Ugonjwa wa ajabu sana umempata mtoto

carcinoma

JF-Expert Member
Mar 5, 2017
4,965
2,000
Mkuu hapo kuna possibilities mbili.
1. Mtoto hajifanyishi kuzimia bali ni kweli anakata moto.. hilo tatizo sio la kiroho ni la psychiatry...jina nimesahau lkn inatokea mtu ana hofu ya ndani kuhusu kitu flani kwahio mwili automatically unakata moto..
Unaweza kukuta mtu anaogopa mitihani ikifika siku ya pepa anaparalize upande mmoja. Sio kwamba anajifanyisha nop... huyo mtoto mpeleke kwa psychiatrist atarudi akiwa mpyaaaaa kabisa.

2.. possibility ya pili ni kwamba dogo anakuectia.
Hapa solution fanya kama member mmoja alivyoshauri juu.. mpeleke shule nyingine kwa siri bila yeye kujua kama anapelekwa shule.. yaani mdanganye mnaenda hospitali kumbe unaenda shule... uone kama atazima njiani

NB: hapa maombi hayahusiki.. hata ukimpeleka kwenye maombi fanya hivyo kwaajili ya psychological treatment lakini ukitegemea ka muujiza katoke anga za mbali kamponye mwanao...sahau!
 
Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
59,467
2,000
Pole sana...

Nacheka kama mazuri vile...

Duniani kuna tabia nyingi sana aisee... mfano kuna wale watoto ambae wakiona chakula tu wanajifanya kusinzia... hawapendi kula kabisa... na wakila basi watatumia hata nusu siku...

Kuna wale watu wazima wakishikwa na msala/tatizo tu wanajifanya kupandisha mashetani... hawa ni unacharaza viboko mashetani yanakwisha...

Huyo mwanao anacheza na akili zenu, hapendi shule... jaribu kuwa mkali, na ikiwezekana charaza viboko haswa ataacha uongo...

Cc: mahondaw
 
MUNDENDE

JF-Expert Member
Jan 6, 2017
817
1,000
Kuna kitu kinaitwa 'attention deficit disorder'. Mtoto akihisi hapati attention ya kutosha basi anatafuta sababu ya kupewa attention kwa lazima. Nakumbuka vizuri nilipokuwa mdogo sana kuna siku niliamua kujifanya naumwa nikawa najitetemesha vibaya kama mtu aliezidiwa na homa, nilijisia raha sana pale baba yangu alivyoacha kazi zake zote na kurudi nyumbani na kunikimbiza hospitali, ofcourse sikukutwa na kitu ila nilijisikia furaha ya ajabu kuona baba ananipenda kiasi kile.
Haahhaha ulikua fala kweli.haah
 
alibaaliyo

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
536
500
Huyu labda kuna mtoto anampiga sana shule na anaogopa kusema huku akipenda shule ila ndio hivyo tena

Bullying ni mbaya sana jaribu kumdadisi sana kwa upole huenda ikawa sababu ni hiyo au ongea na wanafunzi wenzake pia
Fanya ufuatuliaji kuhusu bulling. Inawezekana kuna mtoto /mwanafunzi mwenzie anamfanyia matendo ya kumyanyasa/kumtisha n.k. Inawezekana pia ni mwalimu au njiani akirudi kutoka shule huwezi jua.

Mwone mwanapsycho logia aliyesomea aweza kukusaidia.
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
17,712
2,000
Fanya ufuatuliaji kuhusu bulling. Inawezekana kuna mtoto /mwanafunzi mwenzie anamfanyia matendo ya kumyanyasa/kumtisha n.k. Inawezekana pia ni mwalimu au njiani akirudi kutoka shule huwezi jua.

Mwone mwanapsycho logia aliyesomea aweza kukusaidia.

Unamjibu mwenye mtoto ujue mkuu sio mimi
 
Lordmudy

New Member
Jul 17, 2019
1
20
Habarini za saa hizi ndugu. Ninaamini humu kuna watu wenye experience mbalimbali za maisha. Wapo wenye umri mkubwa (waliokula chumvi nyingi) lkn pia wapo waliopitia visa na mikasa mbalimbali kwenye hii dunia. Lakini pia wapo watu wenye imani mbalimbali na zenye nguvu mbalimbali humu.

Mimi nina mtoto anasoma darasa la Tano shule flani iliyopo Dsm. Huyu mtoto anashindwa kwenda shule, sio kwa kupenda bali kafungwa na nguvu zisizojulikana.
Akiamka anajiandaa kwenda shule, akifika karibu na nahali pa kupanda basi la shule anazimia.
Ukimrudisha nyumbani anaamka na analilia kwenda shule. Ukimchukua tena na gari mnaenda ila mkilikaribia geti la shule anazimia na haamki hata ukae nae hapo kwa muda mrefu kiasi gani.
Ukigeuza tu kumrudisha nyumbani anaamka fresh tu.
Nilijaribu kumuombea shule nyingine nikidhani tatizo ni shule lkn hata hapo alikipelekwa akikaribia geti anazimia.

Hili tatizo limenisumbua kwa muda sasa, wapo watumishi waliopambana nae ili apone na wengine walijipa hadi muda wa kumpeleka shule lkn ilishindikana anazimia mbele yao.
Wapo wataalamu wa miti shamba waliojaribu kumuweka sawa pia hadi sasa haijafanikiwa.

Naombeni ushauri, either kwa waliopitia/kusikia madhila ya aina hii na wakapata solution. Au wanaofahamu mahali pa kupata solution wanisaidie mawazo tafadhali.
Unaweza pia kunifata PM nitashukuru kwa msaada wako. Ninachoamini ni kuwa hili litapita kwa kuwa hakuna shida mpya duniani, isipokuwa litapitaje na lini ndio shida ilipo.
Asanteni.
Habari , mdogo wangu anasumbuliwa na tatizo kama hilo ni mwaka wa pili sasa ni hivyohivyo tumeenda kila sehemu ila nothing.. ni mazito sana haya kwa mtu ambaye hayajamkuta kusema mtoto anajifanyisha ila niamini hajifanyishi.. nitumie msg private tutaongea
 
TUNDALI

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
427
250
Pole kwa kipindi unachopitia,
Fanya uchunguzi mazingira ya tatizo yalianza lini, uwafahamu Rafiki zake shuleni, Mwalimu wake anamuelezeaje kwa tabia darasani na masomo,
Je jirani pia kama kuna watu wazima aliozoeana nao sana na humpa hata zawadi pasipo wazazi kufahamu na aliwahi kupewa nini na kipo wapi,
Je kuna mahali aliwahi kwenda pasipo ninyi kufahamu na alifanya nini huko, maswali au uchunguzi wako ufanye ukiwa umeuvaa upendo sana kwa Mtoto, kama ana hofu ya kukujibu mbembeleze atakueleza tu Hakuna Mtu anaeaminiwa na mtoto kama mzazi na mwalimu,
Je kuna msaidizi wa kazi kwako, unamfahamu vizuri?
Ukishindwa kumuhoji wewe Mtumie Ndugu wa karibu aliemzoea sana..
Mwisho kabisa kuna mambo ya mila mlifanya yakihusisha watoto kulingana na tamaduni zenu,
Utakachobaini kitakufanya uamue ufanye nini, lakini kubwa zaidi utampeleka Nyumba za ibada kwa maombi maalumu, Atapona.
Habarini za saa hizi ndugu. Ninaamini humu kuna watu wenye experience mbalimbali za maisha. Wapo wenye umri mkubwa (waliokula chumvi nyingi) lkn pia wapo waliopitia visa na mikasa mbalimbali kwenye hii dunia. Lakini pia wapo watu wenye imani mbalimbali na zenye nguvu mbalimbali humu.

Mimi nina mtoto anasoma darasa la Tano shule flani iliyopo Dsm. Huyu mtoto anashindwa kwenda shule, sio kwa kupenda bali kafungwa na nguvu zisizojulikana.
Akiamka anajiandaa kwenda shule, akifika karibu na nahali pa kupanda basi la shule anazimia.
Ukimrudisha nyumbani anaamka na analilia kwenda shule. Ukimchukua tena na gari mnaenda ila mkilikaribia geti la shule anazimia na haamki hata ukae nae hapo kwa muda mrefu kiasi gani.
Ukigeuza tu kumrudisha nyumbani anaamka fresh tu.
Nilijaribu kumuombea shule nyingine nikidhani tatizo ni shule lkn hata hapo alikipelekwa akikaribia geti anazimia.

Hili tatizo limenisumbua kwa muda sasa, wapo watumishi waliopambana nae ili apone na wengine walijipa hadi muda wa kumpeleka shule lkn ilishindikana anazimia mbele yao.
Wapo wataalamu wa miti shamba waliojaribu kumuweka sawa pia hadi sasa haijafanikiwa.

Naombeni ushauri, either kwa waliopitia/kusikia madhila ya aina hii na wakapata solution. Au wanaofahamu mahali pa kupata solution wanisaidie mawazo tafadhali.
Unaweza pia kunifata PM nitashukuru kwa msaada wako. Ninachoamini ni kuwa hili litapita kwa kuwa hakuna shida mpya duniani, isipokuwa litapitaje na lini ndio shida ilipo.
Asanteni.
 
kwenda21

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
2,801
2,000
Mimi tanga nilipataga ugonjwa flan mkono wa kuandikia kucheza,ili nifanya kuwa na muandiko mbaya hadi Leo,tatizo lilianza mkono kuwasha
 
mkabasia

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
2,216
2,000
Sasa bora huyu anajizimisha mie nilikua najifanya nna mashetan..lol
Hahahaha,umenikumbusha nnakaa na mtoto wa kakangu yupo std 4.Mwaka Jana alinifanyia huo mchezo(kupandisha mapepo ya uongo).Kumbe dogo anataka arudi Kwa mamake.Hamna cha mashetani wala nini nkikumbuka nacheka sana.

Mtoa mada jaribu kufatilia Kwa umakini zaidi kupitia ushauri mbalimbali humu uujue ukweli kihusu mwanao.Kujifanyisha kupo,na ya ukweli pia yapo.
 
uhurumoja

JF-Expert Member
Mar 2, 2014
2,590
2,000
Tuwe realistic,unaweza ukajifanya kuzimia?hebu jaribu wewe mtu mzima kama ina wezekana,vipi kuhusu mtoto,hiyo experience ya kuzimia kaipata wapi katika huo umri wa darasa la tano?Ushauri wangu ni kuwa simama katika Imani ya uponyaji kwa njia ya maombi na kufunga kama kweli unampenda mtoto wako,yako maroho ambayo wanatupiwa watu kwa nia ya kuharibu future ya mtu,amini hilo kuwa lipo,na kama wengine wanavyokupa ushauri wa kutembelea baadhi ya makanisa fanya hivyo,ila usiende kwenye kanisa kama unaenda hospitali,ili ukipata uponyaji wako urudie kwenye madhambi,ni lazima ujitakase kwa kutubu dhambi ili uanze maisha mapya ya kumtukuza Mungu...
Bora umemsaidia nadhani kuna watu wengi sana humu sio watanzania kabisa na hawajui kabisa maisha ya Tanzania!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom