Ugonjwa wa retina ya macho unaosababishwa na kisukari

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,430
2,000
jicho.jpg

Na Dk Shita Samwel, MwananchiKWA UFUPI
Jicho ni kiungo ambacho binadamu anapaswa kuwa makini kukilinda maana kuwapo kwake kunasaidia viungo kutenda kazi vyema.

Jana Tanzania iliungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha Siku ya Afya ya Macho duniani, safari hii ikiwa na kauli mbiu isemayo Upofu wa Macho Utokanao na Kisukari Unazuilikia, Nenda Kapime.

Labda tujiulize kwanini kisukari kimetupiwa macho katika kauli mbiu mwaka huu? Jibu ni rahisi; idadi ya wagonjwa wengi wakisukari nchini na duniani inazidi kuongezeka. Ugonjwa huu wa macho huwapata watu wenye kisukari cha muda mrefu.

Kuwapo kwa ugonjwa wa kisukari husababisha kuharibika kwa retina. Hii ni sehemu ya nyuma ya jicho ambayo inaundwa kwa utando wa neva ama mishipa ya fahamu. Mishipa hii ya fahamu ni muhimu sana katika kumuwezesha mtu kuona. Ndio inayopokea taswira ya vitu na kuipeleka katika ubongo kwa ajili ya tafsiri.

Kuathirika kwa neva hizi ni tatizo la hatari kwa uwezo wa jicho kuona kwani inaweza kusababisha kuwa na uwezo mdogo wa kutambua taswira ya vitu. Hali hii isipotibiwa mapema, husababisha ulemavu wa kudumu.

Kisukari ni ugonjwa unaoingilia uwezo wa mwili kutumia na kuhifadhi sukari mwilini. Hii husababisha madhara makubwa mwilini.

Sukari ndio nishati inayotegemewa na mwili katika kuendesha shughuli mbalimbali. Kwa kawaida sukari katika mwili inatakiwa iwe katika kipimo cha saba hadi 12 (7-12).

Uwapo wa sukari nyingi katika mzunguko wa damu husababisha madhara mbalimbali mwilini ikiwamo sehemu ya jicho ya nyuma iitwayo retina.

Kadri sukari inavyozidi na muda unavyosogea, mfumo wa mzunguko wa damu katika jicho huathirika. Ugonjwa hutokea pale sehemu ya retina inapokosa lishe kutoka kwenye vishipa vidogo vinavyoathirika kutokana na wingi wa sukari mwilini.

Hali hii ikiendelea husababisha mishipa kuvujisha damu na maji maji hivyo kuzifanya tishu za retina kuvimba na kuwapo na taswira yenye ukungu.

Tatizo hili huathiri macho yote mawili na kadri mtu anavyoendelea kuugua kisukari ndivyo anavyokua katika hatari ya kuathirika na ugonjwa huu zaidi.

Dalili za ugonjwa huu

Kuona ukungu au vidoadoa katika taswira unayotazama. Inawezekana pia akaona mawimbi wakati wa kutazama kitu, kushindwa kuona vizuri hasa nyakati za usiku, kuona giza au kidoa katikati ya taswira inayoonekana.Matibabu
Uchunguzi wa kina katika kliniki za macho hufanyika na tatizo hurekebishwa kwa upasuaji maalum ama kutumia mionzi ya laser na wakati mwingine kwa kutumia dawa za kusaidia kuongeza uwezo wa macho kuona.

Namna ya kuepuka tatizo

Kinachopaswa kufanyika ni mgonjwa kudhibiti wingi wa sukari mwilini kwa kula mlo bora wenye afya na usioongeza sukari mwilini.

Njia nyingine ni kupima mara kwa mara ili kuchunguza kiasi cha sukari mwilini. Vilevile ni muhimu kwa mgonjwa kufanya mazoezi mara kwa mara na kufuata maelekezo ya daktari.

Msukumo wa damu ya mgonjwa unapaswa kudhibitiwa ili kuepusha athari ya retina. Kudhibiti shinikizo la damu kunapunguza madhara zaidi ya kisukari.

Mgonjwa wa kisukari anapaswa kuchunguza macho kila mwaka hasa kwa kutumia wataalamu waliobobea ili kutambua kama macho yameanza kuathirika.chanzo.Ugonjwa wa retina ya macho unaosababishwa na kisukari - mwanzo - mwananchi.co.tz

 

kansinsi

Member
Sep 24, 2013
76
95
Je doctor nini nikitumia asali mbichi ninaweza kupona tatizo LA macho Kama jinsi ulivyo elezea samahani naomba ushauri
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom