Uhaba ujasusi wa kiuchumi na mkwamo wa sekta binafsi

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,985
20,263
UHABA UJASUSI WA KIUCHUMI NA MKWAMO WA SEKTA BINAFSI.

Na Yericko Nyerere

Wakati nafikiria na kuamua kuandika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, nilikuwa nimejiridhisha vya kutosha juu ya uwezo mdogo wa taifa letu na watu wake katika medani ya ujasusi wa KIUCHUMI, na hivyo nikakusudia kuleta msukumo mpya juu ya uwanda huu ili kuokoa taifa na watu wake kufuatia ushindani mkubwa uliopo leo duniani na hata mtani wetu wa jadi Kenya.

Nimekuwa nikiona michakato mingi ya kiuchumi nchini namna inavyokwenda na namna inavyofeli, nakiri bado tunasafari ndefu sana kama taifa ikiwa tunahitaji kufika pale tunapopaota bila kupatendea kazi ipasavyo. Hii ni hatua ndefu, na Leo nimeona nilizungumze kidogo uchumi katika sekta ya anga ambako tumeingia kwa nguvu kubwa, Nitaangaza mapungufu au ukosefu wa ujasusi thabiti katika eneo kuna athali kubwa na athali zake zinalihusu taifa kwakujua au kwakutokujua.

Sheria na Sera za usafiri wa anga Tanzania nafikiri bado ni zilezile zilizoanzishwa na Marehemu Magufuli, Kama ni zilezile basi tukubaliane bado kuna tatizo kubwa sekta hii kufikia malengo. Binafsi naitazama sekta hii kama sekta binafsi ya kiuchumi na si sekta ya biashara ya serikali. Kama tunakubaliana sheria na sera za sekta ya anga ni zilezile, basi..

Nitatumia mfano hai toka kwa mwekezaji wa ndani, Mwaka 2018 katikati ya utawala wa kiimla niliona Rafiki yangu Laurence Masha ambae ni Waziri wa zamani wa Mashauri ya Ndani ameamua kuingia katika biashara ya anga kwakununua hisa za Kampuni ya FastJet Tanzania, hili nilifurahi na nikaona sasa uwekezaji wa ndani unaingia kwa nguvu.

Binafsi niliamini amefanya upembuzi yakinifu juu ya biashara hii kwakusoma vema sera na sheria zake, na kijasusi niliamini anazo taarifa za kutosha kabla hajaingiza pesa yake katika biashara hii. Nilikuja kugundua alikuwa na taarifa chache na potofu yaani misinformations. Hili ni hatari, bahati mbaya vyombo vya ujasusi wa kiuchumi vilivyotakiwa kumpa taarifa sahihi ama havijui ama vimemhujumu, na hili ni kwakuwa (hatuna sheria/mfumo wa kiusalama kiuchumi unaoruhusu investors wageni na wazawa hasa wazawa waliokwenye kundi la "assets" kupewa taarifa za kiuchumi watakazohitaji).

Ukifika katika jiji la Tel Aviv ukataka kuwekeza, cha kwanza kabisa timu ya Mossad ujasusi wa kiuchumi chini ya Waziri wa Mashauri ya kibiashara itakupatia taarifa nyeti za kiuwekezaji, hii ni kwa mzawa na mgeni. Iko mifumo imara ya kuongoza hili. Mfanyabishara katika nchi zinazojitambua ni asset ya nchi. Ni lulu ya taifa, sijui kama watu wanafahamu ni kwanini Mwalimu Nyerere aliwapokea na kuwalinda akina Tramaton na yule waziri wa Somali, kwenye idara ya usalama enzi ikiitwa Tawi Maalumu kulikuwa na mfumo wakutambua kitu kinaitwa assets, na assets hizo zililindwa kwa nguvu..

Ikiwa sera ya anga iko vilevile ilivyokuwa kwa Magufuli, na ukataka kuwekeza katika eneo hilo, namba nianze kwakufafanua mambo machache unayotakiwa kutambua unapoamua kuingia kwenye biashara ya anga Tanzania, na hapa nitaeleza gharama za moja kwa moja unazowajibika wewe mwenye ndege kuzikabili mbele ya mamlaka, ambapo nawe kimsingi utashusha kwa mlaji ambae ni abiria. (direct cost anazokutana nazo abiria apandae ndege)

International passenger
Airport Tax (TRA) 40$, Zaman ilikua 30$.
Security charges (TAA) 5$, Zamani Free.
Safety fee (TCAA) 9$, Zamani 8$
Jumla 54$ x 2350=126,900tzs. Zamani 38$ tu.

Local passenger sasa analipa
AT 10,000/=
SF. 3,000/=
SC 2$.

Hii nikodi ya moja kwamoja ambayo hata kwenye tiket imeandikwa. Hii hajumuishi gharama kama

Navigation charges (TCAA)
Landing & Parking. (TAA)
Mafuta

Huu ndo mzigo anaobebeshwa Abiria, gharama zote hizo kampuni ya ndege inatakiwa kuzikata kwa abiria kabla ya faida yake. Fastjet sio wa kwanza kushindwa soko la aviation Tz, Kwa mwaka 2018 wakati sheria na sera zinaanzishwa kama silaha ya kufufua shirika la ndege Tanzania, Kampuni binafsi zilizotangulia kushindwa kufanya kazi zao Tanzia ni Moshi Aviation, Etihad, British Airways, Air seashells, na Kenya Airways KIA. Nafikiri baadhi wamejaribu kurudi.

Sababu kubwa ya Fastjet PLC kuondoka tz ni sera mpya za anga Tanzania na mizengwe ama tuseme vita vya kibiashara kushindwa. Masha aliponunua Fastjet PLC ya Tanzania alikuta ndege moja ambayo kimsingi uendeshaji wake ni gharama kubwa, hata matengenezo yake kwa aina ya ndege ile yalifanyikia SA jambo lililoongeza gharama.

Moja ya plan za Masha ilikuwa kuongeza njia kwakununua ruti za Kigoma, Mtwara na Bukoba, Soko hili wangeliweza kwa kuleta ndege ndogo aina ya ATR tatu ambazo nazo alikumbana na mizengwe ya mamlaka za nchi juu ya mchakato wa kibali, Mvutano au zengwe alilopigwa Bwana Masha ilikuwa ni mamlaka Tanzania zilimtaka alete mpango biashara ambao ni moja ya masharti ya kukidhi vigezo vya kupata kibali, akakwama hali iliyotafsiliwa wamemnyima kibali.

Aina hii ya ndege za ATR ni rahisi kuzihudumia kwakuwa matengenezo yake wangeweza kufanyia katika karakana za Pression na kuondoa gharama za kupeleka nje ya nchi. Lakini je, Masha mwanasiasa katika kati ya siasa chafu angeweza kuingia kwenye ushindani na ATCL iliyokuwa inafufuliwa na mamlaka ileile iliyomnyima vibali? Jibu liko kwa Masha.

Baada ya makodi kuwa makubwa na baadhi ya mashirika ya ndege kufunga biashara zao Tanzania, Shirika la ndege la ETihad waliomba kukutana na serekali angalau kujadiliana namna ya kukabili sheria hizo mpya za kodi, wakapewa appointment, walipokuja nchini serikali ikawalamba chenga za visigino, Wakafunga biashara zao rasmi October, 2018. Hakuna maelezo rasmi kama walirejea tena.

Ikumbukwe Etihad ni kampuni kubwa sana yenye mtaji mkubwa, ilishindwa kufanya biashara Tanzania, je Kampuni hizi ndogo bila kusaidiwa zitafikia mafanikio?

Nilazima tubadili mfumo, sera na muundo wa Idara ya Usalama wa Taifa ihami uchumi zaidi kuliko ilivyo sasa, Watu kama Masha na wengine ni wajibu wa TISS kumsaidia kuwa mwekezaji nchini, Sera za anga na sheria zake zitazamwe upya zisiwe kikwazo kwa sekta binafsi kufikia malengo. Kadili nchi inavyokuwa na matajiri binafsi, ndivyo nchi inavyokuwa na uchumi imara. Tuna wajibu wa kumsaidia Masha kuliko kumfilisi.

Ninasisitiza Someni Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi,

 
Back
Top Bottom