Ugonjwa wa kifafa: chanzo, dalili, huduma kwa mgonjwa na ushauri juu ya matibabu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa wa kifafa: chanzo, dalili, huduma kwa mgonjwa na ushauri juu ya matibabu

Discussion in 'JF Doctor' started by Slave, Mar 23, 2011.

 1. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu katika JF kabla sijaanza kueleza swahibu lililo nisibu ningependa kukumbushia utani nilio uandika katika jukwaa la joke/utani ndani ya post ile nilisema natafu mfanya kazi wandani wa kike (house girl) ile ilikuwa ni utani lakini mpaka ukawa utani kulikuwa na ukweli fulani ndani yake.

  Mke wangu alikuwa ananisumbua sana kuhusu kutafuta msaidizi wa kazi za ndani.

  yeye anataka lakini mimi niluwa napinga kutokana na ukweli kwamba familia yetu ni ndogo huku nikijaribu kuangalia majukumu ya huyo msaidizi.

  binafsi nikaona mke wangu anajitengenezea mazingira ya kujakuonekana hana maana tenda kama msaidizi atafua,kupika,kuosha watoto,kutandika kitanda nk.ndiyo maana nikaandika utani kwamba natafuta msaidizi wa ndani awe mzuri kuliko mke wangu mpole mcheshi na mwenye kujituma awe tayari kufanya kazi yeyote nitakayo mwambia .

  HUO ULIKUWA UTANI. SASA TUJE KWENYE MADA.

  Baada ya kutafuta mfanyakazi wa ndani hatimae tulifanikiwa kumpata hivi sasa ana wiki.Lakini tangu aanze kazi kufanya amekuwa akisumbuliwa na kichwa.

  Lakini leo hii kaanguka na kuanza kutoka mapovu mdomoni nimeshindwa kutambua kama ni MAJINI AU KIFAFA lengo la mada hii ni kupata ushauri wenu je?

  NITUMIE DAWA GANI ?AU NIFANYE NINI au nimfukuze kama anavotaka wife.

  MSAADA WAJAMENI.
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Kifafa (Epilepsy) kinatokea kunapokuwa na mapungufu katika seli za ubongo. Ubongo unafanya kazi katika mfumo wa umeme au kama umeme hivi, sasa kunapokuwa na hitilafu katika huu mfumo ndio kifafa kinaweza kutokea ambacho dalili zake ni kuona maluwe luwe (aura), kiasha kupoteza fahamu, kuanguka na kutupa miguu na/au mikono, kukaza mdomo, kutoa povu na huwa inamalizia na kutoa haja ndogo au kubwa wakati mwingine.

  Kifafa sio ugonjwa wa kuambukiza, mara nyingi unakuwa kwenye familia kwa kurithi toka kwa mzazi/wazazi, lakini pia wakati mwingine inaweza tokea baada ya kuumia ubongo kutokana na ajali, kiharusi (stroke), kuumia wakati wa kuzaliwa (birth injuries) etc...Kifafa hiki ni tofauti na 'dege dege' kwa watoto au kifafa cha mimba (Eclampsia).

  Kifafa hakitibiki, nikiwa na maana hakitibiwi kikapona kabisa...ila kuna dawa za kupunguza au kuzuia kifafa kutokea mara kwa mara. dawa hizi zinapatikana hospitali, na mgonjwa atakunywa kwa maisha yake yote dozi inategemea na hali ya mgonjwa anapoonwa mara kwa mara kwenye kliniki zao maalum. Kwa sababu kifafa hutokea ghafla, ni muhimu sana mgonjwa anapoanguka utoe vitu vyote vya hatari vyenye kuumiza (watu wengi hukimbilia kumtoa mgonjwa au kumshika na pengine hata kumfunga kamba...hii si sahihi, inatakiwa utoe vitu vitakavyohatarisha mgonjwa kuumia au hata kufa) mfano moto, jiko, vifaa vyenye ncha kali etc. Kuna wagonjwa wengine huwa wanashtukia kifafa kinapoanza (aura) hivyo kujiepusha na sehemu za hatari.

  Baada ya kuanguka kifafa, mgonjwa anaweza akawa kama hana fahamu sawa sawa, amechanganyikiwa au hata kama kichaa...mara nyingi anahitaji msaada badala ya kumnyanyapaa. Siwezi kukushauri umtimue au usimtimue housegirl wako sababu sijui kwa nini wataka kufanya hivyo...kama unaogopa kuwa atawaambukiza, si kweli...kifafa hakiambukizi, kama unaogopa majukumu ya kumlea mgonjwa wa kifafa...lakini kama una moyo wa kumsadia, mpeleke Muhimbili pale Idara ya magonjwa ya akili kuna wataalamu waliobobea, na kuna kliniki maalum kwa ajili ya wagonjwa wa kifafa atapata msaada unaostahiki na maisha yake yataboreka kadri amabavyo zile attacks za kifafa zinapungua.
   
 3. Masika

  Masika JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2011
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 731
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ushauri mzuri wa @riwa naomba uufuate huo huo
   
 4. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  kama unaogopa kuwa atawaambukiza, si kweli...kifafa hakiambukizi, kama unaogopa majukumu ya kumlea mgonjwa wa kifafa... Binafsi siogopi chochote ndio maana nimeomba msaada.najua namna gani mgonjwa ambavyo hujisikia vibaya anapo hisi kutengwa na jamii kuhusiana na ugonjwa wake.ila baada kukaanae kanambia aliwahi kupewa mawani japo nimeshindwa kuoanisha tatizo lake na kuvaa miwani.
   
 5. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Miwani haijawahi kuhusika na tiba ya kifafa, wala kifafa hakiharibu macho kiasi cha kuhitaji miwani...nadhani nia matatizo ma2 tofauti. Ila ni vizuri pia ukamuuliza kama alishawahi kuwa na tatizo hilo la kuanguka anguaka kifafa huko nyuma (kama hajawahi na imeanza ghafla sasa basi atahitaji uchunguzi zaidi), na kama alishawahi kupata matibabu na kuhudhuria kliniki za kifafa.
   
 6. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  riwa huyu dada anaamini yaye tangu zamani ni kuugua kichwa na hiyo mawani anadai ma dr wa mwananyamala walimpa ila alipoenda muhimbili walimkataza kuvaa
   
 7. Papa Diana

  Papa Diana JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu maelezo yako ni sahihi ila tu labda niongeze ....kunabadhi ya wagonjwa wa kifafa hupata tabu sana na mwanga mkali (Photo sensitive epilepsy), hasa kama flash za camera, au mionzi ya jua inapokua reflected; hawa wakitumia miwani inayo block polarised light inaweza punguza incidences za epileptic fits!!
   
 8. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  naanza kupata picha.
   
 9. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Riwa na Papaa diana mmekimbia?
   
 10. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Riwa na Papaa diana mmekimbia?
   
 11. Papa Diana

  Papa Diana JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwani kuna swali jengine??
   
 12. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  ndiyo papaa.
   
 13. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Nimerudi Slave...kama kuna swali lingine karibu!
   
 14. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ahasante sana Riwa. Lakini umeelezea GRAND MAL peke yake. Elezea na PETIT MAL pia maana zote mbili ni kifafa.
   
 15. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na maelezo yaliyotolewa na Riwa. mimi mtoto wangu ana kifafa kilichosababishwa na ubongo kujaa maji kulikotokana na kutotibiwa kwa wakati homa ya uti wa mgongo (meningitis). Kichwa kilianza kuwa kikubwa kwa sababu ya maji ambayo huzalishwa na ubongo wenyewe ili kujisafisha. Katika hali ya kawaida maji hayo hutoka kwa kupitia njia ya uti wa mgongo; lakini kwa mtoto wangu mirija ya uti wa mgongo ya kupitishia maji hayo iliziba ikiwa ni katika harakati za mwili kuzuia wadudu wa homa ya uti wa mgongo kuingia kwenye ubongo. Alikaa muhimbili kwa miezi saba na kwakuwa ni vigumu kufanya operation ya uti wa mgongo waliamua kumuwekea shunt. Hii ni tube ndogo iliyoshonewa karibu kabisa na ubongo na inateremka hadi tumboni ambako maji yanayozidi kwenye ubongo hupelekwa kupitia tube hiyo (iko ndani kwa ndani). Alipata tatizo hilo akiwa na umri wa miezi 8, sasa ana miaka 6. Amekuwa akipata kifafa kwa sababu hiyo.
  Ni kweli basi kuwa kifafa hakiambukizi na si vizuri kumnyanyapaa mgonjwa. Ugonjwa hauna dawa za kitaalamu, zilizopo ni za kutuliza tu.
  Lakini kuna dawa za kienyeji ambazo zinasaidia zadi kuliko za hospitali.
  Nakushauri kwa sasa mpeleke kwa babu wa Loliondo; mimi wangu nimeshampeleka, nimetoka huko wiki iliyopita hivyo ni mapema kujua kama amepona au la. Baada ya miezi miwili nitakuwa na la kusema; ila nina imani atakuwa amepona!
   
 16. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  dah! Pole sana mkubwa.vile vile nashukuru kwa ushauri.
   
 17. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #17
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Kifafa ni ugonjwa wa ubongo.

  Ubongo wa binadamu una mabilioni ya seli za neva.Zinashirikiana na kila moja kupitia chaji ndogo ndogo za umeme ambazo huwaka na kuzima.Wakati baadhi ya ama hizi seli zote kwa ghafla huanza kuwaka kwa pamoja, wimbi la nguvu za umeme hupita kwenye ubongo na husababisha kifafa ama kuzirai.

  Kuzirai kwa ghafla huathiri vile ubongo hufanya kazi.Kunaweza kumsababisha mtu kupata mabadiliko ya ghafla katika fahamu, mwendo ama hisia.

  Mshtuko wa moyo mmoja haumanishi ya kwamba mtoto ana kifafa.Kuzirai mara moja kunaweza kutokea kwa sababu tofauti k.m homa, jeraha la kichwa, kiwango cha chini cha sukari katika damu na kadhalika.

  Kifafa ni jina la kuzirai kwa ghafla kunapotokea zaidi ya mara moja bila ya sababu ya kutibiwa inayojulikana.

  Katika sehemu hii jifundishe zaidi kuhusu huu ugonjwa.

  Dalili na ishara za kifafa Nitajuaje ikiwa niimeathiriwa na kifafa?
  Kuna aina nyingi za kuzirai na mara kwa mara sio mgonjwa ambaye huona ishara za kifafa ilhali ni wale wanaomzunguka. Kuzirai kwingine hutokea kama kupotea kwa fahamu (ugonjwa wa kifafa usio mkali). Hapa, mgonjwa (ambaye huwa ni mtoto) hupoteza makini kwa dakika kadhaa. Wakati huu, hawaitikii jina lao na hawawezi kusikia ama kuelewa chochote. Ni walimu ama wazazi ambao wataona ya kwamba mtoto anazubaa. Wanapopataa nafuu, hawafahamu chochote kisicho cha kawaida kimefanyika. Watoto kama hawa huwa hawafanyi vizuri katika masomo kwa sababu kumakinika kwao huathiriwa.

  Kuzirai kwingine hujumuisha kutingika ambako hakuwezi kudhibitiwa ama msukumano wa sehemu moja ama zaidi za mwili. Wakati huu, mtu hawezi kuzuia kutingika huku. Kutingika huku huanza kwenyewe na huisha baada ya mda fulani. Mgonjwa anaweza kujihisi akiwa mnyonge ama hana hisia katika sehemu hiyo ya mwili kwa mda baada ya kuzirai.

  Aina nyingine ya kuzirai ni wakati mtu anapoanguka chini na kuanza kutetemeka katika mwili wake kwa kipindi fulani na kisha analala usingizi mzito (anapoteza fahamu). Aina hii ya kifafa inaogofya kutazama. Watu huwa hawana fahamu ya vitendo vyao na saa zingine wanapoamka hawawezi kukumbuka kile ambacho kimetoka kufanyika. Ni wale tu ambao walikuwepo wanaweza kuelezea ni nini kimetoka kufanyika.

  Katika aina zingine za kifafa, mtu hupoteza udhibiti wa misuuli yake na huangusha kile walichokuwa wamekishikilia, hujikwa wanapojaribu kutembea ama huanguka chini wasiweze kujizuia ama kujilinda.

  Kwa mukhtasari, wakati mtu anapothiriwa na kutetemeka kusikoweza kudhibitiwa kwa sehemu moja ama zaidi ya mwili wake ama anaanguka chini na kupoteza fahamu, hii inaweza kuwa dalili ya kifafa na ni muhimu kutafuta ushauri wa dakitari haraka iwezekanavyo.

  [h=1]Je kila mtu anayeathiriwa na kifafa anapaswa kupelekwa hospitalini?[/h] La. Sio kila mtu anayeathirika na kifafa anapaswa kupatiwa huduma ya matibabu. Mtu mwenye kifafa ambaye yuko chini ya matibabu labda hahitaji kupelekwa hospitalini mara moja. Kuna visa vingine ambavyo ni muhimu kumpeleka mtu hospitalini kama dharura.


  • Kuzirai mara ya kwanza. Ikiwa mtu anafahamika ya kwamba huwa hana kifafa na kishe azirai, mtu huyu anahitaji kumuona dakitari mara moja.
  • Ikiwa kuzirai kumekaa zaidi ya dakika 5, mpeleke mgonjwa hospitalini.Hili huwa nadra lakini lifanyikapo huwa hatari sana na ni lazima umkimbize mgonjwa hospitalini hata ikiwa bado yuko katika hali hiyo ili kuokoa maisha yake.
  • Ikiwa kupumua hakurudii hali ya kawaida baada ya kuzirai.
  • Ikiwa kuzirai kutaisha na kujirudia tena mara hiyo hiyo Kabla ya mgonjwa kupata nafuu. Nitaendelea hii Topic .................
   
 18. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #18
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Je, kuna tiba ya kifafa? Mara nyingi kile kinachosababisha kifafa hakijulikani, ugonjwa huu hauna tiba inayotambulika. Wakati mtu anapoathiriwa na kuzirai kwa sababu ya hali zingine kama vile uvimbe kwenye ubongo ,ugonjwa wa figo au ugonjwa wa ini unaweza kuwa na nafasi ya tiba ikiwa hali hiyo nyingine imetibiwa. Katika visa vingine, hata hivyo kuzirai huendelea hata kama ikiwa hali hiyo nyingine imeshughulikiwa.

  Ugonjwa wa kifafa unaweza kudhibitiwa kwa kutumia madawa na kufuata matibabu ya mara kwa mara. Ugonjwa wa kifafa uliodhibitiwa vizuri hupunguza idadi ya visa vya kuzirai vinavyomkumba mtu na wakati mwingi mgonjwa hazirai kwa mda mrefu. Hali hii haitibiwi na mgonjwa anaweza kurejelea kuzirai wakati wowote. Dawa hutumiwa KUDHIBITI kuzirai lakini sio kutibu.

  Jinsi nyingine za kudhibiti kifafa Kando na madawa, ni nini kingine ambacho kinaweza kunisaidia ikiwa niko na kifafa?

  Imeonekana ya kwamba kuna vitu ambavyo vinaweza kusababisha mshtuko kwa mtu aliye na kifafa ikiwa hata amedhibitiwa na matibabu. Kukosa usingizi wa kutosha (mtu mzima anahitaji angalau masaa 8 ilhali mtoto anahitaji angalau masaa 9) kunaweza kusababisha mshtuko wa kifafa. Mfadhaiko mwingi utokanao na matatizo unaweza pia kusababisha shambulizi. Homa katika watoto imejulikana kuongeza nafasi ya

  kutokea kwa mshtuko wa kifafa. Taa zinazomemeteka kama vile kioo cha runinga na mataa ya disko yanaweza kusababisha mshtuko wa kifafa katika watu wengine. Kupumua kwa nguvu wakati unapumzika kumetambuka kusababisha mshtuko. Hutokea mara kwa mara katika watoto wakati wako kwenye hali ya kuogopesha sana ama hofu kubwa. Ukiwa unaweza kuepuka haya, unaweza kujisaidia kuepuka kushikwa na mshtuko wa kifafa.

  Kwa nini haupaswi kumwekea mtu kitu mdomoni anaposhikwa na mshtuko wa kifafa? Kwa mda mrefu iliaminika ya kwamba wakati mtu ameshikwa na kifafa, mgonjwa anaweza kumeza ama hata kunyongwa na ulimi wake na kwa hivyo kusababisha kifo. Hivi sasa hali imebadilika na inaeleweka ya kwamba hakuna haja ya kuweka kitu chochote kwenye mdomo wa mgonjwa anaposhikwa na kifafa. Hili linaweza kusababisha madhara zaidi.

  Wakati wa kifafa kuna mshtuko wa ghafla wa misuli.Mikono, miguu na sehemu zingine za mwili huwa na mwendo wa kujirudia rudia ambao ni vigumu kuukabili kwa kutumia nguvu haswa ikiwa mgonjwa ni mkubwa kwa umbo. Kama sehemu ya tendo la misuli, mgonjwa husaga meno yake kwa sababu ya tendo la nguuvu katika taya. Jaribio lolote la kuweka kitu kwenye mdomo linaweza kusababisha kuvunjika kwa meno ya mgonjwa, kunyongwa na kile kilichowekwa mdomoni ama mgonjwa kumuuma vibaya mhudumu wake.

  Kwa hivyo fahamu: USIWEKE kitu katika mdomo wa mgonjwa anaposhikwa na mshtuko wa kifafa.


  Kwa nini wagonjwa wa kifafa hawawezi kugawana madawa yao? Madawa ya kifafa hufanya kazi ya kukomesha shughuli zisizo za kawaida kwenye ubongo. Kuna aina nyingi za kuzirai katika kifafa na hizi zote huitikia kwa njia tofauti kwa madawa tofauti. Hii ndio sababu ya kwanza kwa nini haufai kugawa dawa za kifafa. Dawa ambazo hudhibiti aina moja ya kifafa zinaweza kukosa athari kwa aina nyingine ya kifafa.

  Pili, watu tofauti wanahitaji vipimo tofauti vya dawa iliyotolewa kudhibiti kifafa. Ugonjwa wa kifafa unamaanisha ya kwamba ubongo wa mtu unaweza kufyatuka kwa njia isiyo ya kawaida. Watu tofauti hupata kifafa katika viwango tofauti vya mchangamsho wa ubongo. Watu wengine huchangamshwa kwa urahisi na kuzirai ilhali wengine hawachangamshwi kwa urahisi. Kipimo cha dawa kinachotumiwa kumdhibiti mtu ambaye huzirai kwa urahisi ni tofauti na kile cha yule ambaye hazirai kwa urahisi.

  Tatu, sio vizuri kugawana madawa ambayo yametolewa kufuatia maagizo ya dakitari. Maagizo ya dakitari hutoa dawa kwa mtu mmoja kwa kipindi maalumu cha wakati. Kwa kugawana madawa, mtu ambaye alipewa maagizo ya dakitari ataishiwa na dawa kabla ya ahadi ya kuonana na dakitari inayofuatia. Wanweza kuzirai kwa urahisi kwa sababu hawako kwenye matibabu. Sio salama kwa mtu mwenye kifafa kugawa dawa zake.
   
 19. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #19
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Types of epilepsy
  [​IMG]
  There are many different types of epilepsy, and with each type of epilepsy there are different symptoms. Most forms of epilepsy are named after the the area of the brain that they effect. Most of the forms of epilepsy are very rare, and typically are originated in childhood or even infancy. There are others however that begin in adulthood and old age. We will list some of the most common forms of epilepsy, and explain some of the symptoms and what part of the brain they effect. The most common forms of epilepsy are.
  Absence epilepsy typically is hereditary, and usually always begin in childhood [​IMG]or adolescence. They also usually stop when the subject hits puberty. Absence epilepsy don't have lasting effects on the brain functions or intelligence of the individual. The bad part about absence seizures are that they interfere with school and learning because they can happen so frequently during the day. Absence seizures cause momentary loss of consciousness, and normally last less then 30 seconds. The problem with these seizures is that they can be unnoticed by people because they are so brief and the person that is suffering from there just seem to be staring into space. The problem with absence seizures and it effecting schooling and learning is because they can happen between 50 to 100 times during the day.

  Frontal lobe epilepsy effects the frontal lobe of the brain and it is directly behind [​IMG]the forehead. The frontal lobe is largest of the five lobes in the brain, it controls the personality, and higher thought process, this includes language and speech. Frontal lobe epilepsy cause short seizures that start and stop very quickly. The problem with Frontal lobe epilepsy is that it can be diagnosed as something different when it is first noticed. They seizures that come from this type of epilepsy can look like other mental problems and without proper testing could be diagnosed as that. The seizures that take place can be sensorimotor tics, or other problems dealing with motor skills. And often with these tics, different alterations of consciousness. Laughter or crying in rare cases can also occur during an frontal lobe seizure. These seizures can also travel to other parts of the brain making the seizures do different things depending on where the it has traveled to in the brain.

  Occipital lobe epilepsy involves the Occipital lobe, it lies at the back of the head. Occipital lobe epilepsy is similar to frontal and temporal love epilepsy's, but the only difference is that the seizures usually are related to the eyes. Often seizures begin with hallucinations, rapid blinking, and other symptoms with the eyes.

  Parietal lobe epilepsy effects the Parietal lobe which lies between the frontal and temporal lobes. Parietal epilepsy is similar to those two types of epilepsy because the seizures can spread to other parts of the brain, making the seizures do have different consequences depending on what part it goes to.
  [​IMG]
  Temporal lobe epilepsy is the most common form of epilepsy and the most common cause of Partial seizures and aura. Aura is something that happens to the body before a seizure letting the person know that they are about to suffer one. The different symptoms of this could be a sinking feeling in your stomach, or a sense of deja vu, or can also take a form of a auditory hallucination. Like a song you've heard or a jingle. Temporal lobe epilepsy if left untreated can damage the hippocampus, which is the part of the brain that helps your memory, and learning. The damage is very small and slow but it is still good to get the epilepsy treated as early as possible.
  These are the most common forms of epilepsy, if you know someone that is suffering from any of these symptoms that were listed you should get them to the doctor as soon as you can. The faster you get them diagnosed the faster you can get them treated and on the road to recovery. If you have any questions or comments about types of epilepsy please contact us. We would like to hear any comments or stories you may have.
   
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Matatizo yaweza tokezea wakati wa matibabu? Je kuna jambo ambalo linaweza kuenda mrama nikiwa bado kwenye matibabu?

  Athari ya matibabu ni hisia ya kusinzia na kutokuwa mwepesi ambako hutoweka baada ya mda. Baadhi ya madawa yanaweza kumfanya mgonjwa aongeze uzito. Athari mbaya zaidi ambayo inaweza kutokea ni kwenye ini. Hili ni jambo la kawaida wakati mgonjwa anatumia madawa kadhaa ili adhibiti kifafa.

  Unapoanza matibabu, athari yake kwa kifafa huwa siio ya papo kwa hapo. Inachukua angalau mwezi mmoja kuona athari yoyote ya kudumu na mtu anahitajiwa kuwa mvumilivu. Katika visa vichache, visa vya kuzirai vinaweza kuongezeka unapowekwa kwenye matibabu kabla kuzirai hakujapungua.

  Ni kipi kipimo cha dawa za kutibu kifafa? Kipimo cha dawa ni kile ambacho kitatibu kitadhibiti ama kitatibu hali hii bila ya kusababisha mathara mabaya ya kando. Hii hutofautiana kutoka kwa matibabu hadi matibabu na hali hadi hali. Dawa zingine kama Panadol zina kiwango chake rasmi; watu wazima humeza vidonge 2 kila masaa 6-8. Hali zingine kama malaria isiyo kali zina kiwango cha dawa kinachopeanwa katika kiwango cha kipimo cha dawa kama watu wazima humeza vidonge 2 vya Camoquine mara moja kwa siku 3.

  Hesabu ya kiwango cha kipimo cha dawa hutegemea uzani wa mgonjwa ama umri wake. Kila aina ya dawa ina kipimo kwa uzani ama umri wa mgonjwa uliopeanwa.

  Katika visa vingine vya kifafa, kiwango cha dawa hakiwezi kuhesabika kwa urahisi. Matibabu yanayotolewa ili kudhibiti kifafa huathiriwa kwa urahisi na vipimo vya dawa na hufanya kazi katika kadiri ndogo. Dawa kidogo kwenye damu ama dawa nyingi kwenye damu na udhibiti wa kifafa hupotezwa. Kwa hivyo kila dawa inaweza tu kutumiwa katika kadiri iliyotolewa ya kipimo cha dawa. Ikiwa kuzirai hakuwezi kudhibitiwa katika kadiri hii,dawa ya pili na saa zingine dawa ya tatu inaweza kuongezwa. Hii nyongeza ya madawa hujiathiri na kipimo cha kila dawa kinahitaji kuhesabiwa mara tena ili kila dawa ikuwe katika kiwango kinachofaa katika damu.

  Kufanya mambo kuwa magumu zaidi, kutokea kwa kifafa hakuwezi kutabirika katika watu tofauti. Kuna wale ambao ugonjwa wao wa kifafa unaweza kudhibitiwa kwa urahisi ilhali wengine wanahitaji matibabu 2-3 ili kupunguza visa vya kuzirai bila ya kuvimaliza kabisa. Kwa wagonjwa 2 wenye umri sawa na uzani sawa, matibabu ya kipekee yanaweza kutolewa katika vipimo tofauti ili kudhibiti kuzirai kwao.


  Ni kwa mda upi ambao mtu aliyeathiriwa na kifafa anapaswa kutumia dawa? Mtu aliyeathiriwa na kifafa anapaswa kutumia madawa aliyopewa hadi ashauriwe vingine. Kwa kutegemea wingi wa kutokea kwa visa vya kifafa, wagonjwa wanaweza kutumia dawa kwa maisha yao yote.Katika watoto,hata hivyo mambo yanabadilika. Kitambo, ilichukuliwa ya kwamba mtoto mwenye kifafa angehitajika kutumia

  madawa kwa miaka mingi ya maisha yake. Lakini hali sio hivyo tena. Ikiwa mtoto anatumia madawa kwa njia inayofaa na kwa wakati bila ya kukosa hata kipimo.cha dawa na anabakia bila kifafa kwa angalau miaka 2, basi dakitari anaweza kufikiria kusimamisha utumizi wa madawa. Ni dakitari pekee yake anayeweza kutoa ushauri kuhusu kusimamaisha matumizi ya madawa ya kifafa baada ya kumfuatilia mgonjwa kwa

  kipindi fulani cha mda. Ni muhimu maamuzi haya yafanywe na dakitari, kwa sababu mwanzo utumizi wa madawa umeanza haufai kukatizwa kwa ghafla. Badala yake dakitari atapunguza kipimo cha dawa pole pole hadi matumizi ya dawa umesitishwa. Ukisitisha dawa kwa ghafla, kuna madhara ya kando kama kumwa na tumbo, kutapika na kutomakinika na kuzirai kunaweza kujirudia.

  Kwa hivyo, jambo muhimu ni kuzungumza na dakitari wako kuhusu kusimamisha matibabu. Ikiwa mtoto hajafuzu kwa ajili ya kusitishwa matibabu kwa sasa, na kisha aendele kutokana na ushauri wa dakitari. Ikiwa mtoto atafuzu, basi hili linafaa kufanywa kwa utaratibu. Wakati kipimo cha dawa kinapunguzwa, ni muhimu kukumbuka ya kwamba mtoto anaweza kushikwa na kifafa. Waweke wakiwa salama na waangalie kwa karibu hadi dawa zote zimesitishwa kabisa na kila kitu kiko salama.
   
Loading...