Ugonjwa wa homa ya matumbo (Typhoid) na tiba mbadala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa wa homa ya matumbo (Typhoid) na tiba mbadala

Discussion in 'JF Doctor' started by Zion Daughter, Mar 26, 2010.

 1. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kwa yeyote anayejua tiba mbadala ya typhoid please naomba msaada.Nikisema mbadala namaanisha matunda,mizizi,mimea ama vyakula.

  Bwana Yesu asifiwe.

  ===============

   
 2. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2010
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Mimi pia nshatafuta iyo mizizi kwakweli,dawa za hospitali mateso matupu na usugu juu...kuna dawa inaitwa maghakaa (kisukuma)sijui kutamka, eti inatibu magonjwa mbalimbali na malaria juu.seriously me naumwa sana malaria na tumbo

  jamani dr ndindi sijui yule wa startv nae vipi??
   
 3. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Dr Ndodi ana bei sana.kwa huo ugonjwa wa tumbo peke yake jiandae sio chini ya 1M.Ila dawa zake ni uhakika.
  Lakini kwa maleria unaweza kutumia vitunguu saumu,ni dawa nzuri sana.
   
 4. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tafuteni dawa za kihaya zitawafaa nyote.
   
 5. bht

  bht JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Charity kwani zile za homeoipathic sijui ....samahani spelling mi sijui

  jaribu zile ni hazina madhara/side effects nadhani
   
 6. m

  mpangwa1 JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 279
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  tumia majani ya nyanya pori inaitwa song'imycin kausha kuvulini then loweka kwenye maji salama kunywa kama glasi moja 3x per day for 5days
   
 7. mtuwatu

  mtuwatu Member

  #7
  Mar 27, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Irighaka kwa kikurya,tafuta kata kata kunywa glas moja kwa siku hasa asubuhi baada ya kula mlo wa kwanza!
   
 8. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hiyo typhoid umechunguzwa nini hadi ukaambiwa unayo?

  Typhoid is the most over-diagnosed disease in Tanzania after Malaria.

  Vituo vya afya huwa wanatumia hiyo diagnosis kutengeneza hela tu. Jaribu kufikiria, huwezi kwenda hospitali ya rufaa hata siku moja ukaambiwa unatyphoid si Muhimbili wala KCMC, Bugando au Mbeya.

  Ni zile sehemu ambazo wanataka pesa yako.

  Kama mnataka ufafanuzi zaidi nitarudi
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hey, kama mnazo si muwasiliane nae mumpe huyu dada wakuu?

  Kutamka tu dawa itasaidia?Hapo kwa haraka mnaongelea kwenda Iringa, Mara na Bukoba, wakati mgonjwa (Charity)yuko Kinyerezi!...Kama mna stock fanyeni ze needful.
   
 10. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,819
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Nyanya pori ni nzuri zaidi
   
 11. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  naungana na hoja ya Injinia hapo juu

  Shemeji, Typhoid inataka management hasa baada ya kumaliza dozi ya kwanza, nikiassume kuwa ulikuwa diagnosed kiusahihi

  cha kufanya, ukishamaliza dozi jitahidi kunywa maziwa fresh asubuhi na jioni, pia hakikisha usafi wa kwanza maji ya kunywa....make sure maji unayitumia hasa kunywa yamechemshwa kuanzia yale ya kuswakia!

  jingine, kawaida ya ratio ya wale wajamaa ni 1:20 so huwa wapo tu..hata ukimaliza dawa, usihangaike kutumia nyingine mara moja..kaa kama mwezi hivi ukiifanyia management itaisha

  hospitali zetu nyingi zinachanganya typhoid na malaria vile dalili zinafanana...so kuwa makini sana hapo
   
 12. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,020
  Likes Received: 23,761
  Trophy Points: 280
  Pole sana mamaa.

  Dawa mbadala na ya uhakika ni hiyo hapo kwenye red. Itumie tafadhali, afu uniambie.
   
 13. Suzzie

  Suzzie Member

  #13
  Mar 29, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  kuna miti inaitwa mijohoro hata hapa mjini ipo mingi tu. ni dawa nzuri kwa t4d
   
 14. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hii nimepimwa kwenye zahanati ya Kazini.Hii ni baada ya mfululizo wa kuumwa tumbo hasa wakati wa usiku kama nimebeba kitu kizito tumboni.Nilishaenda kwenye zahanati hiyo nikapewa dawa zilizonisaidia kiasi.Nilipoona tumbo linaaza tena ndio nikaenda na kukuta sina maleria wala vile vidudu vya kwanza.na ndipo walipochukua uamuzi wa kunipima typhoid na kunikuta nayo.kwa sasa sijaanza kutumia dawa walizonipa hospital ila natumia vitunguu saumu,mpka hapo nikikuta havinisaidii.
  Kwa ufupi nadhani hawako kibiashra zaidi ila pengine ujuzi ndio ishu
   
 15. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Nitazipata wapi hizi dia.

  Dah,hizi nyanya pori ndio nyanya chungu?

  Hii irighaka itabidi nimtafute Mwita maranya.

  asante shemeji.ntajitahidi hilo la usafi ila maziwa??????????japokuwa .........
   
 16. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Dah! asante sana hun.wewe ndio unaujua ukweli ambao utaniweka huru completely.Ni YESU tu.
  Asante kwa kuelewa umuhimu wa hili jina lipitalo majina yote.
   
 17. bht

  bht JF-Expert Member

  #17
  Mar 30, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  usijali ntakupeleka mwenyewe my dear
  nimewahi kuzitumia ni nzuri hazikunipa tabu yoyote sio kama kemikali za hospitali
   
 18. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  pole sana ila angalia sana Typhod mara nyingi wataalamu wanasema joto la mwili linapopanda kwa kitu chochote kile wakikupima typhodi watakwambia unayo ni vyema kuwa makini hasa kwa wanaotafuta pesa. bora kupima tena. na inawezekana tumbo lako kuuma ukawa pia unatatizo jingine binafsi nilikuwa na sumbuliwa na tumbo na kila mara hosipitali walikuwa wanaiambia niina typhodi at last kumbe ilikuwa ni dalili ya apendex.
   
 19. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  vile vile pendelea sana kunywa maji mengi ni dawa numbari moja.
   
 20. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #20
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuna ma Dr. humu! mmmmmmmmh! wacha nisikilize tu.Pole mgonjwa!
   
Loading...