Ugonjwa wa kiharusi/ kupooza (stroke): Kinga, tiba na jinsi ya kukabiliana na maradhi haya

Kupooza hisababishwa na kutokulipa pesa za bank pamoja na tala. Hasa pale unapo kumbushwa,malipo
 
Habari wa Tanzania wenzangu
Naomba niwaelimishe kuhusiana na tatizo hili ya kiharusi maana ni tatizo linalokumba nguvu kazi kubwa ya taifa letu.

Kiharusi ni mabadiliko yanayo tokea kwa kasi katika eneo la ubongo /ubongo wote ambayo dalili zake huduma kwa muda zaidi ya masaa 24 na chanzo chake ni ubongo kukosa hewa ya oxygen kutokana na mishipa ya damu eneo la ubongo kupasuka(cerebral haemorrhage) ama kusinyaa (cerebral infarction)[WHO]

Dalili za awali
1.Maumivu ya kichwa kama umepigwa na nyundo (siku nzima/masaa mengu ya siku)

2.Kupata shida ya kuona/kuona vitu viwili viwili au kuona giza

3.Mdomo kuenda upande

4.Kukosa nguvu ya mkono au mguu upande mmoja au kushindwa kuinuka au kudondoka chini wakati unatembea

5. Kupoteza fahamu au kufariki

Kiwago cha athari kutoka repoti ya WHO

Takribani watu milioni 15 wanapata tatizo la kiharusi kila mwaka miongoni mwao milioni 5 hufariki milioni 5 hubaki na ulemavu wa kudumu

Pia kiharusi ni chanzo cha 2 cha vifo dunia nzima na chanzo cha 3 cha ulemavu dunia nzima
asilimia 70% ya kiharusi vinavyotokea duniani hutokea kwenye nchi zenye uchumi wa chini na uchumi wa kati.

Kwa takribani miongo 4 (miaka 40) iliyopita nchi zilizo endelea zimefanikiwa kupunguza idadi ya watu wapya wanao pata kiharusi kwa asilimia 42%. Wakati idadi ya wahanga wapya imeongezeka mara 2 katika nchi zenye uchumi wa chini na wakati.

Kwa Tanzania idadi kamili za wahanga nimeshindwa kuzipata kutokana na ukosefu wa takwimu zilizofanyiwa uchunguzi na kuchapishwa ila kutokana experience yangu idadi ya wahanga wa ugonjwa huu imeongezeka kwa kasi sana na kuwapata hadi vijana wenye umri mdogo.


MADHARA YANAYOTOKANA NA KIHARUSI

1. Kupooza kwa upande mmoja wa mwili
2. Kupoteza uwezo wa kumeza au kutafuna chakula na kupelekea mtu kulishwa kupitia nasogastric tube(NGT)
3. Kushindwa kuongea au kuongea kwa shida
4. Kupoteza kumbukumbu (kusahau) na kushindwa kuconcetrate
5.Ukakamavu wa misuli na viungo
6. Ulemavu wa muda mfupi au wakudumu
7.Msongo wa mawazo kwa mhanga na wanafamilia.
8. Kifo

ATHARI KITAIFA
1. Kupotea na kupungua nguvu kazi ya uzalishaji
idadi kubwa ya wahanga ni watu wenye mchango mkubwa katika uzalishaji wa taifa kwahyo taifa linapata hasara ya kupoteza rasilimali watu katika njanja mbali mbali za uzalishaji.

2. Ongezeko la umasikini kwa familia na taifa kiujumla
wahanga wengi ni nguzo ya utafutaji kifamilia.(Baba /mama/mume/mke)
akipata kiharusi familia inazoroteka kiuchumi . Pia inachangiwa na gharama kubwa za kumhudumia mhanga wa kiharusi. Na wenza kuacha kazi au shughuli za kiuchumi na kumhudumia mgonjwa

3. Matatizo ya kiafya kwa wanafamilia
mfano maumivu ya mgongo katika shughuli za kumbeba na kumgeuza mgonjwa

4.Mifarakano katika Ndoa na Familia
wenza kuwakimbia wenza wao pale wanapopata tatizo hili au kuwanyanyapaa
wanandugu kukimbia majukumu ya kumsaidia mgonjwa na familia yake

NINI KIFANYIKE? kupunguza na kukabili hili tatizo la kiharusi

1. TUBADILI MITINDO YA KIMAISHA
¡. Kupunguza au kuacha matumizi ya vilevi/sigara kupita kiasi au kila siku

¡¡. Kujifunza na kujizoesha tabia ya mazoezi mara 5 kwa wiki . kila siku kwa muda usiopungua dakika 30.

¡¡¡. Kuzingatia milo sahihi
- Hasa kiwango cha chakula kisizidi sana mfano mtu anakula ugali kilo 1 peke yake.
mwili unahitaji kiwango fulani kidogo cha nguvu kutoka kwenye huo ugali mfano labda robo ya ugali. hiyo nusu na robo inayobaki huhifadhiwa kwenye mwili kama mafuta na kukuweka katika hatari ya kupata tatizo la presha na kiharusi

-Kupunguza matumizi ya vyakula vya wanga mfano chapati,maandazi,keki,ugali,wali,mikate nakadhalika

-Kupunguza matumizi ya vyakula vya mafuta mfano mlo sahihi si kula vitu vuzuri au vitamu tamu. Bali ni kuzingatia makindi saba ya chakula. hakikisha chakula chako cha kila siku kina atleast makundi 4 ya chakula/virutubisho

2.KUONGEZA VIWANGO VYA SHUGHULI KATIKA SIKU
Mfano wengi tunakula chakula kingi kulinganisha na shughuli tunazofanya.hii hupelekea kiwango kidogo kilichomeng'enywa kutumika na kingine kinachobaki kuhifadhiwa mwilini kama mafuta.

Hii pia imechangiwa na ongezeka la matumizi ya boda boda ,bajaji ,na magari kwa umbali mfupi. ambao umbali huo zamani tulikuwa tunatembea ila sasa tunatumia vyombo hivyo. kutembea umbali huo kungesaidia mmeng'enyo wa mafuta ya ziada katika miili yetu.

Tuongeze umbali tunaotembea kila siku. sio lazima uende kituoni au kwa dukani au sokoni kwa kutumia boda boda au bajaji

3.TUPIME AFYA ZETU MARA KWA MARA
Kila mwezi ,baada ya miezi 3 au 6 kulingana na hali yako ya kiuchumi.
FAIDA
Kugundua tatizo mapema hasa presha.
Kuzuia tatizo lisitokee na kuwa chronic

4. KUJIUNGA NA KLINIKI ZA MOYO
-Kupata elimu juu ya matatizo hayo

- Kuzingatia ushauri wa matumizi ya dawa za presha . wengi huacha dawa na kufanya presha zao ziwezisizodhibitiwa na kupelekea wao kupata kiharusi

- Kutonunua dawa za presha bila ushauri wa daktari

- Kuto acha matumizi ya dawa za presha bila ushauri wa daktari

Ukiwa na tatizo la presha ni muhimu kutumia dawa za kudhibiti presha kila siku ya maisha yako, na usipo zingatia hayo yaliyotajwa hapo juu. upo kwenye hatari ya kupata kiharusi.

5. HOSPITALI KUFANYA UFUATILIAJI
Kwa wagonjwa wa presha, na wahanga wa kiharusi pale ambapo wamegundulika na presha na wahanga wa kiharusi wanaporuhusiwa kurudi nyumbani.
hii itapunguza vifo na ulemavu unaotokana na kiharusi

6. WATAALAM WAFIZIOTHERAPIA WAHUSIKE KATIKA DISCHARGE YA WAHANGA WA KIHARUSI.

Kwanza itambulike kuwa wataalma wa fiziotherapia ndio wahusika wa mazoezi tiba katika kuwarudishia watu nguvu za misuli na mwili baada ya kupooza.

Wafiziotherapia husaidia
¡ . Kumfundisha mgonjwa mbinu za kugeuka kitandani,kukaa na kuzuia ulemavu na ukakamavu wa viungo

¡¡. Kuwafundisha ndugu wa mgonjwa namna ya kumhudumia mgonjwa akiwa nyumbani - kumrisha,kumyoosha viungo,kumgeuza ,kumkalisha na kuzuia ulemavu

Hii itasaidia sana wagonjwa kupona kwa wepesi bila madhara ya kiharusi.

7. KUANZA MAZOEZI TIBA HARAKA SANA BAADA YA KUPATA KIHARUSI.
Kutokana na kukosa elimu kuhusiana na tatizo hili wahanga wengi hubaki majumbani bila matibabu yoyote hii uchangiwa pia na imani potofu wakizani kuwa wamelogwa la hasha ni matatizo fulani ya kiafya hupelekea tatizo hili.

Kadri mgonjwa anavyozidi kubaki nyumbani bila kuanza mazoezi tiba kwa mtaalamu wa fiziotherapia anazidi kuwa katika hatari ya kupata ulemavh wa kudumu au kifo.

8. OMBI KWA SERIKALI
Hospitali maalum za kutibu magonjwa ya moyo zianzishwe katika ngazi ya wilaya
mfano JKCI

HII ITASAIDIA
¡. Kupunguza vifo na ulemavu kutokana na ukaribu wa huduma kwa wahanga wa kiharusi

¡¡.Kupunguza msongamano kwenye hospitali kubwa ambao msongamano huo huchochea utoaji hafifu wa huduma kwa wahanga na kupelekea athari kama vifo na ulemavu.


Natumai mmeelimika tafadhali wasambazieni na wengine ujumbe huu nao wapate kuelimika.

Kwa ushauri zaidi nitafute kupitia 0718 22 48 40

PSX_20190813_120248.jpeg
 
UJUE UGONJWA WA KIHARUSI/STROKE DALILI ZAKE PAMOJA NA TIBA

STROKE (KIHARUSI)
Kiharusi ni ugonjwa ambao husababishwa na kufa kwa cell za ubongo.Kuna aina mbili za kiharusi.1.Kiharusi cha aina ya kwanza kinachoitwa ischemic hichi husababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu baada ya mishipa hiyo kujaamafuta(cholesterol) na kusababisha damu kutofika vzr kwenye ubongo kama unavyoona kwenye kimchoro cha juu.2.Kiharusi cha aina ya pili kinachoitwa hemorrhagic hiki husababishwa na kupasuka kwa baadhi ya mishipa ya damu kwenye ubongo kama unavyoona mchoro wa chini na kusababisha damu kusambaa kwenye ubongo na kusababisha mmbonyeo ndani ya ubongo na kusababisha kiharusi.watu wenye presha wako kwenye hatari kubwa ya kupata kiharusi na kiharusi huuwa haraka sana.Kiharusi kiko hivi kama ubongo wa upande wa kulia ndio utakaoathirika basi utapararaiz upande wa kushoto,na kama ubongo utaathirika upande wa kushoto basi utapararaizi upande wa kulia.
DALILI ZA KIHARUSI
1.kupooza mguu au mkono.
2.Kuchanganyikiwa kupata shida kuongea au kuelewa.hapa utakuta mnamgonjwa halafu inafikia kipindi anakuwa kama kachanganyikiwa anaongea yasioeleweka na pia anapoteza kumbukumbu,anaweza kuja kumuona mtoto wake kabisa halafu akamuuliza wewe ni nani.
3.kutokuona jicho moja au yote.
4.kuumwa kichwa kikali mara kwa mara pasipojua chanzo.
5.kichefuchefu cha ghafla kuwa na homa na kutapika muda mrefu.
KIHARUSI KINATIBIKA/ pia unaweza tumia kinga

Karibu kituoni kwetu utapata tiba sahihi na kinga ya kiharusi pia tuna huduma ya massage Gharama yake Ni TSH 10,000 tuu.

1.Isomalto
2.Broken gano
derma
3.Fish oil
4.lecithin
5.Gyngkotea
Tibu_kiharusi_Mawasiliano.
0718069047/0688184620.
 
kiharusi???to The best of my KNOWLADGE harusi hushangiliwa kwa kupungiwa mikono,.na wengine hunyanyua miguu...wagonjwa ni wengi,.....
Soma uzi vizuri,halafu utoe komenti ukitaka,au umeshaathirika tayari?Kama tayari mpe anayekuuguza akomenti,samahani lakini.
 
Nitakuona MKUU hili tatizo linamsumbua mama yangu Mzazi huu mwaka 4 hatujui tunaenda wap
UJUE UGONJWA WA KIHARUSI/STROKE DALILI ZAKE PAMOJA NA TIBA

STROKE (KIHARUSI)
Kiharusi ni ugonjwa ambao husababishwa na kufa kwa cell za ubongo.Kuna aina mbili za kiharusi.1.Kiharusi cha aina ya kwanza kinachoitwa ischemic hichi husababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu baada ya mishipa hiyo kujaamafuta(cholesterol) na kusababisha damu kutofika vzr kwenye ubongo kama unavyoona kwenye kimchoro cha juu.2.Kiharusi cha aina ya pili kinachoitwa hemorrhagic hiki husababishwa na kupasuka kwa baadhi ya mishipa ya damu kwenye ubongo kama unavyoona mchoro wa chini na kusababisha damu kusambaa kwenye ubongo na kusababisha mmbonyeo ndani ya ubongo na kusababisha kiharusi.watu wenye presha wako kwenye hatari kubwa ya kupata kiharusi na kiharusi huuwa haraka sana.Kiharusi kiko hivi kama ubongo wa upande wa kulia ndio utakaoathirika basi utapararaiz upande wa kushoto,na kama ubongo utaathirika upande wa kushoto basi utapararaizi upande wa kulia.
DALILI ZA KIHARUSI
1.kupooza mguu au mkono.
2.Kuchanganyikiwa kupata shida kuongea au kuelewa.hapa utakuta mnamgonjwa halafu inafikia kipindi anakuwa kama kachanganyikiwa anaongea yasioeleweka na pia anapoteza kumbukumbu,anaweza kuja kumuona mtoto wake kabisa halafu akamuuliza wewe ni nani.
3.kutokuona jicho moja au yote.
4.kuumwa kichwa kikali mara kwa mara pasipojua chanzo.
5.kichefuchefu cha ghafla kuwa na homa na kutapika muda mrefu.
KIHARUSI KINATIBIKA/ pia unaweza tumia kinga

Karibu kituoni kwetu utapata tiba sahihi na kinga ya kiharusi pia tuna huduma ya massage Gharama yake Ni TSH 10,000 tuu.

1.Isomalto
2.Broken gano
derma
3.Fish oil
4.lecithin
5.Gyngkotea
Tibu_kiharusi_Mawasiliano.
0718069047/0688184620.
 
UJUE UGONJWA WA KIHARUSI/STROKE DALILI ZAKE PAMOJA NA TIBA

STROKE (KIHARUSI)
Kiharusi ni ugonjwa ambao husababishwa na kufa kwa cell za ubongo.Kuna aina mbili za kiharusi.1.Kiharusi cha aina ya kwanza kinachoitwa ischemic hichi husababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu baada ya mishipa hiyo kujaamafuta(cholesterol) na kusababisha damu kutofika vzr kwenye ubongo kama unavyoona kwenye kimchoro cha juu.2.Kiharusi cha aina ya pili kinachoitwa hemorrhagic hiki husababishwa na kupasuka kwa baadhi ya mishipa ya damu kwenye ubongo kama unavyoona mchoro wa chini na kusababisha damu kusambaa kwenye ubongo na kusababisha mmbonyeo ndani ya ubongo na kusababisha kiharusi.watu wenye presha wako kwenye hatari kubwa ya kupata kiharusi na kiharusi huuwa haraka sana.Kiharusi kiko hivi kama ubongo wa upande wa kulia ndio utakaoathirika basi utapararaiz upande wa kushoto,na kama ubongo utaathirika upande wa kushoto basi utapararaizi upande wa kulia.
DALILI ZA KIHARUSI
1.kupooza mguu au mkono.
2.Kuchanganyikiwa kupata shida kuongea au kuelewa.hapa utakuta mnamgonjwa halafu inafikia kipindi anakuwa kama kachanganyikiwa anaongea yasioeleweka na pia anapoteza kumbukumbu,anaweza kuja kumuona mtoto wake kabisa halafu akamuuliza wewe ni nani.
3.kutokuona jicho moja au yote.
4.kuumwa kichwa kikali mara kwa mara pasipojua chanzo.
5.kichefuchefu cha ghafla kuwa na homa na kutapika muda mrefu.
KIHARUSI KINATIBIKA/ pia unaweza tumia kinga

Karibu kituoni kwetu utapata tiba sahihi na kinga ya kiharusi pia tuna huduma ya massage Gharama yake Ni TSH 10,000 tuu.

1.Isomalto
2.Broken gano
derma
3.Fish oil
4.lecithin
5.Gyngkotea
Tibu_kiharusi_Mawasiliano.
0718069047/0688184620.
Asante sana Mkuu.
 
niliona sehemu wanasema tuwe makini na jinsi tunavooga ili kuepuka huu ugonjwa..
KIVIP???

Ni hivi baada ya shuguli nzito zenye kuchosha mwili wengi wetu huamua kuoga ili kupooza mwili na kupunguza uchovu.
SO wakati mtu ukiwa umechoka na kazi mfano kukimbia au kazi ngumu kawaida damu huwa inakuwa speed sana na pia joto lake huwa juu sana ............Inashauriwa kuwa baada ya hizo kazi kabla ya kuoga ni vzr mtu upumzike kidogo ili mwili utulie ndio uende kuoga
Na pia wakati wa kuoga wengi wetu huanza kujimwagia maji kichwani kitu ambacho ni hatari zaidi hasahasa kam hukupumzika kwani ukifanya hivyo mishipa midogo ya damu kichwani hupasuka kwa sababu ya kuwa ni kama unai force damu ipoe ghalfa..Ni vizuri wakati wa kuoga jimwagie maji katika sehemu nyingine kichwani ili kuuweka mwili katika conditioned state then ndio uendelee kuosha kichwa
 
KARDINALI!

What a good expanation! and very usefully... Imeeleweka vema sana.

Just a simple inquiry... Vipi mchango wa emotional factors, psychological au physical shocks ... nafikiri hazina uhusiano wa moja kwa moja labda kupitia risk factor ulizotaja au?
Vyakula vyenye Cholestrol ndio chanzo, kuna forensic autopsy ilifanyika mwaka 1960, kuangalia maiti 300 Uganda na 300 USA (same age na gender) out of 300 in Uganda mmoja tu ndo alikuwa anaonekana alikuwa na matatizo ya moyo kutokana na cholestral ila out of 300 in USA 164 walikuwa wamefariki kutokana na uwepo wa cholestral kwenye moyo. Waka ongeza idadi ya maiti kwa uganda mpaka nadhani 800 issue ikawa ile ile........conclusion ikaonekana ni diet ya watu wa USA inakuwa na vyakula vyenye cholestral nyingi kwa vile ni animal based diets from breakfast to dinner wakat Uganda ni plant based diet from morning to evening and rarely nyama......nadhani emotional, psychological factors na physical shocks ni triggers tu sio causes.........kumbuka accumulation ya cholestral kwenye mishipa inaanza tangu ukiwa mdogo and slowly inaongezeka.....
 
Kiharusi ni ugonjwa mkali wa mishipa ya damu kwenye ubongo unaohatarisha vibaya afya na maisha ya binadamu. Takwimu husika zimeonesha kuwa, kila mwaka watu milioni 1.5 wanapatwa na ugonjwa huo nchini China, na nusu kati yao wanakufa kutokana na ugonjwa huo, na watu wengi wanaopona wanapoteza uwezo wa kufanya kazi kwa viwango tofauti. Hali hiyo imesababisha mzigo mkubwa kwa familia na jamii.

Mzee Wang Qinmei mwenye umri wa miaka 65 ana afya njema na hakuwahi kupatwa magonjwa makubwa. siku moja asubuhi katika majira ya mchipuko mwaka huu, alienda sokoni kwa baisikeli kununua chakula kama kawaida, ghafla alijisikia kizunguzungu na akapoteza fahamu. Baada ya muda mfupi, alipata fahamu na kuomba msaada kutoka kwa wapita njia na akapelekwa hospitali.

Katika chumba cha huduma ya kwanza, daktari alithibitisha haraka ugonjwa uliompata mzee Wang. Daktari wa upasuaji wa mishipa ya damu kwenye ubongo katika hospitali ya 301 ya jeshi la ukombozi wa watu wa China Bw. Wang Jun alisema:

"baada ya kumfanyia upimaji wa CTA, tuligundua sehemu moja nyembamba katika mishipa mikubwa ya damu iliyoko shingoni, na asilimia 90 ya sehemu hiyo ya mishipa ya damu imezibwa. Hali hiyo ni ya hatari sana."

Tatizo la wembamba wa mishipa ya damu ya shingoni ni chanzo kikubwa cha ugonjwa wa kiharusi wa aina ya kukosa damu kwenye ubongo. Asilimia 60 ya wagonjwa wa ugonjwa huo wanatokana na tatizo la kuzibwa kwa mishipa ya damu ya shingoni. Pamoja na kuzidi kuziba kwa mishipa ya damu, dalili za ugonjwa huo zinaonekana kidhahiri na wazi zaidi, hatimaye zinasababisha kiharusi kibaya. Kwa kuwa asilimia 90 ya mishipa ya damu ya shingoni inakuwa imeziba, hali hiyo inaufanya ubongo ukose damu na oksijen, na dalili mbalimbali za ugonjwa huo zote zinasababishwa na tatizo hilo.

Mbali na kiharusi cha kukosa damu kwenye ubongo, aina nyingine ni kiharusi cha kutokwa damu kwenye ubongo. Chanzo kikubwa ni shinikizo kubwa la damu linalosababisha mishipa midogo ya damu kwenye ubongo ivimbe na kupasuka.

Kwanza, ugonjwa wa kiharusi unahusiana na umri na jinsia. Kwa kawaida, watu wenye umri wa zaidi ya miaka 55 wana hatari kubwa zaidi ya kupatwa na kiharusi, na hatari ya kupatwa ugonjwa huo kwa wanaume ni asilimia 50 zaidi kuliko wanawake. Ya pili, ugonjwa huo ni wa kurithi. Aidha, magonjwa ya shinikizo kubwa la damu, kisukari, tatizo la moyo, tatizo la kuwa na uzito kupita kiasi, kuvuta sigara na kunywa pombe zote zinaweza kusababisha kiharusi.

Kwa kawaida, kuna dalili kadhaa zinaonekana kabla ya kutokea kwa kiharusi. Mkurugenzi wa idara ya upasuaji wa mishipa ya damu katika hospitali ya 301 ya jeshi la China Bw. Li Baomin alisema:

"kabla ya kutokea kwa kiharusi, mgonjwa hujisikia kizunguzungu, mwasho kwenye mikono na miguu, na kutoona vizuri. Baada ya muda, hisia hiyo itaisha au itarejea tena. Kama una dalili hizo, ni lazima uchukue tahadhari."

Bw. Li alisema, kama dalili hizo zinatokea mara kwa mara katika siku moja au mbili, na pia una shinikizo kubwa la damu au ugonjwa wa kisukari au ugonjwa wa kurithi, unapaswa kwenda hospitali mara moja kufanyiwa uchuguzi. Hivi sasa, ugonjwa wa kiharisi unaweza kuthibitishwa mapema na kwa usahihi.

