Ugonjwa wa Sukari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa wa Sukari

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Nov 8, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,228
  Likes Received: 4,019
  Trophy Points: 280
  [​IMG]  Watu walio na ugonjwa wa Sukari (kama watu wale wengine) lazima watilie mkazo afya yao ya kila siku.Tofauti imo: walio na ugonjwa wa Sukari, kila siku lazima wapime sukari, wafanye mazoezi na wazingatie afya yao. Ikiwa wewe au mtu unayemjua ana ugonjwa wa Sukari na ameamua kuishi maisha yenye afya, basi Sehemu ya Kujifundisha itakuongezea maarifa kuhusu huu ugonjwa na kukuelekeza kuishi ukiwa na afya.
  Hatua ya 1: Jifunze kuhusu ugonjwa wa Sukari
  Ni vizuri kujua mambo mengi kuhusu ugonjwa wa Sukari ili uweze kuukimu. Hapa ni yale unayotakikana kujua na kufanya.
  Jua ni aina gani ya ugonjwa wa sukari unayo na hatari zake


  Usiogope kuuliza maswali na kujua pale utakapopata majibu.

  Elewa kuhusu kiwango cha sukari damuni mwako na ni tiba ipi utakayo tumia.

  • Fanya mtihani mdogo kuhusu Insulini.
  • Insulini 101
  • Video: Insulini
  • Ugonjwa wa sukari: Kile unachohitaji.
  • Fungua uchapishe hati, inayokufundisha kufuatilia kiwango cha sukari damini yako.
  Fungua uchapishe mpango wa afya nzuri waliye na Ugonjwa wa Sukari.

   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,228
  Likes Received: 4,019
  Trophy Points: 280
  Uja Uzito Na Ugonjwa Wa Sukari

  Vidokezi kwa kina mama waja wazito
  Unapojiandaa kusheherekea furaha tele kwa kupata mtoto, ni muhimu ujue namna ya kukabiliana na ugojwa wa sukari. Hapa vidokezi vitano vya kuweka akilini kila mara:
  1. Husiana kwa karibu na kundi la maafisa wa afya bora ambao ni pamoja

  • Daktari au muhudumu wa kiafya aliye na ujuzi wa kutunza wagonjwa wa Sukari
  • Daktari aliye na maarifa ya uzalishaji anayeweza kushughuikia matatizo katika uja uzito na ambaye amewahi kushughulikia kina mama waja wazito walio na ugonjwa wa Sukari
  • Daktari wa watoto au wa watoto wachanga ambao wamezaliwa ambaye anajua kutibu shida maalum zinazoweza kuwakumba watoto wanaozaliwa na kina mama wanaougua ugonjwa wa Sukari
  • Muhudumu wa ulaji aliyesajiliwa anayeweza kukupangia na kukubadilishia chakula wakati wa uja uzito na baada ya kujifungu
  • Daktari wa ugonjwa wa sukari anayeweza kukusaidia kukabiliana na ugonjwa huu wakati wa uja uzito.
  2. Uwe maakini sana na madawa yako: Iwapo unatumia tembe za ugonjwa wa Sukari, inaweza kuwa vigumu kuendelea nazo wakati wa uja uzito. Daktari wako anaweza kukupa ushauri wa kujitibu kwa kujidunga dawa ya Insulin ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini badala ya kuendelea na hizo tembe.

  3. Kagua kiwango cha sukari katika damu yako: vile tu unavyoagizwa na daktari au muhudumu wako wa afya bora.

  4. Zingatia ushauri wa mjuzi wa lishe bora: fuata mwongozo wake wa aina za vyakula unavyostahili kuvitumia ili kiwango cha sukari mwilini mwako kithibitiwe.

  5. Mazoezi ni muhimu katika kutibu ugonjwa wa Sukari: Haijalishi iwapo wewe ni mja mzito au la. Zungumza na daktari wako akueleze iwapo kuna tatizo lolote linaloweza kutokea iwapo utafanya mazoezi ukiwa mja mzito. Ni muhimu kujua hasa kwa wale ambao wana ugonjwa wa Moyo pamoja na, au kiwango cha juu cha sukari mwilini.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,228
  Likes Received: 4,019
  Trophy Points: 280
  Niko hatarini kiasi cha kwamba naweza kupata ugonjwa wa Sukari?

  Wanasayansi wameshindwa hasa kutambua kinachosababisha ugonjwa wa Sukari mwilini. Pia hakuna hatari zilizo wazi za kuonekana kwa macho kwa aina ya kwanza (Diabetes 1). Lakini aina ya pili (Diabetes 2) ina dalili:
  Unene – Hii ni dalili ya kwanza hatari.Mtu akiwa mzito, ana nafasi kubwa ya mwili mwake kukataa aina ya dawa ya insulin kwa sababu mafuta huzuia namna mwili hutumia dawa yainsulin.

  Ulegevu na uzembe – Maisha ya mtu kukaa tu ndee si mazuri hasa iwapo mtu huyo ni mnene sana. Mazoezi hufanya moyo kupiga vizuri na kuzuia hali mbaya za kiafya mwilini. Mwili ambao una misuli tu ni rahisi kutumia vizuri Insulini kuliko ule ambao umejaa mafuta katika seli (cells). Hivyo basi, mtu anaweza kurahisisha utendaji kazi wa Insulini kwa kusonga hapa na pale. Pia mazoezi hurudisha chini kiwango cha sukari mwilini na hivyo basi kufanya Insulini kufanya kazi yake vizuri zaidi mwilini. Vile vile kupunguza uzito kitu kizuri. Hivyo basi wacha uzembe!

  Mazoea mabaya ya kula: Wagonjwa wengi ambao wamepatikana kuwa na aina ya pili ya ugonjwa wa Sukari pia ni wanene mno. Hawana mazoea mazuri ya ulaji. Chakula kikiwa na mafuta mengi na chakula kilichowekwa kemikali, kile hakina nyuzinyuzi za kutosha, chakula kilicho na kabohaidreti (wanga) nyepesi, vyote huchangia katika kumfanya mtu kupatikana na ugonjwa wa Sukari mwilini. Kula unavyostahiki kwa weza kuzuia aina ya pili ya ugonjwa wa Sukari au hata kuupindua.

  Historia ya familia: Wakati mwingine huwa katika jeni (genes) na unarithishwa katika familia. Watu ambao wana jamaa waliopatikana kuwa na aina ya pili ya ugonjwa wa Sukari wao wana nafasi kubwa sana kupata ugonjwa huu. Hali ya maisha ya mtu ndio hasa hufanya mtu apate au asipate ugonjwa wa Sukari.
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,228
  Likes Received: 4,019
  Trophy Points: 280
  Maswali ambayo yameulizwa sana kuhusu ugonjwa wa Sukari

  Ugonjwa wa Sukari ni nini?

  Ni ugonjwa ambao hufanya sukari iwe nyingi sana damuni. Walio na ugonjwa huu pia wanaweza kuwa na magonjwa mengine kama vile, ugonjwa wa moyo, figo, shida za macho, na hali zingine tata zinazolingana na hizi.

  Kuna tofauti gani kati ya aina ya kwanza na ya pili ya ugonjwa wa Sukari?

  Aina ya kwanza, sana sana hupatikana kwa watoto na vijana. Mwili hausawazishi kiwango cha sukari kabisa. Aina ya pili sana sana hupatikana kwa watu wazima. Mwili hujenga sukari lakini huwa haitoshi kulingana na kile kiwango kinachotakikana.

  Unapataje ugonjwa wa Sukari?

  Huwezi kuzuia aina ya pili ya ugonjwa huu. Husababishwa na mazeoa mabaya ya ulaji, kunenepa sana, na kukaa tu ndee bila kujishughulisha na shughuli zozote muhimu.

  Unawezaje kutibu ugonjwa wa Sukari?

  Aina ya kwanza hutibiwa kwa dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini (Insulin). Aina ya pili hutibiwa kwa kutumia dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini na tembe. Pia, mtu anastahili kufanya mazoezi, kuwa na ratiba nzuri ya ulaji na kupunguza unene.

  Je, dawa ya kusawazisha kiwango cha Sukari mwilini ni nini? (Insulin)

  Ni kemikali iliyoundwa katika kongosho (pancrease). Husaidia kusawazisha kiwango cha sukari mwilini.

  Hebu sema baadhi ya shida za kudumu za ugonjwa wa Sukari?

  Ugonjwa wa Sukari huweza kusababisha magonjwa mengine kama vile ugonjwa wa Moyo, Figo, Kupofuka, Kukatwa kwa viungo vya mwili, huharibu mishipa ya fahamu (neva) na magonjwa ya figo. Ni muhimu ujitunze kwa kutumia dawa zako inayostahili, usikae tu ndee bali ujishughulishe na mambo na ule ulaji unaofaa kwa afya nzuri.

  Ni hali gani hatari inayoweza kusabisha na kukuza ugonjw wa sukari?

  Sababu na hatari za aina ya kwanza ya ugonjwa wa Sukari bado hazitambulikani. Sababu muhimu kubwa ya aina ya pili ni unene kupita kiasi. Hatari zinginezo ni pamoja na uzee, kutofanya mazoezi, historia ya familia, kabila (sana sana watu wa asili ya Afrika, Waresia na wa asili ya Amerika ya Kilatino) na walio na msukumo wa juu wa damu mwilini na Choresterol

  Ni nini baadhi ya njia ambazo kwazo mtu akizifuata atajizuia kupata aina ya pili ya ugonjwa wa sukari?

  Zingatia uzani unaofaa kupitia kwa mazoezi na ratiba mwafaka ya ulaji mwema. Kula vyakula vya madini mwilini visivyo na mafuta mengi na sukari nyingi. Jishughulishe kila wakati kwa kufanya mazoezi: usikae tu ndee. Iwapo unaona kuwa uko hatarini na kuna uwezekano kuwa, unaweza kupata ugonjwa huu

  Je, kuna dawa ya kutibu ugonjwa huu?

  Kwa wakati huu haipo. Hata hivyo kuna dawa nyingi ina matibabu mengi unayoweza kutumia kwa mfano dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini. Matibabu pia huhusisha mtu kupunguza uzani (unene) wako na kuwa na shughuli nyingi pasipo kukaa tu ndee.
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,228
  Likes Received: 4,019
  Trophy Points: 280
  Njia tano za kufuata kama mwongozo wa kukabiliana na ugonjwa wa Sukari

  Mara tu unapoambiwa kuwa una huu ugonjwa, linaweza kuwa ni jambo ngumu kulikubali na kukabiliana nalo. Hisia za kushtuka, hasira, kutamauka, kuogopa na kuwa na majonzi ni za kawaida kwa yeyote baada ya kupata habari kuwa ana ugonjwa wa sukari. Hata hivyo una maisha yako ambayo ni muhimu uyaokoe. Fuata hizi njia tano, kwa uangalifu ili ujue la kufanya wakati wa kukabiiana na hiyo hali yako mpya ya kuwa mgonjwa wa ugonjwa wa sukari.

  Hatua ya 1: Jifunze yote yanayokupasa kuhusu ugonjwa huu.

  Jifunze na uelewe kila kitu ili ujue unachoshughulikia. Muulize daktari ambaye anajua yote kuhusu ugonjwa huu na aliye na uwezo wa kujibu maswali yako yote. Tambua aina ya ugonjwa wa sukari unaokusumbua. Ni hali gani inayokufanya ujipate hatarini?

  Jua vyema kiwango cha sukari kilichoko mwilini mwako na aina ya dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini mwako itakayokufaa maishani mwako. Ni shida gani zinazotarajiwa iwapo utashindwa kuuthibiti ugonjwa huu kwa kiwango kinachotakikana, kulingana na mhudumu wako wa kiafya. Utafiti wako umekusaidia kupata maarifa unayostahili. Kuweza kukabiliana na ugonjwa huu kikamilifu.

  Hatua ya 2: Badili mtindo wako wa ulaji

  Ili kuweza kukabiliana na kiwango cha sukari mwilini mwako ni muhumu upunguze uzani usiofa, kiasi cha chakula unachojipakulia ni lazima kipungue usifikirie kwa misingi ya utaratibu na ulaji bali njia bora ya kutunza afya yako kwa kula chakula kifaacho vyakula vifuatavyo, visikose kwenye orodha ya vyakula unavyohitaji katika taratibu wako wa ulaji; mboga, matunda, chakula cha kutunza mwili na cha kupatia nguvu mwili wako. Zungumza na daktari wako wa utarativu wa ulaji bora kuhusu mpangilio mwafaka wa mlo utakaouzingatia kwa wakati huu.

  Hatua ya 3: Panga mpangilio wa kila siku wa kudumu

  Watu wengi walio na ugonjwa huu mara nyingi huwa wanene kupita kiasi na wenye uzani mzito. Hivyo basi ni muhimu, ufanye mazoezi ya kila mara kama njia mojawapo ya kukabiliana na ugonjwa huu. Ni lazima kuwa daktari wako atakupa ushauri utakaoutaka upunguze uzito. Mazoezi mwafaka zaidi ni kuwa na mpangilio utakaokufanya uwe na nguvu za uthibiti wa moyo wako kwa kufanya mazoezi yanayolenga hayo mambo mawili. Baada ya ushauri wa daktari unaweza kuamua kujiunga na chumba au kiwanja cha michezo ya kuzoeza viungo vya mwili ama ujiunge na kundi la YMCA/YWCA ili upate msaada unaohitaji kuendelea kuyathibiti maisha yako na hali yako ya wakati huu. Kama sivyo, kuna namna nyingi za kujipangia mazoezi ya kibinafsi pale pale tu nyumbani.

  Hatua ya 4: Meza dawa zako inavyotakikana

  Watu wengine walio na aina ya pili ya ugonjwa huu huhitaji kumeza tembe zao inavyostahili ama kujidunga dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini ili miili yao itumie sukari iliyomo katika matunda na mimea kupata nguvu. Aina hii ya sukari huvunjwavunjwa tena wakati wa kuyeyusha chakula kinywani na tumboni ili kifae kuchukuliwa na damu mwilini kama ifanyikavyo na chakula cha namna kilichomo katika nyama, ute wa yai na samaki (chakula cha kutunza mwili) Dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini haipatikani kwa hali ya tembe. Yaliyo chini ya ngozi yako ili ingiie mara moja ndani ya damu yako.

  Hatua ya 5: Tafuta usaidizi (msaada)

  Huenda ikawa, utaweza kukabiliana na huu ugonjwa bila shida lakini ni muhimu utambue kuwa unahitaji msaada wa watu wengine ili mzigo ukuwie mwepesi kidogo. Tegemea jamaa na marafiki wakutegemewa ambao watakuwepo kila mara utakapohitaji msaada wao, katika hiyo hali yako mpya ya kisasa. Jishughulishe na vikundi vya watu walio na hali sawa na yako, pia jihusishe na shughuli za kijamii na kutafuta pesa na kuelimisha watu wanaoishi karibu nawe kuhusu ugonjwa huu.
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,228
  Likes Received: 4,019
  Trophy Points: 280
  DAWA YA UGONJWA WA KISUKARI

  Dawa ya Sukari ! Wabilahi Taufiq


  Dawa ya Sukari (Diabetes)

  Sheikh Saleh Mohammed Tuwaijiri (May Protection of Allah be on him),

  Qadhi Mkuu wa korti ya Tabuk kafanya uchunguzi mkubwa kwa kuvumilivu

  na kwa subira kubwa mpaka kupata hii dawa ya magonjwa ya sukari.


  Siku hizi watu wengi khususan watu wazima, wanaume na wanawake

  wanataabika sana kwajili ya ugonjwa wa sukari.  Ingredients
  :  1 – Unga wa ngano 100 gm


  2 – Gundi (umefanan na ubani wa kiarabu lakini hauna harufu) 100 gm


  3 - Shaair 100 gm


  4 - Habba Soda 100 gm  Namna ya kutengeneza  Chemsha hivyo vitu juu katika vikombe 5 vya maji kwa muda wa dakika

  10.
  Zima moto na wacha ipowe. Ikisha kupowa chuja na utie katika chupa.  Matumizi  Kunywa kikombe kidogo kila siku asubuhi kabla ya kula chochote kwa

  muda wa siku 7.
  Wiki ya pili kunywa siku moja na uwache siku moja.

  Insha-Allah baad hizi wiki mbili utapona na utaweza kula chakula kama

  dasturi.
  Sheikh anaomba muwapelekee wenzune wapate na wao

  kunufaika.
  Insha Allah Allah atajaalia iwe dawa kwa kila mwenye haya

  maradhi. Aameen.
  Kwa hisani zenu musiwasahau kwenye dua zenu Sheikh,

  alieye tarjum kwa Kiswahili na kila anaye ipeleka mbele.
   
 7. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #7
  Dec 2, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,482
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  [​IMG]
   
Loading...