Ugumu wa maisha; Mama anywesha wanae 5 sumu. Wawili wafariki dunia, watatu pamoja naye wanapatiwa matibabu

Jamii ya sasa imejaa ubinafsi, inajenga majumba makubwa kama mahekalu na makasri halafu mtu anaishi na familia yake ya watoto wawili, mke wake na kijakazi wao, hawataki ndugu wakaribie. Cha ajabu wakifa ndugu wanaanza kuhangaika na msiba wa mbinafsi. Huyo mama hakuwa na ndugu wa kumsaidia hata kumpa chakula? Maisha ya kijamaa yalikuwa ni maisha mazuri sana, hutakubali ndugu yako afe njaa wakati wewe unakula na kusaza. Jamii ya sasa hivi haisaidiani kila mtu hufa na msalaba wake, shame on us
 
Huyo mama aache ujinga, miaka 30 anakata tamaa nani alimwambia azae kama simbilisi.
Hii koment yako imenichekesha kwa hasira, kwenye hii taarifa ya kuudhunisha..
Wenyewe wa kanda hiyo wanaona fahari kuzaa sana bila ya kujali uwezo wao wa kutunza hao watoto ndio mana yule ndugu yao alikuwa anahimiza watu wazaane tu elimu bure na wenyewe wanashangilia na kuvutana ndani kutafuta watoto wa kuongeza.
 
Kuna wanaosema lakini hawasikilizwi, dunia ya leo hakuna mwenye habar na mwingine.
Huyo mama kufanya alichokifanya alipitia mengi mno ndo maana akaamua bora afe na watoto wake kuliko kuwaacha wakipata tabu duniani hapa.

So sad
Kweli kila binadamu ana kikomo chake cha uvumilivu
Ingawa yalikuwa ni maamuzi mabaya
Kweli dunia imekuwa mbaya ila wasamaria wema wapo pia
Hao watoto wasingekufa kwa njaa ila ndio hivyo tena
Ndio imekuwa mwisho wao huo
 
Dah...mtoto wa miaka 12 ambae ndio angekua na msaada wa kwenda kuuza walau maembe ndio kaondoka

Eeh Mungu naililia familia hii wakumbuke.
 
Jeshi la polisi mkoa wa Geita linamshikilia Veronica Gabriel (30) mkazi wa Kijiji Cha Mwabagaru kata ya Buseresere wilayani Chato mkoani Geita kwa kuwanywesha sumu ya panya watoto wake watano aliokuwa anaishi nao kwa madai ya kuwa ameshindwa kuwalea kutokana na ugumu wa maisha.

Akizungumza na Waashindi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita kamishina msaidizi ACP Henry Mwaibambe amesema mwanamke huyo baada ya kuwanywesha sumu wanae na yeye alikunywa sumu hiyo kwa dhumuni ya kujiua.

ACP Mwaibambe amesema Kati ya watoto hao watano wawili wamefariki dunia ambaye Jane Mgema mwenye umri wa miaka 12, janeth mkama miaka 2 huku wengine watatu wakiwa wamelazwa kituo cha afya Cha bwanga pamoja na mama yao (mtuhumiwa) akiwa chini ya ulinzi huku hali zao zikiendelea vizuri.
 
Pata picha mama watoto ana miaka 30 na watoto wa 5 juu yake wakimtegemea yeye kwenye kila kitu,hapo Mme kazamia machimboni bwanga au anakula starehe na jimama katoro mjini! Aice hapo usipo mshirikisha muumba kwenye shida zako unaweza jikuta unafanya uamzi mgumu had shetani akabaki anakushangaa.
 
Watu wa huku usukumani hasa geita ni watu flani hivi wanaojihisi wao ni superior kwa kila kitu...hata akiwa na dhiki hawezi kujishusha kuomba ili asaidiwe....mfano hapa ninapoishi kuna uhaba wa maji mtu yuko radhi aingie chooni bila maji aachie kimba na atoke bila kuflash wala kujisafisha anahisi akiomba msaada wa maji atakuwa amejishusha sana....MAMA KAUWA WANAE KWA U SUPERIORITY WA KIPUMBAVU ANGEOMBA MSAADA HATA KWENYE NYUMBA ZA IBADA ANGESAIDIWA TU.....
 
Watoto wawili wamefariki dunia baada ya mama yao mzazi, Veronica Gabriel (30), mkazi wa Kijiji cha Mwabagaru, Kata ya Buseresere, Wilaya ya Chato, mkoani Geita kuwanywesha sumu kisha na yeye kunywa kwa madai ya ugumu wa maisha.

Hata hivyo mama huyo amenusurika kifo licha ya kunywa sumu hiyo kwa madhumuni ya kujiua

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Desemba 2, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe inasema mama huyo mwenye watoto watano aliwanywesha watoto wote sumu ya kuua wadudu kwenye nyanya na wawili kati yao kufariki.

Watoto hao wanumri kati ya mwaka mmoja na miezi tisa na miaka 12.

Watoto waliofariki dunia kutokana na sumu hiyo ni mwenye umri wa miaka 12 na miaka miwili.

“Watoto wengine wamelazwa Kituo cha Afya, Bwanga pamoja na mama yao akiwa chini ya ulinzi wa Polisi,”amesema Mwaibambe

Mwananchi
Kesi kama hii ,kama mm ndyo jaji .naiweka kweny dustibini .
 
30 years with five kids no wonder Hadi amefanya maamuzi ya ajabu afungwe kizazi
Kanda ya ziwa hiyo ni kawaida tena huyo kafata uzazi wa mpango !!! Utakuta mwanamke wa 30 years ana watoto 8
 
Back
Top Bottom