Ugonjwa wa ajabu sana umempata mtoto

Mbona sioni wanaoshauri apelekwe kwa 'ostadhi'?

Mleta mada kwanini unakwepa kutupia taarifa ya maendeleo ya taaluma ya mwanao?

Hata jinsia?

Tupunguzie mzigo wa jinsi ya kukushauri.
 
Aisee

Umenikumbusha tukio langu la utoto khaa!!
Kuna kitu kinaitwa 'attention deficit disorder'. Mtoto akihisi hapati attention ya kutosha basi anatafuta sababu ya kupewa attention kwa lazima. Nakumbuka vizuri nilipokuwa mdogo sana kuna siku niliamua kujifanya naumwa nikawa najitetemesha vibaya kama mtu aliezidiwa na homa, nilijisia raha sana pale baba yangu alivyoacha kazi zake zote na kurudi nyumbani na kunikimbiza hospitali, ofcourse sikukutwa na kitu ila nilijisikia furaha ya ajabu kuona baba ananipenda kiasi kile.
 
Nakushauri kwa njia ambayo mama yangu alitumia kutibu tatizo kama hilo kwa mdogo wangu wa mwisho ambalo lilikua limechukua takribani miezi tisa bila suluhisho
Mdogo wangu alikua darasa la sita na alikua akifika shule anazimia au akiwa njiani kwenda shule tulihangaika na hospital maombi na tiba mbadala bila mafanikio
Naye alikua analilia kwenda shue kama wako ila kumbe gia ya kulilia ilikua ili kutuaminisha kwamba kweli anazimia na anaumwa
Okafikia jatu nasi tukawa tunamlinda asitoke nyumbani ili asijezimia mwisho akafa kabisa
Basi mama mmoja mwenye busara akaongea na mama akanwambia iwe siri yao ajidai anampeleka kwa mtaalsmu (ambaye ndio huyo mama) hivyo mama alimchukua mdogo wangu mpaka kwa yule mama na yule mama akamwambia anampa dawa ya kunywa kutibu igonjwa wa kuzimia ila dawa ina sharti moja kama ambalo ni akawa anamwambia mama unauhakika mwanao kweli anaumwa kuzimia maana kama hana ugonjwa huo akinywa dawa hii atapata kifafa ambacho hakiponi
Na hio dawa nilipaka usoni ( alikua kampaka unga wa ugali akidanganya ni dawa) kama hana ugonjwa atakua na ukurutu uso wote hivyo mama kama unaamini anaumwa basi mpe anyww dawa hii hapahapa anapona
Kabla hajamaliza kusema mdogo wangu akaanza kulia anamuomba mganga yaani yule mm amutoe ile dawa usoni maana alikua anadanganya akaogopa kupata kifafa
Tangu siku hiyo mpaka leo hajazimia na mwezi huu kamaliza digriii
Ila alikua hataki shule
Ushauri wangu jaribu kumchunguza mara mia zaidi kama kweli ni mgonjwa
Yesuuuuui,hv kumbe watoto wana mbinu nyingi hivyonajifunzaaa kwakweli
 
Umeandika vya maana sana
Mkuu pole sana.
Wala usiende kwa waganga jikite tuu kwenye maombi.
Na asiombewe yeye tuu inabidi familia nzima mfanyiwe maombi ya ukombozi. Na nyie wazazi pia muwe mnaomba toba kwa ajili ya watoto wenu na vizazi vyenu. Ulimwengu wa roho una mambo mengi sana. Mtoto wenu anaweza kupona kupitia nyie.

Nakazia, usichoke kwenye kumtegemea Mungu. Yawezekana wakati ndiyo unachoka na Mungu ndiyo alikuwa anaanza kujibu.
 
Nakushauri kwa njia ambayo mama yangu alitumia kutibu tatizo kama hilo kwa mdogo wangu wa mwisho ambalo lilikua limechukua takribani miezi tisa bila suluhisho
Mdogo wangu alikua darasa la sita na alikua akifika shule anazimia au akiwa njiani kwenda shule tulihangaika na hospital maombi na tiba mbadala bila mafanikio
Naye alikua analilia kwenda shue kama wako ila kumbe gia ya kulilia ilikua ili kutuaminisha kwamba kweli anazimia na anaumwa
Okafikia jatu nasi tukawa tunamlinda asitoke nyumbani ili asijezimia mwisho akafa kabisa
Basi mama mmoja mwenye busara akaongea na mama akanwambia iwe siri yao ajidai anampeleka kwa mtaalsmu (ambaye ndio huyo mama) hivyo mama alimchukua mdogo wangu mpaka kwa yule mama na yule mama akamwambia anampa dawa ya kunywa kutibu igonjwa wa kuzimia ila dawa ina sharti moja kama ambalo ni akawa anamwambia mama unauhakika mwanao kweli anaumwa kuzimia maana kama hana ugonjwa huo akinywa dawa hii atapata kifafa ambacho hakiponi
Na hio dawa nilipaka usoni ( alikua kampaka unga wa ugali akidanganya ni dawa) kama hana ugonjwa atakua na ukurutu uso wote hivyo mama kama unaamini anaumwa basi mpe anyww dawa hii hapahapa anapona
Kabla hajamaliza kusema mdogo wangu akaanza kulia anamuomba mganga yaani yule mm amutoe ile dawa usoni maana alikua anadanganya akaogopa kupata kifafa
Tangu siku hiyo mpaka leo hajazimia na mwezi huu kamaliza digriii
Ila alikua hataki shule
Ushauri wangu jaribu kumchunguza mara mia zaidi kama kweli ni mgonjwa
Nadhani wewe umamaliza kila kitu
 
Mpeleke kanisani kwa watumishi wa Mungu iyo na kazi ndigo sana sasa Mungu akusaidie usikutane na wachumia tumbo manabii wa uongo.
 
Pole sana mkuu!
Kama unamwamini Mungu Aliyehai funga na kumwombea mwanao siku mbili kavu pasipo kula, kuonana na mtu wala kufanya jambo lingine lolote la kidunia isipokuwa kuomba, kusoma biblia, kusifu na kuabudu.

Ukiomba kwa imani thabiti lazima tatizo hilo litaisha.
 
Back
Top Bottom