Ugomvi wa mama na baba ni haki kuingilia kama mtoto.??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugomvi wa mama na baba ni haki kuingilia kama mtoto.???

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tabutupu, Dec 25, 2010.

 1. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,648
  Likes Received: 4,383
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  HABARI WAKUBWA ZANGU. NIMEKUJA HAPA MNISAIDIE INAPOTOKEA BABA NA MAMA WANAGOMBANA, MIMI KAMA MTOTO NARUHUSIWA KUWA REFA??.

  1. JE NI HAKI NIKAINGILIA UGOMVI KATI YA MAMA NA BABA??

  2. SOME TIMES NAJUA KUWA MAMA NDO AMEKOSEA LAKINI SIWEZI MWACHA MZEE AENDELEE KUMWANDAMA MOTHER. NIFANYAJE HAPA NAPO

  3. JE HATA KAMA NIKIINGILIA, NIFANYAJE ILI NISIPENDELEE UPANDE MMOJA UKIZINGATIA KUWA NAMPENDA MAMA KULIKO BABA NA HII IMETOKEA HATA SIJUI KWA NINI.

  NAOMBA MASAADA WENU.
   
 2. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,738
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Ukiingilia, isiwe kupendelea upande wowote hata kama unajua aliyekosea. Wapatanishe halafe waeleze wazi, kuwa next time wanapigana wapiganie chumbani kwao, wewe huitaji kujua.
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Dec 25, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hapo ni kutumia busara. Unapima kwanza nini chanzo cha ugomvi maana mara nyingi kwenye haya mambo lazima kunakuwaga na underlying reason(s). Sababu inaeza ikawa imeanzia chumbani na ninyi watoto mnachoona ni zile immediate reasons.

  Si vizuri kuelemea upande mmoja lakini pia inategemea na hali ya ugomvi. Pia si vizuri kuingilia ugomvi wa wazazi lakini hilo nalo inategemea.

  Mimi msimamo wangu ni kutokuingilia unless pale inapobidi. Kwa mfano nikiona maisha ya mmoja yako hatarini then I'll step in but will do so gingerly.
   
 4. smati

  smati Senior Member

  #4
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmm, hii kazi kweli. Busara za kitoto ndoo zinahitajika.
   
 5. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Usiingilie ugomvi wa wazazi labda kama wanagombana mbele yako hadi kufikia hatua ya kutaka kupigana.
  Kama wewe ni mtoto wa kwanza ongea na wazazi wako kwa nyakati tofauti ikiwa lengo lako ni kusuluhisha ila usionekane unapendelea.
  Pole sana.
   
 6. smati

  smati Senior Member

  #6
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unamaanisha nini unapo sema mbela yako, wakiwa chumbani utaacha waumizane wakati unasikia wanagombana ???
   
 7. s

  shosti JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  nimekulia kwenye nyumba ya wazazi wanaogombana kila siku na ndio maana mpaka leo sina mwenza,maana nikiona unyasi tu nashituka
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Dec 25, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,443
  Likes Received: 81,492
  Trophy Points: 280
  Hakuna mtoto (awe bado ni mtoto au hata mtu mzima anayependa kuona wazazi wake wakigombana) kama ni mtu mzima ni lazima uingilie baada ya kupata chanzo cha ugomvi huo toka pande zote husika. Na kwa maoni yangu, ukishajua kiini cha ugomvi ule inabidi kusema ukweli kabisa kama ulivyoufahamu na kama kuna mkosaji ni kumwambia ukweli tu alichokifanya si sawa na pia ujaribu kwa kila hali kuwapatanisha ili baada ya kuzungumza nao ugomvi wao uwe umemalizika.
   
 9. smati

  smati Senior Member

  #9
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana shosti. Ni mapito lakini mungu atakupa mwema mstaarabu, mpole mnyenyekevu na mcha mungu.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Dec 25, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,443
  Likes Received: 81,492
  Trophy Points: 280
  Dah! pole sana lakini usikate tamaa ya kuwa na mwenza wa kimaisha na inawezekana kabisa maisha yenu yakawa tofauti na maisha ya wazazi wako. Pole sana.
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Dec 25, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,443
  Likes Received: 81,492
  Trophy Points: 280
  Yule Marvin Gaye aliuwawa na baba yake baada ya kuingilia ugomvi kati ya wazazi wake. Inasemekana Baba wa Marvin Gaye alikuwa na tabia ya kumnyanyasa mkewe na hata kumpiga kitu ambacho kilikuwa kinamkera sana Marvin na hatimaye siku hiyo kuamua kumtetea mama yake na kusababisha kifo chake.

  YouTube - Sexual Healing - Marvin Gaye
   
 12. n

  nakatamtende Member

  #12
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unatakiwa kuingilia pale unapoona mambo yanaenda mrama usisite kutoa maamuzi,na uwe shujaa
   
 13. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #13
  Dec 25, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  This is off point:

  Ugomvi wa Marvin Gaye na baba yake ulikuwa kuhusu wapi birthday ya MG ifanyike siku ya pili yake, baba alitaka nyumbani kwake, mama na mtoto walikuwa wanataka sehemu nyengine.

  Naikumbuka kama leo maana breaking news zilipotoka nilikuwa huko huko majuu.
   
 14. s

  shosti JF-Expert Member

  #14
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  huwezi amini baadhi ya niliowapoteza huwa nikiwaangalia baadae nagundua nilipoteza zaidi ya mpenzi
   
 15. s

  shosti JF-Expert Member

  #15
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  sidhani maana huwa kuna hali fulani inanipata,mpaka nikija shtuka nishampeteza mtu muhimu sana,mimi mwenyewe ndio huwa najiona kuwa hawastahili kuwa nami maana nitawatoa kwenye mstari,ila ni tatizo nadhani wazazi wangejua wanatengeneza bomu gani kwa watoto zao wangefanya kila namna kuacha ugomvi wa kiloa siku,ndio yashamwagika kaka hayazoleki
   
 16. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #16
  Dec 25, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  inahitajika uwe na busara ya hali ya juu sana otherwise baadaye kuna uwezekano wa wewe kuchukiwa na upande mmoja. Kuna jamaa mapacha walimtwanga baba yao kisa mama yao alichelewa kurudi home, miaka hiyo ya themanini hakuna vi cellular basi mama kaja saa nne usiku baba kanuna kishenzi anamuuliza ulikuwa wapi mama anasema kachelewa sababu wageni walikuwa wengi kwa kaka yake so asingeweza ondoka mapema bila kuhakikisha wageni wale wameondoka. Mmewe hakuridhika si akamkata mkewe kibao, mama akapiga yowe nakufaaaaa wale twins wakaja walipoambiwa maza kapigwa na dingi duu si wakamvaa dingi eti Baba usitupigie mama yetu, kwanza wewe huyu ni MPENZI WAKO TU, sisi huyu ni MAMA YETU tafadhali tutaKUUWA usituumizie mama yetu hahahahahaha dingi alikoma. Cha msingi ni kuwa muungwana kwa pande zote.
   
 17. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #17
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  shosti unapopata mwenza inabidi ufute mawazo kabisa kwamba ndoa ni kugombana la sivyo utafanya kupita tu na kuondoka kwenye ndoa.
   
 18. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pole. Kutokuwa na mwenza pia unajinyima haki yako ya kupendana na mtu. Ukipata mtu mwelewa pendana naye. Ukipendana na mtu, siwezi kuelezea raha yake. Tofauti huwa zinakuwepo, kikubwa ni kujua namna ya ku-handle hizo tofauti.
   
 19. s

  shosti JF-Expert Member

  #19
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  kweli kaka ila tatizo ni pale kaugomvi kadogo tu kanapotokea basi kwangu ni kitu kingine kabisa,labda kuna tofauti ya ugomvi kutoka nyumba moja hadi nyingine,kwetu ilikuwa tofauti kidogo unaposhuhudia mtu anapigwa kipigo cha paka mwizi kisa amezima taa kabla mume hajarudi,au amezidisha kunywa vidonge toauti na maagizo ya dr naomba unielewe kidogo hapo
   
 20. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #20
  Dec 25, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,807
  Likes Received: 1,973
  Trophy Points: 280
  siwezi kumuona mama anadundwa na baba halafu nikakaa kimya, nitaingilia tu hata kama mila haziruhusu,
   
Loading...