Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,665
- 239,156
Miaka miwili iliyopita andiko hili " LEO TUKO HAPA , KIINGILIO 5000/- " lilikuwa andiko maarufu mno , hasa maeneo ya Kinondoni , Temeke kata ya 14 na Chang'ombe jijini D' Salaam.
Andiko hili liliashiria uwepo wa burudani ya muziki wa dansi kwenye eneo husika , ingeweza kuwepo AKUDO , SIKINDE , TWANGA PEPETA , MSONDO ama FM ACADEMIA , hii ni kwa uchache sana , lakini kulikuwa na TOT etc.
Leo hii muziki wa dance umekufa kifo cha mende kutokana na ukosefu wa pesa kwa wananchi , leo bendi za dansi zimekuwa zikiburudisha walevi wa bia na viroba kwa malipo ya tsh Elfu 60 !
Nilitoka machozi nilipomuona Chiriku Bitchuka akiimba Pale Bar ya Pentagon , Kurasini mbele ya walevi wasiolipa chochote , hivi kweli jamani haya ndiyo malipo ya wanamuzi hawa waliosifika ndani na nje ya nchi ?
Hakika maisha ya Wanamuziki wa dansi yamekuwa magumu kuliko binadamu yeyote katika nchi hii , nawahurumia sana !