Ugunduzi wa Erasto Mpemba, (Maji ya moto kuganda haraka kuliko ya baridi) 'The Mpemba Effect' kwanini hatukufundishwa mashuleni?

Ndiyo Tanzania hii ndugu zangu; mpemba amepuuzwa kwa sababu ni mtu mweusi! Dr. Louis aliposema binadamu wa kwanza aliishi tanzania na ana asili ya sokwe, wote tuliamini na bado anaandikwa kwenye vitabu vyetu vya historia....Adui wa mtu mweusi ni mtu mweusi mwenzake; mzungu anafanya finishing tu
 
.
Screenshot_20190225-084944.jpeg

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Shuleni wanafundisha sema ni kitu ambacho sio significant sana so wengi hamuwezi shika kitu kama hiki mkakikumbuka.

Physicists wangapi duniani unaweza kuwataja? Wengi wataishia kusema Einstein, Newton, waliogusagusa advance kidogo wataishia kutaja Planck, Hawking basi.

Kuna physicists waliogundua vitu vingi mno zaidi ya 5,000. Ila ukiambiwa taja utataja chini ya watano kwa sababu hao waligundua vitu ambavyo vilileta mabadiliko makubwa sana. So sioni ajabu Mpemba kutokujulikana, yeye anaungana na physicist wengine wengi tu, hakuna sababu ya rangi wala nini.
 
Unaijua MPEMBA THEORY?

Ni rahisi Sana kwa wanafunzi wa kitanzania wakakujibu iwapo utawauliza kuhusu Archimedes Principle, Pascal's law, Avogadro's Law, Newton's law au theory nyingine maarufu

Lakini iwapo utawauliza kuhusu mpemba theory kati ya wanafunzi laki moja wa kitanzania Hakuna hata mmoja anaeweza kukujibu

Basi ni hivi.........

Mpemba's theory ni theory iliyogunduliwa na mtanzania anayejulikana kama Erasto B. Mpemba mwaka 1963 akiwa kidato cha tatu katika shule ya secondary magamba iliyopo lushoto mkoani Tanga

Nadharia yake ina sema kwamba " MAJI YA MOTO NI RAHISI SANA KUGANDA KULIKO MAJI YA BARIDI"

nadharia hiyo imeendelezwa na wanasayansi wengine akiwemo Profesa Osborne wakasema kuwa unapo yarusha juu maji ya moto kwenye sehemu za baridi kali ni rahisi Sana kuganda na kuwa vibarafu kuliko ukirusha maji ya baridi

Tangu Mtanzania huyu kugundua kanuni hiyo iliyopewa jina la Mpemba effect, mpaka leo ni miaka 50 lakini hatambuliki kabisa na taasisi za kisayansi wala zile za kitaaluma kama vyuo hapa nchini. Jambo la kushangaza, Mpemba ni maarufu sana kwenye taasisi za kimataifa, wanayansi wamehangaisha vichwa kujua sababu ya maji ya moto kuganda haraka zaidi kuwa barafu kuliko yale ya baridi.

Mwaka 2013, The Royal Society of Chemistry, baada ya kuwatangazia wanafunzi wote wa sayansi duniani wanasoma shahada ya uzamili kuwa wafanye tafiti za kugundua sababu za suala hilo.

Kwanini, zaidi ya miaka 50 tangu mpemba atambulishe nadharia yake lakini Hakuna anayemjua Tanzania zaidi ya kujulikana kimataifa?

69904999_2456094277952899_7532292263930494976_n.jpeg
69818914_2456094311286229_6702352716594675712_n.jpeg
 
Hii kitu kuielezea ilishindikana but practically iliwezekana ila alipoulizwa how ikashindikana so na sisi tukameza hivo hivo kama ulivyouliza
Duuh !!! Kusema ukwel mimi mpaka leo bado sijapata majbu kuhusu hii kitu
 
Kwanini huyu Mpemba effect hatukumsoma kuanzia Topic ya Heat form 3 physics mpaka ADVANCED PHZ CHANDS Yoooooooooote mavitabu yoote hamna pahali ameandkwa Mpemba effect

Hapa tunapigwa
 
Kwanini Maji ya Moto yanawahi kuganda yakiwekwa kwenye Friji kuliko Maji yasiyokuwa ya moto ?View attachment 1752205View attachment 1752206

Kama sikosei ni physics ya form 1.

Maji baridi yanapowekwa kwenye friji au katika eneo lenye joto la chini yanapoa na kusinyaa (contraction) , baada ya kusinyaa (contraction) yaani kuwa madogo yanaanza tena kutanuka (Expansion) hii effect inaitwa ANOMALOUS BEHAVIOR . Baada ya expansion ndipo yanaganda.

Maji ya moto yanakuwa yamesha Expand kutokana na joto hivyo inapunguza process ya Contraction na expansion hivyo yanapoa huku yakielekea kuganda moja kwa moja.

Anomalous behavior ya maji ni ya kipekee na hakuna kumiminika kingine chochote chenye tabia kama hii. Vimiminika vingine vina contract na kuganda .
Ila maji yana contract->expand-> ndio kuganda.

Kutokana kwamba maji yana expand wakati wa kuganda, basi barafu itakuwa na eneo/ujazo mkubwa kuliko yale maji yenyewe na ndio maana ukigandisha maji kwenye chupa ya glass iliyofungwa tight itapasuka na pia ndio maana tonge la barafu linaelea kwenye maji kwa sababu lina density ndogo kuliko maji
 
Noted!!!
 
"Most thermodynamicists believe that each observation of the Mpemba effect can be explained with standard physical theory" hakuna theory mpya hapo.
 
Back
Top Bottom