leiya
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 654
- 1,558
Watu sita wamepoteza maisha na wengine 19 kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma, kutokana na kuugua ugonjwa ambao mpaka sasa haujafahamika, na hivyo kusababisha serikali kupiga marufuku mikusanyiko ya watu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Mkuu wa mkoa wa Dodoma Bw. Jordan Rugimbana amewataka wale wote waliokuwa wakiendesha zoezi la usafi kwa matamasha, kuanzia sasa hayataruhusiwa, ili kuzuia ugonjwa huo kuenea.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. James Charles, taarifa za ugonjwa huo zilipatikana katika kijiji cha Mwakisabe wilaya ya Chemba, na dalili zake ni kuhara, kutapika, maumivu ya tumbo, macho kuwa ya njano na mgonjwa kuwa na choo, mkojo na matapishi meusi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amebainisha kuwa kwa sasa sampuli zimeshapelekwa Dar es Salaam kwenye maabara kuu ya taifa ya mkemia mkuu, kwa ajili ya uchunguzi.Hadi sasa ugonjwa huo umeshaenea katika vijiji saba vya wilaya za Chemba na Kondoa na kuathiri watu 19.
Chanzo: Channel 10