Ugumu wa ajira mashirika ya Umma kwa wahitimu waliotoka internship

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,369
7,140
Kuna vijana wengi wahitimu wanaitwa usahili kwenye mashirika ya umma na halmashauri zetu kisha kuwekwa utumishi kwa mpango wa intenship.

Unakuta kijana anatumikishwa miaka hadi minne bado kupata ajira ya kudumu na ujira anapewa mdogo huku kazi amemudu na nafasi ipo.

Mambo haya ni unyonyaji wa nguvu kazi. Mashirika binafsi wanafanya sana kujipatia nguvu kazi kwa bei rahisi huku kijana anabakia na mategemeo ya kuajiriwa. Nachosema taasisi za umma zisifuate mkondo huu wa kunyonya nguvu kazi ya vijana.

Serikali yafaa kutoa maelekezo kuwapa ajira ya kudumu vijana waliyofanya intenship muda mrefu kwenye mashirika yake na halmashauri mbalimbali
 
Yaani mtu anajitolea halmashauri kwa wanyonge halafu anategemea apate ajira.
Halafu unashangaa mtu anatoka kupiga interview utumishi anakukuta hapo bado umebweteka
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom