SoC01 Ugonjwa wa Kisukari: Matajiri wengi wanaangalia pesa zaidi kuliko Afya yako

Stories of Change - 2021 Competition

Salumsas

Member
Jun 19, 2020
39
61
Salute Wakuu

Utangulizi

Wengi mmesikia kuhusu ugonjwa wa Kisukari wengine wakilalamika kuwa na huu ugonjwa hatari au wamekatazwa (hospitali) kutumia baadhi ya vyakula ili kuepuka madhara zaidi ya huu ugonjwa. Trust me I guarantee this is the perfect thread tutaelewa kila kitu hapa na hakuna ataebaki mtupu. Pia hongera sn kwa kuwa tayari kujifunza kuhusu Afya Yako you're one in a million.

Tuendeleee

Miaka kadhaa iliyopita nilimpoteza Marehemu Bibi yangu mpenzi "Mungu amrehemu Amin" Kutokana. na chanzo cha huu ugonjwa wa kiSukari, mm kama kijana na mjukuu wake mpendwa iliniuma sana sana na ilinichukuwa muda mrefu kusahau maumivu yale kutokana na upendo wangu kwake nilijiaahidi One day when I'm growing up I'm gonna be a Doctor specialist for Diabetics Mellitus yaani mtaamlamu wa magonjwa haya ya Kisukari na Matatizo ya Moyo,, Alhamdullihah I'm about to made it. I'm in University of Zambia faculty of healthy. Never the rest.

Ugonjwa wa Kisukari ni nini haswa?
ugonjwa wa Kisukari ni tatizo sugu linalitokana na Matatizo yakiyopo kwenye mfumo wa utoaji vichocheo. Hata hivyo tatizo hili limetokana kuwa kubwa na kuongezeka kutokana na sababu lukuki ambazo watu hushindwa kuziepuka.
Kama ilivyo jina lake Kisukari hutokana na kuongezeka sukari kwenye damu huitwa Glucose na ndio chanzo cha nishati kwenye mwili.
Insulin ndio hufanya glucose iingie kwenye seli na iweze kuunguzwa ili kupata nishati ambayo hutumika kwenye matumizi ya mwili.
Kiufupi Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa ambao hutokea wakati sukari yako ya damu iko juu sana. Insulini, homoni inayotengenezwa na kongosho, husaidia sukari kutoka kwa chakula kuingia kwenye seli zako kutumiwa kwa nguvu.

Twende taratibu sasa..

Ni muhimu sana kuzingatia ulaji wetu wa misosi kama vyakula vya wanga, keki, vileja, biscuit nk ambavyo huchukua kiwango kikubwa Cha sukari Pia vinywaji kama Soda, Juice , Pombe ambayo wafanya biashara huweka kiwango kikubwa sana cha sukari kwenye bidhaa zao. Wafanyabiashara wanachoangalia wao ni Pesa tu na sio Afya Yako Kuna kanuni moja kibiashara inasema kama unataka kutajirika usitatue Matatizo ya asili (natural challenge) tatua Matatizo ya watu ya kujitakia why? Becoz Matatizo haya ni scalable since ujinga ni universal. Uzia watu cheap dopamine kama Sigara, Pombe wajinga wengi watuvuta tu. Angalia mfano kama Coca Cola Ile chupa ya Mil 500 kiwango Cha sukari inawekwa mule ni kama gram350 ambayo ni Sawa na vijiko 8 mpk 12 vya sukari. Can you imagine that jaribu kuimwaga soda kwenye taiz au floor acha ikauke then utaiyona inavyogandiana na sukari hutoitamani tena kuinywa.
sisemi kwamba usinywe soda Lahasha! ila kunywa kwa kurefresh mind tu atleat ones a week or twice. Ukitamani sana jaribu kunywa maji hamu yote itaondoka hio itakua afadhali ×100.

Viko vyanzo mbalimbali, navyo ni

1. Shinikizo la juu la damu (B.P)
2. Viwango vya juu vya triglyceride (Mafuta)
3. Lishe yenye Mafuta mengi na Wanga
4. Utumiaji mkubwa wa Pombe
5. Ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi
6. Mtindo wa maisha usiofaa kiafya
7. Uzito na unene uliozidi
8. Kuto ushughulisha mwili
9. Umri

Sasa twenda kwenye Dalili nazo ni

1. Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati.
2. Kwenda haja ndogo mara kwa mara. Watoto kukojoa kitandani.
3.Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na 4.kujisikia mchovu kila wakati.
5. Kupungua uzito au kukonda.
6. Kusikia njaa kila wakati na kula sana.
7. Wanawake kuwashwa ukeni.
8. Kutoona vizuri.
9. Kupungua nguvu za kiume au hamu ya kujamiiana kwa wanawake.
10. Ganzi, kuchomwachomwa au kutohisi unapoguswa sehemu za miguu, viganja na vidole
11. Miguu kuoza na hata kupata gangrini.
12. Kukaukwa na ngozi.
13. Vidonda au majeraha sehemu yoyote ya mwili.
Majipu mwilini.
14. Kuhara kila wakati.

MADHARA YA UGONJWA WA KISUKARI.

Endapo ugonjwa wa kisukari utapuuzwa au kutotibiwa inavyostahili yako madhara mengi yanaweza kujitokeza, moja ya madhara hayo ni pamoja na;
1. Magonjwa ya moyo.
2. Kiharusi.
3.kupungua kwa nguvu za kiume(uume kutokusimama).
4. Figo kushindwa kufanya kazi
5.Kupata upofu.

Epuka ugonjwa huu kwa kupunguza unene uliozidi, fuata taratibu za kitabibu katika kula na kunywa, epuka matumizi ya pombe, punguza msongo wa mawazo na uvutaji wa sigara.

Kunywa maji ya kutosha, fanya mazoezi na kula kiasi kingi cha mboga mboga na matunda, utaratibu huu utakusaidia kuimarisha afya yako na kupunguza hatari ya uongezekaji wa kiwango kingi cha sukari mwilini.


MWISHO

Kwakumaliza ili tusiharibu thread yetu na kwa kuzingatia vigezo na masharti ya Stories of Change JF tumalizie na
Ugonjwa wa Kaisukari unatibika kwa hali tofauti, pia kufuatana na mda wa tatizo, mara nyingi wagonjwa wamekuwa wakikata tamaa na kuwa wabishi, Ukiona Dalili zoote ambazo huielewi elewi haraka kamuone Daktari wala usione ubahili au usumbufu.
Hatahivyo Waswahili wanasema Bora nusu Shari kuliko Shari Kamili maana yake ni Bora kujua Afya Yako Mapema KABLA ya maji hahaha korogeka ni vyema tukapunguza utumiaji wa Sukari kwaajili ya Afya zetu. You're CEO of your own life. Hakuna mtu atakae kuthamini ww kama ww mwenyewe hujithamini Jipende , Jilinde na ijali Afya Yako.

JamiiForum has been a family since Day One kama una Swali au Maoni kuhusiana na Mada yetu usisite Kutuambia ili kwa Pamoja tujifunze, Tuelemike na Tubadilishane mitazamo.
Pia Guy musisahau kunipigia Kura ili tusonge MBELE.


VOTE plz 🙏.
 
JamiiForum has been a family since Day One kama una Swali au Maoni kuhusiana na Mada yetu usisite Kutuambia ili kwa Pamoja tujifunze, Tuelemike na Tubadilishane mitazamo.
Asante kwa mada nzuri na ukaribisho wa kuchangia mitazamo, nimependa maana upo na ari ya kukielewa na kukidhibiti kisukari.

Ningependa uupatie maoni yako mtazamo ufuatao kuhusiana na chanzo cha kisukari, yaani je nadharia hii ina-make any sense?👇
Nikileta nadharia ya kwamba imani kwamba; "pesa ndo kila kitu, na kuwa nazo nyingi ni jambo zuri. Jitahidi ujikusanyie na kutunza pesa za kutosha. Usizitumie kuwa bahili" inapelekea seli ndani ya mwili kuiga ujinga na kuamini kwamba "Sukari ndio kila kitu, kuwa nayo nyingi ni jambo zuri. Jitahidi ujikusanyie na kutunza sukari ya kutosha. Usitumie sukari kuwa mchumi. Nikasema kuwa zote hizi ni imani mbaya na matokeo yake sio ya afya. Inapelekea kupata ugonjwa wa kisukari!

Bali imani nzuri ni [nadharia inaendelea] "Pesa ni muhimu kuendesha maisha yetu kijamii. Jitahidi utafute pesa kulingana na matumizi yako. Tunza kiasi tu lakini nyingi ziwekeze kwenye shughuli za kuzalisha mali ma kusaidia wewe familia na jamii kwa ujumla. Pesa itumike kwa mambo ya maana." kwamba itapelekea seli za mwilini nazo kutumia sukari kwa mtindo mzuri. Kuipata sukari kuitumia kujilisha na kusaidia shughuli za mwilini?. Bila kulimbikiza. Kumbuka naongelea ile imani tu sio kuwa actually na pesa.
Nasisitiza hizi ni nadharia tu. Sina mamlaka bado ya kitafiti. Tusaidiane kutafiti wote
 
Tunailinda na kuitunza vipi kongosho iweze kutoa vichocheo kulingana na matumizi?

Pale kongosho ipatapo madhara ni njia gani zinaweza kutumika au matibabu yapi yanafanyika kurejesha ufanisi wake?

Natanguliza shukrani.
 
Tunailinda na kuitunza vipi kongosho iweze kutoa vichocheo kulingana na matumizi?

Pale kongosho ipatapo madhara ni njia gani zinaweza kutumika au matibabu yapi yanafanyika kurejesha ufanisi wake?

Natanguliza shukrani.
Mara nyingi hiyo ya kufeli kongosho ni sukari ya aina ya kwanza.

Kama hukuipata tangu mtoto uwezekano ni mdogo kukusumbua ukubwani.

Japo ukiwa mkubwa uwezekano ni kupata hii aina ya pili kwanza kabla haijafikia kuwa na sifa za hiyo ya kwanza.

Katika hii aina ya pili ni pale kongosho linatema vichocheo za kutosha lakini mwili ndio unakataa kuitikia na kutumia sukari iliyopo. Hauitikii kiwango kikubwa tu cha kichocheo[insulini] inayotolewa.

Mfano ni serikali/benki kuamua kutoa pesa nyingi mtaani halafu uzalishaji wala usipande wala nini, pesa inageuka sumu na inauzidi uwezo wa wanachi kuzalisha, wanageukia kuzihifadhi na starehe na ushetani mwingine wa kujiangamiza. Hata ikitoa amri watu watumie hela kufanyia kazi, bado watu wanakataa maana benki[au betting] inawapa hela ya kutosha utawaambia nn? Au ni kweli wangezalisha ila wamepigwa na hofu hivyo wameogopa kuwekeza. Labda wamewaza kuna depression/recession au vita. Wameamua kutunza rasilimali badala ya kuzitumia kwa faida. Mwisho wa siku kunao watakaokosa hata wanachokihitaji kisa kuna watu wamehifadhi zaidi ya wanachostahili. Starving in the land of abundance.

Ndivyo ilivyo kwa sukari hii ya aina ya pili. Ni kwamba ubongo umejilimbikizia sukari [kwa kuiweka katika damu] nyingi na kuwasahau wenzake kina misuli. Misuli ya miguu na mikono huwa ya kwanza kuathirika [waste away] katika kesi za mbele za sukari. Wataalamu wanaita cachexia nadhani.

Huu ni muendelezo wa nadharia though.......................
 
kuwa eti ugonjwa wa sukari au presha ni ugonjwa wa matajiri?? uko ni kujidanganya!
 
Sasa kuacha matumizi ya sukari kwa mtu ambaye ni mcheza mpira au mkimbiaji si atadondoka kwenye mazoezi kwa kukosa nguvu...?
 
Sasa kuacha matumizi ya sukari kwa mtu ambaye ni mcheza mpira au mkimbiaji si atadondoka kwenye mazoezi kwa kukosa nguvu...?
Kila mtu hutengeneza 'kisukari' anapokuwa katika mazingira anayodhani yanayohitaji kutumika nguvu nyingi. Yaani stressful situation.

Mchezaji akiwa uwanjani sukari nyingi kwenye damu aliyonayo anaitumia kuendesha misuli na kupiga mashuti kwelikweli.

Shida ni mtu anapodhani anahitaji nguvu nyingi [mfano hizi stress za kawaida, foleni deadline na kiuchumi] lakini kumbe walaa hali haitatumia nguvu. Huyu huandaa sukari na hubakisha kwenye damu bika matumizi matokeo yake 'inamuunguza' tu na kuwa hasara.

Sukari ni muhimu na ni nzuri ikiwa ina matumizi kweli, lakini sio kutunza tu itaathiri viungo mwili ukakosa afya. Ni kama hela inafaa na ni nzuri ili uitumie kimaendeleo lakini sio kujilimbikizia tu utaadhiri/utaathiri wengine jamii ikakosa afya.
 
Hivi unajua kuwa kuna wAtu wanazaliwa wakiwa tayari wana ugonjwa wa kisukari?? Ki ukweli watu wengi hawaujui ugonjwa wa kisukari, ebu haya mambo mengi ya kitabibu tuwaachie ma doctor, kuliko kupotosha
 
Wenye wagonjwa wa kisukari wamtafute huyu jamaa naona anajitahidi sana dawa zake. Nimeshuhudia watu wawil naowafahamu kawatibu wamepona anaitwa mbaraka 0765 806963.atakayewasiliana nae na kufanikiwa naomba alete mrejesho hapa.asanteni
 
Back
Top Bottom