Uhaba wa viongozi

Wiston Mogha

Senior Member
Feb 13, 2014
149
96
Pamoja na kwamba viongozi wanaweza kuzaliwa na wengine kutengenezwa bado tuna upungufu mkubwa sana wa viongozi kwenye jamii zetu. Hii inasababishwa na kwamba jamii haitengenezi viongozi na hata viongozi waliofanikiwa katika uongozi wamekuwa wanafki na wenye roho mbaya katika kutenengeneza viongozi wa mfano wao. Hivyo viongozi pekee wanaopatikana ni wale waliozaliwa na sifa za uongozi au wachache waliotengenezwa na mifumo mibovu inayopelekea kupata viongozi mizigo.

Mfumo wa maisha wa jamii nyingi hautengenezi viongozi. Watoto wanakuzwa bila ya kujengewa misingi ambayo inawasaidia kuweza kufanya maamuzi kama viongozi. Jamii nyingi zinalea watoto kwa kuwaepusha wasikutane na changamoto ambazo zinawafanya wafikiri zaidi. Kwa njia hii jamii sio tu kwamba haitengenezi viongozi bali inaua sifa za uongozi kwa baadhi ya watoto waliozaliwa nazo. Kwenye jamii kuna watu wengi sana ambao hawana sifa za uongozi, kwa kuwa watoto wanaiga tabia za wanaowazunguka ni rahisi sana kwao kufanana na wanajamii ambao hawana sifa za uongozi.

Kitu kingine kikubwa kinachoua uongozi ni mfumo wa elimu. Mfumo wa elimu hasa kwa nchi yetu Tanzania haujakaa kutengeneza viongozi. Kwanzia darasa la kwanza mpaka elimu ya chuo mtoto anafundishwa kukazania vitu vichache ili kufaulu masomo. Hapewi nafasi ya kufikiri tofauti na kuibua na kupambana na changamoto. Pia mfumo wa elimu unajenga watu kuwa na UBINAFSI na kufikiria maisha yao tu badala ya kufikiri na ya wale wanaomzunguka. Kwa njia hii mfumo wa elimu unashindwa kutengeneza viongozi na inaua sifa za uongozi kwa baadhi ya wenye nazo.
 
Mkuu, kwa mfano hii ilikuwa ni mwaka 2015. Uliongea hoja ya msingi sana. Hoja hii ilikuwa ni moja ya malengo ya awali ya ACT kabla haijabadilika na kuwa chama cha 'yale yale'. Kwa mfano tu, ulitakiwa ujiulize kwa nini hoja nzuri kama hii ilikosa kuungwa mkono hata na hao ACT wenyewe?

Ndipo utakubaliana nami kwamba tatizo liko ndani ya vichwa vya watu bila kujali ni chama gani. Kwa hiyo hata ukihama utakutana na watu walewale wenye tabia zile zile maana watu ni hawa hawa. Sisi wengine mpaka kufikia conclusion hii tumefanya experiments za kutosha.

Kwa hiyo kama hatutaamua kubadilika kuwa watu watofauti na kisha kubadilisha wengine hata kama ni mmoja mmoja (japo ni kazi ngumu), hakuna cha maana kitakachotokea na kutarajia kitokee cha maana ni kuamua kutofikiri.
 
Back
Top Bottom