- Source #1
- View Source #1
Salaam Ndugu zangu,
Zipo tetesi zimesambaa katika maeneno mbalimbali kwamba ugonjwa wa Covid-19 umerejea nchi. Kwa sisi tunaoishi Dar tunashuhudia kulipuka kwa mafua makali yakiambatana na kikohozi fulani na homa.
Je kuna ukweli kiasi gani kwenye hili?
Jamiiforums tunaomba mtusaidie kuuliza kwa mamlaka ili tahadhari ichukuliwe mapema.
Zipo tetesi zimesambaa katika maeneno mbalimbali kwamba ugonjwa wa Covid-19 umerejea nchi. Kwa sisi tunaoishi Dar tunashuhudia kulipuka kwa mafua makali yakiambatana na kikohozi fulani na homa.
Je kuna ukweli kiasi gani kwenye hili?
Jamiiforums tunaomba mtusaidie kuuliza kwa mamlaka ili tahadhari ichukuliwe mapema.
- Tunachokijua
- Kutokana na kusambaa kwa tetesi ya kuibuka wa wimbi la Uviko-19 ambazo zimechochewa na kuwapo kwa sintofahamu ya Watu kuugua Homa za Mafua Makali, Kifua na Kichwa Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa ufafanuzi wa awali kuhusu madai hayo:
Wizara ya Afya imesema inachakata taarifa zilizokusanywa kutoka Hospitali na Vituo vya Afya ndani ya Wiki hii.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kati ya Wagonjwa 288 waliopimwa UVIKO-19 kati ya Mei 6-12, 2023, 6 walithibitishwa kuwa na Corona. Idadi hiyo ni pungufu ikilinganishwa na waliopima kati ya 29 Aprili hadi 5 Mei 2023 na hakuna kifo chochote.
Zaidi ya hayo, Ummy amewataka Wananchi kuondoa hofu kwa kuwa Wizara inaendelea kufuatilia kwa karibu kwenye Hospitali mbalimbali na itatoa taarifa rasmi kuhusu tetesi za Uviko-19.
Kutokana na ufafanuzi huo wa Wizara Jamiiforums itasubiri uchunguzi wa wizara na taarifa kutoka mamlaka husika ili kujua kama hali hii ya mafua, homa na kikohozi ni wimbi la Uviko-19.
Aidha, kutokana na Wizara kuthibitisha kwamba bado kuna wagonjwa wa Uviko-19 nchini japo kwa idadi ndogo ya watu Jamiiforums inashauri wanajamii tuendelee kuchukua tahadhari wakati wote.