Tatizo la Gonjwa la Sukari (Diabets Mellitis): Fahamu chanzo, aina na ushauri wa tiba ya tatizo hili

JamiiForums

Official JF Response
Nov 9, 2006
6,200
4,982
1588679317724.png

Kumekuwepo kilio na maswali mengi ya wadau mbalimbali wakitaka kujua masuala kadhaa kuhusu ugonjwa wa kisukari; tumetengeneza mnakasha huu ili kurahisisha majibu (si yote) kwa wenye uhitaji wa maswali yao.

Zingatia: Ni vema kwenda hospitali kwa tiba ya uhakika, hapa utapata majibu yanayokupa mwanga wa nini cha kufanya.

Case studies, mapendekezo ya tiba, waliopata kutibiwa, madaktari wanaopendekezwa na wadau kwa tiba n.k ndivyo vitawekwa kwenye bandiko la kwanza
===
UFAFANUZI WA KINA KUHUSU UGONJWA HUU
Kisukari ni nini? Kisukari ni ugonjwa unaosababisha glukosi kuzidi kwenye damu (damusuziada) kwa sababu ya ukosefu wa insulini au kongosho kutoa insulini isiyotosheleza mahitaji ya mwili.

Kuna aina ngapi za ugonjwa wa kisukari?
Kuna aina tatu za ugonjwa wa kisukari:

Aina ya kwanza ya kisukari:
Ugonjwa wa kisukari unaosababishwa na kongosho kushindwa kutoa insulini kabisa. Katika ugonjwa kisukari wa aina hii mgonjwa lazima achome sindano ya insulini kila siku kwa sababu kongosho haitoi insulini kabisa.

Aina ya pili ya kisukari:
Ugonjwa wa kisukari unaosababishwa na kongosho kutoa insulini isiyotosheleza mahitaji ya mwili. Aina hii ya kisukari inaweza kutibiwa kwa kutumia vidonge au kwa kupunguza tu kiasi cha sukari kwenye chakula ua kiasi cha chakula chote unachokula.

Kisukari cha ujauzito: Kuna baadhi ya wamama ambao sukari kwenye damu zao hupanda wakati wa uja uzito na huteremka mara wanapojifungua. Baadhi ya wamama hao sukari inaweza isiteremke tena hata baada ya kujifungua na wakabakia wagonjwa kisukari moja kwa moja hasa kama ni wanene kupitiliza na baada ya kujifungua mimba nyingi. ·

Nini tofauti ya aina ya kwanza na ile ya pili ya kisukari?




Dalili


Aina ya kwanza


Aina ya pili
Umri wa kuanza ugonjwa Miaka chini ya 40. Miaka zaidi ya 50.
Muda wa dalili za ugonjwa kabla hajagundulika kuwa na kisukari. Wiki Miezi hadi miaka.
Uzito wa mgonjwa wakati anagulika kisukari Wa kawaida au pungufu Mnene.
Ketoni kwenye mkojo Zipo Hazipo.
Kifo cha haraka hasipotumia insulini. Ndiyo. Hapana.
Matokeotata ya kisukari wakati anagulika kisukari Hakuna. Yapo.
Mtu mwingine mwenye ugonjwa wa kisukari katika familia. Kwa kawaida hayupo Yupo.

Je, Ugonjwa huu unasababishwa na kula sukari nyingi?
La hasha. Kula sukari nyingi sio sababu ya ugonjwa kisukari. Lakini lazima tuseme kwamba kula sukari nyingi si nzuri kwa afya yako kwani utaongeza uzito na kuweza kuathiri uwezo wa mwili wako kujikinga na maradhi tofauti. Hivyo sukari tutumie lakini kwa uangalifu.

Kitu gani husababisha ugonjwa wa kisukari?
- Magonjwa ya ini.
- Unene kupita kiasi.
- Msongo wa mawazo.
- Kurithi kutoka kwa wazazi.
- Kuvuta sigara wakati wa ujauzito.
- Kutumia nyama ilivyofukizwa moshi.
- Kuondolewa kongosho kwa upelesheni.
- Kuharibika kongosho kwa ajali au moto.
- Magonjwa ya kongosho mfano uvimbe kwenye kongosho unaosababishwa na pombe au virusi (mfano: Rubella, mumps, HIV
- Dawa: § Phenytoin. § Thiazide mfano bendrofluazide. § Steroidi mfano prednisolone, dexamethasone n.k.
- Utapia mlo wa mtoto kabla hajazaliwa (intrauterine malnutrition).
- Utumiaji wa maziwa ya ngombe kwa mtoto kabla ya umri wa miezi 3.
- Magonjwa ya yanayotengeneza antibodizi zinazoshambulia mwili (autoimmune disease).

Nini dalili za kisukari na damusuziada?
- Kukonda.
- Kutoona vizuri.
- Kuumwa na kichwa.
- Kuchoka bila ya kufanya kazi.
- Kula sana kwa sababu ya kusikia njaa sana.
- Kunywa maji sana kwa sababu ya kujisikia kiu mara kwa mara.
- Kusikia ganzi, kuchomwachomwa au maumivu kwenye mikono na miguu.
- Kujisaidia haja ndogo mara kwa mara, Mgonjwa hujisaidia zaidi ya mara tatu usiku.

Utafahamuje kama ugonjwa wa kisukari umeutawala vizuri?
Kama huna dalili zozote na unajisikia vizuri. Huamki usiku kujisaidia haja ndogo zaidi ya mara moja. Kama unapima glukozi kwenye damu na unakuta hakuna damusuziada (hyperglycaemia). Glukozi kwenye damu ni sawa ikiwa kati ya miligramu 80-144 kwa kila desilita ya damu (kati ya milimoli 4-8 kwa kila lita ya damu).

Kwa nini uhangaike kuutawala ugonjwa wako wa kisukari?
Utakuwa huna dalili zozote. Utaishi maisha marefu zaidi. Kwa hiyo utaweza kuishi maisha karibu ya kawaida. Mwili utakuwa na nguvu zaidi za kupigana na maambukizo. Utazuia matokeotata (complications) mengi yanyoweza kusababishwa na ugonjwa wa kisukari.

Je, ugonjwa wangu wa kisukari unaweza kupona?
Kwa ujumla, ukishapata ugonjwa wa kisukari utakuwa nao maisha. Lakini hakuna sababu kwa nini usiweze kuishi maisha ya kawaida na mazuri.

Kwa dawa za hospitali mpaka sasa hakuna dawa ya kuondoa moja kwa moja ingawa hasa kwa aina ya 2 watu baada ya kurekebisha vyakula wanaweza kujiweka katika hali hali ambayo mwili unaweza kutumia insulin yake kidogo bila ya kula vidonge au sindano.

Kuna utafiti wa kufanya transplant ili kuongeza insulin mwilini kwa kutumia sehemu (pancreas) ya mtu mwengine lakini bado haujafanikiwa kuweza kutumika kama ni matibabu.

Je, watoto wangu wanaweza kuurithi?
Wakati mwingine zaidi ya mtoto mmoja katika familia wanaweza kuwa na ugonjwa huo. Lakini urithi wa ugonjwa huu kwa watoto ni mdogo sana kwa kawaida. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi.

Je, nikiwa na ugonjwa wa kisukari ninaweza kuoa au kuolea na kuwa na watoto?
Ndiyo. Ugonjwa huu haumzuii mtu kuoa au kuolewa.

Je, ni zipi athari za ugonjwa huu?
Baada ya muda mrefu ugonjwa wa sukari huleta athari ya mishipa ya fahamu na kusababisha kupoteza hisia za ngozi na viganja au nyayo na kupungua nuru ya macho. Pia athari ya mafigo huweza kujitokeza na uzungukaji wa damu unaweza kupungua katika baadhi ya sehemu na kusababisha kufa kwa sehemu za mwili.

Kujitokeza kwa dalili hizi kunategemea ni kiasi gani matibabu yamefanikiwa na wakati wa kuanza kwa matibabu hayo baada ya kujuilikana kwamba mtu ana ugonjwa huu.

Je, ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa wa kuambukiza kama vile kifua kikuu au ukoma? Hapana. Huwezi kuambukizwa ugonjwa wa kisukari.

Vipi naweza kujikinga na ugonjwa huu?
Ikiwa unayo historia katika familia sio lazima kwamba utapata ugonjwa huu. Lakini kwa wale ambao wanaweza kuupata wanaweza kuuchelewesha kwa kujitahidi kuishi maisha ya afya nzuri kwa kula chakula bora, mazoezi, kula mboga mboga kwa wingi na kujiepusha na uzito wa mwili. Pia kupima damu baada ya kila muda ikiwa una historia katika ukoo au una wasi wasi kutokana na dalili zilizotajwa hapo juu.
===
1. AINA YA MLO UFAAO KWA WAGONJWA WA KISUKARI
Idadi ya milo ya kila siku
Si busara kula rundi la maakulati bora kupendelea kula milo midogo midogo
ya mara kwa mara. Njia hii inasaidia kupunguza uzito wa mtu vile vile na
kuifanya insulin kufanya kazi kwa kasi au bora zaidi.

Tahadhari na kukwepa chai au mlo wa asubuhi kwa vile unahitaji kuanza siku ukiwa na chochote tumboni. Baada ya mlo wa asubuhi unaweza kuendelea kula mara mbili zaidi kwa kutwa ikiwa umezoea kula hivyo. Lakini hakikisha kwamba unakula kiwango kidogo kidogo, tofauti na ulivyozoea.

Kula ndimba kubwa kubwa asoruka paka hazina tija kwa siha yako.

Inawezekana kuwa huna njaa baina ya nyakati za kula, lakini inafaa
utambuwe kwamba ni vyema ukila vitu vidogo vidogo vikavu kama ya ngano nzima na ule pamoja na tunda moja. Ulaji huu wa udoho udoho utakufanya usiwe na njaa kali wakati wa milo mikuu na kwa hivyo utakula kidogo zaidi.

Matunda
Matunda ni chakula bora, lakini mengi yao yana sukari nyingi, kwa hivyo ni
vizuri kula si zaidi ya mawili-matatu kwa siku ukihakikisha kupunguza
ulaji wa zabibu, embe, ndizi mbivu, matunda makavu kama tende, zabibu kavu,zeituni kwa vile matunda haya yana sukari nyingi.

Maziwa na mitindi
Maziwa yana sukari-ya-maziwa (lactose) , kwa hivyo mtu anahitajiwa asinywe zaidi ya nusu liter kwa siku, hii ina maana maziwa ya aina mbali mbali kama mtindi na yoghurt bila ya matunda.

Vidonge vya utamu haviathiri kiwango cha sukari katika damu kwa hivyo mtu anaweza kutumia vidonge hivi kwa kutayarishiya maakulati badala ya kutumia sukari ya kawaida. Vidonge hivi viko vya aina tafauti kwa mfano saccharin (sakkarin), cyclamate, acesulframe, aspartame (Nutra-sweet) n.k.

Cyclamate na acelsulframe zinaweza kuchemshiwa bila ya kuharibu ladha.
Nutra-sweet inapoteza ladha yake tamu ikiwa itachemshwa au kubekiwa kwa zaidi ya dakika chache. Sakkarin inageuka kuwa chungu ikiwa itachemshwa zaidi ya digrii 70 kwa muda mrefu.

Epuka na vitu vilvyo tiwa ladha ya utamu kwa matumizi ya sorbitol na au
fructose kwa vile vina ongeza sukari katika damu.

Inafaa mtu anywe vinyaji vilivyo punguzwa utamu au kutiwa utamu wa vidonge yaani vinyaji bila ya sukari. Hakikisha kusoma kama sharubati fulani ina sukari au haina sukari.

Epuka na vyakula vya utamu-utamu kama vile haluwa, jelebi, laddu-laddu,
peremende-pipi, asali, matunda ya kuchemsha, jamu, makeki-keki, kashata
n.k. na ujizoweshe kula vyakula visivyo vitamu tamu.

Mboga-mboga ni vyakula bora na haziongezi sukari katika damu :
mabilingani, mabamia, vitunguu, squshi, kebeji, kerot, tungule/nyanya, tango, koliflower, fiwi, kisamvu, mchicha n.k.

Njegere, kunde, mbaazi, maharage, njugu mawe, muhogo, ndizi mbichi,
majimbi, viazi vikuu ni vyakula vyenye mizizi mizizi ambavyo vinateremsha
sukari katika damu. Tahadhari na ndizu mbivu, za mkono wa tembo, boga na viazi vitamu.

Ukila jibini hakikisha kwamba haijajaa shahamu yaani iwe ya kiasi cha 18%
ambayo itakuwa na shahamu ya kiasi cha gramu 18 kwa kila gramu 100 za
jibini. Kwenye pakiti unaweza kusoma kiasi cha asili mia ya shahamu kwenye jibini.

Samaki ni wenye manufaa makuu kisiha na aina zote zinaruhusiwa
Usile mayai zaidi ya 2-3 kwa wiki.

Wasia wa Chakula bora
Punguza utumiaji wa mafuta, siagi, samli na margarini
Kula mboga mboga kwa wingi, ama za kuchemsha au mbichi
Kula vyakula vya mizizi mizizi
Kula vyakula vyenye ngano nzima na chapati za ngano nzima
Pale inapomkinika soma kwenye paketi/chupa kuhusu kuwemo au kutokuwemo sukari ndani

Maakulati/machopo chopo
Ikiwa mtu atafuata mapendekezo ya hapo juu, anaweza mara 1-2 kwa mwezi kula maakulati kama vile kwenye shughuli, maaliko, sherehe yenye vyakula vyenye mafuta/siagi na sukari kwa wingi.

Matatizo
Baadhi ya nyakati mtu anaweza kufikwa na maafa kama misiba, matatizo ya kifamilia n.k. Na kwa hivyo mtu hupendelea kujiliwaza kwa kula zaidi au
kupoteza hamu ya kula kabisa. Hali hizi zina athiri ugonjwa wa kisukari na
kwa hivyo mtu inambidi aendelee na kula kama ilivyopendekezwa ingawa mara nyengine inaweza kuwa ni vigumu.

Magonjwa mengine
Hutokea kwamba mtu anapata magonjwa mengine juu ya ugonjwa wake wa kisukari, anatakiwa aendelee na matibabu yake ya kisukari kama kawaida.
Na anategemewa apime sukari katika damu mara kwa mara zaidi kuliko kawaida kwa vile magonjwa mengine yanaweza kuifanya sukari ikapanda zaidi ingawa matibabu yanaendelea kwa kawaida. Kwa hivyo kumbuka kuwasiliana na tabibu wako pindi sukari ikipanda.

Safarini
Jambo la mwanzo kumubuka kuchukuwa dawa yako na kipima sukari chako.

Chanzo: Kwa hisani ya Dr. Y. Salim
---
2. MATOKEO YA KUTODHIBITI UGONJWA WA KISUKARI
Matokea ya kutoithibiti sukari ipasavyo(kutofuata matibabu) - Chronic complications

1.Vidonda vya miguuni ambavyo vinachukua muda mrefu kupona.

