Ugonjwa wa kuanguka hovyo wanafunzi

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Matukio ya wanafunzi kupatwa na magonjwa yasiyofahamika ikiwemo kuchekacheka, kushindwa kutembea vizuri na kuanguka hovyo yanaonekana kushamili hapa nchini. Leo vyombo vya habari vimeripoti kizuka kwa ugonjwa wa wanafunzi kukimbia na kuanguka hovyo huko Wilayani Sikonge ulioanza tarehe 18/10/2011na kusababisgha leo Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo kuifunga shule husika ili kuwezesha maombi mazito ya dini zote kufanyika shulen hapo.

Kwa kuwa ugonjwa wa aina hii umekuwa ukizikumba shule nyingi hapa nchini, ni vyema sasa kwa Wizara ya Elimu na ile ya Afya na Ustawi wa Jamii inafanya uchunguzi wa kina kujua vyanzo halisi vya magonjwa kama haya. Ikiwa Serikali itakaa kimya na kuacha wananchi wakiendelea kuamini kuwa ni matukio ya kishirikia, inaweza kuleta madhara makubwa kwa watoto wetu siku za usoni kwani inatokeaje mtu anaweza kuwaloga wanafunzi zaidi ya mia moja kwa wakati mmoja?? Je, ikiwa ilo linawezekana, usalama wa watoto wetu upo wapi huko mashuleni hasa zile shule za bweni (watoto si watakuwa wakichezewa sana usiku na mchana)??
 
Kweli watanzania bado sana, unafunga shule halafu unaitisha maombi, akili yetu iko wapi jamani, huo ni ugonjwa unaitwa hysteria , na unawakumbuka sana watoto wa kike kutokana na stress za shule na famila zao, kwanini watu hawapendi kusoma vitabu na majarida, tubadilke jamani, nyie mnawaza uchawi wenzenu wanakwenda mwezini
 
Back
Top Bottom