Basi kama wagonjwa wakipatwa na kiharusi nyumbani au kwenye sehemu za hadhara tutafanyaje? Watalaamu wanaeleza kuwa, kiharusi kinatokea ghafla, wagonjwa wanaweza kupoteza fahamu, kuanguka, kutikisika au kushindwa kuongea. Watu huchanganyikiwa wakati hali hiyo ikitokea, na hata wanakuwa hawajui la kufanya. kwa kawaida, watawaamsha hata kuwatingisha wagonjwa. Vitendo hivyo vinaweza kuwadhuru wagonjwa hao, hata vinafanya hali yao iwe mbaya zaidi.

Kama mtu akipatwa kiharusi, kwanza jamaa zake wasihangaike, bali wanatakiwa kumtuliza mgonjwa, na ni afadhali wasimwamshe alipo, lakini wanatakiwa kumwita daktari mara moja. na ni bora walegeze nguo za ndani za mgonjwa, hatua hiyo inamsaidia mgonjwa kupumua bila tatizo. Kama mgonjwa akitikisika, hali hiyo ni mbaya, ni lazima wamshtue. Kwa kuwa wakati huo, mgonjwa anaweza kujiuma ulimi, hivyo ni afadhari wazibe mdomo wa mgonjwa kwa nguo. Wagonjwa wengi wa kiharusi wanatapika, ili kuzuia wagonjwa kama hao wasijizibie koo, ni bora kuwalaza shingo upande. Kama matapishi yakibaki mdomoni, ni lazima yatolewe mdomoni kwa vijiti, na kama mgonjwa huyo ana meno bandia, inapaswa kuyatoa ili yasije yakaingia kooni.

Zamani ugonjwa wa kiharusi ulikuwa unatibiwa kwa upasuaji, hivi sasa unatibiwa kwa matibabu yenye usalama, ufanisi na rahisi zaidi. Matibabu hayo ni kuingiza mrija mdogo kwenye mshipa mkubwa wa damu wa pajani na kuifikisha kwenye sehemu yenye tatizo mwilini na kutibu. Kwa kuwa kipenyo cha mshipa mkubwa wa damu ni milimita 15 hivi, na kipenyo cha mirija ni milimita 2 tu, hivyo mrija huo unaweza kupita kwenye mishipa ya damu bila tatizo. Mbali na hayo, kutokana na kuwa hakuna nevu za hisia ndani ya mishipa ya damu, basi wagonjwa hawasikii maumivu.

Mzee Wang Qinmei alitibiwa kwa matibabu hayo. Daktari aliweka chombo maalum cha kupanua mshipa wa damu ndani ya sehemu ya mshipa mkubwa wa damu wa shingoni kwake iliyozibwa kwa kutumia mirija. Mzee Wang alisema:

"Baada ya kuwekewa chombo cha kupanua mshipa wa damu, nilisikia damu inapita vizuri, ghafla hisia ya kizunguzungu iliondoka mara moja."

Matibabu hayo hayahitaji kuwapa wagonjwa nusukaputi ya mwili mzima. Wagonjwa wanaweza kutibiwa wakiwa na fahamu vizuri. Pia kwa kuwa matibabu hayo yanaleta majaraha madogo tu, basi wagonjwa wanaweza kutembea saa 24 tu baada ya matibabu. Hivi sasa, wagonjwa wengi zaidi wa kiharusi wanachagua matibabu hayo.

© China Radio International.CRI. All Rights Reserved.
16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040

china radio international
Swala la kurithi nalitilia shaka, magonjwa mengi yanasababishwa na life style tuliyo nayo especially chakula na sii genetics........
 
Wakati wa sherehe msichana mmoja kwa mashaka na alianguka. Aliombwa aitiwe ambulance, lakini yeye alimwakikishia kila mtu kuwa kila kitu ni sawa na kwamba yeye kajigonga kwa sababu tu ya viatu vipya.
Kwa vile alionekana kuwa na wasiwasi na kuwa anatetemeka kidogo, walimsaidia kumfuta na kumpatia maji ya kunywa. Siku yote baadae msichana huyu aliendelea vizuri na kuonenekana kidogo mwenye furaha. Baadae mume wa msichana amlipigia simu kila kila mtu na kusema kuwa mkewe alikuwa kapelekwa hospitali na Saa 23:00 alifariki. Katika sherehe ile yule msichana alishikwa na kiharusi (acute ischemic stroke)
Kama watu waliokuwa katika sherehe ile wangelijua jinsi ya kuangalia ishara za kiharusi,yule msichana angaliweza kuwa bado anaishi.
Baadhi ya watu baada ya kupata ugonjwa huu wa kiharusi hawafi hapo hapo. mara nyingi wanakutwa katika hali ambayo wanaweza saidiwa au hata kujisaidia wenyewe.
Huu hapa ni ushauri wa kufanya ili kumsaidia mtu nayepatwa ka kiharusi.

Daktari husema kwamba kama ni ndani ya saa 3 tangu mwathirika wa kiharusi hapate hizo dalili, matokeo ya mashambulizi yanaweza kuondolewa. Kitu cha muhimu ni kugundua na kutambua kiharusi na kuanza matibabu ndani ya masaa ya kwanza 3 - ambayo kwa hakika si rahisi wengi wetu.

Kutambua kiharusi: Kuna njia 4 za kutambua kiharusi.

- Uliza mtu kutabasamu (atashindwa kutabasamu)

- Uliza kusema sentensi rahisi (kwa mfano "Leo hali ya hewa ni nzuri")

- Mwulize kuinua mikono miwili (hawawezi au nusu tu na uwezo wa kuchukua)

- Mwulize kuweka nje ulimi (kama ulimi umeeleka upande mwingine an haurudi sawa hiyo pia ni dalili ya kiharusi.)

Kama matatizo haya yanajitokeza, na hata kama ni dalili moja kati ya hizo hapo juuni vema kwa haraka zaidi kumpeleka mgonjwa hospitalini, au kama kuna uwezekano ita ambulance.

ukituma ujumbe huu katika sehemu au kwa watu kumi unaweza okoa maisha ya watanzania wengi.
Nmejifunza kitu kwa hizi pathophysiology
 
Chief nikukumbushe tu tuna vitu viwili we have stroke na we have transient ischaemic attack..hivi vitu viwili vnatofautishwa na how long the attack lasts for....
 
Chief nikukumbushe tu tuna vitu viwili we have stroke na we have transient ischaemic attack..hivi vitu viwili vnatofautishwa na how long the attack lasts for....
Tupe shule mkuu, hilo somo muhimu sana
 
Jaribu hii ponda mizizi au magome ya mlonge mfunge kwa bandeji usikaze kwa dk 10-15 akihisi joto/Moto mfungue ondoa hiyo dawa asubiri kwa siku 3 uone maendeleo yake Kisha Leta mrejesho hapa jf
Mkuu Magome ya mlonge hayawezi kumsaidia kupona maradhi yake. maradhi yake yanasababishwa kwenye ubongo mishipa ya fahamu kwenye ubongo haina mawasiliano na mishipa ya kiganja cha mkono.

Ndio maana mkono wa kiganja chake kimepooza wewe hapo hujatoa tiba umetoa dawa ya kupunguza maumivu sio tiba hiyo dawa uliyo toa.

Ukitaka kumtibia huyu mgonjwa mtibie kwenye ubongo wake akipona huko kwenye ubongo ndio atakapo weza kupona mkono wake ukafanya kazi vizuri. Usikopi na kuweka hapa dawa wakati hujuwi hiyo dawa inatibu maradhi gani?
 
Habari wanaJF, naomba ushauri na maelekezo kidogo kuhusu hiyo hali imemkuta baba

Amepata stroke upande wa kulia tangu Jumamosi na amewahi hospitali hadi sasa wame-control BP lakini hawampi mazoezi japo stroke yenyewe imempiga mkono wa kulia na mguu kukaa hadi akalishwe, mguu wake na mkono wake bado unahisi kwa kiasi ambako anaweza kukunja mguu na kumtingsha mkono na akiguswa anasikia

Naomba ushauri nifanye nini zaidi ile aweze kurudi katika hali yake

Hatua niliyowaza kumuhamisha hospitali kumpeleka hospitali yenye wataalamu wa mazoezi. Please niongezee mawazo.

Niko kituo cha x cha afya (w) Rombo
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom