Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Wakuu pole kwa majukumu

Miaka Kama 8 nilianza kuisi mabadiliko tumboni, Basi nikawa nachukulia poa, tu maana ilkuwa inanitokea siku moja moja, nimependa hivyo mpaka nkaenda shule high level tumbo likawa linanisumbua

Yaani baada ya kunywa chai au chakula tumbo lilikuwa linanitesa, yaani kunawaka moto. Nikaenda hospital wakanipima minyoo wakanipa dawa .

Nilipofika chuo maumivu yakapungua sijui kwakua chuoni nilikuwa sili Sana maharage. Basi nimemaliza nachukulia poa

Mwezi wa tano niliisi maumivu makali ya tumbo upande wa kushoto, yaani tumbo lilikuwa linajaa gesi utadhani nimekula sahani 4 za ugali yaani nikila kidogo tumbo linakuwa limetuna Kama nimeshiba hatari .

Nilikuwa natoa mkojo una harufu mbaya, na choo kina harufu mbaya Sana, nikadhani nimeugua Figo.

Basi nilienda kupima wakachukua sample baada ya kupima nilikutwa na vidonda vya tumbo. Iyo ilikuwa tarehe 2/06/2020. kikawaida dozi ya vidonda vya tumbo Ni ya siku kumi, Ila chakushangaza doctor alisema nitumie iyo dawa kwa miezi mitatu.

Baada yakutumia dawa iyo ndani ya siku tano, yaani gesi yote imeisha, kuvimbiwa kukakata, maumivu makali ya tumbo yakakata, Ila Cha kushangaza toka tarehe 14/6 maumivu ya tumbo yamerudi tena jspo gesi Sina na sivimbiwi.

Wakuu kumeza madonge ya ulcers miezi mitatu imekaaje, na je dawa gani ya kienyeji naweza itumia tumbo likaacha kuuma?

Wakuu nipo hoi tumbo linauma utadhani ndani wembe unapitishwa ndani ya tumbo.

Msaada please
 
Kama kweli unaumwa miezi 3 si kitu, kuna anayetamani kupata ya kunywa mwaka ila Hakuna tiba, Acha masihara
 
Pole sana, acha kula vyakula vifuatavyo,

Maharage,chai ya rang, viazi vitamu, ndizi hasa za kuchemsha,pombe aina yeyote, soda, chipsi,pili pili,nk kidogoooo itakusaidia kupunguza tatizo la muamivu
 
Mimi niko kama wewe ila mpaka sasa napata shida moja asubuhii nikinywa chaii ya sukarii napata naumivu kwelii na usingizi juu.

Kama tumbo liko empty basi jua siwezi kula kitu cha ghafla cha baridi.

Tumbo kuja kawaida ila silii sana choo sasa ndo balaa
 
Pole sana, wewe unapatikana wapi? Kuna Dr yuko mbeya yuko vzuri sana. Waweza niona PM nikupatie namba uzungumze nae.
 
Back
Top Bottom