Uhaba wa mafuta waitikisa Saudi arabia watu wanapanga poleni

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Uhaba wa mafuta washtadi Saudia, raia wapanga foleni ndefu kwenye vituo vya kuuzia mafuta
Sep 20, 2019 16:00 UTC
Kupungua mafuta katika vituo vya kuuzia nishati hiyo, kulikotokana na shambulizi la hivi karibuni la harakati ya wananchi ya Answarullah ya Yemen kwenye taasisi za mafuta za Shirika la Mafuta la Taifa nchini Saudi Arabia (ARAMCO), kumewafanya raia wa nchi hiyo kupanga foleni ndefu kwa masaa kadhaa kwenye vituo vya kuuzia mafuta.
Gazeti la Al-Quds Al-Arabi limeandika leo kuwa, mbali na upungufu huo wa nishati ya mafuta kuukumba mji wa Riyadh, mji mkuu wa Saudia, umeshuhudiwa pia katika miji mingi ya nchi hiyo na kwamba, huduma za usambazaji mafuta katika maeneo mengi zimesimama kikamilifu. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, taasisi ya kukusanya maoni ya Kimarekani ya 'Standard & Poor's' ili Saudia iweze kujidhaminia tena mafuta ya kutosha, inahitaji kwa uchache muda wa mwezi mmoja kwa kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mapipa milioni tatu zaidi kwa siku. Itakumbukwa kuwa, jeshi la Yemen kwa kushirikiana na kamati za wananchi za nchi hiyo na katika kujibu hujuma na mashambulizi ya Saudia na pia mzingiro wa kila upande wa muungano vamizi dhidi ya taifa hilo masikini (Yemen), lilivishambulia vituo vya kusafishia mafuta vya Buqayq na Khurais vya Saudia siku ya Jumamosi iliyopita.
Kutokana na shambulizi hilo, shughuli za uzalishaji mafuta za Riyadh zilisimama kwa muda, na hivyo kupelekea bei ya mafuta katika soko la dunia kupanda bei sambamba na kuporomoka kwa soko la hisa nchini humo kwa zaidi ya asilimia 2. Hii ni katika hali ambayo Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen, Muhammad Ali al-Houthi amesema kuwa, nchi hiyo iliyoharibiwa vibaya na vita inakabiliana na nchi "zenye nguvu kubwa zaidi kijeshi na tajiri zaidi" duniani katika vita vilivyoanzishwa na Saudi Arabia.
 
Ivi ayo makombora yao wasije wakapiga mji mtakatifu, au ni mbali sana
 
Back
Top Bottom