Uhaba, utaratibu mbovu na umbali wa miundombinu ya kumwaga taka chanzo cha uchafuzi wa mazingira jijini Dar es Salaam

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,547
Salaam Wakuu,

Kumekuwa na kampeni mbalimbali za kuhimiza ufanyaji usafi katika Jiji la Dar es Salaam. Viongozi hasa Wakuu wa Mikoa akiwamo Makalla na Mstaafu Makonda wamejaribu kuanzisha kampeni kwa kuwatumia watu maarufu na kushirikisha Media mbalimbali kuhimiza watu na kuweka siku maalum za kufanya usafi.

Pamoja na jitihada hizi lakini bado hali ya usafi jijini Dar ni mbaya, Mitaa mingi ya katika jiji la hili inakubwa na lundo la uchafu na takataka za aina mbalimbali. Jambo linalosababisha harufu nzito katika mitaa mingi Soma: Hivi hii harufu ya baadhi ya mitaa ya jijini Dar naisikia peke yangu tu?.

Nimejaribu kufanya uchunguzi binafsi hasa kwa kuangalia baadhi ya mitaa nikabaini kuwa mitaa hiyo haina maeneo maalumu (Madampo) ya kumwaga takataka hasa zile zinazotoka majumbani.

Sambamba na hilo, mitaa ambayo kuna utaratibu wa kupita magari ya kukusanya taka imekuwa na changamoto ya ratiba ya upitaji wa magari hayo hivyo hupelekea takataka kujaa majumbani na watu wanakosa pa kuhifadhi.

Changamoto za kukosekana kwa miundombinu ya takataka na utaratibu mbovu wa kukusanya taka majumbani imesababisha kuzaliwa kwa tabia mbaya ya watu wa mitaa husika kusubiri giza na kumwaga takataka hizo vichochoroni, kwenye mitalo au vichaka na sehemu zingine zisizofaa. Taza,a picha na video hizi kwenye baadhi ya mitaa niliyopita.

1653997925709.png

Picha: Hapa sio dampo ni sehemu ya wazi ambayo mtu kaamua kuacha taka


Video inaonesha kichaka ambacho watu wanatupa taka mida ya giza

Ushauri wangu
Ili kupunguza shida hii nashauri Mamlaka na wanaohusika na hili waanze kwa kujenga madampo walau matatu kila mtaa ili kupunguza umwagaji holela wa taka mitaani.

Vipi hali ikoje huko mtaani kwenu? Kuna eneo maalumu la kumwaga taka?
 
Elimu ya mazingira, kistaaribika kwa watu na kuamua kwa maksudi kwa wakazi wa dar kutochafua mji wao.

Bila hayo wakuu wa mikoa hata wakiwekwa saba kwa mpigo haitasaidia.
 
Elimu ya mazingira, kistaaribika kwa watu na kuamua kwa maksudi kwa wakazi wa dar kutochafua mji wao
Bila hayo wakuu wa mikoa hata wakiwekwa saba kwa mpigo haitasaidia
Point pia ndugu lakini pia madampo yakiwepo itapunguza kiasi
 
Hata ukiweka dust bin wanatupa chini
Elimu
Elimu
Elimu
Bila elimu hata hzo dust bin wanaiba.
 
Back
Top Bottom