Ugonjwa wa kiharusi/ kupooza (stroke): Kinga, tiba na jinsi ya kukabiliana na maradhi haya

KIHARUSI au ‘stroke’ ni hali inayotokea baada ya sehemu ya ubongo kushindwa kufanya kazi yake kwa sababu ya kukosa kupata mzunguko wa damu inayoelekea kichwani, hivyo chembe hai za ubongo kufa, baada ya kukosa hewa safi yaani ‘oxygen’ na virutubisho vingine vilivyo kwenye damu.

Sehemu hiyo ya ubongo ikiharibika, inasababisha kazi zilizokuwa zinafanywa na sehemu hiyo kutokufanyika. Kiharusi ni hali ya dharura inayohitaji matibabu ya haraka na ya umakini.

Kuna aina tatu za kiharusi:

KIHARUSI CHA KUKOSA HEWA

Kiharusi cha kukosa hewa kwenye ubongo yaani ‘Ischemic stroke.’ Hiyo inatokea baada ya mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye ubongo au mishipa ya damu ya ubongo kuziba au kusinyaa sana.

Hivyo basi, inasababisha sehemu iliyopo mbele ya huo mzibo ‘blockage’ kukosa hewa safi ya oksijeni na virutubisho vingine na kusababisha seli hizo kufa. Kama sehemu hiyo iliyoharibika ilikuwa inashughulikia misuli fulani, basi misuli hiyo utaona imeathirika, kama ni sehemu inayohusika na kuongea, basi mgonjwa atashindwa kuongea n.k.

Aina hiyo ya kiharusi, imegawanyika katika sehemu kuu mbili. ‘Thrombotic Stroke; Hiyo husababishwa na mzibo uliokuwepo ndani ya mshipa wa damu safi (artery), ambayo inalisha ubongo na kutengeneza ‘clots’ zinazoitwa ‘thrombosis’ zinazoweza kuwa katika mishipa mikubwa au midogo.

Mara nyingi, wagonjwa wenye ‘Atherosclerosis’ huwa wanapata kiharusi kwa njia hiyo.

KIHARUSI CHA MZIBO
Aina hiyo ya pili inaitwa ‘Embolic stroke.’ Hiyo inatokana na mzibo unaosababishwa na ‘clot’ ambayo hutokea sehemu nyingine ya mwili, mbali na ubongo na kuingia katika mishipa ya damu ya ubongo na kwenda kuziba ndani ya ubongo.

Mfano mtu mwenye matatizo ya moyo, damu inaweza kuganda kwenye moyo na baadae damu iliyoganda, ikasafirishwa kwenda kwenye ubongo na kiziba huko. Mtu mwenye ‘Atrial Fibrillation’ huwa ana nafasi ya kutokewa na hali hiyo.

KIHARUSI CHA KUPASUKA MISHIPA

Kiharusi aina hii, inatokana na mishipa ya damu ya ubongo kupasuka na damu kuvilia kwenye ubongo. Kitaalamu inaitwa ‘Hemorrhagic stroke.’ Matatizo makubwa yanayosababisha hali hii, kwanza ni inayoitwa kitaalamu Aneurysms’ na pili, ni mishipa ya damu kuzeeka.

Mingine na wengine ni ‘Arteriovenous Malformation’ (AVM),AVM ni matatizo ya kuzaliwa na sio kurithi. Mishipa ya damu safi na damu chafu inaungana bila ya kuwepo mishipa midogo midogo ya ‘capillaries’ kati yao.

Pia husababisha kuta za mishipa hiyo kuwa hafifu na endapo kutatokea msukumo mkubwa wa damu isivyo kawaida, basi mishipa hiyo huwa rahisi kupasuka na damu kuvilia ndani ya ubongo.

Aina hii ya pili ya kiharusi huwatokea mara nyingi watu wenye shinikizo la damu.

KIHARUSI CHA MUDA MFUPI

Aina ya tatu ni ‘Transiet Ischemic Attack (TIA).” Hii inafanana kidogo na ile aina ya kwanza, ila kwenye hii, dalili na madhara ya kiharusi hayakai muda mrefu.

Mtu anaweza kupata dalili hizi kwa muda wa dakika moja hadi tano hivi, na mara nyingi dalili hizo huwa zinapotea katika masaa 24.
Katika aina hii ya kiharusi, mtu huwa hapati madhara ya kudumu, madhara huwa ni ya muda mfupi.

Kikubwa cha kufanya ni kuzuia hali hiyo isitokee tena, kwani inaweza kurudia na kusababisha kiharusi kikubwa. Kitaalamu, hali hiyo ya TIA inaitwa ‘Mini-Stroke’

DALILI ZA KIRAHUSI
Dalili kuu za kiharusi ni kama zifuatazo;

• Kupata ganzi au udhaifu ambao mara nyingi unaanza ghafla. Mara nyingi huwa unatokea upande mmoja wa mwili, yaani kushoto au kulia. Mara nyingi, husababisha upande mmoja wa uso kufa ganzi au kuwa dhaifu.

• Kuchanganyikiwa na kushindwa kuongea, hali inayotokea ghafla.

• Kupoteza uwezo wa kuona. Kitu kimoja, kinaonekana kama vile vipo viwili, ukungu, kupoteza nguvu ya kuona inayoweza kutokea kwenye jicho moja au yote mawili.

• Ghafla, kichwa kinauma sana, bila ya kuwa sababu maalumu na mara nyingine huambatana na kusikia kichefuchefu au mtu anatapika.

• Kushindwa kutembea ghafla, kushindwa kusimama na kusikia kizunguzungu.

• Wakati mwingine mtu anapoteza fahamu.

NAMNA YA KUZUIA KIHARUSI

• Kuangalia au kupima msukumo wa damu yaani, ‘Blood Pressure’

Ni muhimu sana na hasa kwa watu wenye matatizo hayo, kuhakikisha misukumo yao ya damu inakuwa katika hali ya kawaida kila mara.

Msukumo wa damu kuwa juu, una madhara mengi, ikiwemo hilo la kupasuka mishipa ya damu ya kwenye ubongo na kusababisha kiharusi.

• Kuwa na tabia ya kupima wingi wa helemu ‘ Cholosterol levels’

Ni muhimu sana, kila mtu akawa na tabia ya kupima wingi wa lehemu ili kujua aina gani ya lehemu ambayo kwako ipo juu au chini.

Wingi wa lehemu mbaya yaani ‘bad cholesterol’ unasababisha lehemu hiyo kujishikiza au kukaa katika mishipa ya mtu ya damu na kusababisha kupungua tundu la kupitisha damu ndani ya mshipa wa damu.

Wakati mwingine, mafuta hayo huwa yananyofoka kutoka katika kuta za mishipa hiyo ya damu na kwenda kunasa katika sehemu nyingine ya mwili, kwa mfano katika ubongo na huleta madhara ya kiharusi. Hiyo ina maana, itazuia damu kupita kabisa au kupita kidogo sana

• Kuzuia uvutaji sigara na unywaji wa pombe uliopitiliza.

Utafiti mwingi umefanyika na kugundua madhara makubwa ya sigara. Uvutaji sigara na unywaji pombe uliopitiliza, husababisha kiharusi. Kemikali zilizokuwepo kwenye sigara zina uwezo mkubwa wa kuharibu kuta za mishipa ya damu.

Kibaya zaidi ni kwamba, kama mvutaji wa sigara ana mwili mnene uliopitiliza, ana ugonjwa wa shinikizo la damu au kisukari, inamuweka katika wakati mbaya zaidi.

Kwa wale wanaotumia dawa za kulevya, kwa mfano aina ya Herroin, wana hatari kubwa ya kupata kiharusi, kwani utegemezi wa kilevi hicho huzaa madhara makubwa katika moyo wake na kuharibu mfumo mzima wa msukumo wa damu, hali inayotishia maradhi ya kiharusi.

• Kufanya mazoezi; Mazoezi ni muhimu sana kwa afya ya mwanadamu. Mazoezi yanaweza kuzuia nafasi ya mtu kupata ugonjwa wa shinikizo la damu na kisukari.

• Kupunguza msongo wa mawazo; Ni muhimu sana kupunguza msongo wa mawazo hasa kwa mtu mwenye ugonjwa wa shinikizo la damu na kisukari.

Mtu anapokuwa kwenye msongo wa mawazo mwili wake unatengeneza homoni zinazosababisha kuongezeka kwa msukumo wa damu, pia kutengeneza homoni zinazosababisha mwili kutoa sukari katika ini ambako ilihifadhiwa na kuiingiza kwenye damu.

Hivyo, iwapo mtu ana ugonjwa wa kisukari, hapo ndio inaleta shida, maana sukari yake kwenye damu, itakuwa juu wakati yeye anatumia dawa. Hivyo, hali hiyo ya sukari kuwa juu mwilini anaweza asiitambue.

• Jifunze au uwe na tabia ya kula vyakula vyenye mafuta kidogo. Vyakula vyenye mafuta kwa wingi, husababisha mwili kuwa na mafuta mengi, hali ambayo si nzuri kiafya na inaweza kusababishia magonjwa ya moyo na hatimaye kiharusi.

• Kula vyakula vyenye chumvi kidogo. Asilimia kubwa ya chumvi inayotumiwa, ina madini ya ‘sodium.’ Hiyo ni kemikali ambayo ipo zaidi katika majimaji yaliyomo mwilini mwetu, hasa nje ya chembehai zilipo.

Mwili unakuwa na kiwango maalumu cha kemikali hiyo na iwepo wa kemikali hiyo kwa wingi, unasababisha kuongezeka kwa msukomo wa damu.

Hivyo basi, tukila chumvi kidogo maana yake tunaingiza hiyo ‘sodium’
kidogo na kutunusuru kwa kupanda kwa msukumo wa damu na maana yake kutupunguzia athari za kupata kiharusi.

Kwa ujumla, ni vizuri kubadili mfumo wa maisha tunayoishi ili kujinusuru
na kupata kiharusi.
Tupatie tiba yake hayo maradhi ya Kiharusi Mkuu?
 
DAWA YA STROKE AU KIHARUSI
By Salim Mikdad

KIHARUSI (STROKE DISEASE)

Maradhi ya KIHARUSI(stroke disease) ni miongoni mwa maradhi ambayo yanasababisha watu wengi kupatwa ulemavu na kuharibikiwa na mambo mengi katika maisha.



kuna KIHARUSI ambayo husababishwa na majini aina ya UMMU SUBIANI,

Ambayo hii hutoka na mtu KUANGUKA CHOONI.

Kisha kuna kiharusi inayo sababishwa na DAMU kutokufika kwenye UBONGO ipasavyo ambapo hali huii hupelekea UBONGO kutokupata OXYGEN ipasavyo au nutrients ambazo zikikosekana husababisha seli za UBONGO kufa .

Ama kuhusu Tiba ya ANAE ANGUKA CHOONI huitajika KISOMO na MADAWA ya kula pamoja naya kufusha

TIBA YA UGONJWA WA KIHARUSI



1)SIKI YA MNAZI

2) DAMU YA NJIWA

3) MAZIWA YA MBUZI

Kisha CHANGANYA pamoja, na baada ya kuchanganya uwe unampaka mgonjwa mwili wote kwa SIKU 19 mpaka SIKU 27 ambapo ni ASUBUHI NA USIKU.

kisha dawa ya kunywa ni

KAMUN AS WAD

HABAT SAUDA za UNGA,

unachanganya kisha unachemsha KIJIKO KIKUBWA halafu unaweka maji Vikombe vikubwa VITATU yachemke mpaka yabaki vikombe 2 kisha unakunywa asubuhi na usiku siku hizo hizo.
 
Hata kama tunaendelea kupuuzia tiba hiz asilia tukumbuke kama ndoo mpango mzima ,,, mm ckujui ww ndoo wajitambua lkn tiba hii ni zaid ya tiba karibu tuungane pamoja asanten na majukum mema ya kaz zenu
 
Tiba ya huo ugonjwa wa Kiharusi ni ngumu kutibika .

Kiharusi
ni ugonjwa mkali wa mishipa ya damu kwenye ubongo unaohatarisha vibaya afya na maisha ya binadamu. Takwimu husika zimeonesha kuwa, kila mwaka watu milioni 1.5 wanapatwa na ugonjwa huo nchini China, na nusu kati yao wanakufa kutokana na ugonjwa huo, na watu wengi wanaopona wanapoteza uwezo wa kufanya kazi kwa viwango tofauti. Hali hiyo imesababisha mzigo mkubwa kwa familia na jamii.

Mzee Wang Qinmei mwenye umri wa miaka 65 ana afya njema na hakuwahi kupatwa magonjwa makubwa. siku moja asubuhi katika majira ya mchipuko mwaka huu, alienda sokoni kwa baisikeli kununua chakula kama kawaida, ghafla alijisikia kizunguzungu na akapoteza fahamu. Baada ya muda mfupi, alipata fahamu na kuomba msaada kutoka kwa wapita njia na akapelekwa hospitali.

Katika chumba cha huduma ya kwanza, daktari alithibitisha haraka ugonjwa uliompata mzee Wang. Daktari wa upasuaji wa mishipa ya damu kwenye ubongo katika hospitali ya 301 ya jeshi la ukombozi wa watu wa China Bw. Wang Jun alisema:

"baada ya kumfanyia upimaji wa CTA, tuligundua sehemu moja nyembamba katika mishipa mikubwa ya damu iliyoko shingoni, na asilimia 90 ya sehemu hiyo ya mishipa ya damu imezibwa. Hali hiyo ni ya hatari sana."

Tatizo la wembamba wa mishipa ya damu ya shingoni ni chanzo kikubwa cha ugonjwa wa kiharusi wa aina ya kukosa damu kwenye ubongo. Asilimia 60 ya wagonjwa wa ugonjwa huo wanatokana na tatizo la kuzibwa kwa mishipa ya damu ya shingoni. Pamoja na kuzidi kuziba kwa mishipa ya damu, dalili za ugonjwa huo zinaonekana kidhahiri na wazi zaidi, hatimaye zinasababisha kiharusi kibaya. Kwa kuwa asilimia 90 ya mishipa ya damu ya shingoni inakuwa imeziba, hali hiyo inaufanya ubongo ukose damu na oksijen, na dalili mbalimbali za ugonjwa huo zote zinasababishwa na tatizo hilo.

Mbali na kiharusi cha kukosa damu kwenye ubongo, aina nyingine ni kiharusi cha kutokwa damu kwenye ubongo. Chanzo kikubwa ni shinikizo kubwa la damu linalosababisha mishipa midogo ya damu kwenye ubongo ivimbe na kupasuka.

Kwanza, ugonjwa wa kiharusi unahusiana na umri na jinsia. Kwa kawaida, watu wenye umri wa zaidi ya miaka 55 wana hatari kubwa zaidi ya kupatwa na kiharusi, na hatari ya kupatwa ugonjwa huo kwa wanaume ni asilimia 50 zaidi kuliko wanawake. Ya pili, ugonjwa huo ni wa kurithi. Aidha, magonjwa ya shinikizo kubwa la damu, kisukari, tatizo la moyo, tatizo la kuwa na uzito kupita kiasi, kuvuta sigara na kunywa pombe zote zinaweza kusababisha kiharusi.

Kwa kawaida, kuna dalili kadhaa zinaonekana kabla ya kutokea kwa kiharusi. Mkurugenzi wa idara ya upasuaji wa mishipa ya damu katika hospitali ya 301 ya jeshi la China Bw. Li Baomin alisema:

"kabla ya kutokea kwa kiharusi, mgonjwa hujisikia kizunguzungu, mwasho kwenye mikono na miguu, na kutoona vizuri. Baada ya muda, hisia hiyo itaisha au itarejea tena. Kama una dalili hizo, ni lazima uchukue tahadhari."

Bw. Li alisema, kama dalili hizo zinatokea mara kwa mara katika siku moja au mbili, na pia una shinikizo kubwa la damu au ugonjwa wa kisukari au ugonjwa wa kurithi, unapaswa kwenda hospitali mara moja kufanyiwa uchuguzi. Hivi sasa, ugonjwa wa kiharisi unaweza kuthibitishwa mapema na kwa usahihi.

Basi kama wagonjwa wakipatwa na kiharusi nyumbani au kwenye sehemu za hadhara tutafanyaje? Watalaamu wanaeleza kuwa, kiharusi kinatokea ghafla, wagonjwa wanaweza kupoteza fahamu, kuanguka, kutikisika au kushindwa kuongea. Watu huchanganyikiwa wakati hali hiyo ikitokea, na hata wanakuwa hawajui la kufanya. kwa kawaida, watawaamsha hata kuwatingisha wagonjwa. Vitendo hivyo vinaweza kuwadhuru wagonjwa hao, hata vinafanya hali yao iwe mbaya zaidi.

Kama mtu akipatwa kiharusi, kwanza jamaa zake wasihangaike, bali wanatakiwa kumtuliza mgonjwa, na ni afadhali wasimwamshe alipo, lakini wanatakiwa kumwita daktari mara moja. na ni bora walegeze nguo za ndani za mgonjwa, hatua hiyo inamsaidia mgonjwa kupumua bila tatizo. Kama mgonjwa akitikisika, hali hiyo ni mbaya, ni lazima wamshtue. Kwa kuwa wakati huo, mgonjwa anaweza kujiuma ulimi, hivyo ni afadhari wazibe mdomo wa mgonjwa kwa nguo. Wagonjwa wengi wa kiharusi wanatapika, ili kuzuia wagonjwa kama hao wasijizibie koo, ni bora kuwalaza shingo upande. Kama matapishi yakibaki mdomoni, ni lazima yatolewe mdomoni kwa vijiti, na kama mgonjwa huyo ana meno bandia, inapaswa kuyatoa ili yasije yakaingia kooni.

Zamani ugonjwa wa kiharusi ulikuwa unatibiwa kwa upasuaji, hivi sasa unatibiwa kwa matibabu yenye usalama, ufanisi na rahisi zaidi. Matibabu hayo ni kuingiza mrija mdogo kwenye mshipa mkubwa wa damu wa pajani na kuifikisha kwenye sehemu yenye tatizo mwilini na kutibu. Kwa kuwa kipenyo cha mshipa mkubwa wa damu ni milimita 15 hivi, na kipenyo cha mirija ni milimita 2 tu, hivyo mrija huo unaweza kupita kwenye mishipa ya damu bila tatizo. Mbali na hayo, kutokana na kuwa hakuna nevu za hisia ndani ya mishipa ya damu, basi wagonjwa hawasikii maumivu.

Mzee Wang Qinmei alitibiwa kwa matibabu hayo. Daktari aliweka chombo maalum cha kupanua mshipa wa damu ndani ya sehemu ya mshipa mkubwa wa damu wa shingoni kwake iliyozibwa kwa kutumia mirija. Mzee Wang alisema:

"Baada ya kuwekewa chombo cha kupanua mshipa wa damu, nilisikia damu inapita vizuri, ghafla hisia ya kizunguzungu iliondoka mara moja."

Matibabu hayo hayahitaji kuwapa wagonjwa nusukaputi ya mwili mzima. Wagonjwa wanaweza kutibiwa wakiwa na fahamu vizuri. Pia kwa kuwa matibabu hayo yanaleta majaraha madogo tu, basi wagonjwa wanaweza kutembea saa 24 tu baada ya matibabu. Hivi sasa, wagonjwa wengi zaidi wa kiharusi wanachagua matibabu hayo.





0905.jpg
Umefahamisha vzr sana
 
DAWA YA STROKE AU KIHARUSI
By Salim Mikdad

KIHARUSI (STROKE DISEASE)

Maradhi ya KIHARUSI(stroke disease) ni miongoni mwa maradhi ambayo yanasababisha watu wengi kupatwa ulemavu na kuharibikiwa na mambo mengi katika maisha.



kuna KIHARUSI ambayo husababishwa na majini aina ya UMMU SUBIANI,

Ambayo hii hutoka na mtu KUANGUKA CHOONI.

Kisha kuna kiharusi inayo sababishwa na DAMU kutokufika kwenye UBONGO ipasavyo ambapo hali huii hupelekea UBONGO kutokupata OXYGEN ipasavyo au nutrients ambazo zikikosekana husababisha seli za UBONGO kufa .

Ama kuhusu Tiba ya ANAE ANGUKA CHOONI huitajika KISOMO na MADAWA ya kula pamoja naya kufusha

TIBA YA UGONJWA WA KIHARUSI



1)SIKI YA MNAZI

2) DAMU YA NJIWA

3) MAZIWA YA MBUZI

Kisha CHANGANYA pamoja, na baada ya kuchanganya uwe unampaka mgonjwa mwili wote kwa SIKU 19 mpaka SIKU 27 ambapo ni ASUBUHI NA USIKU.

kisha dawa ya kunywa ni

KAMUN AS WAD

HABAT SAUDA za UNGA,

unachanganya kisha unachemsha KIJIKO KIKUBWA halafu unaweka maji Vikombe vikubwa VITATU yachemke mpaka yabaki vikombe 2 kisha unakunywa asubuhi na usiku siku hizo hizo.
Asante kwa dawa
 
kiharusi???to The best of my KNOWLADGE harusi hushangiliwa kwa kupungiwa mikono,.na wengine hunyanyua miguu...wagonjwa ni wengi,.....
Siji kusahau siku niliyochapia kama hivi mbele ya watu hakika ilikuwa ni dhahama..
 
Stroke(kuharusi)
Ni hali ya ubongo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla, kwa sekunde mpaka dakika au Zaidi kutokana na damu kushindwa kufika sehemu husika za ubongo. Amabapo sehemu ya ubongo iliyo athirika haiwezi kufanyta kazi vizuri sababu ya kukosa mzunguko wa damu. Hali hii husababisha miguu,mdomo na uwezo wa kuona kupungua au hata kufa.
Chanzo:
1. Shinikizo la juu la damu
Shinikizo la juu ka damu(Hypertension) ni hatari sana katika kusababisha stroke sababu msukumo wa kasi katika vishipa vya damu katika ubongo hufanya vishipa hivyo kupasuka na damu kuenea katika ubongo hivo kusababisha kiharusi
2. Kiwango kikubwa cha rehemu(lipids)
Mtu mwenye mafuta mengi kwenye nishipa ya damu anakuwa katika hatari kubwa ya kupata stroke sababu mafuta hayo huziba mishipa isiweze kupeleka damu katika ubongo hivo husababisha stroke
3. uvutaji wa sigara
uvutaji wa sigara husababisha shinikizo la damu, kupungua kwa kiwango cha mazoezi hufanya damu kuwa nzito pia husabaisha kuganda na hivo kuongeza hatari ya kupata stroke
Jinsi ya kuepuka stroke
Acha uvutaji wa sigara
Fanya mazoezi mara kwa mara
Kula mlo bora
Kwa wanaosumbuliwa na stroke green world ina products za kumaliza tatizo lako
Green world chitosan capsule
Green world lipid care tea
Green world super CQ-10
Green world deep sea fish oil
Green world Gingko biloba
Green world garlic oil
Green world super nutrition,


Phone no, 0713…871599



attached pictures below ,,,
View attachment 383890
Asante kwa kutujulisha dawa
 
Habari wana JF.

Mdogo wangu mwenye umri wa miaka 24 anashida, ni mwezi wa pili sasa kigacha cha mkono wa kulia hakifanyi kazi, kimepooza. Kwa sasa imepelekea kushindwa kushika kalamu wala kitu chochote.

Naomba msaada wa kimawazo, sijui anaumwa nini, tumeenda hospital kadhaa wanampiga x-ray wanasema hakuna shida. Sasa labla sijui ni daktari gani mtaalamu wa magonjwa ya aina hiyo.

Naomba msaada wa mawazo hata kwa anaejua tiba za asili. Natanguliza shukrani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaribu hii ponda mizizi au magome ya mlonge mfunge kwa bandeji usikaze kwa dk 10-15 akihisi joto/Moto mfungue ondoa hiyo dawa asubiri kwa siku 3 uone maendeleo yake Kisha Leta mrejesho hapa jf
 
Habar wana jf naomba kuulza ugonjwa was kupooza ni nn na ubasababishwa na non,dalil zake n zp, unpimwaje,tiba take na jinsi ya kujizuia
 
Mara nyingi hutokea baada ya kiharusi (stroke). Tiba pamoja na dawa mama cheza (physiotherapist) wana mchango mkubwa sana.
Kuna aina mbili za stroke lakini zote husababisha ukisefu wa oxygen kwenye ubongo.

1. Damu kuganda kwenye mishipa ya damu hivyo kisababisha damu yenye oxygen kutofikia ubongo. Hii mara nyingi hutokea mwili ukiwa na mafuta mengi.

2. Mishipa ya damu kupasuka kutokana na pressure ya damu kuwa juu. Mara nyingi hii husababishwa na shock or enxiety.

Uchunguzi ni kupitia CT scan
 
...mzee mshtuko mkubwa wa ghafla ndo chanzo cha kuupoza. Kuna boss mmoja wa ardhi alikuwa anaishi na binti mdogo sana. Na hakuzaa naye mwisho wa siku yule binti kashika mimba kwingine na na kamtema mzee , mzee kurudi kwa bimkubwa soo kaanza kuumwa mwisho kapooza
 
Habar wana jf naomba kuulza ugonjwa was kupooza ni nn na ubasababishwa na non,dalil zake n zp, unpimwaje,tiba take na jinsi ya kujizuia
Mgonjwa kapooza nini na nini au sehemu gani ya mwili? Maana wadau wanakujibu kuhusu stroke ambayo mara nyingi mtu hupoonza sana upande mmoja wa mwili, lakini pia kuna kupooza miguu peke yake, kupooza mwili wote kasoro kichwa na shingo, kupoona mgoo au mkono mmoja, Nk
 
Back
Top Bottom