Ugonjwa wa Masundosundo mwilini na sehemu za siri (Genital & Skin Warts)

CANNY DRAMA

JF-Expert Member
May 10, 2019
383
500
Mimi nikiwa Na miaka 18 vilinishika hadi kwenye pumbu, Na kwenye kibofu hata jinsi ya unyoaji wa nywele ilikua shida, Na kwenye vidole vya mikononi nilikua navikata Na wembe kila vikiota vile vya sehem Za siri navinyukua Na kucha. Damu zilikua zinatoka sana, badae waknambia kama unavitoa utapata Cancer nikaviacha hadi baadae vikaisha vyenyewew. Bila kutumia dawa yoyot
 
Kapepo

JF-Expert Member
Aug 14, 2015
823
1,000
kuwa mpole zitatoka usipende kutumia vitu vinavyo jibu hapo hapo mkuu iyo dawa ni nzuri
pia harufu yake naijua ipo kama asali tumia ukiwa unalala na angalia usipakee mboo nzima
itatoka magamba kama nyoka
sawa mkuu assante sana kwa ushauri
 
Kapepo

JF-Expert Member
Aug 14, 2015
823
1,000
Mimi nikiwa Na miaka 18 vilinishika hadi kwenye pumbu, Na kwenye kibofu hata jinsi ya unyoaji wa nywele ilikua shida, Na kwenye vidole vya mikononi nilikua navikata Na wembe kila vikiota vile vya sehem Za siri navinyukua Na kucha. Damu zilikua zinatoka sana, badae waknambia kama unavitoa utapata Cancer nikaviacha hadi baadae vikaisha vyenyewew. Bila kutumia dawa yoyot
pamoja mkuu
 
Oct 12, 2015
49
95
Wanabodi habari zenu nina mdogo wangu wa kiume ameota tuvipele kwenye eneo la kibofu akaonwa ikasemekana ni genital warts akapewa silver pencil ya kuvichoma ila haviishi na vingine vinaota,je kuna dawa ya kunywa au dawa ipi ingine inafanya kazi vyema kuleta matokeo??
 
Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
9,685
2,000
Nenda kwa mtaalamu bingwa wa magonjwa ya ngozi aone tatizo moja kwa moja na hii ni hospitali kubwa.

Hapa unaweza shauriwa dawa lkn tatizo likawa kubwa kuliko uwezo wa dawa.
 
Mbanti

JF-Expert Member
Apr 29, 2017
229
250
nimerud tena kuleta mrejesho, nimetumia hii podophyllin siku ya tatu leo, kwa maeleze ya watu wanasema hii dawa inaunguza ila kwangu mm naona ni tofauti haiunguzi pili sioni matokeo yeyote hadi hivi sasa hakuna mabadiriko kabisa naombeni mnisaidie wakuu kimawazo namna ya kuondoa hizi skin tags kwenye uume View attachment 1658060
Picha tafadhali tuone mrejesho
 
bcsolution

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
383
250
Wanabodi habari zenu nina mdogo wangu wa kiume ameota tuvipele kwenye eneo la kibofu akaonwa ikasemekana ni genital warts akapewa silver pencil ya kuvichoma ila haviishi na vingine vinaota,je kuna dawa ya kunywa au dawa ipi ingine inafanya kazi vyema kuleta matokeo??
Habari mkuu.

Pole na mdogo wako kuumwa.
Umenitumia Dm na kuniuliza kuhusu CASTOR OIL kama inafaa kweli kuhusu hizo GENITAL WARTS.

Nimeona nikujibu hapa na sio DM ili iwe kwa manufaa ya wengine pia.

Kwanza nikukumbushe tu kuumwa ugonjwa wowote sio AIBU kwa sababu .

Na wahenga walisema MFICHA MARADHI KIFO HUMUUMBUA.

Sasa basi ikiwa unaumwa wewe au mdogo wako USIONE AIBU.

Nirudi katika mada husika.

Mimi pia miaka inafika 15 nyuma kama sikosei niliumwa GENITAL WARTS.

Zilinitesa sasa, zilikuwa zinawasha tena hasa kipindi cha usiku nikiwa nimelala.

Nilikuwa najikuna mpaka najiumiza na kutoa damu.

Hapo mwanzoni sikujua kama ni Genital warts. Nilihisi nimepata fangas.

Nikaona maduka ya Dawa yaani Famas na kuwaambia nawashwa sana sehemu za siri , walinipa cream za kupaka inaitwa SONADERM nikawa nikiipaka muwasho unaacha na usiku nalala vizuri.

Lakini sikupona na baadae ndo vikaanza kutoka hivyo Viwarts na ndo nikaanza kuviona kwa macho.

Nikaanza kufanya SEARCH kwenye Mitandao kama sikosei enzi hizo nilikuwa natumia YAHOO SEARCH sikumbuki kama Google ilikuwa tayari inawezekani haikuwa maarufu.

Baada kuserch nikagundua ni GENITAL WARTS , nikaanza kusachi tiba zake, tiba zikawa aina tofauti ya kwanza ilikuwa KUVICHOMA Na kuvikata kwa laser.
Tiba ingine nakumbuka nilioiona ilikuwa OPERESHEN.

Lakini nikasoma ushuhuda wa watu wengi waliofanyia hizo Tiba ni kwamba WARTS zilirudi tena.

Nikaogopa.

Nikasema Ngoja niende nikamuona SPECIAL DOCTOR wa magonjwa ya Ngozi.

Nikaenda pale njia ya kuelekea Hospital ya Muhimbili pale kulikuwa na profesa wa magonjwa ya ngozi.

Alinikagua na yeye akasema ni GENITAL WARTS.

Akanipa Dawa za kupaka zilikuwa Cream sikumbuki jina lake hiyo cream na akanipa vidonge vya kumeza pia.

Nilitumia hizo Dawa lakini sikupona.
Isipokuwa tu ilinisaidia muwasho ukapungua na usiku nikawa naweza kulala.

Baada siku kadhaa vilizidi kujaa ni vikawa vingi zaidi , ni nikiacha zile cream basi najikuna kama vile nataka kuchuna ngozi.

Dahh nilichanganyikiwa.

Niliamua kurudi katika mitandao na kufanya search tena.

Nilikesha kwenye kompyuta.

Mpaka nikampata mtu yuko marekani anadai anayo dawa yake.

Nakumbuka huyo mtu alidai anataka malipo kidogo tu kama ya Dola 10 ili anipe hiyo dawa na alisema hanitumii dawa ila dawa nitaipata katika nchi yangu hapa hapa kwa mchanganyiko atakaonipa.

Na akasema pesa nitakapoituma tu akipata atanitumia email namna ya huo mchanganyiko unavyofanya kazi.

Basi nikaanza kuwasiliana nae na nikasema ata akiniibia basi nitashukuru mungu tu .

Nikatuma pesa dola 10 ikachukua kama wiki hivi akaipata.

Alipoipata ile pesa akanitumia email ya ule mchanganyiko.

Akaniambia kwamba hivi.

Anza na dawa hii chukua CASTROL OIL ambayo sio ya viwandani, akimaanisha iwe ya asili ipakaze kwenye hizo warts mara 2 au 3 kwa siku.

Na kama mafuta hayatulii basi weka pamba yenye hayo mafuta halafu funga kitambaa au bandika plasta mafuta yakae pale.

Akaniambia kama warts zako sio sugu utaona ndani ya wiki 1 au 2 .

Na kama sugu fanya hivi

Chukua kitunguu thaumu ( garlic ) kiponde na kitunguu maji (red onion) kiponde changanya na hayo mafuta ya castrol oil halafu pakaza pale mara 2 au 3 kwa siku.

Mimi baada kupata hayo maelekezo nikaenda pale soko la kariakoo pembeni ya stendi ya magari ya mwenge kuna maduka mengi yanauza dawa za asili.

Nikanunua chupa ya nusu lita kwa 2000 elfu mbili tu enzi hizo. Sijui sasa wanauzaje, yananuka lakini nilijikaza sana.

Nikaanza hiyo tiba.

Huwezi amini baada wiki tuu na hata sikumaliza wiki yenyewe nikapona.

Nilifurahi sana.

Nikarudi kwa yule jamaa wa marekani kumshukuru , naye alifurahi.

Lakini sasa sikumbuki tena pale nilipompata kwenye mitandao ningekupa umsome umuone na ndo mana nikazitoa hapa hizo dawa bure mwenye kutaka atumie.

Hii ni dawa ya asili na sidhani kama ina madhara yoyote na pia kwa ushauri ni bora ukaanza kwanza hospitali kuhakikisha nini unaumwa , na ukishapata uhakika nini unaumwa na ukitaka unaweza ukaijaribu hiyo Dawa ambayo ni mafuta tu.

La mwisho mimi sio dokta wala sina ujuzi wowote wa tiba asili.

Nilichofanya nimetoa ushuhuda wangu kwa kile kilichonitesa mimi wakati huo.

Kwa ushauri zaidi waone wataalamu wa afya mahospitalini au wataalamu wa tiba za asili wanaotambulika.

Nakutakia upone haraka ikiwa wewe au mdogo wako.

MUNGU atakusaidia usisahau pia kumuomba MUNGU.

Kama umeowa mtibu na mwenza wako, mpone wote kwa pamoja.

Vinaambukiza , na kwa wanawake vinajificha kwa ndani huvioni.

Nakutakia maisha mema. Ahsante.
 
Teamanaconda

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
471
500
Wanabodi habari zenu nina mdogo wangu wa kiume ameota tuvipele kwenye eneo la kibofu akaonwa ikasemekana ni genital warts akapewa silver pencil ya kuvichoma ila haviishi na vingine vinaota,je kuna dawa ya kunywa au dawa ipi ingine inafanya kazi vyema kuleta matokeo??
Mkuu pole sana,mimi hili hivyo vidude viliniota mpaka kimoja kikaota kwenye uume,nikaenda hospital ya kwanza wakanipa ile pencil ya kuvichoma,lakini vikarudi tena,nikaenda hospital nyingine dokta akainichukua vipimo akaniambia hauna tatizo ila pandisha kinga za mwili vitapotea,akanipa na dawa ya kupaka lakini havikuisha,kuna jamaa mmoja nikakutumia nae wtsp akaonyesha dawa ya kuvitibu kumuuliza akania dawa moja ni elf 65 na ziko mbili ya kupaka na vidonge,ila nikaona ananilazimisha sana kununua hizo nikaachana nae,huwezi amini kuanzia majuzi nimeamka asubuhi nimekuta vyote vimepotea hakuna hata kimoja,simshauri atumie ile pencil ya kuvichoma kwanza inauma pili haviponi,
 
Kwa hyo ww ulipona bila dawa au hyo ya 65k ndo ulitumia?
 
Teamanaconda

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
471
500
Kwa hyo ww ulipona bila dawa au hyo ya 65k ndo ulitumia?
Yani hiyo dawa yake sikununua kwa kweli vimeisha bila dawa, ndio nikakumbuka yule dokta alieniambia kinga ya mwili ikiwa vizuri vitapotea,mimi nilikuwa sio mpz sana wa kula matunda na pia nilikuwa nachelewa sana kulala na j2 nikipumzika nyumbani silali mchanana,ila baada ya dokta kuniambia vile nikaanza kula sana matunda na nikawa natafuna sana karoti na nikaanza kulala mchana siku za j2,kwa kweli nikaanza kuuona mwili wangu unastarehe vizuri sana,ila sijui kama ndio chanzo cha kupona, vinakera sana hasa kimoja kiliota kwenye mashine pembeni,
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom