Ugumu wa maisha; Mama anywesha wanae 5 sumu. Wawili wafariki dunia, watatu pamoja naye wanapatiwa matibabu

Watoto wawili wamefariki dunia baada ya mama yao mzazi, Veronica Gabriel (30), mkazi wa Kijiji cha Mwabagaru, Kata ya Buseresere, Wilaya ya Chato, mkoani Geita kuwanywesha sumu kisha na yeye kunywa kwa madai ya ugumu wa maisha.

Hata hivyo mama huyo amenusurika kifo licha ya kunywa sumu hiyo kwa madhumuni ya kujiua

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Desemba 2, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe inasema mama huyo mwenye watoto watano aliwanywesha watoto wote sumu ya kuua wadudu kwenye nyanya na wawili kati yao kufariki.

Watoto hao wanumri kati ya mwaka mmoja na miezi tisa na miaka 12.

Watoto waliofariki dunia kutokana na sumu hiyo ni mwenye umri wa miaka 12 na miaka miwili.

“Watoto wengine wamelazwa Kituo cha Afya, Bwanga pamoja na mama yao akiwa chini ya ulinzi wa Polisi,”amesema Mwaibambe

Mwananchi
View attachment 2031087
Mkuu Chachu Ombara umekua adimu sana humu jamvini
 
dah hatari sana, kanda ya ziwa na haya matokeo.

Tuliambiwa maisha bora kwa kila mtanzania.
Tukaambiwa pia tupo uchumi wa kati...

Kuna watu inabidi wafunguliwe kesi kutokana na hivi vifo..
 
Wakat anazaa hovyo hovyo hakujua kama maisha ni magumu.

Alisikiliza maneno ya pimbi yule kuwa wafyatue tu
 
Back
Top Bottom