Ugumi wa kupata "a" kwenye vyuo vyetu.

m_kishuri

JF-Expert Member
Jan 27, 2010
1,485
369
FROM:MATONDO  • Utakuta darasa lina wanafunzi 100, na kati ya wanafunzi hawa pengine wawili, watatu na hata mmoja tu ndiyo atapata "A". Hata madarasa makubwa yenye wanafunzi 300, eti wanafunzi wanne au watano tu ndiyo wanapata "A". Kwa nini? Ni kwa sababu masomo ni magumu sana? Wanafunzi hawajisomei sawasawa (Na kama hawajisomei ni kwa nini?), maprofesa hawafundishi vizuri kiasi kwamba wanafunzi hawawaelewi? Au maprofesa wanatunga mitihani migumu kupindukia? Au pengine wanafunzi wa vyuo vikuu vyetu ni mbumbumbu na hawana uwezo wa kupata A?
  • Ninacholalamikia hapa siyo kila mwanafunzi kupata A bali ule ugumu uliopo wa kupata alama hizi kwani siamini kama kweli eti katika darasa la wanafunzi 300, ni wanafunzi watatu au wanne tu ndiyo wana uwezo wa kufaulu vizuri. Kama hivi ni kweli basi ni wazi kuna tatizo kubwa katika mfumo wetu wa elimu.
4. Hali ilivyo hapa Marekani
  • Hapa kupata A ni jambo la kawaida na maprofesa na wanafunzi wanalijua hili. Mahusiano kati ya wanafunzi na maprofesa ni ya wazi na wanafunzi wanaweza kuuliza maswali na kujadili masuala ya gredi watakazozipata na maprofesa wao kwa uwazi. Hali hii inasababisha matatizo fulani na haya nitayaongelea siku nyingine.
  • Ati, kwa nini ni vigumu sana kupata A na hatimaye "first class" katika vyuo vikuu vyetu? Tatizo hasa ni nini? Ni mfumo wa elimu tuliorithi kutoka kwa Waingereza? Pengine inabidi tulifikirie jambo hili kwani inawezekana tukawa tunawahujumu wanafunzi wetu kwa kuwapotezea nafasi za ufadhili katika mashirika mbalimbali vikiwemo vyuo vikuu, jambo ambalo si jema hasa katika kipindi hiki ambapo kusema kweli mambo yako wazi sana kuhusu masuala ya ufadhili wa kimataifa.
Maoni ya msomaji:
Maprofesa wazee waliopitwa na wakati nao wanachangia. Pia umalaya kwa wanafunzi wa kike, uzembe, wivu na kutotakiana mema. Sababu ni nyingi. Mpaka imefikia hatua sasa msichana mzuri kama mimi ukipata A eti watu wanakuzushia kwamba umevua chupi kwa profesa. Tunahitaji kubadilika jamani, lakini hili ni tatizo kubwa sana na linavunja moyo kweli. Mtu unajisomea weeee halafu unaambulia B - hata kama mtihani ni take home.

#Wanajamii, nimelileta hili suala hapa jukwaani ili tusaidiane kimawazo kuhusu hili suala, kwani naamini kuna wanajamii wengi ambao wamepitia aidha Mlimani au SUA. J e ni vibaya kumpa mtu A+ au A kwa sababu Prof. ataonekana hajui kufundisha ? Binafsi sijuwi hii dhana wameitowa wapi.
 
Nanren

JF-Expert Member
May 11, 2009
2,040
1,277

Lakini, kabla ya kulinganisha vyuo vya TZ na vya huko USA na kupelekea kuwalaumu maprofessor wetu, labda tungejiuliza zaidi, matokeo ya wanafunzi shule za msingi, secondary vyuo vya diploma hapa TZ. Je kila mtu anapata A? Je ni vigumu kuipata hiyo A? Sijui.

Ninachofahamu mimi ni kuwa darasa lolote lile ambalo wanafunzi wemeingia bila upendeleo/mchujo maalum(kama wanavyochuja shule za seminari) huwa linatakiwa lifuate 'Normal distribution". Haiyamkiniki, eti darasa lote linakuwa na vipanga watupu na wote wanapata A kama mtihani ni standard au wa kiwango kinachofaa au darasa zima wawe vilaza/viazi wafeli wote. Mtihani ambao wengi wanapata A au wengi wanafeli ni substandard au upo juu zaidi ya kiwango. Darasa la kawaida lilkifanya mtihani ambao ni "objective" na ni wa standard inayofaa, kutakuwa na A chache. This applies to our universities too. Suala la kwamba Maprofessor wanatoa marks za chupi, ni uvumi tu ambao hauwezi kuthibitika. Na kama upo, ni kwa wachache. Kumbuka suala la Ngono lazima wote mridhie, vinginevyo ni ubakaji. Na je Maprofessor wanawake nao huwa wanataka Ngono kutoka kwa vijana? Sometimes Kwenye vyuo huwa kunakuwepo na fikra/tuhuma zinazoanzishwa na wanafunzi wenyewe lakini zinakuwa si za kweli, mfano ni pale msichana akipata A na labda ana mvuto fulani, na tena anawapiga chini vijana darasani kwake, halafu walimu wanaonekana kumtajataja darasani (kutokana na uelewa wake), vijana wanaanza kusema, huyo demu anapata marks za chupi. Lakini mvulana akiwa ndio anatajwa na anapata A, hakuna anayesema huyo kijana katoa/kapokea rushwa ya ngono!
 
m_kishuri

JF-Expert Member
Jan 27, 2010
1,485
369
Nanren, je na wale maprofessor wenye kusema hivi utawafafanua vipi;
"Hivi mimi nitafundishaje watu wote hawa, mmmh, natumai ikifika mwisho wa semister hii nitakuwaa nimebakiwa na robo ya darasa...na mwisho wa semister nyingine, sana sana nitakuwa na watu kumi tano katika somo langu. Sijawahi kubakia na watu zaidi ya hao."
 
Mimi nawachukulia kama wachimba mkwara tu. Kama mwanafunzi ni Kichwa, atafaulu tu huo mtihani hata kama Professor anatishia hivyo. Nimeishawahi kutishiwa kwenye darasa letu, lakini ikapelekea wanafunzi kusoma kwa nguvu sana na wengi tulifaulu mtihani wa aliyetutisha. Pia kumbuka kuna Maprofessor wengine hata hawatoi vitisho vyovyote, wanafundisha vizuri sana, wako very friendly, lakini bado unakuta wanafunzi wengi wanakamatwa kwenye masomo yao.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom