Ugonjwa wa moyo unaosababishwa na simanzi/kuachana na mpenzi wako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa wa moyo unaosababishwa na simanzi/kuachana na mpenzi wako

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, May 30, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Ugonjwa wa moyo unaosababishwa na simanzi au kuachana na mpenzi/mwenza wako yoyote yule hujulikana kitaalamu kama Takostubo au broken heart syndrome.
  Ugonjwa huu husababishwa na kudhoofika ghafla kwa misuli ya moyo kwa muda mfupi na hauuhusiani na tatizo la

  kukosekana kwa damu ya kutosha katika moyo.Tatizo hili hujulikana kamabroken heart syndrome kwa sababu hutokana na mtu;
  - Kufiwa na mpenzi/mwenza wake
  - Kuachana na mpenzi/mwenza wake
  - Kuwa na wasiwasi mara kwa mara kwa muda mrefu
  Vilevile tatizo hili huweza kupelekea moyo kushindwa kufanya kazi ghafla (Acute heart failure), moyo kupiga bila

  mpangilio usio wa kawaida (lethal ventricular arrhythmia) .

  Dalili:


  • Maumivu makali ya kifua
  • Matatizo ya upumuaji au kuhema kwa shida
  • Uchovu
  • Mapigo ya moyo yasiyo na mpangilio
  [​IMG]Je tatizo hili husababishwa na nini?  Tatizo hili huweza kusababishwa na mambo yafuatayo:


  • Habari ya kufiwa na mpenzi wako
  • Kutambua unaugua ugonjwa sugu kama vile saratani
  • Kupoteza hela nyingi
  • Sherehe ya kushtukiza (surprise parties)
  • Kutakiwa kuongea hadharani
  • Ukiwa na matatizo kama ugonjwa wa pumu, maambukizi, ajali ya gari au baada ya upasuaji mkubwa.

  Vipimo


  • ECG
  • X-ray ya kifua
  • Echocardiogram
  • MRI
  • CAG
  • Kipimo cha damu kuangalia vimengÂ’enyo vya kwenye moyo
  • Ni muhimu kutofautisha na Shambulizi la moyo na hili tatizo,

  Matibabu


  Hakuna tiba ya madawa iliyo maalum kwa ajili ya kutibu tatizo hili pekee. Matibabu yake yanaweza kufanana na matibabu ya shambulio la moyo, na mgonjwa anaweza kuhitaji kulazwa hospitali kwa muda ingawa si mara zote huwa hivyo.

  Daktari akishathibitisha kuwa chanzo cha dalili zako ni broken heart syndrome na wala si shambulio la moyo anaweza kukupatia dawa kama vile zilizo katika kundi la angiotensin-converting enzyme (ACE) inhibitors mfano Benazapril, kundi

  la beta blockers kwa mfano carvedilol au kundi la diureticskama vile frusemide (lasix). Dawa hizi husaidia kupunguza mzigo katika moyo na pia kuzuia usipate shambulio jipya.
  Kwa kawaida wagonjwa wengi hupata nafuu baada ya muda wa kama mwezi mmoja au miwili hivi. Hata hivyo ni vema kumuuliza daktari wako unapaswa kutumia dawa kwa muda gani.

  Kinga

  Kuna uwezekano mkubwa sana wa hali hii kujirudia tena mara baada ya shambulio la kwanza. Mpaka sasa hakuna dawa zilizothibitishwa zinazoweza kusaidia kuzuia hali hii isijitokeze tena, ingawa baadhi ya madaktari wanashauri matumizi ya muda mrefu ya dawa zakundi la beta blockers kama vile atenolol, carvedilol, au dawa zenye kuzuia

  uzalishaji wa homoni zenye kuchochea shinikizo katika moyo.
  Pamoja na matumizi ya dawa, ushauri nasaha pamoja na kubadili mfumo wako wa maisha ni mambo ya muhimu zaidi kusaidia kukukinga na tatizo hil
  Ugonjwa wa Moyo Unaosababishwa na Simanzi/Kuachana na Mpenzi Wako
   
 2. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Sijawasiliana kwa Muda mrefu na Afrodenzi je na mimi naweza pata huu ugonjwa?
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mkuu@duduwasha kwani wewe unampenda Mkuu@Afrodenzi?
   
 4. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  smile huko wapi jamani na mimi napokaribu kupatwa na huu ugonjwa ..njooo jamani...
   
 5. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Bila Shaka
   
Loading...