2.Diabetes neuropathy, Nervedamage -Kupungukiwa na hisia kwenye miguu ambako kuna peleka kutohisi maumivu haswa miguuni (Diabetes foot). Mfano unaweza uwe umevaa viatu vya kubana lakini usihisi hivo hata kupeleka kupata vidonda.

3.Diabetes retinopathy, eye damage - sukari inaharibu mishipa ya damu iliyopo kwenye macho kupeleka matatizo kwenye kuona au ukipofu.

4.Diabetes nephropathy - matatizo kwenye mafigo kupeleka mafigo kuharibika kwa mafigo.

5.Matatizo ya moyo - Heart attack.

6.Stroke - Kupooza.

7.Erectile dysfunction - Inasababishwa na kutokuwa na msukumo wa damu wa kutosha kwenye uume kwasababu mishipa ya damu kupungua upana/ukubwa kutokana na calcification)
===
1592336798825.png

UFAFANUZI, USHAURI NA MAONI YA WADAU KUHUSU TATIZO HILI:
Njia tano za kufuata kama mwongozo wa kukabiliana na ugonjwa wa Sukari

Mara tu unapoambiwa kuwa una huu ugonjwa, linaweza kuwa ni jambo ngumu kulikubali na kukabiliana nalo. Hisia za kushtuka, hasira, kutamauka, kuogopa na kuwa na majonzi ni za kawaida kwa yeyote baada ya kupata habari kuwa ana ugonjwa wa sukari. Hata hivyo una maisha yako ambayo ni muhimu uyaokoe. Fuata hizi njia tano, kwa uangalifu ili ujue la kufanya wakati wa kukabiiana na hiyo hali yako mpya ya kuwa mgonjwa wa ugonjwa wa sukari.

Hatua ya 1: Jifunze yote yanayokupasa kuhusu ugonjwa huu.

Jifunze na uelewe kila kitu ili ujue unachoshughulikia. Muulize daktari ambaye anajua yote kuhusu ugonjwa huu na aliye na uwezo wa kujibu maswali yako yote. Tambua aina ya ugonjwa wa sukari unaokusumbua. Ni hali gani inayokufanya ujipate hatarini?

Jua vyema kiwango cha sukari kilichoko mwilini mwako na aina ya dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini mwako itakayokufaa maishani mwako. Ni shida gani zinazotarajiwa iwapo utashindwa kuuthibiti ugonjwa huu kwa kiwango kinachotakikana, kulingana na mhudumu wako wa kiafya. Utafiti wako umekusaidia kupata maarifa unayostahili. Kuweza kukabiliana na ugonjwa huu kikamilifu.

Hatua ya 2: Badili mtindo wako wa ulaji

Ili kuweza kukabiliana na kiwango cha sukari mwilini mwako ni muhumu upunguze uzani usiofa, kiasi cha chakula unachojipakulia ni lazima kipungue usifikirie kwa misingi ya utaratibu na ulaji bali njia bora ya kutunza afya yako kwa kula chakula kifaacho vyakula vifuatavyo, visikose kwenye orodha ya vyakula unavyohitaji katika taratibu wako wa ulaji; mboga, matunda, chakula cha kutunza mwili na cha kupatia nguvu mwili wako. Zungumza na daktari wako wa utarativu wa ulaji bora kuhusu mpangilio mwafaka wa mlo utakaouzingatia kwa wakati huu.

Hatua ya 3: Panga mpangilio wa kila siku wa kudumu

Watu wengi walio na ugonjwa huu mara nyingi huwa wanene kupita kiasi na wenye uzani mzito. Hivyo basi ni muhimu, ufanye mazoezi ya kila mara kama njia mojawapo ya kukabiliana na ugonjwa huu. Ni lazima kuwa daktari wako atakupa ushauri utakaoutaka upunguze uzito. Mazoezi mwafaka zaidi ni kuwa na mpangilio utakaokufanya uwe na nguvu za uthibiti wa moyo wako kwa kufanya mazoezi yanayolenga hayo mambo mawili. Baada ya ushauri wa daktari unaweza kuamua kujiunga na chumba au kiwanja cha michezo ya kuzoeza viungo vya mwili ama ujiunge na kundi la YMCA/YWCA ili upate msaada unaohitaji kuendelea kuyathibiti maisha yako na hali yako ya wakati huu. Kama sivyo, kuna namna nyingi za kujipangia mazoezi ya kibinafsi pale pale tu nyumbani.

Hatua ya 4: Meza dawa zako inavyotakikana

Watu wengine walio na aina ya pili ya ugonjwa huu huhitaji kumeza tembe zao inavyostahili ama kujidunga dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini ili miili yao itumie sukari iliyomo katika matunda na mimea kupata nguvu. Aina hii ya sukari huvunjwavunjwa tena wakati wa kuyeyusha chakula kinywani na tumboni ili kifae kuchukuliwa na damu mwilini kama ifanyikavyo na chakula cha namna kilichomo katika nyama, ute wa yai na samaki (chakula cha kutunza mwili) Dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini haipatikani kwa hali ya tembe. Yaliyo chini ya ngozi yako ili ingiie mara moja ndani ya damu yako.

Hatua ya 5: Tafuta usaidizi (msaada)

Huenda ikawa, utaweza kukabiliana na huu ugonjwa bila shida lakini ni muhimu utambue kuwa unahitaji msaada wa watu wengine ili mzigo ukuwie mwepesi kidogo. Tegemea jamaa na marafiki wakutegemewa ambao watakuwepo kila mara utakapohitaji msaada wao, katika hiyo hali yako mpya ya kisasa. Jishughulishe na vikundi vya watu walio na hali sawa na yako, pia jihusishe na shughuli za kijamii na kutafuta pesa na kuelimisha watu wanaoishi karibu nawe kuhusu ugonjwa huu.
---
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Oktoba 2018
  • Idadi ya watu wenye ugonjwa wa kisukari imeongezeka kutoka milioni 108 mnamo 1980 hadi milioni 422 mwaka 2014.
  • Ugonjwa wa kisukari * miongoni mwa watu wazima zaidi ya miaka 18 kumepanda kutoka asilimia 4.7 mnamo 1980 hadi 8.5% mwaka 2014 (1).
  • Ugonjwa wa sukari umekuwa ukikua kwa kasi zaidi katika nchi zenye kipato cha kati na cha chini.
  • Ugonjwa wa kisukari ni sababu kubwa ya upofu, kuharibika kwa figo, mshtuko wa moyo, kiharusi na kukatwa miguu.
  • Mnamo mwaka wa 2016, wastani wa vifo milioni 1.6 vilisababishwa moja kwa moja na ugonjwa wa sukari. Vifo vingine milioni 2.2 vilitokana na sukari kubwa ya damu mnamo 2012 **.
  • Karibu nusu ya vifo vyote vinavyotokana na sukari kubwa ya damu kutokea kabla ya umri wa miaka 70. WHO ilikuwa sababu ya saba ya kusababisha vifo mnamo 2016.
  • Lishe yenye afya, mazoezi ya kawaida ya kiwmili, kudumisha uzito wa kawaida wa mwili na epuka tumbaku ni njia za kuzuia au kuchelewesha mwanzo wa ugonjwa wa kisukari cha aina ya 2.
  • Ugonjwa wa kisukari unaweza kutibiwa na madhara yake kuzuiliwa au kucheleweshwa kwa lishe, shughuli za mwili, dawa na uchunguzi wa mara kwa mara na matibabu.

8aa416e309c2e767f5cfe774f963cf3f.jpg


UFAHAMU UGONJWA WA KISUKARI NA TIBA YAKE

Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) hutokea pale tezi kongosho (pancrease) inaposhindwa kutengeneza homoni au kichocheo aina ya Insulin, au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho cha insulin na kusababisha kuongezeka kiwango cha sukari kwenye damu (hyperglycemia).

Insulin ni kichocheo au homoni inayotengenezwa na kongosho ili kudhibiti kiwango cha sukari.

Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababishwa kuwa na kiwango kidogo cha Insulin mwilini, mwili kutosikia kichocheo hicho au yote mawili. Ili kuelewa vyema ugonjwa wa kisukari ni muhimu kwanza kuelewa namna chakula kinavyovunjwa vunjwa na kutumiwa na mwili ili kuzalisha nguvu.

Wakati chakula kinapoyeyushwa matukio kadhaa hutokea.

1.Tukio la kwanza ni sukari inayoitwa glucose ambayo ni chanzo cha nguvu mwilini huingia katika damu.

2.Tukio la pili ni kiungo kinachoitwa kongosho (pancrease) kutengeneza kichocheo cha Insulin. Kazi ya Insulin ni kuondoa glucosei katika damu na kuingiza katika misuli, seli za mafuta na ini, ambako hutumiwa kama nishati.

Watu wenye ugonjwa wa kisukari huwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kwa sababu miili yao haiwezi kupeleka sukari kwenye seli za mafuta, ini na misuli ili ihifadhiwe kwa ajili ya kuzalisha nguvu.

Hii ni kutokana sababu zifuatazo.

1.Kongosho kutokuwa na uwezo wa kutengeneza insulin ya kutosha, au--->

2.Seli za mwili haziathiriwi na insulin kama inavyotakiwa ama sababu zote hizo mbili.


AINA ZA KISUKARI

KISUKARI AINA YA KWANZA(TYPE 1 DIABETES MELLITUS)

Hii ni aina ya kisukari inayowaathiri zaidi watoto na vijana. Aina hii hutokea iwapo seli maalumu zinazotengeneza homoni ya insulin zinapokosekana katika tezi kongosho au zinapoharibika kutokana na sababu yeyote ile, na hivyo kusababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu.

Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa seli hizi katika tezi kongosho ni pamoja na kushambuliwa tezi kongosho kunakoweza kufanywa na magonjwa ya kinga ya mwili ya mtu mwenyewe au autoimmune diseases, au kushambuliwa na vyanzo visivyojulikana.

KISUKARI AINA YA PILI (TYPE 2 DIABETES MELLITUS)
Hii ni aina ya kisukari inayotokea zaidi ukubwani. Aina hii ya kisukari husababishwa na kupungua utendaji kazi wa homoni ya insulin, au seli kushindwa kutumia insulin ipasavyo.

Hali hii mara nyingi husababishwa na unene uliopitiliza yaani obesity, au hali ya kutoushughulisha mwili kabisa (physical inactivity).

Kwa vile, katika aina hii ya kisukari, insulin huzalishwa kwa kiwango cha kutosha isipokuwa tatizo lipo kwenye ufanisi na utendaji kazi wake,

KISUKARI CHA UJAUZITO (GESTATIONAL DIABETES MELLITUS)
Ni aina ya kisukari kinachotokea pindi kunapokuwa na ongezeko la kiwango cha sukari katika damu (hyperglycemia) wakati wa ujauzito. Aina hii ya kisukari huathiri karibu asilimia 2 hadi 5 ya mama wajawazito wote ingawa wengi wao hupata nafuu na kupona kabisa mara tu baada ya kujifungua.

Hata hivyo karibu asilimia 20 mpaka 50 ya mama wajawazito wanaopata aina hii ya kisukari huweza kuendelea kuwa na ugonjwa huo hata baada ya ujauzito na hatimaye kuwa na aina ya pili ya kisukari.


SABABU ZA KISUKARI
Sababu za kisukari hutofautiana kulingana na aina ya ugonjwa huo.

Aina ya kwanza ya kisukari ina uhusiano mkubwa sana na kurithi. Aidha aina hii pia husababishwa na maambukizi virusi kama vile Coxsackie virus type B4.

Visababishi vingine ni pamoja na sumu inayotokana na kemikali za

baadhi ya vyakula (food borne chemical toxins), na kwa baadhi ya watoto wachanga maziwa ya ng'ombe yanaweza kuchochea kinga ya mwili wa mtoto uushambulie mwili wenyewe na hivyo kusababisha uharibifu katika tezi kongosho.

Aina ya pili ya kisukari kwa ujumla husababishwa zaidi na jinsi mtu anavyoishi na pia matatizo ya kijeneteki. Aidha kuongezeka uzito na unene kupita kiasi (obesity).

Sababu nyingine ni pamoja na kuongezeka umri, maisha ya kivivu na kutofanya mazoezi na pia ugonjwa wa tezi kongosho (pancreatitis) ambao hufanya insulin inayozalishwa kuwa na ufanisi mbovu au ya kiwango cha chini.

DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI

Kukojoa mara kwa mara
Kuhisi kiu kali na kunywa maji kwa kiwango cha kupitiliza (polydipsia).
Kuhisi njaa na kula mara kwa mara (polyphagia).
Kuchoka haraka
Kupungua uzito
Vipele mwilini (diabetic dermadromes).
Kutoa harufu ya acetone inayofanana na harufu ya pombe.
Kuhisi maumivu ya tumbo na kupoteza fahamu
Na wagonjwa wa kisukari pia huwa katika hatari ya kupata maambukizi katika kibofu cha mkojo, ngozi na kwa wanawake sehemu za siri.

Baada ya mtu kuwa na dalili za ugonjwa wa kisukari matibabu huanza baada ya kufanyiwa vipimo na kuthibitisha kwamba kweli ana ugonjwa huo.

Chini ya 5.6 mmol/l au 100 mg/dl: Sukari kwenye damu yako ni sawa.

Zaidi ya 5.6 mmol/l au 100 mg/dl lakini chini ya 6.9 mmol/l au 125 mg/dl: Hii ni ishara ya tahadhari-unapaswa kufanya mabadiliko katika maisha yako sasa ili kupunguza hatari ya kupata kisukari. Kama matokeo yamekaribia kiwango cha juu, ni muhimu hasa kufanya juhudi za ziada za ulaji wenye afya, na kupata mazoezi au kujishughulisha.

Zaidi ya 6.9 mmol/l au 125 mg/dl: Una kisukari na unahitaji matibabu. Kadri kiwango kinavyopanda, ndivyo kuongezeka kwa hatari ya dharura kutokana na kiwango cha sukari kwenye damu kuzidi kupita kiasi, au matatizo makubwa ya kiafya

Madhara ya Kisukari
Kisukari huweza kusababisha madhara yafuatayo kwa muhusika iwapo hakitatibiwa inavyopaswa.
  • Kuziba kwa mishipa mikubwa ya damu kutokana na kuzungukwa na mafuta (Atherosclerosis)
  • Mgonjwa kushindwa kuona vizuri au kushindwa kuona kabisa na kuwa kipofu (diabetic retinopathy)
  • Kushindwa kufanya kazi vizuri kwa figo
  • Mgonjwa kuhisi ganzi na kupoteza kuhisi mikononi na miguu kwa sababu ya kuharibika kwa neva (diabetic neuropathy)
  • Kupungua kwa nguvu za kiume.
  • Vidonda (diabetic ulcers) hususani vidoleni. Hali hii wakati mwingine hupelekea mgonjwa kukatwa viungo vyake.
  • Mgonjwa kuwa hatarini kupata maambukizi ya vimelea mbalimbali hasa bakteria kutokana na kuharibiwa na kushindwa kufanyakazi vizuri kwa chembe nyeupe za damu (White Blood Cells)
Matibabu

Matibabu ya kisukari hutegemea na aina ya kisukari ingawa kwa ujumla kuna hujumuisha matumizi ya dawa na njia ya kubadilisha mfumo (staili) wa maisha.

Kwa aina ya pili ya kisukari (type 2 DM au NIDDM): Aina hii ya kisukari huweza kutibiwa kwa ama dawa au kubadili mfumo wa maisha au vyote viwili kwa pamoja. Katika kubadili mfumo wa maisha, ni muhimu mgonjwa kutilia maanani na kuwa makini na vitu kama aina ya vyakula anavyokula, na kujitahidi na kuongeza kufanya mazoezi ya mwili ili kuepuka kuongezeka uzito kupita kiasi. Kuhusu aina ya vyakula inashauriwa sana
  • kupunguza kula vyakula vyenye lijamu (cholesterol) ambayo ni mafuta mabaya yaani kula walau chini ya miligramu 300 za lijamu kwa siku.
  • kujitahidi sana kula vyakula vya kujenga mwili (protein) angalau kwa asilimia 10-15. Vyakula hivi ni pamoja na nyama na mboga za majani.
  • kuwa makini na ulaji wa vyakula vya wanga (carbohydrate). Hakikisha visizidi asilimia 50-60 ya chakula unachokula kwa siku. Yaani visiwe ndiyo chakula kikuu kwa siku.
  • kupunguza utumiaji wa chumvi katika chakula.
  • Kuacha na kuwa muangalifu kutumia pombe.
Suala la ufanyaji mazoezi ni jambo la muhimu kwa vile mazoezi husaidia sana kupunguza uzito, kuondoa mafuta mwilini yanayopunguza utendaji kazi wa insulin na hivyo kuongeza ufanisi na utendaji wa insulin mwilini.

Hali kadhalika, mgonjwa mwenye aina hii ya kisukari anaweza pia kupewa dawa ambazo atatakiwa kunywa kila siku huku akiendelea kufuata ushauri mwingine kama ilivyoelezwa hapo juu.

Dawa hizo ambazo huitwa pia dawa za kushusha kiwango cha sukari mwilini (Oral Hypoglycemic drugs) ni pamoja na zile za kundi la Biguanides kama vile Metformin, za kundi la Sulphonylureas kwa mfano Glipizide, za kundi la Meglitinides, za kundi la Alpha glucosidase inhibitor, zinazojulikana kama Thiazolidinediones, Incretin-mimetic au za kundi la Dipeptidyl peptidase IV inhibitors kwa mfano sitagliptin

Ifahamike pia kuwa wapo baadhi ya wagonjwa wa aina hii ya pili ya kisukari (Type 2 DM) ambao pamoja na kutumia dawa za kunywa za kushusha sukari na kufuata ushauri wa daktari kuhusu mfumo wao wa maisha bado njia hizo zinaweza zisishushe sukari inavyotakiwa. Katika hali kama hiyo, wagonjwa hawa huweza kudungwa pia sindano za insulin kwa muda ili kushusha kiwango cha sukari.

Matibabu maalum
  • Matibabu ya hyperosmolar non-ketotic coma (HONKC): Matibabu haya hutolewa hospitali. Mkazo huwekwa katika kusahihisha upungufu wa maji mwilini ambapo mgonjwa hupewa kati ya lita 8 hadi 10 za maji aina ya Normal saline. Aidha, lita kati ya 1 hadi 2 hutolewa katika masaa ya mwanzo tangu mgonjwa kufkia hospitali. Iwapo kuna ugumu katika kusahihisha kiwango cha kisukari mwilini kwa kutumia dawa za kunywa, Insulin inaweza kutolewa.
  • Matibabu ya Diabetic ketoacidosis (DKA): Kama ilivyo kwa hyperosmolar non-ketotic coma, matibabu ya DKA nayo hutolewa hospitali chini ya uangalizi maalum wa madaktari. Hii ni hali ya hatari, ambapo kama isipotibiwa kwa umakini, inaweza kupelkea kifo cha mgonjwa. Jambo la muhimu katika matibau ni kusahihisha upungufu wa maji mwilini kwa kutumia Normal saline, ambapo lita 1-3 hutolewa ndani ya masaa mawili ya mwanzo, kusahihisha kiwango cha potassium kilichopo katika damu na kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu kwa kutumia Insulin.
---
Poleni wenge haya maradhi
Kwa uzoefu wa Mzee.,mtu mzima 60+ ,aliumwa kidogo akapimwa kakutwa sukari 22..tangu hapo akawa ana'control diet...lishe yake imejikita kwenye protein na vitamins na mbogamboga kwa wingi...wanga anakula brown bread na viazi ulaya tu au akimiss kitu mfano wali anaonja tu
Ishashuka iko 6-10 hapo anajitahidi

Hata hivyo baada ya muda ikabidi apewe dawa pia mana 'nerves'/mishipa ya fahamu ilikua inamshtua

Nilichojifunza
1.Chakula kiliwe kwa kiasi hasa wanga na vitu vya mafuta na vya sukari
-Jioni tule kidogo zaidi
2.Ulaji wa mbogamboga na jamii ya kunde na maharage ni mzuri zaidi
3.Mazoezi ni muhimu
4.Uzito wa mwili uwe wastani tu...zama za kuona unene na vitambi ni sifa tuachane nazo..ni maradhi yale
---
DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI NA JINSI YA KUJIKINGA







KISUKARI ni moja ya magonjwa yanayoathiri watu wengi siku hizi nchini mwetu na hata nje.

Kati ya hao, wengi huishi na ugonjwa huo kwa muda mrefu na kuja kugundua kwamba wana
kisukari baada ya muda wa kama miaka mitano hivi, baada ya mwili kuanza kuonesha dalili kuu za kisukari.

Ndani ya kipindi hicho cha miaka mitano, tayari mwili unakuwa umepoteza baadhi ya uwezo wake katika macho, figo, fizi na neva za fahamu. Kisukari hakina dawa ya kutibu kabisa, bali vipo vichocheo (hormone) na dawa zinazosaidia kurekebisha kiwango cha sukari mwilini.




Je, vipi mtu aweza kutambua kuwa na kisukari mwilini? Zipo dalili kadhaa zinazotokea kwa
wenye kisukari. Baadhi ya hizo ni kiu ya maji isiyoisha, njaa kali, kwenda haja ndogo mara kwa mara na vidonda au michubuko kuchukua muda mrefu kupona.

Nyingine ni ngozi kuwa kavu na kuwasha, mgonjwa kupoteza uzito bila sababu, kuwa na ukungu machoni, kuchoka kusiko kwa kawaida, hisia kupungua katika vidole na viganja
mikononi na miguuni na kuwa na ukungu katika fizi, ngozi na kibofu cha mkojo.

Hatua za mwanzo za kisukari huwa na dalili chache sana, hivyo inawezekana kabisa mtu asifahamu kuwa ana kisukari, ingawaje madhara yanaweza kuwa yameshatokea katika macho, figo na mfumo wa usukumaji damu mwilini.

Watu wengi wanaopatwa na kisukari huangukia katika makundi ya wenye umri unaozidi miaka 30, uzito mkubwa na uzito uliokithiri (uwiano kati ya uzito na urefu zaidi ya 25 na 30),
kadhalika, watu wasiofanya shughuli za kuupa mwili mazoezi huwa katika hatari hiyo, kama
ilivyo kwa wale wanaozaliwa katika familia ambayo mmoja kati ya wanandugu wa karibu ana kisukari. Mwanamke kujifungua mtoto mwenye uzito wa zaidi ya kilo nne na aliyekuwa na kisukari cha ujauzito anaangukia pia kwenye kundi hilo, sawa na wale wanaokuwa wamepata ajali na kuumia sehemu za tumboni au kula chakula chenye sumu ambacho kinaweza kuumiza
kongosho.

Upo umuhimu wa kupima kisukari mapema basi, ili kuepuka mtu kuishi nacho kwa muda mrefu pasipo kujua, na kusababisha madhara kusambaa mwilini na kumwathiri mwathirika.
Ni muhimu kuzingatia mazoezi, uzito, lishe na ushauri wa wataalamu wa afya, kwa sababu husaidia kupunguza makali na madhara yatokanayo na kisukari.

Watu wenye kisukari wapo katika hatari zaidi ya kupatwa na magonjwa ya moyo, kiharusi, matatizo na kuharibika kwa kibofu cha mkojo, shinikizo la juu la damu, upofu, kufa neva za fahamu, uharibifu katika fizi na ugonjwa wa fangasi.

Mtu anapokuwa na kisukari, mzunguko wa damu miguuni hupungua na hii ndiyo sababu kubwa ya kufa kwa neva za fahamu na hivyo mtu kukosa hisia katika eneo hilo la mwili.
Matokeo ya hali hiyo ya kutohisi punde mtu anapodhurika na kusababisha kidonda ambacho mara nyingi mhusika anakuwa hafahamu hadi anapofahamishwa na mtu wa karibu au atakapokagua miguu yake.

Hii ndiyo sababu kubwa ya watu kushauriwa kukagua miguu yao kila siku kabla ya kulala kuona kama kuna mchubuko wa aina yoyote au ukucha unaoweza kuchimba ngozi. Kutokuzingatia masharti ya kujikagua huweza kusababisha kidonda kukua, kutotibika na hatimaye mgonjwa kuishia kupoteza kidole, unyayo au hata mguu.

Vile vile, kutokuzingatia masharti ya kujua kiwango cha sukari mwilini huweza kusababisha mtu akapoteza fahamu kutokana na mwili kuzidiwa sukari asidi (diabetic ketoacidosis), na hii huweza kusababisha kifo mara moja.

Mgonjwa anaweza kuzuia madhara yatokanayo na kisukari kwa kuzingatia maelekezo, masharti na ushauri wa wahudumu wa afya, hasa kuhusu chakula na mazoezi na maelekezo ya utumiaji sahihi wa dawa au insulin.

Mgonjwa hatakiwi kuvuta sigara, awe anapima kiwango chake cha shinikizo la damu mara kwa mara na kuhakikisha kiwango chake cha lehemu kipo katika uwiano unaotakiwa. Takwimu zinaonesha kuwa uzingatiaji wa hayo yaliyotajwa umesaidia watu wengi kupunguza madhara
ya kisukari kwa asilimia 75.

Lishe mahsusi kwa mtu mwenye kisukari ni mlo wenye kiwango kidogo sana cha mafuta, kiwango kidogo cha chumvi na kiwango kidogo cha sukari. Mlo uwe na mchanganyiko wa
nyuzinyuzi kama vile dona (unga wa mahindi yasiyokobolewa), nafaka, tambi, ndizi za kupika, mtama, uwele nk.

Vile vile matunda machachu na mboga za majani zilimwazo na zile za porini ziliwazo kama mchunga, tembele, majani ya maboga, majani ya kunde na mbilimbi. Ni vyema kujitahidi kula kiasi kidogo cha chakula walau mara tano kwa siku kuliko mlo mkubwa mara mbili au tatu kwa siku.

Isipokuwa kwa sababu zisizozuilika, mgonjwa asiache kula, kwani ni mbaya kwa utendaji kazi wa mwili. Katika kudhibiti kiwango cha sukari mwilini, ni muhimu mwathirika kupata maelekezo yahusuyo njia na jinsi ya kupima na kujua kiwango cha kawaida cha sukari mwilini.

Watu wengi wenye kisukari huwapasa kutumia aina ya insulin kabla ya kula chakula kulingana na kiasi cha wanga ulio kwenye chakula anachotarajia kula. Kupima wingi wa wanga katika
chakula husaidia kupanga mlo.

Kujitambua wakati kiwango cha sukari kikiwa juu kupindukia ni kwa kupima damu angalau mara tatu kwa siku, ikiwa ni pamoja na kabla ya kwenda kulala. Mara nyingi watu hupima asubuhi au alfajiri wanapoamka, mchana wa adhuhuri au alasiri na jioni au usiku kabla ya kulala.

Ikiwa sukari mwilini ni nyingi kupindukia, inaweza kumlazimu mgonjwa kutumia insulin ya ziada inayofanya kazi ndani ya muda mfupi (short acting insulin) ili kurejesha kiasi cha sukari
katika kiwango cha kawaida.

Mgonjwa atafahamishwa na mhudumu wa afya au daktari kuhusu kiwango cha insulin cha kutumia kulingana na wingi wa sukari aliyo nayo mwilini kwa wakati huo. Licha ya kuwapo wingi wa sukari mwilini, kuna kisukari ambacho mgonjwa huwa na upungufu wake pia.

Matumizi yasiyo sahihi ya insulin au kutokula chakula husababisha kiwango cha sukari kwenye
damu kupungua kuliko kawaida na hivyo mwili kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo.

Dalili za hali hiyo ni kuhisi uchovu bila sababu, kupiga miayo kupindukia, kushindwa kuzungumza au kufikiri vyema, kupoteza stamina, kutoka jasho, kupata vichomi, degedege karibu na kuzimia, kuhisi kuishiwa nguvu au pamoja na kuzimia na mwili kupauka.

Mtu akipatwa dalili hizo inabidi atafute kinywaji kitamu anywe. Aina ya vinywaji vifaavyo ni kama juisi ya matunda (nanasi, zabibu, tufaa, papai ) vile vile soda (si diet soda) au alambe kiasi cha sukari nyepesi (glucose) au pipi.

Baadhi ya maeneo huuza vidonge vya glucagon, ambavyo ni vizuri kubebwa na kuhifadhiwa nyumbani kwa matumizi ya nyakati kama hizo. Glucagon pia hupatikana katika njia ya sindano na hii inaweza kutolewa na mtaalamu au mtu aliyeruhusiwa kuitoa kupitia kwenye mishipa ya
damu (intravenous glucagon injection).

Inawezekana kuishi maisha ya kawaida kabisa ikiwa mhusika atakuwa makini kulinda afya yake
kwa kuzingatia ushauri na mafundisho ya wataalamu wa afya.
---
[h=2]Dawa mbadala 10 zinazotibu Kisukari[/h]Katika makala hii tutaangalia dawa mbadala mbalimbali 10 zinazotibu ugonjwa wa kisukari. Labda utakuwa unajiuliza, Je kisukari kinatibika? Ndiyo kisukari kinatibika. Mhimu ni upate tiba mbadala au tiba asilia ambazo ni sahihi. Ili kujifunza mengi na kufahamu mengi kuhusu ugonjwa wa kisukari, kwamba kisukari ni nini? Au ugonjwa huu hutokeaje mwilini, Nakushauri usome kwanza makala hii => Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Kisukari

Umakini unahitajika sana hasa kwa mgonjwa yule ambaye ameanza kutumia dawa za hospitalini kila siku. Nakushauri usianze kuzitumia hizi dawa moja kwa moja ukiwa peke yako bila uangalizi wa karibu wa daktari au mganga wa tiba za asili.
Twende sasa tuzichambuwe hizi dawa moja baada ya nyingine kama ifuatavyo;


1. UWATU
Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa uwatu unao uwezo mkubwa katika kutibu kisukari. Uwatu huzisisimua seli katika kongosho kitendo kinachofanya uzalishwaji wa insulini kuongezeka. Maajabu haya ya uwatu yanasemekana kufanyika kutokana na uwatu kuwa na asidi amino mhimu sana ijulikanayo kama ‘4-hydroxyisoleucine'. Miaka mingi kabla hata ya huu utafiti kufanyika, uwatu umekuwa ukitumika kama moja ya dawa bora kabisa za asili katika kutibu kisukari.

Namna ya kuutumia Uwatu kujitibu kisukari
• Chota mbegu za uwatu vijiko 4 na uziloweke katika maji robo lita kwa usiku mmoja. Asubuhi ponda ponda hizo mbegu za uwatu ndani ya maji kisha zichuje na upate maji yake. Kunywa maji haya kila siku asubuhi kwa muda wa miezi 2.
• Chukuwa uwatu ya unga vijiko vikubwa 2 na uweke ndani ya maziwa au maji ya uvugu uvugu robo lita, koroga vizuri na unywe kila siku kutwa mara 2 kwa miezi 2.
• Chukuwa gramu 100 za mbegu za uwatu na gramu 50 za binzari manjano. Unaweza kuongeza kiasi kidogo cha pilipili manga nyeupe kwenye mchanganyiko huu. Ongeza kijiko 1 cha mchanganyiko huu wote katika maziwa robo lita na unywe kutwa mara 2 kila siku.
• Unaweza pia kuongeza uwatu ya unga katika unga wako unaotumia kutengenezea mkate au hata chapati.


2. MDALASINI

Utafiti uliofanywa kwa watu wenye kisukari aina ya pili umeonyesha kuwa utumiaji wa gramu 1 hadi 6 za mdalasini kwa siku unaweza siyo tu kupunguza kaisi cha damu sukari mwilini, bali pia unaweza kupunguza kiasi cha mafuta mazito katika damu (triglyceride) na hata kudhibiti kolesto!

Waathirika wa kisukari pia hutokewa kuwa na matatizo katika mfumo wao wa upumuwaji, hivyo utumiaji wa mdalasini kwao unaleta maana zaidi kwakuwa mdalasini unao uwezo mkubwa katika kuzuia magonjwa katika mfumo wa upumuwaji pia. Mdalasini ya unga hushusha kiwango cha damu sukari kwa kuziamsha shughuli za insulini. Mdalasini pia ina faida kwa watu waliogunduliwa kuwa na kisukari cha mwanzo (pre-diabetes status) na hivyo matumizi ya mdalasini kwao yatasaidia kuzuia wasipatwe na kisukari katika siku za usoni.

Hata hivyo aina ya mdalasini unaotumia pia inahusika katika kutibu kisukari au maradhi mengine. Nashindwa kupata maneno haya kwa Kiswahili lakini kuna aina kama mbili hivi za mdalasini ambazo ni ‘Cassia cinnamon' ambao wenyewe huwa na kitu kingine ndani yake kiitwacho 'coumarin' ambayo ni sumu na husababisha matatizo katika ini. Mdalasini nzuri kwa kutibu kisukari na ambayo bei yake ipo juu kidogo ni ile iitwayo kwa kiingereza kama 'Ceylon cinnamon'.

Namna ya kutumia mdalasini kutibu kisukari
• Chukuwa lita 1 ya maji na uyachemshe. Mara yatakapoanza kuchemka, ongeza vijiko 3 vikubwa vya mdalasini ya unga na uache kwa dakika kama 15 hivi kisha ipuwa chuja na unywe ikiwa bado ya uvugu uvugu kutwa mara moja kila siku kwa mwezi 1.
• Ongeza mdalasini kijiko kidogo kimoja cha chai katika kikombe kimoja (robo lita) cha maji ya uvugu uvugu, koroga na unywe kila siku.
• Unaweza pia kuongeza mdalasini ya unga ndani ya kachumbari kila unapokula.


3. MAJANI YA MANJANO
Utafiti unaonyesha kuwa, kutokana na kuwa na kiasi kingi cha madini kama vile madini ya chuma, Zinki, na shaba; majani ya manjano ni mhimu sana katika kuutunza usawa wa glukozi katika damu. Madini haya huziamsha seli za kongosho zinazohusika na uzarishwaji wa homoni ya insulini. Majani ya manjano pia husaidia umeng'enywaji wa wanga mwilini. Yanao uwezo wa kuviamsha upya vimeng'enya katika figo na ini ambazo zinahusika katika kumeng'enya wanga na kuurudisha katika hali yake ya kawaida na hivyo kusaidia kutibu kisukari.

Wagonjwa wa kisukari huwa wana tatizo la kuwa na uwezo mdogo kudhibiti sumu mwilini jambo ambalo hupelekea seli zao za mwili kufa katika kiwango kingi. Utafiti unaonyesha kuwa majani ya manjano yana uwezo wa kupunguza kiasi cha seli kufa, seli ambazo ni mhimu katika uzarishwaji wa insulini.

Majani ya manjano yanaweza kushusha usawa wa damu sukari na ni mhimu sana kwa watu wanaopata kisukari kama matokeo ya uzito kuzidi. Ikiwa kisukari kinazunguka katika familia yenu, jitahidini kutumia majani ya manjano kwakuwa yamethibitika kuthibiti pia hata kile kisukari cha kurithi.

Namna ya kutumia majani ya manjano kujitibu kisukari
• Tafuna majani freshi ya manjano 7 mpaka 10 kila siku asubuhi.
• Tumia majani ya manjano kwenye kila chakula unachopika kila siku.


4. MSHUBIRI (Aloe Vera)
Wakati mshubiri umekuwa ukitumika kwa miaka mingi katika kutibu kisukari, baadhi ya tafiti za hivi karibuni zimeonyesha kuwa mshubiri unao uwezo pia katika kushusha kiwango cha damu sukari na mafuta katika mzunguko wa damu kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na kisukari. Mshubiri umethibitika katika kutibu kisukari cha aina ya kwanza na hata cha aina ya pili.

Jinsi ya kuandaa mshubiri kutibu kisukari
Changanya vifuatavyo:

• Jeli ya mshubiri kijiko cha chai 1
• Unga wa majani ya matunda ya damu ya mzee kijiko cha chai 1
• Unga wa manjano kijiko cha chai 1
Kunywa mchanganyiko huu kila siku kabla ya chakula cha mchana na jioni.

5. MAJANI YA MUEMBE
Wakati tunda la embe halina uwezo wa kutibu kisukari, majani ya mti wa muembe yanao uwezo huo! Waganga wengi wa Nigeria wamekuwa wakitumia sana majani ya muembe katika kutibu kisukari. Yanao uwezo wa kupunguza ufyonzwaji wa glukozi katika utumbo mkubwa hivyo kusaidia kupunguza usawa wa sukari katika damu. Pia yana uwezo mkubwa katika kudhibiti kiwango cha mafuta katika damu.

Namna ya kuandaa
• Loweka majani 10 mpaka 15 ndani ya nusu lita ya maji kwa usiku mmoja. Chuja maji haya asubuhi mapema na uyanywe kabla ya kula chochote. Subiri lisaa limoja lipite ndipo ule chakula cha asubuhi.
• Kausha majani ya muembe kwenye kivuli. Yatakapokuwa yamekauka kabisa, yasage kupata unga wake na hifadhi unga huu katika chombo kisafi na kisha lamba unga huu nusu kijiko kidogo cha chai kila siku kabla ya chakula cha mchana na jioni.

6. MREHANI
Mrehani (basil) una faida nyingi sana kiafya. Nje ya kudhibiti kisukari, Mrehani pia una sifa na uwezo katika kudhibiti asthma, kuondoa mfadhaiko, kudhibiti bakteria, kudhibiti virusi, kudhibiti vivimbe, kuondoa sumu mwilini, kudhibiti asidi tumboni, na kuongeza kinga ya mwili. Mrehani huzisaidia pia seli za kongosho kufanya kazi zake vizuri na kusaidia utolewaji au uzarishwaji mzuri wa insulini.

Jinsi ya kuutumia mrehani kutibu kisukari
• Tafuna majani mawili mpaka manne ya mrehani kila siku asubuhi kabla hujala chochote.
• Ponda majani ya mrehani kupata juisi yake kama kijiko kimoja hivi cha chai na unywe kila siku asubuhi kabla ya kula kitu chochote.

7. BAMIA
Bamia zina kiasi kingi cha vitamini A, B6, C, K, magnesium, potassium, zinki, na faiba. Bamia ina uwezo mkubwa katika kusawazisha usawa wa sukari mwilini. Mbegu za Bamia zina kidhibiti kiitwacho alpha-glucosidase ambacho huzuia wanga kujibadili kuwa glukozi. Faiba iliyomo kwenye bamia husaidia kurekebisha kiwango ambacho sukari humeng'enywa katika utumbo mkubwa.

Jinsi ya kutumia Bamia katika kujitibu Kisukari
Mahitaji:

• Bamia 2 mpaka 3
• Maji glasi 1
Jinsi ya kuandaa:
• Zisafishe bamia vizuri kabisa.
• Ondoa au ikate sehemu ya kichwa na mkia katika bamia na utupe. Kisha kata kila bamia katikati kwa urefu ili kupata vipande 2, hivyo utapata jumla vipande 4 kwa bamia hizo 2.
• Hivyo vipande 4 viweke ndani ya glasi iliyojaa maji, funika na uache hivyo kwa usiku mmoja.
• Asubuhi na mapema kunywa hayo maji yote yaliyokuwa na bamia kabla ya kula kitu kingine chochote. Ukiweza unaweza kula hata hizo bamia pia. Bamia mbichi zinafaida zaidi mwilini kuliko zilizopikwa.
• Fanya hivi kila siku kwa miezi kadhaa.

8. MBEGU ZA KATANI
Mbegu za katani zina kiasi kingi cha mafuta mhimu sana yajulikanayo kama "essential omega-3 fat alpha-linolenic acid (ALA)'', pia zina protini, faiba na muunganiko wa mmea uitwao 'lignans'. Hii lignans hufanya kazi kama kiuaji sumu au kwa maneno mengine hufanya kazi ya kuondoa sumu mwilini. Baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa mbegu za katani zinao uwezo wa kusawazisha usawa wa damu sukari mwilini kwa vile zina kiwango kikubwa cha faiba ndani yake. Mbegu za katani zinasaidia katika kazi za kumeng'enya chakula, pia husaidia katika ufyonzaji mzuri wa mafuta na sukari. Kama unatumia mara kwa mara hizi mbegu za katani, kiasi chako cha sukari chaweza kushuka hadi asilimia 28 kwa wakati mfupi.

Jinsi ya kutumia mbegu za katani katika kutibu kisukari
• Ongeza kijiko kikubwa kimoja cha unga wa mbegu za katani ndani ya glasi ya maji au maziwa na unywe wakati wa chakula chako cha asubuhi.
• Ongeza kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa mbegu za katani katika nafaka zako unazotumia wakati wa chakula cha asubuhi.
• Ongeza pia unga wa mbegu za katani katika supu.


9. Chai ya Majani ya Mpapai
Majani ya mpapai ni mazuri katika kuongeza ufanisi wa insulini. Ni mazuri kwa watu wenye kisukari cha aina ya pili. Pia majani ya mpapai husaidia kupunguza matatizo yawezayo kuwatokea watu wenye kisukari, matatizo kama vile mafuta kwenye ini, matatizo katika kibofu cha mkojo na pia husaidia kupunguza mfadhaiko/stress. Kuna faida nyingine kubwa zaidi ya kutumia majani ya mpapai ambayo ni uwezo wake katika kutibu vidonda vitokanavyo na kisukari kwa haraka zaidi. Waganga wengi wa tiba asili kutoka Japani na Australia Na wengine wengi toka mataifa mbalimbali wamekuwa wakitumia majani ya mpapai kutibu kisukari kwa miaka mingi sasa.

Mahitaji:
• Majani 10 ya mpapai
• Maji lita 2

Maandalizi:
• Tumbukiza hayo majani ya mpapai katika maji.
• Chemsha hayo majani katika maji kwenye moto hadi maji yatakapobaki nusu yake (lita 1).
• Ipuwa na uache ipowe
• Kunywa maji haya kidogo kidogo kutwa nzima. Fanya hivi kwa mwezi mmoja mpaka miwili.
Juisi hii ya majani ya mpapai iliyoandaliwa kwa mtindo huu ni nzuri katika kuondoa sumu mwilini na kurekebisha afya yako kwa ujumla huku ikirekebisha matatizo katika mfumo wa umeng'enyaji wa chakula na kuongeza kinga ya mwili wako.


10. Juisi mchanganyiko ya asili
Hii ni juisi nzuri sana kwa mtu yeyote anayesumbuliwa na kisukari na hata shinikizo la damu, vitu vingi vinavyoingia katika juisi hii ni tiba nzuri kwa magonjwa mengi mwilini. Hii ni juisi inayotengenezwa kutokana na mchanganyiko wa vitu tofauti vifuatavyo.
  • Vitunguu swaumu 12
  • Vitunguu maji 12
  • Tangawizi 12
  • Asali ya nyuki wadogo lita 1
  • Ndimu 12
  • Chumvi ya mawe kijiko kidogo kimoja

Namna inavyoandaliwa
  • Saga (blendi) kwa pamoja vitunguu saumu na vitunguu maji pamoja na maji lita 2 na uchemshe kwenye moto kwa dakika kumi. Ikipoa chuja vizuri kupata juisi yake.
  • Saga tangawizi pamoja na maji lita 1 Ikipoa chuja vizuri kupata juisi yake, weka pembeni kwenye bakuli safi
  • Chukuwa limau au ndimu kata katikati kila moja na uchemshe kwenye moto na maji lita moja kwa dakika 15. zikishachemka subiri zipowe kisha zikamuwe na uchuje kupata juisi yake.
  • Changanya hizo juisi zote hapo juu katika chombo kimoja kikubwa na kisha
  • Ongeza asali ya nyuki wadogo mbichi nzuri lita moja, na mwisho ongeza chumvi ya mawe kijiko kidogo cha chai kimoja, koroga vizuri kwa pamoja.

Ukifuata vizuri maelezo haya mwishoni utapata juisi ya ujazo wa lita 5 au 6.
Kunywa juisi hii kikombe kimoja (robo lita) kutwa mara 3 kwa muda wa mwezi mmoja. Juisi hii inaweza kukaa bila kuwekwa kwenye friji wiki 2 hadi 3 bila kuharibika.

VITU MHIMU VYA KUZINGATIA KWA MTU YEYOTE ANAYESUMBULIWA NA UGONJWA WA KISUKARI:
  1. Acha kabisa soda ya aina yeyote pamoja na juisi za viwandani
  2. Acha chai ya rangi na kahawa
  3. Jishughulishe zaidi na mazoezi
  4. Ongeza unywaji maji na utumiaji wa chumvi hasa ya mawe ile ya baharini
  5. Dhibiti uzito wako, hakikisha una uzito ule unaotakiwa kuwa nao kwa mjibu wa urefu wako
  6. Tumia vyakula ambavyo havijakobolewa, mfano kama ni ugali tumia unga wa dona na siyo wa sembe n.k
---
Wapendwa hebu tujadili.Nilipima mwezi January nilikua na 1,22 g /L,nikapima February ikawa 1,16g/L,nikapima mwezi March ndani ya kila siku kumi na tano kwa mwezi nilikuwa 1,25g/L na 1,20 g/L respectively.Na pia nilipima mkojo wakakuta sukari .

Ila vipimo vyote hivyo nilichukua nikiwa nimefunga kula,inamaanisha kama napima kipimo kesho,leo kuanzia saa tatu usiku sili wala kunywa chochote mpaka nitakapochukuliwa kipimo kecho yake asubuhi.

Nilipoenda kumwona Dr alipoona kipimo cha mwisho akasema"Una kisukari"Nilimbishia maana mimi naona nipo kwenye limit.

Ila tokea kipimo cha kwanza nimeshaacha kabisa kula sukari,ingawa bado nakula wanga ,nafanya mazoezi.

Kiukweli hii stuation inaniumiza sana maana hata miaka 40 sijafika ingawa nimeshavuka miaka 30.

Sitaki kufa mapema kwa kisukari.
Tujadiliane wananzengo.

==============
Duniani takwimu zinaonyesha kila sekunde 10 mtu mmoja mwenye kisukari hufariki na zaidi ya watu 40,000 wenye kisukari Tanzania hukatwa miguu pia zaidi ya watu milioni 422 wana kisukari duniani hivyo kupelekea ugonjwa huu kushika nafasi ya 5 kama kisababishi cha vifo duniani. Ugonjwa wa kisukari ni moja ya ugonjwa unaowahangaisha watu wengi duniani kwani mtu anaweza akaishi na ugonjwa huu kwa muda mrefu takribani miaka 5 na kuendelea bila hata ya kujijua kuwa anatatizo la kisukari, kwa kiwango kikubwa hutokana na mfumo wa maisha wa mtu atakavyoamua kuishi, hivyo huu ugonjwa unaweza ukampata kila mtu mtoto kwa mtu mzima

Ugonjwa wa kisukari ni nini? ni ugonjwa unaotokana pale insulin inaposhidwa kubalansi sukari, ambayo homoni ya insulin hutengenezwa kwenye kongosho(pancreas) na kongosho inaposhindwa kufanya kazi vizuri hupelekea homoni ya insulin kupungua au kuongezeka na ndo hapo hutokea utofauti wa kisukari, pia ugonjwa huu hauambukizwi kutoka kwa mtu kwenda kwa mtu. Ikumbukwe kuwa kisukari huwapata mpaka watu wasio wanene(wembamba) na mama wajawazito

VISABABISHI VINAVYOPELEKEA MTU APATE UGONJWA WA KISUKARI.

Vyanzo vinavyopelekea mtu aweze kuwa mwathirika wa ugonjwa wa kisukali endapo asipovizingatia kwa umakini vyazo vikuu vipo vya aina mbili ambazo ni mfumo wa maisha na kurithi.

Mfumo wa maisha. Hii imekuwa sababu kubwa ya kuathiriwa na ugonjwa wa kisukari kwa haraka zaidi kuliko chochote na hii inatokana na ulaji (vyakula na vinywaji), kutokana na uandaaji wa vyakula kutoka vinalimwa hadi kuja kuingia kinywani mwa binadamu imekuwa ni changamoto kwa sababu ya kemikali zinazotumika kutunzia vyakula lakini pia na mtu yeye mwenyewe kama anapenda kula vitu vitamu vitamu ni kirahisi zaidi mtu huyo kuathirika kwa ugonjwa huu, uchunguzi uliofanyika huko marekani unasema kuwa mtu anaependa kula vyakula vyenye sukari nyingi au vitamu kuwa anakiwango kikubwa cha bacteria wabaya mwilini na hao bacteria hupendelea kula vitu vitamu kwahiyo inakuwa ni kirahisi sana kuchochea homone na kushidwa kwa kongosho kubalansi kiwango cha sukari mwilini.

Unene (obesity). Uzito uliopitiza kiwago ni moja ya sababu zinazopelekea mtu kuugua ugonjwa wa kisukari kwa sababu mwili wa mtu mnene unakuwa na sukari nyingi au kuwa na glucose nyingi

Kazi za ofisini. Mtu anaefanya kazi za kukaa kwa muda mrefu bila kufanya mazoezi anakuwa na hatari ya kuwa na kiwango kingi cha sukari kwa sababu anakuwa hafanyi zoezi lolote la kuweza kuunguza mafuta na sukari mwilini mwake hii ni tofauti na miaka ya 1980’s miaka hiyo watu wengi shughuri zao zilikuwa siyo za ofisini knazi zao nyingi zilikuwa za kuushughurisha mwili na hivyo ilikuwa ni kirahisi zaidi kuunguza mafuta bila hata ya kufanya mazoezi hii ni tofauti na sasa.

Kurithi. Haijafahamika kuwa nini sababu inayopelekea kurithi huu lakini kama kwenye ukoo kulikuwa na mgonjwa wa kisukari hivyo ugonjwa usishangae mtu kuugua kisukari bila hata ya hizo visababishi vya juu.

Baada ya kujifunza juu ya visababishi vinavyopelekea kuadhirika kwa ugonjwa wa kisukari hivyo ni muhimu kufahamu kuwa mtu anapokuwa na kisukari anakuwa na dalili zipi, zifuatazo ni dalili za mtu alie na ugonjwa wa kisukari.

DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI

Unapoona hizi dalili siyo kwamba ni moja kwa moja tayari una ugonjwa wa kisukari ni vema zaidi ukafika hospital ukachukua vipimo pale unapoona baadhi ya dalili ili kupata uhakika wa afya ya mwili wako japo dalili za mtu mwenye kisukali ni kama zifuatazo;

i. Kukojoa mara kwa mara. Mtu mwenye kisukari hukojoa mara kwa mara ni pamoja na insulin kushidwa kubalansi sukari mwilini na kufanya sukari iwepo kwenye damu nyingi ndo maana huchochea kukojoa mara kwa mara.

ii. Kiu isiyoisha. hii ni kwa sababu mwili wako unapoteza maji mengi kwa njia ya mkojo na hivyo husababisha mwili uhitaji mengi isivyo kawaida.

iii. Njaa kali. Ni kwasababu insulin yako haiwezi kubeba glucose mwilini mwako au hauna insulin ya kutosha ambayo husaidia kubeba lishe zilizomo kwa vyakula na kukufanya upate vitamin vya kutosha.

iv. Kuongezeka uzito. Hii inatokana na dalili ya kusikia njaa kali na hivyo humfanya mtu kula vyakula vingi na kwenda kuchochea homoni mwilini kufanya kazi pasivyo kawaida na ndio hapo unamkuta mgonjwa wa kisukali ananenepa tu.

v. Kupungua uzito. Hupungua uzito hasa pale mgonjwa wa kisukari anapokosa hamu ya kula na hivyo mwili wake hukosa lishe au virutubisha na kupoteza madini mengi mwilini mwake na seli zake hukosa chanzo cha chakula.

vi. Kukojoa mkojo na wadudu kama sisimizi na nzi kuuzingira. Kama nilivyosema hapo mwanzo kuwa bacteria wabaya wanapenda vitu vitamu hivyo na wadudu nao hivyo hivyo mgonjwa wa kisukari huwa anatoa mkojo wenye sukari nyingi na ndio maana huo mkojo unakuwa rafiki na wadudu.

vii. Kuchoka. Ili mtu awe na nguvu za kutosha ni lazima sukari ibadirishwe kutoka kwenye vyakula kwenda kwenye misuri, hivyo basi mgonjwa wa kisukari, sukari yake hubaki kwenye damu na siyo kwenye misuli na ndo maana huchoka bila hata kufanya kazi yoyote anaweza kuamka asubuhi kutoka kitandani na anakuwa kachoka.

MADHARA KWA MGONJWA WA KISUKARI NA BAADHI YA VIUNGO VINAVYOATHIRIKA ZAIDI.

Kupenda vitu vitamu hususani jamii ya sukari huwa ni tamu sana kwenye ulimi lakini changamoto inakuja kule inakoelekea kwa ajili ya kutunzwa na kutumika, hapo ndo husababisha changamoto mbalimbali mwilini hasa kwenye baadhi ya viungo vya mwili. Yafuatayo ni madhara ya sukari inapozidi mwili na kiwango sahihi cha sukari inayotakiwa mwili pale unapokuwa umekula chakula:

·vidonda vya miguuni (diabetes foots). Ugonjwa wa kisukari huathiri miguuni hasa pale unapopata ganzi inapelekea kushidwa kuhisi maumivu hivyo hata ukipata jeraha au mchubuko unakuwa huhisi maumivu ya aina yoyote unakuwa hauna tofauti na aliechomwa sindano ya ganzi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji,
vidonda vya mtu mwenye kisukari ni vigumu sana kupona kwa sababu damu inakuwa haifiki ya kutoshakwenye kidonda na asilimia kubwa bacteria wabaya
huanza kukishambulia kwa kasi kwa sababu kinakuwa ni kitamu

diabetes6


kwa bacteria na kinaonekana kuwa na malengelenge ya mafuta na hao bacteria hushambulia kwa kasi hivyo kusababisha kuongezeka kwa kidonda na mwishoe kukatwa endapo hatawahi huduma mapema ya kujikinga.

Kutokuona vizuri au mtoto wa jicho. Mishipa ya kwenye macho huwa ni midogo midogo sana na iko laini sana ukiliganisha na mishipa ya sehemu zingine za mwili hivyo inapoingiliwa na sukari damu hushidwa kupita ya kutosha sehemu za macho na kumfanya mtu awe anaona ukungu ukungu au kutokuona kabisa.

Madhara ya figo. Figo inapokuwa imezidiwa na kiwago kingi cha sukari hulazimika kupunguza maji ya ziada na utengenezaji wa calcium kwa ajili ya kulinda mifupa hivyo sukari nyingi kukimbilia kwenye damu na baadaye huwa sumu mwilini.

Kiharusi (stroke). Kwa kuwa madhara ya sukari mojawapo ni kudhoofisha mishipa kwenye mwili hivyo mtu wa kisukari ana hatari kubwa ya kupata stroke kwa sababu baadhi ya mishipa kwenye ubongo huathiriwa na kukosa uwezo wa kupitisha damu ya kutosha na mwishoe kupasuka na kusababisha kiharusi.

Maradhi ya moyo. Vyanzo vya mishipa huanzia kwenye moyo na kusambaa pande zingine za mwili, moyo huathiriwa na ugonjwa wa kisukari kwa sababu sukari hudhoofisha mishipa na kumfanya mtu kuwa dhaifu hivyo kama damu haipiti ya kutosha kwenye mishipa inakuwa ni kirahisi kupata magonjwa ya moyo kama vile moyo kupanuka, moyo kuwa na tundo pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo.

·Kwa wanaume kuishiwa nguvu za kiume. Hili ni tatizo kubwa kwa wanaume kwa sababu mfumo wa uzazi wa mwanaume umeundwa kwa mishipa na misuli, kama patakuwa hakupati ujazo mzuri wa damu inakuwa ni rahisi sana kushidwa kushiriki tendo ndoa na wengi wao wanapopatwa na hali kama hii huigiwa na presha au msongo wa mawazo na kuibuia matatizo mengine tena.

Hayo ni baadhi ya madhara anayopatwa mtu mwenye kisukari japo anaweza kupatwa na changamoto zingine nyingi kwenye mwili wake na kumpelekea kupata shida awe mtoto au mtu mzima, lakini jinsi kwa kukosa uelewa na umakini zaidi kundi la watu wengi huishia kukatwa baadhi ya viungo na mwishoe kifo.

Lakini ujue kuwa kama ugonjwa siyo wa kuambukizwa itashidikanaje kuuzuia ili usiendelee kukudhuru usipatwe na madhara makubwa ya kiafya , moja ya suluhisho ambalo limesaidia watu kadha wa kadha linalotokana na mimea, mitishamba mboga mboga ambazo husaidia kurudisha ubora wa mwili kama mwanzo na badae unakuwa na afya njema jifunze kuhusu hii program inavyofanya kazi.


Changamoto ya kisukari inaweza kabisa kuepukika endapo tu ukiwa na nia ya kujiimarisha bila kukata tamaa ya kuitumia hii program, kama wengine imeweza kuwaimarisha na wakawa vizuri kwanini isiwe kwako pia. Kuna ubora gani kwa hii program.
  • Inasaidia kuogeza uwezo wa kinga mwilini na kukupa nguvu hivyo kuondoa uchovu wa bila sababu
  • Inaimarisha uwezo wa tendo la ndoa kwa pande zote kwa wanaume na kwa wanawake, pia inaimarisha tezi dume kwa wanaume.
  • Inaondowa hatari ya kupata kiharusi kwani hewa(oxygen) na damu vitakuwa inapita vyema kwenye ubongo
  • Inasaidia kuondoa sumu mwilini na kubalansi kiwango cha sukari mwilini kama imepanda zaidi huishusha na kama imeshuka zaidi huipandisha.
  • Inasaidia kuondoa bacteria wabaya na kuwapandisha uwezo wa utendaji kazi wa bacteria wazuri.
  • Inasaidia kuhakikisha mzunguko wa damu uko sawa na ujazo ulio sawa kwenye mishipa
  • Endapo kama tayari mwathirika anavidonda sehemu yoyote ya mwili hufanya kazi kukausha vidonda na kuondoa bila kuonyesha makovu.
  • Inaisaidia kongosho utoaji wa insulin kufanya kazi vizuri
  • Inamchanganyiko wa mbogamboga ambazo hufanya kazi ya kukupa damu na nyuzi nyuzi ili kusaidia upataji wa choo usiwe wa shida.
  • Inasaidia kuondoa matatizo ya macho na kuondoa mtoto wa jicho bila kukwanguliwa kwa kutumia vifaa
Hakuna changamoto ya kudumu chini ya jua vyote vina suluhisho, amuwa kuwa wa tofauti kwa kutafuta suluhisho kwa matendo. Wasiliana nasi ili kujua zaidi kuhusu kisukari na suluhisho lake kwani hatukuumbwa ili tuteseke na kisukari bali tuishi wenye afya tele.

=====

Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni magonjwa ambayo hayasambazwi kwa mtu mwingine kwa kuwa hakuna vimelea mwilini vinavyohusiana na magonjwa hayo. Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni kama ya moyo na mishipa ya damu, figo, saratani, kifua sugu, kisukari, magonjwa ya akili na mengine ya kurithi kama vile ugonjwa wa selimundu (Sickle Cell Disease).

Ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ya 2013, inadai magonjwa yasiyo ya kuambukiza ndio chanzo kikubwa cha vifo ulimwenguni, yakifanya asilimia 63 ya vifo vyote kwa mwaka. Magonjwa yasiyo ya kuambukiza huua watu zaidi ya milioni 36 kila mwaka. Asilimia 80 ya vifo vinasababishwa na magonjwa hayo hutokea nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi hizo. Inakisiwa kuwa mwaka 2020 magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza yatasababisha asilimia 73 ya vifo vyote duniani na asilimia 60 ya ukubwa wa tatizo la magonjwa duniani.

Nchini Tanzania, katika mpango wa upimaji wa afya kwa magonjwa yasiyoambukiza jijini Dar es Salaam, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umebaini kuwa idadi kubwa ya wanaume wanapatwa na magonjwa hayo kuliko wanawake. Uchambuzi huo umeonyesha magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari, shinikizo la damu na saratani zote ambazo zimekuwa chanzo cha vifo hivyo, huku serikali ikisema imeamua kuongeza juhudi za makusudi kupambana nayo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mfuko wa Bima ya Afya, athari ya magonjwa yasiyoambukiza ni mara nne zaidi ya watu waliopo mijini kuliko vijijini, huku asilimia 12.8 ya wanaougua wakiwa wako mijini na asilimia 3.1 wako vijijini kutokana na mfumo wa maisha.

Uchunguzi mwingine uliofanywa na jopo la madaktari bingwa kuanzia mwaka 2011 hadi 2014 ulibaini asilimia 79 ya watanzania wazee waligundulika kuugua magonjwa ya kisukari, macho na shinikizo la damu. Pia walidai magonjwa hayo yamekuwa kikwazo cha maendeleo kutokana na kuwasumbua wazee na hata wenye umri wa kati ya miaka 40 na 50.

Kisukari ikiwa ni moja ya muuaji wa kimya kimya katika kundi hili la magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Watu milioni 285 duniani kote wameathiriwa na kisukari ambayo ni sawa na asilimia 6.6 ya idadi ya watu wote ulimwenguni pia ikishika nafasi ya 5 kwa kusababisha vifo duniani.

Nchi zinazoongoza kwa idadi kubwa ya watu wenye kisukari ni China wagonjwa milioni 43.2, India wagonjwa milioni 40.9, Marekani wagonjwa milioni 25.8, Urusi wagonjwa milioni 9.6 na Brazil wagonjwa milioni 6. Nchi zenye idadi kubwa ya watu wazima wenye kisukari ni Nauru kwa asilimia 30, Bahrain kwa asilimia 25.5, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa asilimia 25, Saudi Arabia kwa asilimia 23.7 na Mauritius kwa asilimia 20.

KISUKARI NI NINI HASWA?

Sukari mwilini hutokana na vyakula pamoja na vinywaji tunavyotumia kila siku na hutumika kuupa mwili nguvu. Glukosi ni aina ya sukari ambayo huzipa chembe za mwili nishati. Hata hivyo ili glukosi iingie ndani ya chembe hizo inahitaji insulini. Insulini ni kemikali (Homoni) ambayo hutokezwa na kongosho (Pancrease).

Kisukari ni ugonjwa unaotokana na mtu kuwa na sukari nyingi kupita kiasi kwenye damu. Ugonjwa huo huvuruga utaratibu wa kuingiza sukari ndani ya chembe kutoka kwenye damu kwa kuwa chembe huhitaji sukari ili kupata nishati.

Ugonjwa wa Kisukari hutokea pale ambapo tezi ya kongosho inaposhindwa kutengeneza kichocheo (Homoni) aina ya insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho na kusababisha kuongezeka kwa sukari (Hyperglycemia) au kushuka kwa kiwango cha sukari (Hypoglycemia). Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababishwa na kuwa na kiwango kidogo cha insulin mwilini, mwili kutosikia kichocheo hicho au yote mawili.

TAKWIMU MBALIMBALI ZA UGONJWA WA KISUKARI

Kulingana na ripoti mbalimbali karibu watu milioni 316 ulimwenguni pote wana kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu, ingawa wengi wao hawajui wana kiwango hicho. Kwa mfano, nchini Marekani pekee asilimia 90 ya watu wenye sukari nyingi kwenye damu hawatambui kama wana tatizo hilo. Ingawa asilimia 8.3 ya watu watu wa Marekani wana Kisukari ambayo ni sawa na watu milioni 25.8 na kufanya Kisukari cha 7 kusababisha vifo vya watu Marekani.

Mamilioni ya watu wana ugonjwa huo lakini hawana habari! Ni ngumu zaidi kutibu ugonjwa wa kisukari kwa kuwa mtu anaweza kuishi nao kwa muda mrefu kabla haujagunduliwa. Hiyo ndiyo sababu watu husema kwamba ugonjwa huo huua kimyakimya.

NINI CHANZO HASA CHA KISUKARI?

Ili kuelewa vyema ugonjwa wa kisukari ni muhimu kwanza kuelewa namna chakula kinavyovunjwa vunjwa na kutumiwa na mwili ili kuzalisha nguvu. Wakati chakula kinapoyeyushwa matukio kadhaa hutokea. Moja ni sukari inayoitwa glucosi ambayo ni chanzo cha nishati/nguvu mwilini huingia katika damu. Tukio la pili ni kiungo kinachoitwa kongosho (Pancrease) kutengeneza kichocheo cha insulini. Kazi ya insulini ni kuondoa glucosi katika damu na kuingiza katika misuli, seli za mafuta na ini, ambako hutumika kama nishati.

Watu wenye kisukari huwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kuliko inavyotakiwa kwa sababu miili yao haiwezi kupeleka sukari kwenye seli za mafuta, ini na misuli ili ihifadhiwe kwa ajili ya kuzalisha nguvu. Hii ni kutokana na moja ya sababu zifuatazo, huenda kongosho zao haziwezi kutengeneza insulini ya kutosha au seli za mwili wao haziathiriwi na insini kama inavyotakiwa au sababu zote hizo mbili.

Main Symptoms of Diabetes FikraPevu.com
Kama wewe ni mnene kupita kiasi, hufanyi mazoezi kwa ukawaida au una watu wa ukoo walio na kisukari, huenda tayari una kiwango cha juu cha sukari kwenye damu. Ongezeko la sukari kwenye damu mbali na kuwa kisababishi cha kisukari, hali hiyo inahusianishwa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa akili uitwao 'DEMENTIA'.

Kula sukari nyingi sio sababu ya ugonjwa wa kisukari. Lakini lazima tuseme kwamba kula sukari nyingi si nzuri kwa afya yako kwani utaongeza uzito wa kuweza kuathiri uwezo wa mwili wako kujikinga na maradhi tofauti. Ugonjwa wa kisukari umeitwa kwa kufaa "ugonjwa unaoathiri kiini cha nishati ya mwili". Mwili unaposhindwa kutumia glukosi, mifumo mbalimbali ya mwili inaweza kuacha kufanya kazi au hata kusababisha kifo.

Ugonjwa wa Kisukari kitaalamu hujulikana kama 'DIABETES MELLITUS'. Jina 'Diabetes Mellitus' linatokana na neno la Kigiriki linalomaanisha 'kunyonya' na neno la Kilatini linalomaanisha 'tamu kama asali'. Maneno hayo yanafafanua vizuri sana ugonjwa huo, kwani maji hupita mwilini mwa mtu aliye na ugonjwa wa kisukari kana kwamba yananyonywa na mdomo na kupitia kwenye njia ya mkojo kisha kutoka nje ya mwili. Isitoshe mkojo huwa na ladha tamu kwa kuwa una sukari. Ndiyo sababu kabla ya kuvumbua njia bora za kupima ugonjwa huo, mbinu moja ya kutambua kama mtu ana ugonjwa wa kisukari ilikuwa kumwaga mkojo wa mgonjwa karibu na kichuguu cha sisimizi. Ikiwa sisimizi wangevutiwa na mkojo huo basi hilo lilimaanisha kwamba mkojo una sukari.

NI NANI ANAWEZA KUWA NA UGONJWA WA KISUKARI?

Watu walio katika makundi yafuatayo wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kisukari:-

– Wenye uzito uliozidi,

– Wenye historia ya kuwa na wagonjwa wa kisukari katika familia zao,

– Wanawake waliozaa watoto wenye kilo 4 au zaidi,

– Watu wasiojishughirisha au wasiofanya mazoezi,

– Wenye shinikizo la damu,

– Wenye msongo wa mawazo na

– Wenye matumizi makubwa ya pombe na sigara.

Watu hawa wanashauriwa kupima sukari yao kila mwaka wakiwa na umri wa miaka 45 na kuendelea.

Kuna hatari kubwa ya kuugua ugonjwa huo ikiwa mtu ana mafuta mengi katika tumbo na kiuno chake kuliko katika mapaja yake. Mafuta katika kongosho na ini huvuruga uwezo wa mwili wa kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu.

Wavutaji wa sigara wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi kwani zoea hilo hudhuru moyo na mfumo wa mzunguko wa damu na kubana mishipa ya damu. Kitabu kimoja kinasema kwamba asilimia 95 ya watu wanaougua kisukari ambao hulazimika kukatwa viungo ni wavutaji wa sigara.

DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI

~ Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati.
~ Kwenda haja ndogo mara kwa mara. Watoto kukojoa kitandani.
~ Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.
~ Kupungua uzito au kukonda licha ya kula vizuri.
~ Kusikia njaa kila wakati na kula sana.
~ Wanawake kuwashwa ukeni.
~ Kutoona vizuri.
~ Kupungua nguvu za kiume au hamu ya kujamiiana kwa wanawake.
~ Ganzi, kuchomwachomwa au kutohisi unapoguswa sehemu za miguu, viganja na vidole.
~ Miguu kuoza na hata kupata gangrini.
~ Kukaukwa na ngozi na pia kupata aina ya ngazi katika miguu.
~ Vidonda au majeraha sehemu yoyote ya mwili kutopona haraka.
~ Majipu mwilini.

Wenye dalili hizi wanashauriwa kupima sukari ili kubaini kama wana kisukari.
----------------------------
Ugonjwa wa Kisukari ni miongoni mwa magonjwa sugu yanayoendelea kuathiri afya za mamilioni ya watu wa nchi nyingi duniani ikiwamo Tanzania.
Ugonjwa huu hutokea pale ambapo tezi ya kongosho inaposhindwa kutengeneza kichocheo aina ya Insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho na kusababisha kuongezeka au kushuka kwa kiwango cha sukari kwenye damu au hyperglycemia.

Aina za kisukari
Kisukari kimeanishwa katika makundi yafuatayo:

Kisukari Namba Moja
Hii ni aina ya kisukari inayowaathiri zaidi watoto na vijana. Aina hii hutokea iwapo seli maalum zinazotengeneza homoni ya insulin zijulikanazo kama beta cells of Islet of Langerhans. Iwapo tezi kongosho zitakosekana au zitaharibika kwa sababu yeyote ile, na hivyo kusababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu.

Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa seli hizi katika tezi kongosho ni pamoja na kushambuliwa kwa tezi hiyo.
Mashambulizi katika kongosho huweza kufanywa na magonjwa yanayosababisha upungufu wa kinga ya mwili. Uharibifu katika tezi kongosho hupelekea kukosekana kabisa kwa wa tezi ya insulin au huifanya tezi hiyo kuzalishwa kwa kiwango kidogo.

Wagonjwa wa aina hii ya kisukari huhitaji kupewa dawa za insulin kwa njia ya sindano katika maisha yao yoteili waweze kuishi. Ndiyo maana aina hii ya kisukari huitwa pia kisukari kinachotegemea Insulin au Insulin Dependent Diabetes Mellitus (IDDM)

2. Aina ya Pili ya Kisukari
Hii ni aina ya kisukari inayotokea zaidi ukubwani. Aina hii ya kisukari husababishwa na kupungua kwa ufanisi utendaji kazi wa homoni ya insulin.

Hali hii husababishwa na unene uliopitiliza yaani obesity, au hali ya kutofanya mazoezi kabisa (physical inactivity).
Kwa vile, katika aina hii ya kisukari, insulin huzalishwa katika kiwango cha kutosha isipokuwa tatizo lipo kwenye ufanisi wa utendaji kazi wake.

Wagonjwa wa aina hii ya kisukari hawahitaji kupewa insulin kwa njia ya sindano. Ndiyo maana aina hii hujulikana pia kama kisukari kisichotegemea insulin au Non-Insulin Dependent Diabetes Mellitus (NIDDM)

3. Kisukari cha Ujauzito
Ni aina ya kisukari kinachotokea pindi kunapokuwa na ongezeko la kiwango cha sukari katika damu (hyperglycemia) wakati wa ujauzito. Aina hii ya kisukari huathiri karibu asilimia 2-5 ya wanawake wajawazit, ingawa wengi wao hupata nafuu na kupona kabisa mara tu baada ya kujifungua.

Hata hivyo, karibu asilimia 20 mpaka 50 ya wanawake wajawazito wanaopata aina hii ya kisukari huweza kuendelea nacho hatimaye kuwa aina ya pili ya kisukari maishani.

Kisukari husababishwa na nini?
Visababishi vya kisukari hutofautiana kulingana na aina husika ya kisukari.

1. Visababishi vya aina ya kwanza ya kisukari
Aina ya kwanza ya kisukari ina uhusiano mkubwa sana na kurithi. Aidha aina hii pia husababishwa na maambukizi ya Coxsackie virus type B4.

Visababishi vingine ni pamoja na sumu inayotokana na kemikali za baadhi ya vyakula (food borne chemical toxins), na kwa baadhi ya watoto wachanga maziwa ya ng’ombe yanaweza kuchochea kinga ya mwili wa mtoto kuushambulia mwili wenyewe (autoimmune reaction) na hivyo kupelekea uharibifu katika tezi kongosho.

2. Visababishi vya aina ya pili ya kisukari
Kwa ujumla aina hii ya kisukari husababishwa zaidi na mfumo wa maisha na matatizo ya kurithi. Aidha vitu kama kuongezeka uzito na unene kupita kiasi (obesity) nayo pia huchangia kutokea kwa aina hii ya kisukari.
Sababu nyingine ni pamoja na Kuongezeka umri, maisha ya kivivu na kutofanya mazoezi (physical inactivity).

===
PIA UNASHAURIWA KUSOMA MADA HIZI:
- Tambua siri ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari - JamiiForums

- Dawa nyingi mbadala za Ugonjwa wa kisukari zinazotangazwa ni utapeli mtupu, fuata ushauri huu - JamiiForums

- Usizidharau ishara hizi 8 za ugonjwa wa kisukari - JamiiForums
 
Siku hizi watu wengi khususan watu wazima, wanaume na wanawake wanataabika sana kwajili ya ugonjwa wa sukari.

LISHE KWA MGONJWA WA KISUKARI

Suala la lishe kwa wagonjwa na hapa tunamuangalia mgonjwa wa kisukari. Kama tulivyokwisha ona katika makala nyingine zilizopita, mgonjwa yeyote wa magonjwa hatari kama presha, moyo, saratani, kisukari n.k, ni lazima ajue vyakula anavyopaswa kula au kutokula.

Elimu ya lishe ni muhimu sana, kwani madhara ya ugonjwa huonekana haraka na hata kusababisha kifo upesi, iwapo mtu ataendelea kula bila kujijua vyakula vilevile vilivyosababisha tatizo la kiafya alilonalo.

Kwa ujumla, mgonjwa wa kisukari (Diabetic), hana mipaka mingi ya vyakula, anaweza kuendelea kula vyakula vingi kama kawaida iwapo atajua jinsi ya kula, kiasi gani na kwa wakati gani. Hata hivyo, kama ulaji wake ulikuwa hauzingatii ulaji sahihi, baada ya kuugua hana hiyari bali kufuata kanuni za ulaji sahihi.


Kanuni kuu ya ulaji anayopaswa kuzingatia mgonjwa wa kisukari ni kula kiasi bila kushiba sana, kula kwa muda uleule kila siku, na kula mchanganyiko wa matunda, mboga na nafaka zisizokobolewa. Hii ina maana kwamba mgonjwa anatakiwa asisikie njaa wala shibe muda wote wa siku.

KITU GANI UNAKULA?

Bila kujali kama una kisukari au la, afya bora iko mikononi mwako kwa kuwa na hiyari ya kuchagua unachokula. Lakini unapokuwa tayari mgonjwa, unakuwa huna hiyari tena ya kuacha kuzingatia ulaji sahihi, vinginevyo unakiita kifo haraka. Kimsingi, mgonjwa wa kisukari azingatie zaidi ulaji wa vyakula vitokanavyo na mimea, aache kula vyakula vya kusindika, vyenye sukari na mafuta mengi.

WAKATI GANI WA KULA?
Suala la kujali muda wa kula kwa mgonjwa wa kisukari ni la lazima, kwa sababu atatakiwa wakati wote kudumisha kiwango cha sukari mwilini mwake kwa kula kwa wakati uleule ili kuepuka kusikia njaa ambayo husababisha sukari kushuka kwa kasi.

KIASI GANI UNAKULA?
Vilevile suala la kula kiasi kwa mgonjwa wa kisukari si la hiyari tena, bali ni la lazima. Hata mtu akila vyakula bora vyenye virutubisho vya hali ya juu kiasi gani, kama akivila kupita kiasi huweza kusababisha unene ambao ni sababu moja wapo ya ugonjwa wa kisukari, hivyo ni muhimu kuzingatia kiasi.
Mgonjwa wa kisukari hahitaji kuwa na chakula maalumu, bali anatakiwa kutilia maanani ulaji wa mboga, matunda na nafaka zisizokobolewa. Lishe ya mgonjwa wa kisukari ni ya kawaida tu yenye vyakula vyenye virutubisho vingi na mafuta kidogo na kiasi kidogo cha wanga.

ZINGATIA

Mgonjwa wa kisukari anashauriwa kula matunda, lakini anakatazwa kunywa juisi za matunda. Halikadhalika, matunda kama ‘Apples’, ‘Peas’ na mengine ya jamii hiyo, ni bora yaliwe pamoja na maganda yake.
Miongoni mwa matunda bora kabisa kwa mgonjwa wa kisukari ni zababi mbivu, hizi zikiliwa kila siku mara tatu kwa siku, huweza kuwa tiba kabisa ya kisukari.

Halikadhalika majani ya embe nayo ni dawa ya kisukari. Loweka majani mabichi ya mwembe, kiasi cha kiganja kimoja (gramu 15), kwenye nusu lita ya maji usiku kucha, kisha asubuhi yakamue upate maji yake, kunywa kila siku asubuhi na unaweza kukidhibiti kisukari, hasa kile kinachopanda nyakati za asubuhi.
 
Salaam!

Katika milo yote iwe kifungua kinywa, mchana, usiku ama kati ya hiyo- mgonjwa wa kisukari anatakiwa kupunguza vyakula vya wanga- wali, ugali n.k.

Kwa ujumla vyakula vinavyoshauriwa ni vile vyenye "glycemic index ama glycemic load" ndogo.

Vyakula kama 'wholegrains' zina fibre kibao na ndio vizuri zaidi. Kwa hiyo ni vizuri kula matunda na mbogamboga zaidi.

Vinywaji visivyokuwa na sukari pia sio mbaya. Ikiumbukwe kuwa vinywaji vyenye sukari, soda za kawaida kwa mfano sio nzuri hata kwa wasio na kisukari! Zaleta tatizo la kuongezeka uzito-

Kisha mazoezi ni muhimu sana kwa mgonjwa wa kisukari.

Diet ya kuangalia tu kwenye mtandao sio nzuri sana- ingawa waweza kuangalia baadhi ya vyakula, ni nzuri zaidi kuongea na daktari wako ili muweze kupanga nini cha kula- kutokana na mahali mtu anapoishi.

Pombe ni ya kuepuka vilevile.

Kila la kheir.
 
Insulin resistance hutokea kwa watu wote ambao ni obese na hii husababishwa na kemikali ambazo hutolewa na adipose tissue,lakini hii hali(insulin resistance) uweza kusababisha ugonjwa wa kisukari kama pancrease itakuwa haifanyi kazi vizuri,ila kama itakuwa inafanya kazi vizuri itaweza kuzuia hali hiyo hivyo kuweza kuzuia tatizo lisitokee.

Causes of diabetes
TYPE I-caused by completely abscent of insulin hormone due to auto destruction of the pancrease gland.

TYPE 2-caused by few number of insulin receptors (GLUT-4) or their abnormality,another cause is insulin resistance ,only possible if the portion of the pancrease responsible for secrection of insulin is not able so secrete sufficient amount so as to overcome this resistance.
 
DAWA YA UGONJWA WA KISUKARI

Upate aina za dawa zifuatazo, kila moja kiasi cha gram 100, saga pamoja na dawa zifuatazo:

1. Shubiri
2. Ubani
3. Mvuje
4. Ukwaju
5. Habasoda (kiasi cha dawa hizi hazijatwangwa, hivyo jaribu kukadiria mwenyewe) baada ya kusaga vizuri, gawanya katika mafungo matatu yaliyosawa.

Changanya fungu moja na maji kiasi cha chupa mbili na uchemshe kwa dakika kumi. Ipua na iwache ipoe, chuja na hifadhi katika chupa nadhifu. MATUMIZI YA DAYA YENYEWE Tumia kila siku kikombe kimoja cha kahawa kabla ya kula chochote asubuhi kwa muda wa siku 13. Ikiisha dawa hii basi chukua fungu la pili na uchemshe kama ulivofanya kwa fungu la mwanzo. Tumia daya hii tena kwa muda ule ule wa siku 13.

Itakapokwisha dawa hii basi chukua fungu la tatu na uitayarishe kamaUlivyofanya mafungu mawili ya mwanzo. Tumia dawa hii kama dawa hizo mbili za mwanzo ila tu kwa muda wa siku 14 , hii itafanya jumla ya siku za kunywa daya kuwa siku 40. Baada ya siku hizo 40 utajisikia kuwa ugonjwa wa kisukari umekwisha na unaweza kuanza kula vitu vyote ulivyokuwa umekatazwa. Inshallah kwa kudra zake mwenyezi mungu utakuwa umepona maradhi hayo.

Ndugu yangu muislam, ninakuomba unisaidie kuieneza karatsi hii bila malipo ya kipesa na inshallah utapata malipo yaliomema hapa duniani na kesho akhera. Kufanya hivyo utakuwa unaendeleza bidii kubwa iliyofanywa na Kadhi mkuu wa Tabuk Shaikh Saleh Mohammed Al-Tanjisiy amabaye alifanya juhudi kubwa kwa muda mrefu kufanya majaribio ya dawa hii. Mwenyezi mungu amjaze na kumfikishia kila la kheri duniani na akhera pamoja na sisi sote, Amein.

Maandishi haya yamechapishwa upya na Hamoud Hilal Al-Rawahy kwa Nia ya kuyaboresha maandishi haya na kwa nia ya kusambaza ujumbe huu kwa watu wengi inavyowezekana.
 
Nimekuwa na diabetes kwa miaka 12 uzito nilikuwa 92kg,miaka ya karibuni nimeanza kufanya mazoezi mara 3 kwa wiki,kukimbia,kupunguza kula,kulala mapema na kunywa maji mengi.

Kwanza nilikuwa nameza vidonge 8 kwa siku,baada ya kuanza mazoezi nikapunguziwa mpaka 2 kwa siku.Sasa nina uzito 78kg na niko fit sichoki nikikimbia au mozoezini.Kwa muda wa mwezi sijahitaji kumeza dawa mwili umeweza kumudu.

Daktari kanishauri niendelee kupima glucose asubuhi na usiku mwenyewe na kit yangu kwa muda wa mwezi mwingine na kama nitaendelea hivi nitakuwa nimepona.Nilikuwa na type 2 nawashauri wenzangu wenye diabetes wajaribu haya labda nao watafaidika.
 
@Lagatege,
Same here. Nilikuwa kama wewe, uzito huhuo, nimefanya mazoezi, dieting, kuepuka kula mafuta na vyakula vya starch, kula mboga za majani, matunda etc, acha pombe hasa beer, utajikuta uko fit kwa kila hali.
 
Asante sana,hata mie ninakisukari lakini situmii dawa mara nyingi nakula brown bread na jioni sile chochote,nataka kuanza mazoezi hivi karibuni kwani nilikuwa nimeacha sababu ya kazi, nakunywa maji sana,asante kwa ushauri
 
Nadhani mazoezi na dieting ni njia natural kwa kupamabana na ugonjwa huu. Nawashauri wenye kazi za kukaa na usafiri wa gari watumie ngazi badala ya lift.
 
Ndugu naomba mpangilio wa diet yako kwa mfano je hizo mbogamboga zinakuwa chukuchuku au,je diet sodas zinafaa na je ndio kwamba huwezi kula ugali au.
tafadhali nisaidie huo mpangilio wa unavyokula,
asante
 
Ndugu naomba mpangilio wa diet yako kwa mfano je hizo mbogamboga zinakuwa chukuchuku au,je diet sodas zinafaa na je ndio kwamba huwezi kula ugali au.
tafadhali nisaidie huo mpangilio wa unavyokula,
asante
Inafaa tukumbuke tena kwamba ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa wa shahamu (cholesterol) vile vile.

Mtu anaweza kuendelea kula chakula chake cha kawaida ili mradi anakumbuka kwamba ni suala muhimu sana kupunguza utumiaji wa mafuta, siagi, samli na margarin.

Mtindo wa kumimina mafuta moja kwa moja katika sufuria au kikaangio si mtindo wa busara hata kidogo. Ni jambo la maana na busara kutumia kijiko cha kulia katika kupima kiasi gani cha mafuta mtu anatia katika mapishi:

Hakikisha kwamba unatia kijiko kimoja cha kulia kwa kila mtu mmoja katika ukoo.

Chakula cha kuchemsha ni cha siha zaidi kuliko cha mikaango kwa sababu ya upungufu wa mafuta.

Afadhali kula chapati/mkate wa kusukuma wa ngano nzima upikwao mkavu bilaya mafuta kushinda ule unaokaangwa kwa mafuta.

Epuka pilau na wali wa nazi na afadhali ule wali wa maji.

Hakikisha kwamba unaitoa, kuikeketa na kutupa shahamu yote ya nyama kabla hujaitia chunguni.
 
Nilipogundulika nina diabetes nilichanganyikiwa na masharti mengi niliyoelezwa na madaktari na watu wengine kuhusu kula mpaka nilipoelekezwa na doctor mmoja kuwa naweza kula vyakula vya kawaida lakini badala ya kula milo 3 mikubwa nile milo 5 midogo kwa siku,mafuta yanayokatazwa ni yanayotokana na wanyama,kijiko 1-2 cha mafuta yoyote ya mimea ni nzuri.

Badala ya kula matunda mengi mara 1 na kupandisha glucose kula kwa mfano ndizi asubuhi,kipande cha papai mchana na embe jioni.Vegetables unaweza kula kiasi utakacho.Kuna kitu ambacho kila mwenye diabetes inabidi ajue,kijiko kidogo cha dalasini-abdalasini(cinammon) katika chai au kahawa asubuhi kinapunguza asilimia 20% ya glucose mwilini na kwa mtu ambaye sukari yake haiko juu sana inatosha kuidhibiti.
 
Diabetes.jpg




Watu walio na ugonjwa wa Sukari (kama watu wale wengine) lazima watilie mkazo afya yao ya kila siku.Tofauti imo: walio na ugonjwa wa Sukari, kila siku lazima wapime sukari, wafanye mazoezi na wazingatie afya yao. Ikiwa wewe au mtu unayemjua ana ugonjwa wa Sukari na ameamua kuishi maisha yenye afya, basi Sehemu ya Kujifundisha itakuongezea maarifa kuhusu huu ugonjwa na kukuelekeza kuishi ukiwa na afya.
Hatua ya 1: Jifunze kuhusu ugonjwa wa Sukari
Ni vizuri kujua mambo mengi kuhusu ugonjwa wa Sukari ili uweze kuukimu. Hapa ni yale unayotakikana kujua na kufanya.
Jua ni aina gani ya ugonjwa wa sukari unayo na hatari zake


Usiogope kuuliza maswali na kujua pale utakapopata majibu.

Elewa kuhusu kiwango cha sukari damuni mwako na ni tiba ipi utakayo tumia.

  • Fanya mtihani mdogo kuhusu Insulini.
  • Insulini 101
  • Video: Insulini
  • Ugonjwa wa sukari: Kile unachohitaji.
  • Fungua uchapishe hati, inayokufundisha kufuatilia kiwango cha sukari damini yako.
Fungua uchapishe mpango wa afya nzuri waliye na Ugonjwa wa Sukari.

 
Uja Uzito Na Ugonjwa Wa Sukari

Vidokezi kwa kina mama waja wazito
Unapojiandaa kusheherekea furaha tele kwa kupata mtoto, ni muhimu ujue namna ya kukabiliana na ugojwa wa sukari. Hapa vidokezi vitano vya kuweka akilini kila mara:
1. Husiana kwa karibu na kundi la maafisa wa afya bora ambao ni pamoja

  • Daktari au muhudumu wa kiafya aliye na ujuzi wa kutunza wagonjwa wa Sukari
  • Daktari aliye na maarifa ya uzalishaji anayeweza kushughuikia matatizo katika uja uzito na ambaye amewahi kushughulikia kina mama waja wazito walio na ugonjwa wa Sukari
  • Daktari wa watoto au wa watoto wachanga ambao wamezaliwa ambaye anajua kutibu shida maalum zinazoweza kuwakumba watoto wanaozaliwa na kina mama wanaougua ugonjwa wa Sukari
  • Muhudumu wa ulaji aliyesajiliwa anayeweza kukupangia na kukubadilishia chakula wakati wa uja uzito na baada ya kujifungu
  • Daktari wa ugonjwa wa sukari anayeweza kukusaidia kukabiliana na ugonjwa huu wakati wa uja uzito.
2. Uwe maakini sana na madawa yako: Iwapo unatumia tembe za ugonjwa wa Sukari, inaweza kuwa vigumu kuendelea nazo wakati wa uja uzito. Daktari wako anaweza kukupa ushauri wa kujitibu kwa kujidunga dawa ya Insulin ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini badala ya kuendelea na hizo tembe.

3. Kagua kiwango cha sukari katika damu yako: vile tu unavyoagizwa na daktari au muhudumu wako wa afya bora.

4. Zingatia ushauri wa mjuzi wa lishe bora: fuata mwongozo wake wa aina za vyakula unavyostahili kuvitumia ili kiwango cha sukari mwilini mwako kithibitiwe.

5. Mazoezi ni muhimu katika kutibu ugonjwa wa Sukari: Haijalishi iwapo wewe ni mja mzito au la. Zungumza na daktari wako akueleze iwapo kuna tatizo lolote linaloweza kutokea iwapo utafanya mazoezi ukiwa mja mzito. Ni muhimu kujua hasa kwa wale ambao wana ugonjwa wa Moyo pamoja na, au kiwango cha juu cha sukari mwilini.
 
Niko hatarini kiasi cha kwamba naweza kupata ugonjwa wa Sukari?

Wanasayansi wameshindwa hasa kutambua kinachosababisha ugonjwa wa Sukari mwilini. Pia hakuna hatari zilizo wazi za kuonekana kwa macho kwa aina ya kwanza (Diabetes 1). Lakini aina ya pili (Diabetes 2) ina dalili:
Unene – Hii ni dalili ya kwanza hatari.Mtu akiwa mzito, ana nafasi kubwa ya mwili mwake kukataa aina ya dawa ya insulin kwa sababu mafuta huzuia namna mwili hutumia dawa yainsulin.

Ulegevu na uzembe – Maisha ya mtu kukaa tu ndee si mazuri hasa iwapo mtu huyo ni mnene sana. Mazoezi hufanya moyo kupiga vizuri na kuzuia hali mbaya za kiafya mwilini. Mwili ambao una misuli tu ni rahisi kutumia vizuri Insulini kuliko ule ambao umejaa mafuta katika seli (cells). Hivyo basi, mtu anaweza kurahisisha utendaji kazi wa Insulini kwa kusonga hapa na pale. Pia mazoezi hurudisha chini kiwango cha sukari mwilini na hivyo basi kufanya Insulini kufanya kazi yake vizuri zaidi mwilini. Vile vile kupunguza uzito kitu kizuri. Hivyo basi wacha uzembe!

Mazoea mabaya ya kula: Wagonjwa wengi ambao wamepatikana kuwa na aina ya pili ya ugonjwa wa Sukari pia ni wanene mno. Hawana mazoea mazuri ya ulaji. Chakula kikiwa na mafuta mengi na chakula kilichowekwa kemikali, kile hakina nyuzinyuzi za kutosha, chakula kilicho na kabohaidreti (wanga) nyepesi, vyote huchangia katika kumfanya mtu kupatikana na ugonjwa wa Sukari mwilini. Kula unavyostahiki kwa weza kuzuia aina ya pili ya ugonjwa wa Sukari au hata kuupindua.

Historia ya familia: Wakati mwingine huwa katika jeni (genes) na unarithishwa katika familia. Watu ambao wana jamaa waliopatikana kuwa na aina ya pili ya ugonjwa wa Sukari wao wana nafasi kubwa sana kupata ugonjwa huu. Hali ya maisha ya mtu ndio hasa hufanya mtu apate au asipate ugonjwa wa Sukari.
 
Maswali ambayo yameulizwa sana kuhusu ugonjwa wa Sukari

Ugonjwa wa Sukari ni nini?

Ni ugonjwa ambao hufanya sukari iwe nyingi sana damuni. Walio na ugonjwa huu pia wanaweza kuwa na magonjwa mengine kama vile, ugonjwa wa moyo, figo, shida za macho, na hali zingine tata zinazolingana na hizi.

Kuna tofauti gani kati ya aina ya kwanza na ya pili ya ugonjwa wa Sukari?

Aina ya kwanza, sana sana hupatikana kwa watoto na vijana. Mwili hausawazishi kiwango cha sukari kabisa. Aina ya pili sana sana hupatikana kwa watu wazima. Mwili hujenga sukari lakini huwa haitoshi kulingana na kile kiwango kinachotakikana.

Unapataje ugonjwa wa Sukari?

Huwezi kuzuia aina ya pili ya ugonjwa huu. Husababishwa na mazeoa mabaya ya ulaji, kunenepa sana, na kukaa tu ndee bila kujishughulisha na shughuli zozote muhimu.

Unawezaje kutibu ugonjwa wa Sukari?

Aina ya kwanza hutibiwa kwa dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini (Insulin). Aina ya pili hutibiwa kwa kutumia dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini na tembe. Pia, mtu anastahili kufanya mazoezi, kuwa na ratiba nzuri ya ulaji na kupunguza unene.

Je, dawa ya kusawazisha kiwango cha Sukari mwilini ni nini? (Insulin)

Ni kemikali iliyoundwa katika kongosho (pancrease). Husaidia kusawazisha kiwango cha sukari mwilini.

Hebu sema baadhi ya shida za kudumu za ugonjwa wa Sukari?

Ugonjwa wa Sukari huweza kusababisha magonjwa mengine kama vile ugonjwa wa Moyo, Figo, Kupofuka, Kukatwa kwa viungo vya mwili, huharibu mishipa ya fahamu (neva) na magonjwa ya figo. Ni muhimu ujitunze kwa kutumia dawa zako inayostahili, usikae tu ndee bali ujishughulishe na mambo na ule ulaji unaofaa kwa afya nzuri.

Ni hali gani hatari inayoweza kusabisha na kukuza ugonjw wa sukari?

Sababu na hatari za aina ya kwanza ya ugonjwa wa Sukari bado hazitambulikani. Sababu muhimu kubwa ya aina ya pili ni unene kupita kiasi. Hatari zinginezo ni pamoja na uzee, kutofanya mazoezi, historia ya familia, kabila (sana sana watu wa asili ya Afrika, Waresia na wa asili ya Amerika ya Kilatino) na walio na msukumo wa juu wa damu mwilini na Choresterol

Ni nini baadhi ya njia ambazo kwazo mtu akizifuata atajizuia kupata aina ya pili ya ugonjwa wa sukari?

Zingatia uzani unaofaa kupitia kwa mazoezi na ratiba mwafaka ya ulaji mwema. Kula vyakula vya madini mwilini visivyo na mafuta mengi na sukari nyingi. Jishughulishe kila wakati kwa kufanya mazoezi: usikae tu ndee. Iwapo unaona kuwa uko hatarini na kuna uwezekano kuwa, unaweza kupata ugonjwa huu

Je, kuna dawa ya kutibu ugonjwa huu?

Kwa wakati huu haipo. Hata hivyo kuna dawa nyingi ina matibabu mengi unayoweza kutumia kwa mfano dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini. Matibabu pia huhusisha mtu kupunguza uzani (unene) wako na kuwa na shughuli nyingi pasipo kukaa tu ndee.
 
Njia tano za kufuata kama mwongozo wa kukabiliana na ugonjwa wa Sukari

Mara tu unapoambiwa kuwa una huu ugonjwa, linaweza kuwa ni jambo ngumu kulikubali na kukabiliana nalo. Hisia za kushtuka, hasira, kutamauka, kuogopa na kuwa na majonzi ni za kawaida kwa yeyote baada ya kupata habari kuwa ana ugonjwa wa sukari. Hata hivyo una maisha yako ambayo ni muhimu uyaokoe. Fuata hizi njia tano, kwa uangalifu ili ujue la kufanya wakati wa kukabiiana na hiyo hali yako mpya ya kuwa mgonjwa wa ugonjwa wa sukari.

Hatua ya 1: Jifunze yote yanayokupasa kuhusu ugonjwa huu.

Jifunze na uelewe kila kitu ili ujue unachoshughulikia. Muulize daktari ambaye anajua yote kuhusu ugonjwa huu na aliye na uwezo wa kujibu maswali yako yote. Tambua aina ya ugonjwa wa sukari unaokusumbua. Ni hali gani inayokufanya ujipate hatarini?

Jua vyema kiwango cha sukari kilichoko mwilini mwako na aina ya dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini mwako itakayokufaa maishani mwako. Ni shida gani zinazotarajiwa iwapo utashindwa kuuthibiti ugonjwa huu kwa kiwango kinachotakikana, kulingana na mhudumu wako wa kiafya. Utafiti wako umekusaidia kupata maarifa unayostahili. Kuweza kukabiliana na ugonjwa huu kikamilifu.

Hatua ya 2: Badili mtindo wako wa ulaji

Ili kuweza kukabiliana na kiwango cha sukari mwilini mwako ni muhumu upunguze uzani usiofa, kiasi cha chakula unachojipakulia ni lazima kipungue usifikirie kwa misingi ya utaratibu na ulaji bali njia bora ya kutunza afya yako kwa kula chakula kifaacho vyakula vifuatavyo, visikose kwenye orodha ya vyakula unavyohitaji katika taratibu wako wa ulaji; mboga, matunda, chakula cha kutunza mwili na cha kupatia nguvu mwili wako. Zungumza na daktari wako wa utarativu wa ulaji bora kuhusu mpangilio mwafaka wa mlo utakaouzingatia kwa wakati huu.

Hatua ya 3: Panga mpangilio wa kila siku wa kudumu

Watu wengi walio na ugonjwa huu mara nyingi huwa wanene kupita kiasi na wenye uzani mzito. Hivyo basi ni muhimu, ufanye mazoezi ya kila mara kama njia mojawapo ya kukabiliana na ugonjwa huu. Ni lazima kuwa daktari wako atakupa ushauri utakaoutaka upunguze uzito. Mazoezi mwafaka zaidi ni kuwa na mpangilio utakaokufanya uwe na nguvu za uthibiti wa moyo wako kwa kufanya mazoezi yanayolenga hayo mambo mawili. Baada ya ushauri wa daktari unaweza kuamua kujiunga na chumba au kiwanja cha michezo ya kuzoeza viungo vya mwili ama ujiunge na kundi la YMCA/YWCA ili upate msaada unaohitaji kuendelea kuyathibiti maisha yako na hali yako ya wakati huu. Kama sivyo, kuna namna nyingi za kujipangia mazoezi ya kibinafsi pale pale tu nyumbani.

Hatua ya 4: Meza dawa zako inavyotakikana

Watu wengine walio na aina ya pili ya ugonjwa huu huhitaji kumeza tembe zao inavyostahili ama kujidunga dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini ili miili yao itumie sukari iliyomo katika matunda na mimea kupata nguvu. Aina hii ya sukari huvunjwavunjwa tena wakati wa kuyeyusha chakula kinywani na tumboni ili kifae kuchukuliwa na damu mwilini kama ifanyikavyo na chakula cha namna kilichomo katika nyama, ute wa yai na samaki (chakula cha kutunza mwili) Dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini haipatikani kwa hali ya tembe. Yaliyo chini ya ngozi yako ili ingiie mara moja ndani ya damu yako.

Hatua ya 5: Tafuta usaidizi (msaada)

Huenda ikawa, utaweza kukabiliana na huu ugonjwa bila shida lakini ni muhimu utambue kuwa unahitaji msaada wa watu wengine ili mzigo ukuwie mwepesi kidogo. Tegemea jamaa na marafiki wakutegemewa ambao watakuwepo kila mara utakapohitaji msaada wao, katika hiyo hali yako mpya ya kisasa. Jishughulishe na vikundi vya watu walio na hali sawa na yako, pia jihusishe na shughuli za kijamii na kutafuta pesa na kuelimisha watu wanaoishi karibu nawe kuhusu ugonjwa huu.
 
DAWA YA UGONJWA WA KISUKARI

Dawa ya Sukari ! Wabilahi Taufiq


Dawa ya Sukari (Diabetes)

Sheikh Saleh Mohammed Tuwaijiri (May Protection of Allah be on him),

Qadhi Mkuu wa korti ya Tabuk kafanya uchunguzi mkubwa kwa kuvumilivu

na kwa subira kubwa mpaka kupata hii dawa ya magonjwa ya sukari.


Siku hizi watu wengi khususan watu wazima, wanaume na wanawake

wanataabika sana kwajili ya ugonjwa wa sukari.



Ingredients
:



1 – Unga wa ngano 100 gm


2 – Gundi (umefanan na ubani wa kiarabu lakini hauna harufu) 100 gm


3 - Shaair 100 gm


4 - Habba Soda 100 gm



Namna ya kutengeneza



Chemsha hivyo vitu juu katika vikombe 5 vya maji kwa muda wa dakika

10.
Zima moto na wacha ipowe. Ikisha kupowa chuja na utie katika chupa.



Matumizi



Kunywa kikombe kidogo kila siku asubuhi kabla ya kula chochote kwa

muda wa siku 7.
Wiki ya pili kunywa siku moja na uwache siku moja.

Insha-Allah baad hizi wiki mbili utapona na utaweza kula chakula kama

dasturi.
Sheikh anaomba muwapelekee wenzune wapate na wao

kunufaika.
Insha Allah Allah atajaalia iwe dawa kwa kila mwenye haya

maradhi. Aameen.
Kwa hisani zenu musiwasahau kwenye dua zenu Sheikh,

alieye tarjum kwa Kiswahili na kila anaye ipeleka mbele.
 
Kisukari ni ugonjwa unaosumbua sana naomba kujua tule chakula gani? ukiondoa kufanya mzoezi, naomba msaada mnaojua vizuri.
 
Pole ndugu,
Kuna aina nyingi ya vyakula ila nitakuambia vichache, kwanza natakiwa ajue ni nini hatakiwi kula

Aina zote za nyama kama Ya ng`ombe (beef) with brown rice, brown bread.
Kuku, aina zote za samaki, (sea food)
Mayai
Maziwa
Mboga mboga kwa wingi na matunda Green beans, uyoga, vitunguu, maboga, nyanya.

CORNWELL QUALITY TANZANIA
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom