UGONJWA WA UBINAFSI NA KUSHIBA MAWAZO KWA WATANZANIA

Jehanamu Hii

Member
Dec 16, 2016
41
31
UGONJWA WA UBINAFSI NA KUSHIBA MAWAZO KWA WATANZANIA

Kuna huu ugonjwa ambao watanzania wengi tunao. Kumbuka nimetumia 'tunao' siyo 'mnao'. Huu ugonjwa uko hivi:

1) Hatuna haja ya kujifunza jambo jipya kutoka kwa mwingine/ kwingine. Nikimaanisha wengi hatuna utayari wa kusikiliza mawazo ya watu au mambo mapya bila kujali yeye ni nani, rangi, ama utaifa wake. Yaani mtu akianza tu kuongea tunamkata kauli kwa kurejelea uzungu wake, elimu yake, jinsia yake, kama amekaa ughaibuni ama la n.k.

2) Tunaamini tu kile tulichonacho. Kwa mfano, wengi tunaamini kuwa sisi tu ndiyo tuna utamaduni, tuna heshima, tuna mandhari nzuri, na vitu vingine. Tunasahau kuwa watu wengine pia wana utamaduni wao. Kama vile, Wamarekani, Wachina, Watu wa Uingereza nakadhalika.

3)Tunaamini kwamba watu wa tamaduni zingine wanapaswa kuheshimu na labda kufuata tamaduni zetu, lakini si sisi kuheshimu (hatupaswi kuheshimu) na labda kufuata tamaduni zao.

4)Tunaaamini kuwa sisi ndiyo tunaweza kubaguliwa lakini sisi hatuwezi kuwabagua wengine. Kwa mfano, niko katika vita ya kupiga vita fimbo. Maoni ya watu katika posti zangu ni kama vile 'unaiga uzungu'. Wengi wanasema neno 'uzungu' halina ubaguzi ndani yake pindi litumiwapo na mswahili. Je katika mfano huo nilioutaja hapo juu, unaona kuna ujumbe wowote mzuri ndani yake? Yaani kujaribu kufikiria njia zingine za uadabishaji ni 'uzungu?' Vipi kama mzungu angesema 'Acha uafrika/utanzania' ungefurahishwa na sentensi hiyo? Huo ndiyo ubaguzi tusioufikiria.

5) Wengi tunasahau kuwa binadamu ni Wamoja. Na laiti
ingewezekana kufanya dunia hii kuwa wamoja zaidi ya ilivyo sasa. Katika nchi za Marekani wanajaribu kuelemisha watu kuheshimu tamaduni za watu wengine wa sehemu tofauti kulingana na kuwa sote ni binadamu. Katika nchi za Tanzania tunahimizwa kukumbatia utanzania na kudharau utamaduni wa watu wengine.

Kuna mambo mengi tunatakiwa kuyafikiria kwa akili ndogo tu ya kuzaliwa, mengi, mengi sana. Tena mambo madogomadogo. Tunatakiwa kukumbuka kuwa mkuki kwa kunguruwe pia ni mchungu. Si mchungu kwa binadamu tu. Tuache kuendeleza wazo kwamba 'Mkuki kwa nguruwe ni mtamu, nguruwe haumiagi bwana, binadamu tu ndiyo tu anaumia' Ninakuambia wazi kuwa nguruwe pia anapata maumivu kama yale unayoyapata binadamu. Ni vile tu hawezi kusema. Kuwa tayari kujifunza.
 
Back
Top Bottom