Uhaba wa magari kwa magereza nchini inaleta ulazima wa kuwekeza kwenye teknolojia

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
669
Nimesoma ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kuhusu magereza yetu nchini ambayo mbali na kuwepo na matatizo mengi. Ametaja shida ya kutokuwepo kwa magari kwa ajili ya kuwasafirisha wafungwa na mahabusu kutoka magereza hadi mahakamani. Ripoti imeonesha magaereza zina uhaba wa magari kwa 57% hali inayoleta shida kwa wafungwa na mahabusu wenye uhitaji wa kusafiri kusikiliza kesi zao. na magari yaliyopo yapo katika hali mbaya.

Mbali na hitaji kubwa la kusafiri mahakama ilianzisha suala la kuweka masuala ya kusikiliza kesi mtandaoni na hapa ndipo kunapohitajika magereza kuwa na mtandao na vifaa vya tehama kwa ajili ya kuendesha kesi mtandaoni wakati serikali ikisubiri muda wa kununua magari kwa ajili ya kusafirisha wafungwa.

Wakati magari yanaweza kuwa na gharama kubwa ambayo inaweza leta shida kuipata kwa muda mfupi, uwezekano wa kununua Routers na laptop unaweza kugharimu padogo na wafungwa wakawa wanaweza kuhudhuria kesi kwa mitandao ikiwemo google, meet, microsoft team, zoom, skype nk.

Teknolojia

Signed
OEDIPUS
 
Kesi zihamishiwe jela mahakimu wawe wanazunguka. Unakuta mkoa au wilaya Ina gereza moja kwanini mahakimu na waendesha mashtaka wao wasiende jela kuwafata wafungwa kuliko wafungwa kuwafata wao.
Kwani hakimu kwa siku anakuwa na kesi za waliopo magerezani peke yake? Vipi waliopo nje kwa dhamana?
 
Na mashahidi nao waende gerezani kutoa ushahidi wao ama?
Usafiri ni shida kwa mahabusu na wafungwa walioko jela. Mashahidi hawategemei usafiri wa magereza. Wanaweza kufika mahakamani kama kawaida na mfungwa akabaki magereza wakaendelea na kesi
 
Back
Top Bottom