Ugonjwa wa Dr. Mwakyembe ni Huu!, Jee Unasababishwa na nini?!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa wa Dr. Mwakyembe ni Huu!, Jee Unasababishwa na nini?!.

Discussion in 'JF Doctor' started by Pascal Mayalla, Feb 18, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,227
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Kufuatia malumbano yanayoendelea kuhusu ugonjwa wa Dr. Mwakiyembe. Hatimaye leo Dr. Mwakyembe mwenyewe ameka wazi ugonjwa unaomsumbua ni
  Uchunguzi wa Apollo haujakamilika kujua chanzo, two facts are definite
  1. Anaumwa Ugonjwa wa Ngozi!.
  2. Source ni something kwenye bone marrow!.

  Kwa vike humu jukwaani tunao madaktari kibao wanaoweza kutusaidia ugonjwa huu ni ugonjwa gani, unasababishwa na nini na labda matibabu yeke ni nini?.

  Angalizo, hili ni jukwaa la JF Doctor, nawaombeni sana this now is medical professional issue sio politics, hivyo kama na wewe ni mwenzangu na mimi, hujui lolote kuhusu ugonjwa huu, nakusihi sana jipitie tuu na kujinyamazia, na usichangie chochote ambacho hakihusiani na ugonjwa huu!.

  Asante!

  Pasco.
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,558
  Trophy Points: 280
  Pasco mchokonozi!! Haya madaktari toeni ufafanuzi!
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kwani we pasco huwezi kugoogle
   
 4. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kama ni mionzi kwenye ngozi hebu tuangalie maelezo haya ya kitaalamu.....

   
 5. L

  LISAH Senior Member

  #5
  Feb 18, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi napita tu but ntapita sana kujua nyie watabibu mnasemaje maana manumba si dr so siamini aliyo sema!
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,227
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jackbauer, thanks for a good try, zile ulizoweka ni zile za matokeo ya chemotherapy ndio maana wengi hushauriwa kunyoa nywele zote kabla hazijanyonyoka. Hii ya doctor ni skin disorder due to something kwenye bone marrow. Naendelea kuwasubiria madaktari wetu, walijiunga wengi wakati ule wa mgomo natumaini bado wapo!.
   
 7. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  umezielewa lakini?ha ha ha ngoja tusubiri wataalamu.
   
 8. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  sasa we mwenzangu na mimi Pasco mbona umeongea? kwanini na mimi mwenzako nisiongee? are you a doc? najivunia uhuru wa kuongea
   
 9. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  ... wala sio journalism !! Ha ha haaa!
   
 10. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Kwa kuwa yeye na nduguze wameamua kuyaongelea mambo ya ugonjwa wake kwenye majukwaa ya kanisa, halafu akija kwenye mics za mapaparazi anageuza kauli, tumuache tu augulie. Huenda ndugu zake watatoa kauli ya maana endapo Mungu atamchukua baada ya yeye kushindwa kuongea ukweli. Atakuwa anahofia kususwa akajikuta akienda Appolo kwa gharama zake badala ya zile za serikali.

  Umasikini na ufungwa wa akili ni mbaya kuliko kitu kingine chochote duniani. Jamaa ameamua kufa mwenyewe kwa faida ya magamba. Taaabu kweli kweli!
   
 11. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Pasco.......

  Kwani Mwakyembe anaumwa ugonjwa gani?........

  Nimeisoma taarifa ya Mwakyembe sijaona sehemu aliyotaja ugonjwa unaomsumbua zaidi ya kusema kuna kitu kwenye bone marrows(uboho) ambacho ndicho kinachochea hali hii aliyonayo sasa na kwamba madaktari wanaendelea na uchunguzi ili kugundua hicho ni kitu gani.......

  Sidhani kama kulikuwa na haja ya kuanzisha Thread hii..........
   
 12. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mkuu naomba uweke maelezo kamili ya [FONT=&amp]Dk. Harrison G. Mwakyembe (Mb), NW-UJ[/FONT]
   
 13. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  Dk. Harrison Mwakyembe, kabla ya kuumwa na kupelekwa India kwa matibabu.​


  Dk. Harrison G. Mwakyembe (Mb), NW-UJ
  Dar es Salaam
  18/02/2012  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  Nimelazimika leo Jumamosi, tarehe 18 Februari, 2012 kutoa taarifa hii kwa vyombo vya habari kufuatia mkutano wa DCI Robert Manumba na waandishi wa habari jana (17/02/12) kuongelea, pamoja na mambo mengine, hali yangu ya afya na kuhitimisha, kienyejienyeji tu kuwa "sikunyweshwa sumu" ila naumwa tu ugonjwa wa ngozi bila kufafanua ugonjwa huo wa ngozi umesababishwa na nini!

  Napenda nisisitize mapema kabisa kuwa msimamo huo wa Jeshi la Polisi umenikera sana katika hali niliyonayo ya ugonjwa, kwanza kwa kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina kuhusu kiini chake unaoendelea hospitali ya Apollo nchini India ambako bado sijahitimisha matibabu yangu; pili kwa ufinyu wa uelewa unaojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa "sikunyweshwa sumu" wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu; na tatu kwa Jeshi la Polisi kujiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.

  Itakumbukwa kuwa tarehe 9 Februari, 2011 nilimwandikia barua IGP Said Mwema kumtaarifu kuhusu njama za kuondoa maisha yangu na ya viongozi wengine. Kwa kutambua kuwa Jeshi la Polisi la Tanzania daima husisitiza kuletewa ushahidi kwanza ndipo lifanyekazi, nilihakikisha nimeainisha katika barua hiyo kila ushahidi nilioupata au kupewa. (Utaratibu huu wa Jeshi la Polisi kusubiri kuletewa ushahidi mezani, kama ambavyo mahakimu wanavyosubiri ushahidi mahakamani, haupo popote pale duniani (ila Tanzania tu) kwani kazi ya msingi ya Polisi si kuletewa, ni kutafuta ushahidi. Polisi wanachohitaji duniani kote ni kupata clue au tetesi tu. Hiyo inatosha kufukua ushahidi wote unaohitajika). Pamoja na kujitahidi kuanika kila aina ya ushahidi niliokuwa nao, mambo manne yalijitokeza ambayo yalionyesha wazi kuwa Polisi hawakuwa na dhamira ya dhati ya kupeleleza suala hilo:

  (i) Siku chache baada ya kumkabidhi IGP barua hiyo, nilitumiwa timu ya "wapelelezi" ofisini kwangu kuja kuchukua maelezo yangu ya ziada. Timu hiyo ilikuwa inaongozwa na ACP Mkumbo, afisa wa polisi ambaye wiki chache zilizokuwa zimepita alikuwa miongoni mwa askari waliotuhumiwa kupokea rushwa kwa lengo la kumbambikizia madawa ya kulevya mtoto wa Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, suala ambalo mpaka leo hii uongozi wa Polisi umeshindwa kulitolea maelezo ya kuridhisha. Kwa msingi huo, nilikuwa nimeletewa mtuhumiwa wa rushwa/ ujambazi kuendesha uchunguzi wa watuhumiwa wengine wa ujambazi! Nikatambua mara moja kuwa zoezi zima lilikuwa la mzaha, tena mzaha mkubwa!

  (ii) Wiki chache baada ya barua yangu kuwasilishwa kwa IGP na timu ya ACP Mkumbo "kuanza kazi", Jeshi la Polisi likachukua hatua ya kuwapongeza na kuwazawadia askari niliowatuhumu kushirikiana na majambazi! Huhitaji kuwa profesa wa falsafa kuelewa kuwa huo ulikuwa ujumbe tosha wa kunipuuza.

  (iii) Hivi karibuni tuhuma za askari polisi kujihusisha na vitendo vya ujambazi mkoani Morogoro zilipopamba moto na kuwagusa askari "wale wale" niliowatuhumu kwenye barua yangu, IGP alichukua hatua ya kuwahamishia mikoa mingine!

  (iv) ili kunikatisha tamaa kabisa, barua yangu ya "siri" kwa IGP ikavujishwa kwa makusudi kwenye vyombo vya habari na kuchapishwa kama habari ambayo ilikebehi na kukanusha taarifa nzima niliyotoa, sijui kwa faida ya nani! Lakini huu ni mchezo wa kawaida kwa polisi kwani hivi karibuni Mhe. Waziri Samuel Sitta alipohojiwa na ofisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi ofisini kwake, wakiwa wawili tu, taarifa ya kikao hicho ikawa magazetini ikikebehi ushahidi aliotoa Sitta! The integrity of the police force leadership is on the line.

  Nimeelezea vizuri katika barua yangu kwa IGP kuwa kundi hilo la mauaji lilikuwa limeelekezwa kuniua kwa kutumia sumu, taarifa ambayo kwa karibu mwaka mzima Polisi hawakutaka kuifuatilia kwa sababu wanazozijua wenyewe. Sasa huu msukumo mpya wa Jeshi la Polisi kutaka kujua kama nilipewa sumu au la na kukurupuka kutoa tamko hata kabla ya kunichunguza nilivyo, kunihoji mimi na wasaidizi wangu ofisini na hata kuongea na mabingwa wa Kihindi wanaonifanyia uchunguzi, umetokea wapi?

  Aidha napata taabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matatibabu yangu au walisoma taarifa "nyingine", na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au "walisomewa"
  ! Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa wandishi wa habari hakifanani kabisa na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya Apollo ambayo inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukidhibiti/ kukiondoa huku vyombo vyetu vya dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi na bila aibu: "hakulishwa sumu", "hakulishwa sumu"!

  Nimesoma darasa moja Kitivo cha Sheria Mlimani na DCI Manumba. Baadaye IGP Mwema alikuwa mwanafunzi wangu wa sheria Mlimani. Vigogo hawa wawili wa usalama wa raia nchini hawajanitendea haki, nao wanajua. Wanajua vilevile kuwa sitakaa kimya au kumung'unya maneno come what may pale ambapo haki inakanyagwa.

  Tuendelee kuombeana afya na uhai ili tutendeane haki na vilevile tuitendee nchi yetu haki kwa kuvimalizia viporo vinavyokera vya Dowans, EPA, Kagoda n.k. kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

  Mungu Ibariki Tanzania.
   
 14. hollo

  hollo JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2012
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 781
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Huo ugonjwa husababishwa na sumu.
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,227
  Trophy Points: 280
  Kaisome tena halafu urudi, sio wote wenye uwezo wa kusoma in between the lines!. Hii ni thread ya kuulizia madaktari kuhusu ugojwa huo!. Ugonjwa ameutaja na Uchunguzi ulishafanyika uko kwenye ripoti yake. Amini nakuambia anarudi for check up sio uchunguzi tena!. Kwa kukusaidia tuu,
  "Uchunguzi wa Apollo haujakamilika kujua chanzo, two facts are definite
  1. Anaumwa Ugonjwa wa Ngozi!.
  2. Source ni something kwenye bone marrow!."
  Wewe unaujua huo ugonjwa wa ngozi ambao source ni something kwenye bone marrow?. Naamini wewe hujui, bali unawasubiria hao madaktari wa Apollo ndio watuambie ni nini?.

  Mimi pia sijui ndio maana nimeuliza, ila badala ya wote kuwasubiria hao madaktari wa Apollo ndio watujulishe, nimewauliza madaktari wetu humu jf watuambie wanachojua!. Nimeuliza anaejua aseme, ila pia nimeshauri asiye jua na ajinyamazie!. Hawa wenzako wote Pierre King,
  Edwin Mtei,
  Vome,
  TONGONI,
  Kimokole,
  anjnr,
  ndyoko,
  Pinokyo Jujuman,
  Jahom,
  Mtanzania haswa,
  Jackbauer,
  Domo Zege,
  RedDevil, pia wapo na wamejinyamazia!, kwani lazima uchangie kila posti?, nyingine kama hujui pitia tuu na kujinyamazia!.
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,227
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ng'wanza Madaso, maelezo kamili ni marefu na politics nyingi mule, hii ni thread ya kuujadili ugonjwa huo tuu na sio siasa za issue hii!
   
 17. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #17
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Nimesoma na kuyaelewa na sijaona mahali ambapo Mwakyembe ametaja ugonjwa unaomsumbua......Ugonjwa ambao umewataka wana JF wakueleze unasababishwa na nini.....Ni vema ungetaja jina laugonjwa badala ya kusema tu kwamba Mwakyembe ana ugonjwa ambao chanzo chake ni something kwenye bone marrows.....Kumbuka kuna magonjwa mengi ambayo source yake ni something kwenye bone marrows...


  [h=2]Re: Ugonjwa wa Dr. Mwakyembe ni Huu!, Jee Unasababishwa na nini?!.[/h]
   
 18. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2012
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Jamani mbona ukisoma taarifa inaonekana wazi kwamba Dr. anaamini (anahakina?) kapewa sumu, na ana'link' waliompa sumu na Mafisadi wa EPA etc.
   
 19. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  Pasco, kwa kuwa uliwahi kulazwa kwenye moja ya hospitali za Apollo baada ya kuanguka na pikipiki, ni vyema ukatumia urafiki wako na madaktari wa huko wakuibie taarifa ya ugonjwa wa Mwakyembe na sababu zilizosababisha, kuliko kuja kuuliza madaktari wa hapa JF ambao hata hivyo wengi wao hatuna uhakika kama ni madaktari kweli. Ujue humu JF hata Kupeng'e siku hizi anajiita Dr. Kupeng'e, wakati hoja zake wengi tunazijua humu.

  Madaktari wako wa India wanaweza wakawa na msaada mkubwa kwako unayehitaji sababu za ugonjwa huo.
   
 20. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #20
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Pasco,
  Sikuwa na nia ya kuchangia hii thread lakini umenilazimisha kufanya hivyo.

  Ndugu yangu punguza siasa kwenye taaluma za watu. Taarifa ya mwakyembe wote tumeisoma, hakuna mahali ametaja ugonjwa anaoumwa, zaidi ya kusema mzizi wa tatizo lake uko kwenye bone marrow, sasa wewe mwanasiasa- mwanahabari umezipata wapi hizo facts?

  Unajaribu kuwaongoza madaktari kwenye fani yao ili iweje? Una upande katika huu ugonjwa wa Dr. Mwakyembe?

  Ilitosha tu kuweka taarifa ya Dr. Mwakyembe na kuwaacha madaktari wenyewe waogelee. Lakini kwakuwa umei-jeopardise mwenyewe hoja yako uwe mvumilivu na sisi wanasiasa wenzako tunaopotoa maoni yetu dhidi ya hoja zako, wakati huo nikiwaomba madaktari wajielekeze kwenye taarifa ya Mwakyembe wanapojibu.

  Ni vizuri ukaacha siasa ktk jukwaa la JF Doctors ili sote tunufaike kuliko kujaribu kuwapotosha madaktari, sijui kwa faida ya nani!?
   
Loading...