenzi, nini faida ya kuwa na WAKALA wa vipimo na TBS hapa Tanzania?

Baba Heri

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
1,171
2,000
Unanunua nondo unaambia ina ukubwa wa inch 16 lakini ukipima hata kwa macho unaona kabisa umepigwa, flat bar ya 3 mm² ni nyembamba kama wembe, ukija kwenye aina zote za chuma ukipima hazifikii ukubwa unaoambiwa, bati ndo usiseme siku hz bati ya 32 gauge inakaribia kuwa laini kama foil wakati kuna nyumba za miaka ya 90 zimepauliwa na bati za 32 gauge hadi leo zipo vizuri, misumari hali kadhalika ni dhaifu vibaya sana. Halafu pia bati unanunua haimalizi mwaka imepauka haitamaniki.

Cha kusikitisha zaidi vifaa vya ujenzi jinsi vinavyopanda bei kila siku ndio vinazidi kuwa hafifu. Gypsum boards au ceiling boards siku hizi zipo kama maboksi. Mbao unanunua unaambiwa ni 3x2" lakini ukipima unakuta ni 2x2" iliyochangamka.

Cement kg 50 zamani ilikuwa kg 50 kweli lakini kwa sasa ule mfuko hata kg 40 sidhani.
Ukirudi kwenye ujazo na ubora wa haya marangi tunayoambiwa sijui silk au weather guard ndo usipime. Nyumba za miaka 40 iliyopita hadi leo zipo na rangi za mafuta hazijafubaa ni kuosha tu lakini hizi za sasa zikimaliza miezi 8 tu zinajikataa.

Najua kuna hoja kwamba watu wanapigwa wanauziwa vitu FEKI lakini je ni jukumu la nani kudhibiti ubora na usahihi wa vipimo? Maana si kila anayeenda kununua material ni muelewa au mzoefu, na ukimuamini fundi akununulie material anakupiga "kipeuo cha pili".

Nasikitika sana ofisi za wakala wa vipimo zipo mikoani, TBS wapo, wataalamu wapo wanalipwa, viongozi wapo lakini UBAYA unatamalaki tu.
 
Hazchem plate

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
10,553
2,000
Kuna TBS na NBS pamoja na FCC hawa jamaa wanatakiwa wafanye kazi sana ya kulinda walaji.

TBS wamehikita kucertify wanaongia kwenye market baada ya hapo ni wazito sana kucheck kama wana conform standards agreed.

Taasisi nyingi za umma zimejikita kukusanya mapato kukuko hata kufanya kazi zao .
 
wajingawatu

JF-Expert Member
Jan 20, 2013
1,416
2,000
Nunua bidhaa zako kutoka kwenye wazalishaji wa kuaminika kama vile ALAF!
Haisaidii kwa sababu, ALAF hana uwezo wa kuzalisha mabati ya kutosheleza mahitaji yetu wote. Suluhisho ni tbs, fcc, CCC na wengineo kujivalia njuga swala la bidhaa feki, kuhakikisha bidhaa hizo zinaharibiwa na wahusika wanashitakiwa au kifilisiwa
 
DocJayGroup

JF-Expert Member
Jan 17, 2020
1,079
2,000
Unanunua nondo unaambia ina ukubwa wa inch 16 lakini ukipima hata kwa macho unaona kabisa umepigwa, flat bar ya 3 mm² ni nyembamba kama wembe, ukija kwenye aina zote za chuma ukipima hazifikii ukubwa unaoambiwa, bati ndo usiseme siku hz bati ya 32 gauge inakaribia kuwa laini kama foil wakati kuna nyumba za miaka ya 90 zimepauliwa na bati za 32 gauge hadi leo zipo vizuri, misumari hali kadhalika ni dhaifu vibaya sana. Halafu pia bati unanunua haimalizi mwaka imepauka haitamaniki.

Cha kusikitisha zaidi vifaa vya ujenzi jinsi vinavyopanda bei kila siku ndio vinazidi kuwa hafifu. Gypsum boards au ceiling boards siku hizi zipo kama maboksi. Mbao unanunua unaambiwa ni 3x2" lakini ukipima unakuta ni 2x2" iliyochangamka.

Cement kg 50 zamani ilikuwa kg 50 kweli lakini kwa sasa ule mfuko hata kg 40 sidhani.
Ukirudi kwenye ujazo na ubora wa haya marangi tunayoambiwa sijui silk au weather guard ndo usipime. Nyumba za miaka 40 iliyopita hadi leo zipo na rangi za mafuta hazijafubaa ni kuosha tu lakini hizi za sasa zikimaliza miezi 8 tu zinajikataa.

Najua kuna hoja kwamba watu wanapigwa wanauziwa vitu FEKI lakini je ni jukumu la nani kudhibiti ubora na usahihi wa vipimo? Maana si kila anayeenda kununua material ni muelewa au mzoefu, na ukimuamini fundi akununulie material anakupiga "kipeuo cha pili".

Nasikitika sana ofisi za wakala wa vipimo zipo mikoani, TBS wapo, wataalamu wapo wanalipwa, viongozi wapo lakini UBAYA unatamalaki tu.
Nilinunua tiles za milioni 5. Na kuziweka mifuko ya cement 100 na kitu. Ni za GoodOne. Ukipiga deki.. maji yanazama hadi ndani. Quality ovyo sana sijawahi ona. Niliwalalamikia ila haikufika popote. Cement ya 42.5 ndio ya 32.5 quality. Misumari.. bati nazo aluminium inafuja. Nafikiri wanachakachua ili kupata faida sababu wanapigwa sana na serikali. Kweli hali Tz ni mbaya sana all around.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom