Ugonjwa wa Pumu (Bronchial Asthma): Chanzo, dalili na tiba

Sawa asante sana kiongozi tunasubiri mrejesho
Mkuu sijapata jibu la uhakika sana zaidi nimeambiwa kwa mtoto ni rahisi kutibika kuliko kwa mtu mzima, ikitokea nikipata anaefahamu dawa ya uhakika nitaleta mrejesho ili kusaidia wahanga.
 
Sawa asante sana kiongozi tunasubiri mrejesho
Mkuu nimefanikiwa kupata moja ambayo ni baada ya kuuuliza sana, siwezi iweka hadharani maana binafsi sijaithibitisha japo mlengwa kanihakikishia iko poa na hain amadhara kiafya, so mlengwa anaweza nicheck nikampa maelezo yote
 
Wakuu nasumbuliwa sana na ugonjwa wa pumu au mzio, kuna mda ikipanda napumua kwa shida sana na hua inasababishwa na vitu flan hivi mfano baadhi ya vyakula nikitumia kama dagaa, bamia but hivyo vitu nimeacha saivi.

Ila mawingu ndio yananitesa maana wingu likifunga basi pumu hunijia. Naombeni msaada nasikia kuna dawa za asili zinaponyesha. Nimejaribu vitu vingi ila sijabahatika kupona hadi sasa.

Kwa mwenye ujuzi na hili swala naomba tusaidiane.
 
Wakuu nasumbuliwa sana na ugonjwa wa pumu au mzio, kuna mda ikipanda napumua kwa shida sana na hua inasababishwa na vitu fulan hivi mfano baadhi ya vyakula nikitumia kama dagaa, bamia but hivyo vitu nimeacha saivi....
Wewe una Severe Persitent Asthma.

Unaitaji kutumia dawa mbili za hospitali za kuvuta mapafu
Dawa hizo lazima utumie walau ku control ugonjwa.

Pumu ni ugonjwa ambao mara nyingi uko ndani ya vinasaba vyako usitegemee upone kabisa...Na unapoanza kutafuta mitishaba ambazo hazijawafanyiwa tafiti ndo unapotea kabisa.

Hauwezi kuponyesha moja kwa moja Bali ku control na uache kubanwa...unaweza achieve hiki kitu hospitalini but haikuondolei vinasaba vyako.
 
Wakuu nasumbuliwa sana na ugonjwa wa pumu au mzio, kuna mda ikipanda napumua kwa shida sana na hua inasababishwa na vitu flan hivi mfano baadhi ya vyakula nikitumia kama dagaa, bamia but hivyo vitu nimeacha saivi...
Usitegemee kabisa kupona kwa dawa Labda kwa maombi ya Mungu pumu ni kujikibal tu kuwa unayo na kuepuka vile ambavyo vinaweza kusabbisha attack mfano vyakula, dawa fulani hivi zile za group la non steroid inflammatory mfano ibuprofen declofanic aspirin na dawa zote zenye content ya non steroid, mavumbi, shellfish, moshi, vitu baridi, na vyenginevyo.

Mimi dawa ninazotumia tokea nizaliwe until now natumia salbutamol inhaler ile ya kupuliza mapafu au ventolin.

natumia hydrocortisone vidonge.

natumia cetrizine nikiona flue zinaanza kuja kuepusha allergy.

dawa za maumivu natumia panadol tu.

natumia bennylin 4flue natumia.

natumia Otrivin nasal drop ya maji hii kwenye pua.

kwa flue natumia vaporub vix inhaler kuvuta puani natumia vaporub vix kupaka kwenye pua na kifua

Na nikifkia hapo kama nikiona bado zinanisunbua kwa muda wa siku mbili Na kuendelea basi naenda hospital napigwa sindano moja safi kabisa ya hydrocortisone mama hivo inaingizwa kwenye mshipa na kupigwa dawa ya mvuke salbutamol cjui wanachanganya na nini wanakuvalisha mask kwa ni nubilizer mashine inaingia dawa mdomon kwa njia ya mvuke kwenda mapafuni na hapo nikitoka mapafu yanakua yameachia napata unafuu walau kwa masaa 10

Kwaio hapo jaribu hizo vix kwa flue uwe nazo ndani na hiyo otrivin na hydrocortisone vidonge but nenda hospital wakupangie dose
 
Wakuu nasumbuliwa sana na ugonjwa wa pumu au mzio, kuna mda ikipanda napumua kwa shida sana na hua inasababishwa na vitu flan hivi mfano baadhi ya vyakula nikitumia kama dagaa, bamia but hivyo vitu nimeacha saivi...
Pole sana kwa hali unayopitia Mungu akusaidie upate ufumbuzi na kupona.
 
Imenisumbua sana primary mpaka sekondary, ilikuwa ikibana naenda kuchomwa sindano kweny mshipa inaachia. Nilitumia sana dawa za kienyeji za kuchanganya na asali Mara mwisho kunibana ilikuwa 2009.

Hadi nahisi nilishaponaga mana sijawahi kubanwa tena na asthma labda itokee nifanye shughuli yoyote ya kutimua vumbi kama kusafisha stoo ndio huwa nafeel kwa mbaali pumzi kubana Ila huwa haizid siku moja nakuwa kawaida.

Maza huwa haamini nikimwambia sijawah kubanwa tena asthma tokea wakati huo, mana alinihangaikia sana.
 
Wakuu nasumbuliwa sana na ugonjwa wa pumu au mzio, kuna mda ikipanda napumua kwa shida sana na hua inasababishwa na vitu flan hivi mfano baadhi ya vyakula nikitumia kama dagaa, bamia but hivyo vitu nimeacha saivi....
Pole,

Unaweza kupata daw ambazo zinaweza kuondoa kwenye hali uliyonayo.

Unahitaji kufika hospitali, mwone physician/daktari bingwa wa magonjwa ya ndani kama kwa eneo ulilopo unaweza kumpata.

Kwani daktari husika anahitaji kujua historia na kwa kiasi gani tatizo lipo. Pia kufanya vipimo ili kutambua uwezo wako wa mapafu kwa sasa, kwani huo ndio msingi wa upewe dawa za aina gani na mara ngapi ili kukuweka huru na mashambulizi ya pumu ya mara kwa mara.

Pia ushauri wa ziada wa nini ufanye na nini usifanye. Kipi utumie na kipi usitumie kulingana na hali halisi.
 
Nenda hospital na ujikubali,mie Nina pumu tangu nikiwa mtoto na Sasa ni mtu mzima na mazoezi nafanya kwa wingi kwa KADRI YA UWEZO WA NGUVU WA MAPAFU...nilipokuwa mtoto ikianza masika mawingu yakiandama naumwa...nikienda mashineni kusaga sababu ya vumbi naumwa....Hadi mpira wa miguu ukanipita kushoto!

Nilipojikubali nikaanza mazoezi na kujilinda na vumbi...naweza kumaliza masika bila kunywa dawa ya Asthma/inhaler

Muone daktari jikubali, no short cut
 
Wakuu nasumbuliwa sana na ugonjwa wa pumu au mzio, kuna mda ikipanda napumua kwa shida sana na hua inasababishwa na vitu flan hivi mfano baadhi ya vyakula nikitumia kama dagaa, bamia but hivyo vitu nimeacha saivi...
Maradhi ya pumu hakuna dawa ya hospitali itakayo weza kukuponyesha ukapona kabisa utapata unafuu.

Zipo tiba za asili za kutibu maradhi ya pumu na utaweza kupona kabisa maradhi yako nitafute kwa wakati wako nipate kukutibia maradhi yako.
 
Maradhi ya pumu hakuna dawa ya hospitali itakayo weza kukuponyesha ukapona kabisa utapata unafuu. Zipo tiba za asili za kutibu maradhi ya pumu na utaweza kupona kabisa maradhi yako nitafute kwa wakati wako nipate kukutibia maradhi yako.
Naomba tiba ya sikio moja kuziba baada ya maji kuingia. Uwezo wake wa kusikia pia umepungua. Nasikia uzito Sana katika Hilo sikio lililoingia maji.

Asante
 
Siyo mbaya nisikilize nami ushauri wa madaktari. Hujafa hujaumbika. Ndo nasubscribe hivo😁
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom