Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,534
Ugonjwa wa Kipindupindu umerejea ukiwa umepita mwezi mmoja tangu uongozi wa mkoa wa Mwanza utangaze kuisha kwa ugonjwa huo mwezi April mwaka huu.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk.leonard Subi ametoa tahadhari ya kurejea kwa mlipuko wa ugonjwa huu na kusema umerejea mwishoni mwa Mei.
Mpaka sasa wagonjwa walioripotiwa ni wawili kutoka wilaya ya Nyamagana na wamelazwa katika kambi ya wagonjwa wa kipindupindu iliyopo Kituo cha Afya Igoma.