Ugonjwa wa jaji wakwamisha kesi ya Askofu Dk. Mokiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa wa jaji wakwamisha kesi ya Askofu Dk. Mokiwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 7, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Askofu Dk. Valentino Mokiwa


  Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Fatma Massengi, aliyepaswa kutoa uamuzi wa kesi kuhusu pingamizi zilizotolewa na upande wa utetezi katika kesi ya kumpinga Askofu Stanley Hotay kusimikwa kuwa Askofu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Mount Kilimanjaro, ameshindwa kufanya hivyo baada ya kwenda India kwa matibabu.


  Msajili wa Wilaya, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, George Albert,alithibitisha jana kuwa Jaji Msengi ameenda India kwa matibabu.


  Pamoja na Askofu Hotay, mlalamikwa mwingine katika kesi hiyo ni Mkuu Kanisa la Anglikana nchini, Askofu Dk. Valentino Mokiwa anayelalamikiwa kukiuka katiba, sheria, taratibu na kanuni za kanisa kumteua Askofu Hotay kuongoza Dayosisi ya Mount Kilimanjaro.


  Waumini watatu wa kanisa hilo walifungua kesi hiyo mwaka jana wakiwakilishwa na wakili Mainrad D’Souza. Mlalamikaji Godfrey Mhone alijitoa.


  Walalamikaji waliobaki katika kesi hiyo ni Loti Olerevu na Frank Jacob ambao wamefungua madai Mahakama Kuu kupinga Hotay kusimikwa ngazi ya uaskofu kwa madai kuwa kulikuwepo ukiukwaji wa taratibu za Kanisa Anglikana Tanzania na kutoa taarifa za uongo kuhusu umri wake.


  Katika madai yao ya msingi, waumini hao wanaiomba mahakama kuzuia Askofu Hotay kusimikwa kuongoza dayosisi hiyo kwa madai kuwa uchaguzi wake ulikiuka katiba, kanuni na taratibu za kanisa.


  Aidha wanamtuhumu Askofu Hotay aliyesimiwa uaskofu mwaka jana kuwa aliwasilisha vyeti na taarifa za kughushi kwenye ngazi ya uteuzi na upigaji kura na hivyo kufanikiwa kupata wadhifa huo kinyume cha sheria.


  Askofu Hotay alitawazwa mwaka jana, lakini kanisa hilo lilishindwa kumpagia kituo cha kazi kutokana na pingamizi la lililowasilishwa mahakamani hapo kupinga kusimikwa kwake kuwa askofu wa Dayosisi ya Mount Kilimanjaro.


  Mawakili wa Utetezi, Albert Msando na Joseph Thadayo, ndio waliowasilisha pingamizi hizo mahakamani hapo wakidai
  kuwa mahakama hainamamlaka wala uwezo wa kuingilia maamuzi yaliyofanywa na vikao halali vya Kanisa.


  Awali kesi hiyo ilikuwa inasikilizwa na Jaji Kakusulo Sambo,ambaye alijitoa baada ya Mahakama ya Rufaa kutengua amri yake ya kukamatwa kwa Askofu Mokiwa pamoja na Askofu Hotay.


  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...