Ugonjwa wa ajabu sana umempata mtoto

Hajawajua tu watoto...yaan huyo anajifanyisja 100%...huyo unamchapa mboko akijizimisha ataamka mwenyeweee...
Kuna kitu kinaitwa 'attention deficit disorder'. Mtoto akihisi hapati attention ya kutosha basi anatafuta sababu ya kupewa attention kwa lazima. Nakumbuka vizuri nilipokuwa mdogo sana kuna siku niliamua kujifanya naumwa nikawa najitetemesha vibaya kama mtu aliezidiwa na homa, nilijisia raha sana pale baba yangu alivyoacha kazi zake zote na kurudi nyumbani na kunikimbiza hospitali, ofcourse sikukutwa na kitu ila nilijisikia furaha ya ajabu kuona baba ananipenda kiasi kile.
 
Habarini za saa hizi ndugu. Ninaamini humu kuna watu wenye experience mbalimbali za maisha. Wapo wenye umri mkubwa (waliokula chumvi nyingi) lkn pia wapo waliopitia visa na mikasa mbalimbali kwenye hii dunia. Lakini pia wapo watu wenye imani mbalimbali na zenye nguvu mbalimbali humu.

Mimi nina mtoto anasoma darasa la Tano shule flani iliyopo Dsm. Huyu mtoto anashindwa kwenda shule, sio kwa kupenda bali kafungwa na nguvu zisizojulikana.
Akiamka anajiandaa kwenda shule, akifika karibu na nahali pa kupanda basi la shule anazimia.
Ukimrudisha nyumbani anaamka na analilia kwenda shule. Ukimchukua tena na gari mnaenda ila mkilikaribia geti la shule anazimia na haamki hata ukae nae hapo kwa muda mrefu kiasi gani.
Ukigeuza tu kumrudisha nyumbani anaamka fresh tu.
Nilijaribu kumuombea shule nyingine nikidhani tatizo ni shule lkn hata hapo alikipelekwa akikaribia geti anazimia.

Hili tatizo limenisumbua kwa muda sasa, wapo watumishi waliopambana nae ili apone na wengine walijipa hadi muda wa kumpeleka shule lkn ilishindikana anazimia mbele yao.
Wapo wataalamu wa miti shamba waliojaribu kumuweka sawa pia hadi sasa haijafanikiwa.

Naombeni ushauri, either kwa waliopitia/kusikia madhila ya aina hii na wakapata solution. Au wanaofahamu mahali pa kupata solution wanisaidie mawazo tafadhali.
Unaweza pia kunifata PM nitashukuru kwa msaada wako. Ninachoamini ni kuwa hili litapita kwa kuwa hakuna shida mpya duniani, isipokuwa litapitaje na lini ndio shida ilipo.
Asanteni.
Mkuu,Pole sana,Ungeweka historia kidogo ya jinsi hali ilivyoanza na ilianza wakati gani na kama kuna tukio lolote linalohusiana na hio hali lilimtokea mtoto.

Kisha amka nenda naye shule bila kumvalisha uniform wala kumuandaa yaani nenda naye mpaka shule ila sio kwa ratiba ya kwenda shule.Kabla ya kuendoka nyumbani hakikisha unachukua chumvi,magadi,maji ya bomba pamoja na kipande cha ndimu unachanganya unasali kwa mujibu wa imani yako kisha unavitakasa hivyo vitu kwa ajili ya kumtakasa mtoto.Baada ya hapo hakikisha nyumba nzima mnaogea maji yaliyochanganywa na huo mchanganyiko.Yaani wote hata kama ni nani.Fanya Hivyo kisha ulete mrejesho.
 
Pole sana kwa yanayokutokea. Una uhakika hajifanyishi kwa makusudi? Nauuliza hivi kwa sababu nimeshakutana na kesi kama hii. Mtoto wa kike alikuwa na miaka kama 15 lakini alikuwa ni actor mzuri sana sana. Yeye akifika tu shule ''anazimia''. Mpaka waje kugundua kuwa anaigiza ilichukuwa muda mrefu sana. Kama una uhakika kuwa hafanyi acting basi huenda ni tatizo la kisaikolojia.


Bora useme ww...huyu anajifanysha tu...! Mie nikipokua mdogo km 10yrs baba akichukua likizo alikua anaenda Kwao..sasa mm nilikua kivuruge na mkorofi sana..kwahyo mama alikua akinipiga sana...baba alikua akinitetea sana coz nilikua nna akili...nikaanza kijifanyisha naumwa sana kila baba akichukua likizo...hhahaa then najifanya nna mashetani yanasema baba asiende Mwanza...πŸ˜‚πŸ˜‚mission yangu ikawa imekamilΓ¬ka..kwahyo baba akawa anabaki hom hasafiri....!mie sitapata mtoto atakayenizidi akili aisee!
 
Amna mkuu, hata muda huu hapa yuko nyumbani analia apelekwe shule, tumeficha hadi funguo ya geti mana likibaki wazi analazimisha kwenda shule ila njiani ndio hivyo. Analalamika tu hapa mana hata yeye hajui kwa nini hawezi kwenda.
Kulilia kwenda shule si ndio anaona raha anavyowaendesha, darasa la tani si mdogo, anajua mchezo anaowafanyia, huyo ana 'attention disorder'
 
Kuna kitu kinaitwa 'attention deficit disorder'. Mtoto akihisi hapati attention ya kutosha basi anatafuta sababu ya kupewa attention kwa lazima. Nakumbuka vizuri nilipokuwa mdogo sana kuna siku niliamua kujifanya naumwa nikawa najitetemesha vibaya kama mtu aliezidiwa na homa, nilijisia raha sana pale baba yangu alivyoacha kazi zake zote na kurudi nyumbani na kunikimbiza hospitali, ofcourse sikukutwa na kitu ila nilijisikia furaha ya ajabu kuona baba ananipenda kiasi kile.



πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hii ishu nilishaishuhudia ila kwa mdada mkubwa kabisa. Yeye alipambana mpaka akafika chuo ila huko majanga yalimzidia hasa kwenye mitihani full kuzimia.
Yeye ndio alishauri tumpeleke shule nyingine mana anasumbua hadi kulia apelekwe shule lkn aki attempt kwenda ndio yanatokea hayo. Hii ni issue serious msiichukulie kimzaha.
 
Mkuu,Pole sana,Ungeweka historia kidogo ya jinsi hali ilivyoanza na ilianza wakati gani na kama kuna tukio lolote linalohusiana na hio hali lilimtokea mtoto.

Kisha amka nenda naye shule bila kumvalisha uniform wala kumuandaa yaani nenda naye mpaka shule ila sio kwa ratiba ya kwenda shule.Kabla ya kuendoka nyumbani hakikisha unachukua chumvi,magadi,maji ya bomba pamoja na kipande cha ndimu unachanganya unasali kwa mujibu wa imani yako kisha unavitakasa hivyo vitu kwa ajili ya kumtakasa mtoto.Baada ya hapo hakikisha nyumba nzima mnaogea maji yaliyochanganywa na huo mchanganyiko.Yaani wote hata kama ni nani.Fanya Hivyo kisha ulete mrejesho.


Hakuna cha kutakasa wala utakaso..dogo anajifanyisha
 
Lazima kuna Logical explanation tu, inawezekana anajifanyisha huyo mtoto. Fanya kitu kinaitwa Placebo, mwambie kwamba kesho mnaenda hospitali kwa ajili ya checkup, lakini kumbe unampeleka shule, vioo vyote vya garicviwe tinted na asione mbele mnakoenda, ikiwezekana badilisha njia unayotumia, hakikisha anaamini kwamba mnaenda hospitali na sio shule, na wakati mnaingia geti la shule asijue na asishuke kwenye gari, asione wanafunzi wenzake hadi aingie mapokezi, kishwa mwambie mnamsubiri daktari, hatozimia.
Mtoto wa miaka 11 is that dumb? πŸ™„πŸ™„
 
Tuwe realistic,unaweza ukajifanya kuzimia?hebu jaribu wewe mtu mzima kama ina wezekana,vipi kuhusu mtoto,hiyo experience ya kuzimia kaipata wapi katika huo umri wa darasa la tano?Ushauri wangu ni kuwa simama katika Imani ya uponyaji kwa njia ya maombi na kufunga kama kweli unampenda mtoto wako,yako maroho ambayo wanatupiwa watu kwa nia ya kuharibu future ya mtu,amini hilo kuwa lipo,na kama wengine wanavyokupa ushauri wa kutembelea baadhi ya makanisa fanya hivyo,ila usiende kwenye kanisa kama unaenda hospitali,ili ukipata uponyaji wako urudie kwenye madhambi,ni lazima ujitakase kwa kutubu dhambi ili uanze maisha mapya ya kumtukuza Mungu...
 
Tuwe realistic,unaweza ukajifanya kuzimia?hebu jaribu wewe mtu mzima kama ina wezekana,vipi kuhusu mtoto,hiyo experience ya kuzimia kaipata wapi katika huo umri wa darasa la tano?Ushauri wangu ni kuwa simama katika Imani ya uponyaji kwa njia ya maombi na kufunga kama kweli unampenda mtoto wako,yako maroho ambayo wanatupiwa watu kwa nia kuharibu future ya mtu,amini hilo na kama wengine wanaotoa ushauri wa kutembelea baadhi ya makanisa fanya hivyo,ila usiende kwenye kanisa kama unaenda hospitali,ili ukipata uponyaji wako urudie kwenye madhambi,ni lazima ujitakase kwa kutubu dhambi ili uanze maisha mapya ya kumtukuza Mungu...



Sasa bora huyu anajizimisha mie nilikua najifanya nna mashetan..lol
 
Matokeo yake darasani yakoje kabla ya hilo tatizo? Inawezekana tatizo liko genuine au ana fake tu ila hiyo sio ishu . Anakupa meseji kuhusiana na mambo ya shule, ni kama mtoto kikojozi, anayekula kucha, n.k . Mtafute Dk wa Psychology mzuri akusaidie.
 
Mkuu pole sana.
Wala usiende kwa waganga jikite tuu kwenye maombi.
Na asiombewe yeye tuu inabidi familia nzima mfanyiwe maombi ya ukombozi. Na nyie wazazi pia muwe mnaomba toba kwa ajili ya watoto wenu na vizazi vyenu. Ulimwengu wa roho una mambo mengi sana. Mtoto wenu anaweza kupona kupitia nyie.

Nakazia, usichoke kwenye kumtegemea Mungu. Yawezekana wakati ndiyo unachoka na Mungu ndiyo alikuwa anaanza kujibu.
 
Haya mambo ni magumu sana halafu nashangaa watu wanachukulia kirahisi rahisi tu, haiwezekani mpaka mtoto wako anafikisha huo umri akawa anajifanyisha kwenye baadhi ya mambo mzazi usijue binafsi nakataa..

Huyo mtoto kuna masuala ya kiroho yamemsibu, mapepo machafu au ametupiwa mapepo machafu.. Jitahidi na maombi na ikiwezekana muamishe mpeleke mkoa mwingine au mazingira mengine wakati wa maombi na atokee huko kwenda shule... Kama hapo ulipo ni mtaa umepanga hama na familia yako msimuage yeyote na mhamie mnapokujua wenyewe huku mkiendelea na maombi.. Fatilia pia historia ya familia yako na mkeo..
 
Back
Top Bottom