Ugonjwa wa Vichwa vikubwa na mgongo wazi kwa Watoto! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa wa Vichwa vikubwa na mgongo wazi kwa Watoto!

Discussion in 'JF Doctor' started by Kennedy, Mar 10, 2012.

 1. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,329
  Likes Received: 2,980
  Trophy Points: 280
  Heshima kwenu vyote wana JF. Naomba madokta na wote wenye kufahamu juu ya ugonjwa tajwa hapo juu,pia dalili zake. Maana nimeona kwenye tv ama kwahakika watoto wanateseka sana. Je ni ugonjwa unarithishwa au unakuwaje mpaka mtoto anakuwa nao,Mikoa hasa iliyotajwa kuwa na watoto wengi wanaosumbuliwa ni LINDI na MTWARA. Natanguliza shukrani tele kwa msaada wa michango yenu yenye kuleta manufaa.
   
 2. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Asante sana kwa swali lako. Ugonjwa wa mtoto kuzaliwa na nafasi kwenye uti wa mgongo unaitwa Spina Bifidaugonjwa huu hutokana na upungufu wa vitamin B9 (foliac acid). mama mjamzito hutakiwa kutumia vitamin B9 wakati wa ujauzito au wakati anpopanga kuwa mjamzito. vit hivi huzsaidia kukuwa kwa neva na ubongo mwilini.Dalili ya kawaida ya upungufu wa Vit B9, Vitc ni pamoja na kuharisha, anemia na udhaifu au kupumua kwa taabu, uharibifu wa neva (mishipa ya fahamu)na mwili kuwa una kufa ganzi matatizo ya mimba, kuchanganyikiwa akili, usahaulifu au kumbukumbu kuwa ndogo, majonzi ya akili (depression), au vidonda katika ulimi, midomo , maumivu ya kichwa, mapigo ya moyo kwenda haraka , kuwashwa, na matatizo ya kitabia. Kiwango cha chini cha Vit B9 na Vt C pia husababisha mkusanyiko homocysteine. DNA zisip okarabati huharibika na hii inaweza kusababisha maendeleo ya kansa.
  Vyakula vyenye vitamini hii ni mboga za majani ya kijani, mbazi, choroko nk.
   
 3. k

  kamili JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 714
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60

  Kichwa kikubwa kinaitwa Hydrocephalus, ni neno la kigiriki lenye maana ya maji ndani ya kichwa.(but sio kila mwenye kichwa kikubwa ana hydrocephalus) Kwa kawaida ndani kabisa ya ubongo kuna sehemu nne zenye uwazi, ambazo wataalamu huziita ventricles. Sehemu hizo huwa haziko wazi na hivyo kuwa na kiasi Fulani ya majimaji (Fluid). Majamaji hayo ambayo jina lake halisi ni Cerebral Spinal Fluid hutengenezwa kutoka kwenye damu na cells ambazo zipo kwenye kuta ya hizo ventrices. Majimaji hayo ambayo hutengenezwa ndani kabisa ya ubongo kwenye hizo ventricle hupitia sehemu maalum na hivyo kutoka nje ya ubongo na kuuzunguka ubongo na hivyo kufanya ubongo kama vile unaelea kwenye majimaji hayo. Kwa maana hiyo ndani kabisa ya ubongo kuna ventricles ambazo zina hayo maji na kwa nje ubongo umezungukwa na hayo maji. Ili kuhakikisha maji hayo hayazidi kichwani mwili unao mfumo kamili ambao unahakikisha kuna uwiano kati ya maji yanayotengenezwa na maji ya nayofonzwa na kurudishwa kwenye damu. Majimaji hayo yanafaida nyingi moja miongoni mwa hizo ni kuweka uwiano wa msukumo (balance intracranial pressure) na kuzuia mtikisiko wa ubongo, (Shock absorber)

  Yapo baadhi ya magonjwa ambayo hufanya majimaji hayo yatengezwe kwa wingi kuliko yanavyorudishwa mwilini au maji yanayotengenezwa ni ya kawaida lakini ufyozwaji haupo, na hivyo kuanza kujazana kichwani na kufanya kichwe kiwe kikubwa. Magojwa hayo mengi ni yale mtoto anayezaliwa nayo yaani congenital defect. Pia mtoto anaweza kuzaliwa bila ya shida hiyo lakini akaipata baadae kutokana na kupata magonwa yanayoshambulia zile sehemu zinazofyonza maji hayo. Magonwa hayo ni kama Meningitis, Toxoplasmosis, Cytolomegalovirus nk. Lakini pia kama mtoto atapata baadhi ya kansa ambazo zinashambulia ule utando unaozunguka ubongo (meninges) aweza apate shida hiyo.
  Tiba yake madaktari huweka mpira (tube) unaoitwa VP shunt set, kutoka kichwani na kuyapeleka maji hayo tumboni na hapo tumboni hufyonzwa na kurudishwa kwenye damu.
  Mgongo wazi unaitwa spina bifida, ni ugonjwa au hali ambayo mtoto anazaliwa nayo huku uti wa mgongo ( ule mshipa wa fahamu mkubwa unaotoka kwenye ubongo) ukiwa wazi, kutokana na mifupa ( vipingili vya uti wa mgongo) kutokufunga vizuri. Kwa kawaida mara tu baada ya mimba kutunga uti wa mgongo hutengenwa nusu upande mwingine na nusu upande mwingine. Na baada ya hapo nusu ya mkono wa kulia huunganiswa na nusu ya mkono wa kushoto kama vile mtu anayefunga zip ya nguo. Ni wakati wa muunganiko huo ndio kasoro inaweza itokee na hivyo sehumu Fulani ikawa haijaziba, kama vile ambayo zip ikiharibika inaweza iache katundu mahali. Sababu zinazofanya kasoro hiyo itokee ni kama kupigwa X ray mama mja mzito, matumizi ya dawa za kifafa, upungufu wa Folic acid, na maambukizi ya baadhi ya virus kwa mama mjamzito.
  Shida hii inaweza ikatokea peke yake au pamoja na hydrocephalus. Mara nyingi hutokea peke yake lakini baadae ile sehemu iliyowazi hupitisha mambukizi na kusababisha meningitis, ambayo hushambulia ule utando unaofyonza Cerebral Spina Fluid na hivyo kufanya maji yaanze kurundikana kwenye kichwa.
  Spina bifida huwapata watoto 3 kila watoto 10000 wanaozaliwa. Tiba yake ni upasuaji wa kuziba lile tundu. Na mama mja mzito aweza apunguze uwezekano wa kupata mtoto huyo kwa kumeza folic acid wakati wa mimba, kuepuka x ray, pamoja na kuepuka baadhi ya madawa ya kifafa kama anacho.
  Mama aliyewahi kuzaa mtoto mwenye spina bifida aweza azae tena. Sina hakika kama Mtwara na Lindi ndio zinazoongoza kwa sasa.
   
 4. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,329
  Likes Received: 2,980
  Trophy Points: 280
  Nashukuru sana JF Dokta.
   
 5. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,329
  Likes Received: 2,980
  Trophy Points: 280
  Asante.
   
Loading...