benbry
Senior Member
- Apr 3, 2012
- 183
- 54
Habarini za saa hizi ndugu. Ninaamini humu kuna watu wenye experience mbalimbali za maisha. Wapo wenye umri mkubwa (waliokula chumvi nyingi) lkn pia wapo waliopitia visa na mikasa mbalimbali kwenye hii dunia. Lakini pia wapo watu wenye imani mbalimbali na zenye nguvu mbalimbali humu.
Mimi nina mtoto anasoma darasa la Tano shule flani iliyopo Dsm. Huyu mtoto anashindwa kwenda shule, sio kwa kupenda bali kafungwa na nguvu zisizojulikana.
Akiamka anajiandaa kwenda shule, akifika karibu na nahali pa kupanda basi la shule anazimia.
Ukimrudisha nyumbani anaamka na analilia kwenda shule. Ukimchukua tena na gari mnaenda ila mkilikaribia geti la shule anazimia na haamki hata ukae nae hapo kwa muda mrefu kiasi gani.
Ukigeuza tu kumrudisha nyumbani anaamka fresh tu.
Nilijaribu kumuombea shule nyingine nikidhani tatizo ni shule lkn hata hapo alikipelekwa akikaribia geti anazimia.
Hili tatizo limenisumbua kwa muda sasa, wapo watumishi waliopambana nae ili apone na wengine walijipa hadi muda wa kumpeleka shule lkn ilishindikana anazimia mbele yao.
Wapo wataalamu wa miti shamba waliojaribu kumuweka sawa pia hadi sasa haijafanikiwa.
Naombeni ushauri, either kwa waliopitia/kusikia madhila ya aina hii na wakapata solution. Au wanaofahamu mahali pa kupata solution wanisaidie mawazo tafadhali.
Unaweza pia kunifata PM nitashukuru kwa msaada wako. Ninachoamini ni kuwa hili litapita kwa kuwa hakuna shida mpya duniani, isipokuwa litapitaje na lini ndio shida ilipo.
Asanteni.