Ugonjwa wa homa ya manjano (Yellow fever)

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Ugonjwa wa homa ya manjano (Yellow fever) husababishwa na vimelea vya virusi kutoka genus (jinasi) ya Flavivirus ambao huenezwa na Mbu.

Mbu hao hupatikana kwa wingi katika sehemu za ukanda wa Joto, barani Afrika na Amerika ya Kusini.

80F12128-0A53-4429-B787-F01051BADC79.jpeg
DALILI
Dalili za ugonjwa huanza kuonekana kati ya siku 3 hadi 6 tangu kuingiwa na vimelea. Baadhi ya dalili hizo ni homa, maumivu ya kichwa, misuli na mgongo, kupoteza hamu ya kula na kutapika.

Asilimia 15 ya visa vyote vya maambukizi huingia kwenye hatua ya pili ambayo ni hatari zaidi. Dalili za hatua hii ni uwepo wa homa kali na umanjano wa mwili, hususan kwenye ngozi na macho. Pia, viungo vya mwili hasa ini na figo huashindwa kufanya kazi, kujisaidia mkojo mweusi na kuvuja damu kutoka sehemu za wazi za mwili zikihusisisha mdomo, masikio na pua. Ni hatua ambayo uhai wa watu wengi hupotea.

MATIBABU
Msaada wa matibabu kwa mgonjwa hutolewa kulingana na muonekano wake pamoja na athari zilizo sababishwa na ugonjwa husika kwa wakati huo. Kwa kiasi kikubwa, wagonjwa wanaowahishwa kupelekwa hospitalini hupona haraka, na huepukana na changamoto kubwa za ugonjwa huu.

KINGA
Njia bora ya kujikinga na ugonjwa huu ni kupata chanjo. Hutolewa mara moja pekee, ni salama na hupatikana kwa bei nafuu sana. Makundi haya yanaweza kupata chanjo-
  • Binadamu yeyote, kuanzia umri wa miezi 9 na kuendelea
  • Mtu anayesafiri kuelekea nchi yenye ugonjwa huu
  • Mtu anayesafiri kwenye nchi zilizo na matakwa ya kisheria ya kuonesha cheti cha chanjo hii baada ya kuwasili
Isipokuwa wakati wa mlipuko na hatari kubwa ya tishio la kusambaa kwa ugonjwa huu, wanawake wajawazito huwa hawashauriwi kupata chanjo hii.

Chanzo: WHO/ STG NEMLIT 2021
 
Kwa anayejua, kuna kituo cha kutoa chanjo ya homa ya manjano Rusumo? Vipi kwenye hospitali za wilaya au vituo vya afya?
 
Back
Top Bottom